Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

LADY JAYDEE ASHIRIKI KWENYE WIMBO RASMI WA KOMBE LA DUNIA

$
0
0
Msanii mkongwe wa muziki nchini Judith Mbimbo maarufu kama Lady Jaydee ameshiriki kuimba wimbo maalum wa kombe la dunia 2014 akishirikiana na David Correy na rapper wa Kenya, Octopizzo

Katika wimbo huo, Lady Jaydee na Correy wameimba kwa lugha ya Kiingereza huku Octopizzo ‘akichana’ kwa Kiswahili.

Wimbo huo ulipigwa kwa mara ya kwanza wiki hii jijini Dar es Salaam wakati kampuni ya Coca-Cola ilipozindua promosheni yake mpya ya miezi miwili ya Kombe la FIFA la Dunia 2014 ambayo itawawezesha wateja wake kujishindia zawadi mbalimbali zikiwamo tiketi za kwenda kushuhudia mechi za robo fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil.

PIC OF THE DAY...DAVID MOYES AKITIMULIWA KWA MASHOKA NA MARUNGU

$
0
0
Kamata Mwizi.....Huyooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo

NEY WA MITEGO" VIDEO YA KUVALISHWA PETE SIWEMA NI YA MIAKA MIWILI ILIYOPITA"

$
0
0
Siku ya leo Ney wa Mitego Amesikika Radio Clouds akiongelea ile habari iliyomake headlines week hii ya Mchumba wake kuonekana kwenye Video akivalishwa Pete na Jamaa....Ney Amesema kuwa hiyo Video ni ya Miaka Miwili iliyopita wakati huo hakuwa na Siwema na Kabla hajakuwa na Siwema Bi Dada huyo Alimwambia kwahiyo si kitu kigeni kwake..Yeye anachojua ni kwamba sasa hivi Siwema ni Wake, huyo aliyeonekana anamvalisha Pete yalishaisha siku nyingi......So Jamaa Embu Acheni Kupanic Basi....

MATOKEO YA YANGA NA KAGERA PAMOJA NA KILICHOTOKEA MECHA YA AZAM NA RUVU

$
0
0
Mabingwa wa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania bara Yanga ya Dar es salaam leo imepata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Kagera Sugar.
Katika mchezo huo uliopigwa katika dimba la uwanja wa taifa jijini Dar, Yanga waliuanza mchezo huo kwa kasi na kufanikiwa kupata goli kupitia Hamis Kiiza katika dakika ya 3 tu mchezo.
Didier Kavumbagu aliiongezea Yanga goli la pili kwenye mchezo  huo katika dakika ya 34 na mpaka mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa 2-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na timu kushambuliana kwa zamu na katika dakika ya 64, Kagera wakapata bao la kufutia machozi kupitia kwa Daudi Jumanne.
Katika hatua nyingine mchezo wa Azam FC dhidi ya Ruvu uliokuwa ukifanyika huko Mlandizi ulihairishwa kutokana na mvua kubwa iliyoonyesha na kuharibu uwanja – mchezo huo sasa utapigwa kesho.

UWEZI AMANI ETI HUYU NI SHILOLE KABLA HAJAJA MJINI

$
0
0
Picha hii kutoka kwa Shilole enzi zake zamani kabla hajaanza kazi kwenye kiwanda cha burudani.
Hapo alikuwa anaitwa Zuwena kabla ya majina ya Shilole na Shishi baby hayajaanza kutumika.
Kweli Mjini patamu........

DIAMOND AELEZA JINSI ALIVYOKUTANA NA DON JAZZY NA KUSHIRIKI KATIKA WIMBO WAO

$
0
0
Hivi karibuni Diamond Platnumz atasikika kwenye wimbo wa wasanii wakubwa wa Nigeria, Don Jazzy, Waje na Dr Sid waliomshirikisha kwenye nyimbo zao alipokuwa nchini humo mwezi huu.

Staa huyo amezungumza na Bongo5 kuhusiana na jinsi alivyokutana na wasanii hao.

“Wakati nipo Nigeria nimebakiza siku moja kurudi wakaniemail wakaniambia ‘Mavin Records, Don Jazzy na Dr Sid wangependa kufanya kazi na wewe kama bado upo Nigeria,” Diamond ameiambia Bongo5. “Niliona ni jambo zuri kufanya kwasababu Don Jazzy ni mtu mkubwa na ukiangalia industry ya muziki ni mtu ambaye ana sehemu yake. So nikakaa na uongozi wangu nikawaambia ‘nimepata email kutoka kwa Don Jazzy anasema anapenda kufanya kazi na sisi. Basi nikawa link na menejimenti yangu wakazungumza wakapanga vitu vyote vinavyotakiwa tukaenda tukafanya,” ameongeza.

Amesema katika wimbo huo wa Dr Sid, Don Jazzy ambaye ndiye producer naye ameweka sauti yake. Hata hivyo Diamond amesema wimbo alioshirikishwa na Waje ndio alioupenda zaidi na kwamba utakuwa moto wa kuotea mbali.

Msikilize zaidi hapa.

UEFA:MAN U YACHAPWA...MADRID YAPETA

$
0
0
Haya ni matokeo ya Mechi za Jana


NDOA YA WEMA, DIAMOND AGOSTI

$
0
0
MTABIRI mwenye jina kubwa kwa sasa Bongo, Maalim Hassan Yahya Hussein ambaye ni mrithi wa kazi za marehemu Yahya Hussein ameibuka wiki hii na kuanika kwamba, Agosti mwaka huu Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Wema Sepetu watafunga ndoa

Akizungumza na Amani jijini Dar es Salaam juzikati, Hassan alisema amepiga mahesabu ya kinyota kwa wapenzi hao na kubaini kuwa, Agosti ndoa yao itafungwa mahali popote nchini Tanzania.

Akaongeza: “Kama wapo kwenye mipango au maandalizi wakazane, kwani mwezi Agosti ndiyo wenyewe kwa mujibu wa nyota za wote

“Lakini nawapa angalizo muhimu, wakae wakijua kwamba kama ndoa hiyo haitatimia Agosti kutokana na sababu zao wenyewe, haitafungwa tena hadi mwaka 2016, kwa sababu lazima ndoa yao iwe kwenye mwaka unaogawanyika.”
GPL

WIMBO WA BABY MADAHA WACHAGULIWA KUWANIA MTV EUROPE AWARDS

$
0
0

Wimbo wa Baby Madaha uitwao ‘Nice and Slow’ umechaguliwa kuwania tuzo za MTV Europe mwaka 2014. Msanii huyo wa Candy n Candy Records, ameiambia Bongo5 kuwa kwa sasa anasuburi kutumiwa code kwaajili ya kuuwezesha wimbo huo kupigiwa kura.

“Nilitoa song inaitwa ‘Nice and Slow’ ni whisper song (wimbo wa kunong’oneza) haiendani na mazingira ya kitanzania. Kwahiyo nikawa nimeipeleka moja kwa moja kwenye reverbnation chart, nilivyoipeleka UK kwasababu unajua Joe, huyu meneja wa Candy n Candy, ile kampuni tuliyoingia nayo ubia wa kusambaza movie pia wanasambaza muziki. Kwahiyo walipoisambaza UK ikawa imeingia kwenye chart za reverbnation, sasa hivi ipo namba mbili. Kwahiyo ni wimbo pekee kutoka Afrika ambao umefanya poa especially Afrika Mashariki,” amesema.

‘Kwahiyo kwenye group ya upcoming artists, MTV wameniandikia barua wakaniambia ‘umekuwa nominated, usubiri code kwaajili ya kupigiwa kura.”

Katika wimbo huo, Baby Madaha amemshirikisha bosi wake, Joe Kairuki ambaye ni CEO wa label hiyo. Hata hivyo akiongea na gazeti la The Star la Kenya, Kairuki alidai kuwa ili wimbo huo uingie kwenye kinyang’anyiro cha mwisho ni lazima upigiwe kura 2000.

“All we are urging our fans is to vote highly for the song once it’s put up for voting this Friday. the song must amass 2000 or more votes in order to be nominated for the awards and we hope our fans will not let us down,” alisema.

Muimbaji huyo amesema pia kuwa wimbo huo umetajwa kuwania tuzo zingine ziitwazo International Music Entertainment Awards, IMEA.

“Tuzo nyingine ni IMEA so nasubiri code ili kura zianze. Naomba watu waniunge mkono niipaishe Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. I am so happy for that kupiga hatua kimataifa,” ameongeza.

Msikilize zaidi hapa.

JE UNASUMBULIWA NA KISUKARI, PRESSURE NA MAGONJWA MENGINE AMBATANISHI?

$
0
0
Diabetes/ cardiovascular disease screening
Management of Patients with diabetes and Cardiovascular diseases
Diet Counselling



Contact Details

St. Laurent Diabetes Centre
Second Floor, Wing B
MMDC Building opp. CCBRT
P.O.Box 2769
Dar es Salaam
E mail: info@stlaurentdiabetes.co.tz
Phone: +2550737210812
Mission
To be a centre of excellence in providing complete spectrum of diabetes care services from prevention to managing diabetes complications through personalised diabetes care plans

CHEGE CHIGUNDA AMEMPA MAKAVU LIVE BINTI ANAYEDAI KUWA MPENZI WAKE

$
0
0
Kutoka kwenye Instagram ya Msanii Chegge leo ameweka maneno ya Binti moja akimwambia mwingine kuhusu mahusiano yake na Chegge. Kwenye post ya Chegge anaonekana kutomfahamu kabisa binti huyu. Chegge ameandika maneno haya


 ” Kupoteza time na kufungua AC feki ili kutibua Watu kwanza niushamba pili usilazmishe ukaribu na mtu ambae hata time ya kutaka kukujua hana sishangai sana coz najua kuna watoto walozaliwa kitandani na wengine walizaliwa chooni japo kwa bahati mbaya,sio kwamba inanisumbua bt nimekwita mshamba coz unajificha,nautaendelea kua mshamba coz naamini hutojitokeza utaishia kufanya ushamba wako mpk utapojigundua unaofanya niushamba basi utaacha”

OLE SENDEKA AAIBIKA KWA JITIHADA ZA KUZUIA HOJA ZA LUPUMBA BUNGENI

$
0
0
Mzee wa Simanjiro, Ole Sendeka ameipata ya moto baada ya kukutana na Zomea zomea ya ajabu pale alipotaka kufanya jitihada za kuzuia hoja kali za Prof Lipumba alizokuwa anazijenga alipokuwa akitolea ufafanuzi wa mapendekezo ya wajumbe wachache wa kamati namba kumi. Hoja za Lipumba zilikuwa zinaelekea kuwavua nguo wakubwa kwa jinsi alivyochambua mapato na matumizi ya serikali na ubadhirifu wa pesa hzo mpaka kuwaletea hofu ya kuzmudu serikali 3. Hapo Ole Sendeka akaona aokoe jahazi kwa kufifiza au kupunguza hoja za Lipumba kwa kuomba utaratibu wa kijinga na ndipo alipokutana na zomeazomea ya hali ya juu iliyotulizwa kwa nguvu kubwa ya mwenyekiti Sitta.

MTANZANIA AKAMATWA KENYA KWA KOSA LA UGAIDI

$
0
0
Juma Hamisi and his wife Misaid Athman when they appeared before court, the two have been remanded. A man and his wife have been charged in Mombasa with child abduction and possessing material inciting terrorism.

They were arrested last week in Mombasa's Likoni slums following the March 23 massacre of worshipers at the Joy of Jesus Church and the infants they are accused of stealing are the children of a terrorism suspect killed by police in February last year.

Juma Hamisi and Misaid Athman, a Tanzanian were arraigned before magistrate Justus Kituku Wednesday facing the charge of possessing materials with information contrary to the law. The prosecution alleged that the couple was arrested with material on Digital Versatile Disks DVDs and Video Compact Disks VCDs which police claim have messages inciting terrorism. The DVDs and VCDs include some entitled Khilafa ni Suluhisho , Nasaha Kwa Vijana, Dua for Mujahidun, Cowboys in Iraq, Rijal, Lfe Under the Shade and two other unmarked DVDs which police allege were seized when they raided the couple's house on Tuesday last week.

On April 3 this year, police received court permission to detain them for more days to enable investigations and now the prosecution claims the material has been used in instigating the commission of terrorism act by "providing and facilitating the provision of training instructions to any person or member of a terrorism group in the practice of military exercise and movements. "This was with the knowledge that such instructions are intended for the use in the commission of terrorist act in contrary to the terrorism act." In the second count they are accused of  "denying eight years old Abdukarim Shaban and seven years old Hudhafa Shaban their rights to live and be cared for by their parents Fauzia Nasonga (their mother) by taking them away from the custody of their mother." See Also: Christian, Muslim clerics hold talks on insecurity The two suspects who are unrepresented pleaded guilty to the first charge but denied the second.

Police told the court that the two infants were children of the late Shaban Namusanga who was shot dead on February in the year 2013 after being suspected of being a terrorist. His wife, the mother of the children relocated to Kakamega where she is alleged said to have remarried to one Musa Kassim. She is now facing the charge of neglecting the children. The two suspects pleaded with the magistrate to set them free on bond to take care of their children.

AZAM NOMA SANA...UBINGWA WANUKIA...ISIPOCHUKUA KOMBE KUNA MKONO WA MTU

$
0
0
Zimebaki pointi tatu tu Azam FC kuwa mabingwa wa Ligi Kuu Bara kwa mara ya kwanza, hilo halina ubishi.
Azam FC wameshinda mabao 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa leo kwenye Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi.

Kwa mujibu wa salehjembe.blogspot.com iwapo Azam FC itaifunga Mbeya City katika mechi yake itakayofuata, Azam ambayo sasa ina pointi 56 itatawazwa rasmi kubwa mabingwa.

Katika mechi ya leo magoli ya Azam FC yalifungwa na mshambuliaji mkongwe, Gaudence Mwaikimba, Himid Mao na Kipre Tchetche

TAARIFA ZILIZO ZAGAA KUWA MBEYA CITY IMEHONGWA NA AZAM KUWAPATIA USHINDI

$
0
0
Kwanza nachukua nafasi hii kuwashukuru kwa dhati wapenzi wote wa mchezo wa mpira wa miguu na wapenzi wa Mbeya City Fc popote pale walipo kwa kuiunga mkono timu yao muda wote wa michezo ya ligi kuu inayoelekea ukingoni hivi sasa.Klabu inathamini nafasi ya wapenzi na washabiki katika kujenga timu imara na yenye ushindani kama walivyofanya kwa timu yetu.
Timu yetu ilianza ligi msimu huu 2013/2014 ikiwa na malengo ya kuchukua ubingwa au kuwa katika nafasi za juu za ligi yetu.Hiyo ndiyo dhamila iliyokuwepo kwa viongozi,wachezaji pamoja na benchi la ufundi.
Michezo miwili imesalia kwa timu yetu kabla ligi kuu ya Vodacom kumalizika katika msimu huu 2013/2014.katika safari yetu ya ligi kuu kwa mara ya kwanza msimu huu, changamoto nyingi za kiutawala na za kimtazamo kutoka kwa wadau wote wanaohusika na mchezo wa mpira wa miguu nchini tumezishuhudiaChangamoto hizo ikiwemo upangaji wa ratiba usiokuwa na uwiano mzuri.
Baadhi ya mechi kuamuliwa vibaya na waamuzi wa mchezo, wizi wa mapato ya milangoni unaotokana na mfumo mbaya wa uuzaji wa tiketi, uadilifu mdogo kwa baadhi ya viongozi wenye dhamana ya kusimamia mpira katika ngazi zote n,k.
Kuelekea mchezo wetu wa tarehe 13/04/2014 dhidi ya AZAM FC kumezuka propaganda chafu na ambazo si sahihi katika ukuzaji wa mpira hasa wa ligi ndogo kama ya Tanzania.
Nachukua nafasi hii kutoa ufafanuzi wa baadhi ya mambo ambayo yamekuwa sehemu ya propaganda hizo:
1.    Klabu imehaidiwa kununuliwa na inajiandaa kutoa ushindi kwa kwa timu ya AZAM Fc na kuwarahisishia mazingira ya Ubingwa.
Halmashauri ya jiji la Mbeya limekuwa katika mchakato wa kutafuta na kununua basi kwa ajili ya matumizi mbalimbali  ya Halmashauri ikiwemo kutumiwa na timu zake ( Netiboli na Mpira wa miguu)ambazo zote zipo ligi kuu ya michezo husika kwa kufuata sheria ya manunuzi ya Umma.
Mchakato huo ulianza tarehe 8/8/2013 halmashauri ilipotangaza nia hiyo katika gazeti la “the guardian” la tarehe hiyo kwa tender no.LGA/069/2013-2014/MCC/G/01   hii ni baada ya Halmashauri kutenga bajeti ya fedha za makusanyo yake ya ndani  kwa mwaka wa fedha 2012/2013 na 2013/2014 ili kukidhi haja hiyo.
Tangazo hilo halikupata mzabuni mwenye sifa za kufanya usambazaji wa basi hilo hivyo tangazo hilo lilirudiwa tena tarehe 12/2/2014 katika gazeti la majira kwa Tender No.LGA/069/2013-2014/MCC/G/01 (Re-advitised), Mchakato na maandalizi ya ufunguaji  wa ufanyaji wa tathmini wa zabuni hiyo unaendelea kwa mujibu wa sheria ya manunuzi ya Umma.
Pamoja na mchakato huo hapo juu,pia klabu inaendelea na mazungumzo na wadau mbalimbali wenye nia ya kuwekeza kwa udhamini wa bidhaa zao,moja ya maeneo ya udhamini ni pamoja na ununuzi wa basi la wachezaji  taratibu na makubaliano haya yatakapo kamili umma wa wapenda mchezo wa mpira wa mguu utajulishwa.
Hivyo propaganda hiyo kuwa klabu imehongwa basi si za kweli na si sahii ila zina nia ya kuidhalilisha timu yetu.
2.    Propaganda kuwa Mwalimu Juma Mwambusi kanunuliwa nyumba Maeneo ya chamazi ili apange kikosi dhaifu siku ya mchezo tarehe 13/4/2014.
Mwalimu(Kocha) Juma Mwambusi ni muajiliwa wa Halmashauri ya jiji la Mbeya,kwa maana hiyo ni mtumishi wa Umma. Mwalimu Mwambusi amekuwa na timu yetu kwa muda mrefu sasa na ataendelea kuwepo.Kumekuwepo na maneno yasiyofaa dhidi ya mwalimu wetu toka mzunguko wa pili wa ligi kuanza.
maneno haya yamekuwa na nia ya kuaribu muenendo wa timu ili ianze kufanya vibaya lakini zaidi ya hapa yana nia ya kumdhalilisha mwalimu wetu na taaluma ya ukocha nchini.
Mwalimu amefedheheshwa  sana na taarifa hizo.
3.    Propaganda kuwa wachezaji wote wa kikosi cha kwanza wamepewa hongo wacheze chini ya kiwango 13/4/2014.
Wachezaji ndiyo wachezaji wenye nidhamu kubwa katika ligi ya mwaka huu ndani na nje ya uwanja muda wote,ni waadirifu na wanajua wanataka nini.Mpira ndiyo ajira yao kama watumishi wa umma ndani ya Halmashauri ya jiji la Mbeya.Hawajawahi na wala hawatawahi kuchukua rushwa kwa lengo la kupanga matokeo.
Klabu yetu haisadiki katika upangaji wa matokeo ya mchezo wa mpira wa miguu kwani tunajua fika kuwa hakutaisadia kama klabu lakini pia kama taifa katika kuendeleza mpira wa miguu nchini.
Hitimisho,
Mchezo wa mpira wa miguu una matokeo matatu kushinda,kushindwa na kutoka sare. Klabu inaamini kuwa timu iliyojiandaa vizuri kama yetu inastahili kupata matokeo mazuri uwanjani.Falsafa mojawapo ya timu yetu ni kushinda mechi kwa kucheza mpira unaovutia na kuwaburudisha watazamaji.
Tuhuma mbalimbali za upangaji matokeo katika ligi yetu zimeanza kuota mizizi hasa ligi inapoingia mzunguko wa pili ,katika suala hili kama ambavyo linataka kuhusishwa nasi yawezekana propaganda hizi kwa upande wa timu inayotuhumiwa kuandaa michakato hiyo wana uzoefu nalo na yumkini ndiyo chachu ya mafanikio yao mpaka kufikia hatua hiyo waliofikia sasa.
Kama timu hiyo inauwezo wa kirasilimali wa kufanya uovu huo wote iweje ishindwe kuwa na timu imara na ya ushindaji mpaka itegemee kutafuta wachezaji wa timu pinzani kupata matokeo mazuri?
Timu yetu ndiyo timu pekee changa miongoni mwa timu tano zinazoongoza msimamo wa ligi yetu kwa sasa,si hivyo tu bali ndiyo timu pekee inayoundwa na wachezaji wengi wapya katika ulimwegu wa soka na inayoundwa na Watanzania watupu kuanzia wachezaji,benchi la ufundi pamoja na viongozi.Hii inathibisha kuwa kama taifa tunaweza kufanya kazi nzuri bila kutegemea wachezaji toka nje baadhi yao wasiokuwa na tija.
Mpira ni ajira hatuna budi kuuratibu vema ili kutoa nafasi inayostahili kwa vijana wetu ili kupunguza tatizola ajira nchini lakini pia kutumia vipaji vyao kulipa taifa muonekano stahili.
Mamlaka zinazohusika hazina budi kuanza kufuatilia na kuchukua hatua kali kwa baadhi ya timu zinzohusishwa na upangaji wa matokeo ili kulinda heshima ya mchezo huo bila kuogopa uwezo wa rasilimali wa timu hizo.
E.E.Kimbe
KATIBU MKUU
MCC FC
9.04.2014

JUMA NATURE NYOTA KUBWA INAYOELEKEA KUZIMIKA

$
0
0
Daaah. Nakumbuka jamaa akipita mtaa wa Kongo watu walikuwa wanaacha biashara zao na kufunga mtaa, nakumbuka matamasha ya wazi pale mnazi mmoja, Coco Beach na Biafra Kinondoni yani alikuwa tatizo Juma Nature, mikoani ndio usiseme. Aliwahi kuonekana mkoani Kigoma yani wafanya biashara waliacha maduka kwenda kuangalia gari la matangazo alilokuwa amepanda Juma Nature.

Nakumbuka interviews alizokuwa akifanya Star TV, EATV na kwingineko, viewerz walikuwa wengi wakickia kipindi flani atakuwepo Juma Nature. Nakumbuka mkutano wa CCM Dodoma, watu waliacha kupanga foleni kumpungia mkono Kikwete na badala yake mamia kwa mamia walienda kusukuma gari alilokuwemo Juma Nature. 

Jamaa now imebak historia.

I MADE DAVIDO POPULAR-TANZANIAN MUSIC STAR, DIAMOND BOASTS

$
0
0

Tanzanian artiste, Naseeb Abdul, aka Diamond Platnumz, is a popular artist in his home country. He holds eight Kilimanjaro awards.

The singer recently did a hit with Nigerian music star, Davido in the remix of his single ‘Number One’ and he disclosed his happiness for achieving so much.

Speaking about the collabo, the singer revealed that the duet with Davido has now made the Nigerian star popular in Tanzania.

“I met Davido when he came over to Tanzania for a show and when we were together, he heard my song. I told him I would love to feature him on the remix of my song, ‘Number One’, and he agreed. Currently the song is topping charts in various African countries.”

“Shortly after, he released Aye and that made him very popular in my country as well. They love the song in my country. I featured Davido on the track because I wanted to launch myself into the West African market and he was the best person for the job. I used Davido to break into the West African market,” the Tanzanian singer said further.

VERA SIDIKA IS NOW PREZZO'S NEW GAL

$
0
0
Vera Sidika is, beyond a iota of a doubt, one of the most bustluscious and bootylicious divas of our time. Part of the reason she attracts love and hate in an almost equal measure. Ever since the sands beneath the Nairobi social setting started shifting, a new crop of influential persons were thrown into the scene. They codified snobbery, they made careers out of fame, and they did some “amazing things” for this city; they are socialites. One of them is Vera. Even she absolutely hates that word (so do many other women to whom you might once have affixed the label) she’s one of the most sought after video vixens in Kenya. So far she’s only featured in one Kenyan music video with a couple more from West Africa. And now, his “rapcellency” Prezzo hooked up with her and made her his “new gal”. Take This is the first single from Prezzo’s 2014 album, Rapcellency.

MSEKWA ATOBO SIRI YA MUUNGANO

$
0
0
Wiki mbili kabla ya Tanzania kuadhimisha miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Pius Msekwa ametoboa siri ya Muungano huo akisema “mchakato wa kuundwa kwake ulifanywa kwa siri na haraka sana,” kutokana na upepo wa kisiasa na usalama wa kipindi hicho.

Akizungumza katika moja ya mfululizo wa vipindi vya miaka 50 ya Muungano vinavyorushwa na Redio ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC Taifa), Msekwa alisema woga wa hayati Abeid Amani Karume kupinduliwa na maadui, ulikuwa ni miongoni mwa sababu za kuharakisha Muungano huo.

Msekwa aliyekuwa Katibu wa Bunge la Tanganyika wakati Muungano unaasisiwa, alisema pia yeye na wenzake walichelewa kujua kwamba Mwalimu Julius Nyerere (Rais wa Kwanza wa Tanganyika) na Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Karume walikuwa na majadiliano ya kuunganisha nchi hizo.

“Kikubwa cha kusema ni kwamba mazungumzo ya Muungano huo yalifanywa kwa siri.... kwa siri sana baina ya waasisi wa nchi hizo. Kwa nini yalifanywa kwa siri? Siyo kwa sababu walikuwa wababe, la hasha, bali kwa mazingira ya wakati ule, kulikuwa na maadui ambao wasingependa nchi hizi kuungana,” alisema Msekwa na kuongeza:

“Kwa woga huohuo, ndipo Mwalimu alipokubaliana na mwenzake wafanye mazungumzo ya siri mpaka waliposaini yale makubaliano na kunijulisha.”

Msekwa ambaye pia amewahi kuwa Spika wa Bunge la Muungano, alisema baada ya makubaliano ya Muungano, Nyerere alimwita na kumjulisha kuwa walishakubaliana (na Karume) kuungana, hivyo walihitaji baraka za Bunge kuridhia Muungano huo.

“Mwalimu akaniambia, ‘wewe Katibu wa Bunge unaweza ukawaita wabunge wakaja kwa harakaharaka kuridhia makubaliano?’

“Nakumbuka siku hiyo ilikuwa Jumanne na Mwalimu alipendekeza wabunge wafike Ijumaa ya juma hilohilo, nao wabunge wakaja wakaridhia.”

Simulizi hii ya Msekwa kuhusu Muungano imekuja wakati kukiwa na vuguvugu la muundo wa Muungano katika Bunge Maalumu la Katiba, kutokana na mapendekezo yaliyomo kwenye Rasimu ya Katiba kupendekeza serikali tatu badala ya Serikali mbili za sasa.

Bunge kuridhia

Aliongeza kuwa, baada ya Bunge la Tanganyika kuridhia Mwalimu Nyerere aliutaka muswada huo “kwa haraka sana”  ili aufanye kuwa sheria na alitaka kupelekewa kwa mkono.

“Baada ya wabunge kuridhia pale Karimjee, nikauchukua muswada na kuupeleka Ikulu, sio mbali pale.

“Mwalimu alifurahi sana, alishajua kuwa ulikuwa umesharidhiwa kwa sababu alikuwa anafuatilia mkutano wa Bunge kupitia redio, ukumbuke zamani hakukuwa na televisheni,” Msekwa anasimulia.

Sababu za kuharakisha

Msekwa alisema kulikuwa na sababu kuu mbili za kuharakisha Muungano; moja ni Mwalimu Nyerere kutaka nguvu ya Afrika itokane na miungano ya nchi, wakati Karume alitaka kuimarisha usalama wa Zanzibar miezi miwili baada ya kuuondoa utawala wa Sultani Januari 12, 1964.

Aliongeza kuwa Nyerere alikuwa amejifunza kutokana na makosa ya awali ambapo maadui waliharibu mpango wa kuziunganisha nchi za Afrika ya Mashariki na kuwa shirikisho.

Hata hivyo, Msekwa aliongeza kuwa, Mwalimu alimwambia Karume wangoje kwa muda, lakini kiongozi huyo wa Zanzibar hakuafikiana na wazo hilo kutokana na masuala yake ya kiusalama.

Alisema hata wakati Bunge la Tanganyika likiridhia muswada wa kuanzisha Muungano, tayari wenzao wa Zanzibar walikuwa wamekwishauridhia.

Muundo wa Muungano

Msekwa alisema suala la kubuni muundo wa Muungano ambalo linasumbua vichwa wajumbe wa Bunge la Katiba sasa, halikuwa tatizo kubwa wakati huo, japo Karume alimwomba Nyerere watengeneze Serikali moja.

“Karume alimtaka Mwalimu waunde serikali moja; yeye awe Makamu wa Rais na Nyerere awe Rais. Lakini Mwalimu hakutaka wazo hilo akihofia maadui wangesema ameimeza Zanzibar na pia alizingatia udogo wa nchi hiyo pamoja na hofu ya kuwa mkoloni mamboleo,” alisimulia Msekwa.

Msekwa alisema mara tu baada ya Nyerere kusaini muswada wa Muungano kuwa sheria, alianza kuunda Serikali ya Jamhuri ya Muungano na aliwachukua wajumbe 20 kutoka Zanzibar kuingia katika Bunge la Muungano.

Alisema baada ya Muungano huo hakukuwa na chokochoko zozote na hata maadui waliotaka kuipindua Serikali ya Zanzibar walikata tamaa.

“Hakukuwa na kitu kinachoitwa kero za Muungano mpaka pale Aboud Jumbe alipoingia madarakani baada ya kifo cha Karume 1972. Jumbe na wenzake walikuwa wanahoji Tanganyika tuliyoungana nayo ipo wapi?” alisema.

BIASHARA ZA FIGO YASHAMIRI NCHINI..ZAUZWA KAMA KARANGA

$
0
0
Katika kile kinachoonekana kukithiri kwa hali ngumu ya maisha, baadhi ya Watanzania wameanza biashara ya kuuza figo zao kwa gharama kubwa kwa watu wenye mahitaji ya kiungo hicho muhimu mwilini.

Uuzaji huo umetokana na ongezeko la maradhi ya figo miongoni mwa Watanzania kwani takwimu za Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii zinaeleza kuwa kuna wagonjwa 470,000 nchini ambao figo zao zimeshindwa kufanya kazi kabisa na wanahitaji upandikizaji. Katika uchunguzi wake, mwandishi wa gazeti hili alifanya kazi ya kutafuta kama wafanyavyo watu wengine wenye mahitaji hayo na alifanikiwa kukutana na watu kadhaa ambao walikuwa tayari kumwuzia lakini kwa gharama kubwa.

Kijana mmoja alikuwa tayari kumwuzia figo mwandishi wetu. Katika kufikia makubaliano mazungumzo ya kijana huyo, Abiyudi Mtaki na mwandishi wetu yalikuwa hivi:

Mwandishi: “Habari yako kaka, nimepata namba yako kutoka kwa (jina linahifadhiwa) amesema upo tayari kuuza figo yako, mimi nina shida kwa sababu mama yangu anahitaji na hali yake si nzuri.”

Muuzaji: “Nitumie meseji nipo kwenye gari.”

Alipotumiwa meseji alijibu hivi: “Dada yangu mimi naelekea Uganda, kuna mtu kanitumia tiketi jana, wakala nilimwambia kuwa nauza, ila yeye hakuniambia iwapo kuna mtu wa Dar es Salaam anayehitaji.”

Mwandishi: “Jamani kaka tusaidie kwa sababu tuna shida, kwani huyo wa Uganda anakupa shilingi ngapi?”

Muuzaji: “Napata milioni 80 aisee!”

Mwandishi: “Basi sitaweza kupata hizo fedha, ngoja niangalie namna nyingine.”

Muuzaji: “Kwani we ulikuwa na ngapi?”

Mwandishi: “Tuna shilingi milioni 20 tu.”

Kiwango hicho hakikukubaliwa na muuzaji huyo.

Mei mwaka jana, Mwanahabari wa Gazeti la The Telegraph la Uingereza alituma ujumbe kwenye ukurasa wake wa facebook na kujifanya kuwa ni kaka wa mwanamke anayehitaji kupandikizwa figo hivyo anahitaji mtu anayeuza.

Ndani ya wiki moja alipata wateja zaidi ya 16 kutoka Uingereza, India na Tanzania waliojitolea kuuza figo zao kwa gharama ya Euro 20,000 hadi 30,000, zaidi ya Sh68 milioni. Daktari Bingwa wa figo kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Linda Ezekiel alisema uuzaji wa figo ni kosa la jinai kwani kisheria ni makosa kuuza kiungo cha binadamu kwa gharama yoyote.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Figo Tanzania, Jaji Frederick Werema alishangazwa na hatua za baadhi ya watu kuchukua uamuzi wa kuuza figo kwa ajili ya kujipatia fedha.

“Kutoa figo ni kosa la jinai, lakini si hivyo tu, kutoa figo ni lazima ufuate taratibu za kisheria na za kitabibu,” alisema Jaji Werema, ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Msemaji wa Wizara ya Afya, Nsachris Mwamaja alisema miongozo na sera za Wizara ya Afya hazikubaliani na biashara ya uuzaji wa figo kama ilivyo kwa uuzaji wa damu.
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live


Latest Images