Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

MWANAMUZIKI H-Baba Alikumbuka Penzi la Irene Uwoya

$
0
0
Unaweza kusema kuwa bado Mwanamuziki H baba anateseka kwa kumkosa aliyekuwa mpenzi, muigizaji Irene Uwoya, kutokana na kuendelea kumkumbuka mrembo huyo hadi katika siku yake ya kuzaliwa.


H Baba ambaye kwa sasa ni mume wa mwigizaji Flora Mvungi amemtakia kheri katika siku yake ya kuzaliwa mpenzi wake wa zamani Irene Uwoya kwa kupost picha yake Instagram na kumpa ujumbe kuwa kuachana siyo vita mpaka washindwe kutakiana kheri katika maisha yao ya kila siku.

Katika ujumbe huo H Baba amesema ukweli wa mambo yote wanaujua wao wawili na mwisho wa siku saizi kila mtu ana maisha yake na maisha yanasonga mbele.

"Kuachana siyo vita ya mimi nisikutakie mafanikio mema kwenye maisha yako ukweli unaujua wewe na mimi. Kikubwa tunaheshimiana, uliolewa nikaoa, una mtoto nina watoto, Una Ndiku mimi nina Mvungi wangu. Mapenzi siyo vita uwoya kazaliwa Happy Birthday Irene Uwoya 'Allah' akuongoze vyema kwenye maisha yako na mafanikio yako nakuombea baraka telee kwenye maisha yako". Aliandika H Baba

AJALI yaua Watu Wanne Wakiwemo Polisi Wawili

$
0
0
Watu wanne wakiwamo polisi wawili, wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupindua katika kijiji cha Seruka kata ya Chipogoro tarafa ya Rudi wilayani Mpwapwa mkoa wa Dodoma.

Ajali hiyo ilitokea Desemba 19, mwaka huu, saa 11:30 jioni katika kijiji hicho baada ya gari walilokuwa wakisafiria T517 CDL Toyota Alphat katika barabara kuu ya Dodoma- Iringa, kuacha njia na kupinduka na kusababisha vifo vya watu wanne na majeruhi tisa.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo, Ernest Kimola, amesema gari hiyo iliyokuwa ikiendeshwa na Aggrey Lucas, baada ya kufika katika kijiji hicho, liliacha njia na kupinduka na kusababisha vifo vya askari Konstebo Mahende na Konstebo Sasi Mwita ambaye ni askari mkoa wa Songwe.

Kamanda Kimola amewataja wengine waliofariki katika ajali hiyo ni mke wa Konstebo Mwita, Pendo Mwita na Emaculata Nyangi.

Amewataja majeruhi wa ajali hiyo ni Neema Mwita (8), Jenifa Mwita (4), Nyangi Wambura (23), Konstebo Nashon (23) ambaye ni polisi kituo cha Tunduma na Baraka Chacha (9).

Wengine ni Juli Mwita (6), Pc Enock ambaye ni mmiliki wa gari lililopata ajali, Makongoro Charles na Elizabeth Cosmas ambao wote wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Dodoma.

Aidha, kamanda Kimola amesema miili ya marehemu hao waliofariki katika ajali hiyo, imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa wa Dodoma.


VIDEO:Mwanamke Tako..Sura Tutapaka Make up

MAHAKAMA Kuu Yakubali Ombi la Godbless Lema Kuongezewa Muda wa Rufaa ya Dhamana Yake

$
0
0
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, imelikubali ombi la  Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema,  la kuongezewa muda wa kuwasilisha Notisi ya nia ya kukata rufaa ya dhamana yake.

Akitoa uamuzi wake kuanzia saa 12:26 hadi saa saba mchana, Jaji Dk. Modesta Opiyo wa Mahakama hiyo, alisema Mahakama hiyo imeruhusu maombi ya kuwasilisha Notisi ya kuomba kuongezewa muda wa kuwasilisha notisi ya nia ya kukata rufaa ya dhamana yake.

Jaji Opiyo amesema hoja za Upande wa serikali zilizowasilishwa na Wakili Hashim Ngole za kudai waleta maombi hayo walikuwa wazembe na walichelewa siku nne kuwasilisha Notisi baada ya rufaa yao kuondolewa na Jaji Fatuma Masengi Desemba 2 hazina mashiko.

Alisema kuondoa kesi mahakamani haimaanishi kuwanyima fursa ya kupigania nia ya kukata rufaaa, bali milango inakuwa wazi haijafungwa.

Aidha amesema siku nne zinazolalamikiwa kuwa walichelewa kutoa maombi hayo, mahakama inaona hoja hizo hazina mashiko sababu siku mbili kati ya hizo zilikuwa siku za mapumziko Jumamosi na Jumapili, hivyo walitumia siku mbili kuandaa nyaraka na kuleta maombi hayo.

Pia alisema katika maombi hayo wametoa pia sababu za nia ya kutaka kukata rufaa na sababu hizo ziko wazi.

“Katika hili hakuna uvunjifu wowote wa sheria uliofanywa na kutokana na hilo Mahakama hii inatumia busara zake kuruhusu maombi haya ya kutoa Notisi ya kuomba kuongezewa muda wa kukata rufaa juu ya dhamana yake Mbunge huyu,” alisema Jaji Opiyo.

Amesema Mahakama inatoa siku kumi pekee kuanzia uamuzi huo utolewa mleta maombi (Lema) kuwasilisha Notisi yake ya kuomba kuongezewa muda wa kukata rufaa hadi tarehe 30 shauri hili likakaposikilizwa tena.

Baada ya kutolewa kwa maamuzi hayo, tayari Wakili Sheck Mfinanga ameshakata Notisi Mahakama Kuu Kanda ya Arusha na kupokelewa.

Mfinganga amesema wanasubiri mahakama ili wapangiwe Jaji waendelee na kesi hiyo ya hatma ya dhamana ya Lema.

BARAKA Da Prince Aumbuliwa Vibaya Studio na Msanii Aliyemuibia Nyimbo

$
0
0
Baraka da prince aliumbuliwa vibaya kwenye studio za East Africa Radio baada ya kualikwa yeye na msanii waliyekuwa studio moja huko Mwanza, msanii huyo alisema baraka alimuibia nyimbo ya 'Baby sio fine' lakini baraka akabisha, alipozidi kubanwa akawa ana hasira na kutaka kuondoka studio
Ila msanii Mo music ambaye alikuwa na Baraka studio hiyo moja alithibitisha baraka kuwa hiyo nyimbo sio ya kwake Angali VIDEO:

SHILOLE Atoa Kauli Nzito kuhusu Diwani Baba Levo, Amfananisha na Mwanamke

$
0
0
Shilole amesema Baba Levo anamchukulia kama mwanamke mwenzake kwani anaweza akalala naye kitanda kimoja asimfanye kitu.

VIDEO:BARAKA DA PRINCE AUMBULIWA VIBAYA STUDIO NA MSANII ALIYEMUIBIA NYIMBO 

VIDEO:Hali Mbaya Usafiri Ubungo Msimu wa Sikukuu Wadorora

$
0
0

VIDEO:Hali Mbaya Usafiri Ubungo Msimu wa Sikukuu Wadorora 

VIDEO:Mwanamke Tako..Sura Tutapaka Make up

$
0
0

VIDEO:Mwanamke Tako..Sura Tutapaka Make up, Angalia Video Hapa chini:

CHEKA Adai Hakupigwa India, Aeleza Alichofanyiwa na Mwamuzi

$
0
0
Bondia Mtanzania Francis Cheka ambaye mwishoni mwa wiki alipoteza pambano lake nchini India alilopigana na raia wa nchi hiyo Vijender Singh, ameibuka na kusema kuwa mpinzani wake huyo hakumpiga, ila alibebwa na mwamuzi.


Akiongea katika kipindi cha 5Sports cha EATV kwa njia wa simu kutoka nchini India, Cheka amesema katika raundi hiyo ya tatu, alipata tatizo katika kifaa chake cha kulinda meno kwa kuwa alikuwa akisumbuliwa na kikohozi, na wakati anakifanyia marekebisho, ndipo mwmuzi akatangaza mshindi, bila kumuuliza Cheka mwenyewe kama alikuwa anaendelea au la.

“Tatizo nilikuwa nakohoa, nilijiandaa vizuri kumpiga yule Vijender,” alisema Cheka.

Pia katika mtandao wake wa Instagram aliandika:

Pale ambapo matokeo yamepangwa, tunaenda kukamilisha ratiba tu, Refa unaona mouth guard imetoka na unaendelea kuchezesha… Watanzania nadhani mmeona, tusiwage wanyonge kwao na kwetu pia… Nadhani nimeliwakilisha taifa vyema, kuitangaza Morogoro, Tanzania, Kiswahili na Kimakonde pia. VIDEO:

ALIYEBADILI Dini Afariki Baada ya Kubatizwa

$
0
0
Mkazi wa Mailisita wilayani Hai, Paulo (35) amekufa maji baada ya kuzama katika mto Kikafu, dakika chache baada ya kubadili dini na kubatizwa na maji ya mto huo kwa imani ya dini ya Kikristo.

Paulo ambaye jina lake la awali lilikuwa Issa Juma kabla hajabadili dini, alifariki Jumapili iliyopita katika mto huo, wakati shamrashamra za kubatizwa kwake zikiendelea pembeni ya mto.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi lililazimika kuwakamata wachungaji wawili wa kanisa la Efatha waliombatiza lakini waliachiliwa baada ya Polisi kujiridhisha kuwa Paulo alikufa maji baada ya kubatizwa.

Habari zilizothibitishwa na Polisi, zimeeleza baada ya kubatizwa saa 8:30 mchana na wakati waumini wakiimba kwa ajili ya kurudi kanisani, ndipo Paulo na mwenzake waliamua kurudi kuogelea.

RAIS Magufuli Akataa Shule Kuitwa Jina Lake

$
0
0
Rais John Magufuli amekataa shule ya msingi iliyojengwa hivi karibuni eneo la Bunju, Wilaya ya Kinondoni kuitwa kwa jina lake badala yake ameagiza iitwe kwa jina la Mkuu wa wilaya hiyo, Ally Hapi.

Taarifa ya badiliko la jina haikutolewa na Idara ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu kama ilivyozoeleka bali na mkuu wa wilaya hiyo wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa mbalimbali vya usafi kwa uongozi wa shule hiyo.

“Shule hii imejengwa kwa fedha zilizopatikana baada ya Serikali Kuu kubana matumizi. Tukaamua iitwe John Magufuli lakini yeye akatoa agizo shule ipewe jina la mkuu wa wilaya sina budi kukubaliana na hilo,” alisema Hapi.

Shule hiyo mpya iliyopo Bunju jijini imejengwa kwa lengo la kupunguza msongamano wa wanafunzi katika Shule ya Msingi Bunju A ambayo ilikuwa na wanafunzi 3,224.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo mpya, Ali Mwakapalila alisema ingawa inatarajiwa kuanza kupokea wanafunzi Januari 9 mwakani inakabiliwa na changamoto mbalimbali.

“Hakuna umeme wala maji, hii inaweza kuleta madhara kwa wanafunzi hasa linapokuja suala la matumizi ya vyoo,” alisema.

Baada ya hafla hiyo, Hapi alikwenda kwenye kiwanda cha saruji cha Twiga Cement ambako alipokea msaada wa mifuko 600 ya saruji kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa madarasa na majengo mengine.

Akipokea msaada huo, Hapi alisema msaada kutoka Twiga Cement unaunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano inayoipa sekta ya elimu kipaumbele ili kuhakikisha inatolewa katika mazingira bora.

“Msaada huu umekuja muda muafaka. Tumeshajenga shule ila tunataka kuongeza madarasa, maabara, ofisi ya elimu na kuzungushia uzio ili watoto wawe katika mazingira salama. Lengo ni kuifanya shule hii iwe ya kisasa na itakuwa mfano kwa shule zote za Wilaya ya Kinondoni,” alieleza.

Pia, Hapi alisema wilaya hiyo ipo kwenye mipango ya kujenga maktaba ya kisasa kwa kushirikiana na kampuni hiyo ya saruji.

Mkurugenzi Mtendaji wa Twiga Cement, Alfonso Velez alisema kuchangia katika shughuli za kijamii ni moja ya mambo ambayo wamekuwa wakiyapa kipaumbele zaidi.

“Kushiriki shughuli za maendeleo katika jamii ni jambo ambalo tunalipenda zaidi. Yalipo maendeleo Twiga Cement ipo pia,” alisema Velez. VIDEO:

BIASHARA ya Meno ya Tembo yamtupa Jela Miaka 25, Faini Sh 3.7 Bilioni

$
0
0
Mahakama  ya Hakimu Mkazi Tanga imemuhukumu kifungo cha miaka 25 ama  kulipa faini ya Sh 3.7 bilioni mfanyabiashara, Charles Kijangwa baada ya kupatikana na hatia ya kujihusisha na biashara ya meno ya tembo.

Hakimu Mkazi, Cresian Kisongo ametoa hukumu hiyo leo kwa Kijangwa ambaye aliruka dhamana tangu mwaka 2010, takribani miaka sita sasa.

Hatua hiyo ilifikiwa baada ya kikosi cha kuzuia ujangili Kanda ya Mashariki na Pwani kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Wilaya ya Lushoto kufanikisha jitihada za kumtafuta kwa  kumkamata na kumkabidhi mahakamani hapo.

Wakili wa Serikali Mwandamizi,  Saraji Iboru alidai mahakamani kuwa mshtakiwa Kijangwa alikuwa akitafutwa na Serikali kwa muda mrefu tangu mwaka 2010 ambapo aliruka dhamana katika kesi ya uhujumu uchumi namba 6 ya mwaka 2007 iliyokuwa ikimkabili yeye pamoja na wenzake Michael Msuya na Nyaisa Makori.

VIDEO:BARAKA DA PRINCE AUMBULIWA VIBAYA STUDIO NA MSANII ALIYEMUIBIA NYIMBO

NENO la Shukrani Kwa Wote Kutoka Kwa Mmiliki wa Jamii Forums Baada ya Kuachiwa Kwa Dhamana

$
0
0
Heshima kwenu wakuu!

Shukrani:

Kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia kuiona siku ya leo nami kuwa nanyi siku hii ninapoandika waraka huu mfupi ukilenga zaidi kutoa shukrani. Shukrani hizi nilitamani nimtumie mmoja mmoja lakini nimeshindwa kwani ni wengi wanaostahili kushukuriwa.

Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru wote walioshiriki kwa namna moja ama nyingine kupaza sauti zao (kwa njia yoyote ile) ili aidha nifikishwe mahakamani au niachiwe bila masharti yoyote (nilipokuwa Kituo cha Kati) na baadae kuendelea kupaza sauti kutaka mahakama initendee haki niwe huru baada ya kupelekwa gerezani Keko.

Nawashukuru mawakili wangu na wengine walioamua kujitolea kuingia katika utetezi wangu hata bila kuombwa. Kipekee, namshukuru na kumpa pole sana Ndg. Albert Msando ambaye tayari alishaonesha nia ya kuwa mtetezi wangu lakini yakamkuta yaliyomkuta, tumwombee kwa Mwenyezi Mungu apate uponyaji wa haraka.

Nipende kuwashukuru wana JamiiForums wote kwa mijadala iliyoendelea wakati wote ambao sikuwepo; vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi vilivyoshiriki katika hatua hii ya awali (kazi ndio imeanza); watumiaji wa mtandao wa Twitter(bila kutaja mmoja mmoja) kwa jitihada zao ambazo zimenishangaza kuhakikisha hashtag ya #FreeMaxenceMelo ina-trend na kuwa tayari kwao kutoa maoni yao kwa vyombo vya habari pale walipohitajika kufanya hivyo; nawashukuru Wahisani mbalimbali na wadau wa maendeleo ambao walituma wawakilishi wao Central na Gerezani kufuatilia napitia maisha gani na hata kuwasiliana na mamlaka zinazohusika kutaka nitendewe haki.

Aidha, nawashukuru sana wafanyakazi wa Jamii Media ambao naelewa kwa kiwango gani kilichotokea kilivyowaathiri kisaikolojia na hata kiutendaji. Nawashukuru Asasi za Kiraia zikiongozwa na THRDC, LHRC, Sikika, C-Sema, TMF, ChangeTanzania n.k kwa kuwa mstari wa mbele kufuatilia na kuelewa kinachoendelea na hata kujitoa kwa ajili ya udhamini wangu pale walipoombwa na wengine hata bila kuombwa. Jukwaa la Wahariri(TEF) – Asanteni sana!

Nichukue fursa hii kuwashukuru pia watanzania katika makundi mbalimbali ya WhatsApp, Facebook na Telegram kwa ushirikiano waliouonesha. Watumiaji wa Instagram(nashindwa kutaja mmoja mmoja), nawashukuruni sana kwani nimeona posts nyingi toka kwa watu hata ambao hawanifahamu lakini walioelewa ninachosimamia wakitoa support kubwa sana.

Ndugu, marafiki na majirani zangu – asanteni sana kwani mlikuwa nasi bega kwa bega wakati wote. Watanzania na wote ambao si watanzania mliojitahidi kufika Central na Gerezani kunijulia hali – Asanteni sana na Mungu awabariki sana!

Kuna wale ambao hata hawajaelewa kesi inahusu nini hasa na wameanza kuwashambulia waliokuwa wakinitetea, nao nawashukuru kwani naamini ni kwakuwa hawajajua nini kimo kwenye kesi. Ila niwahakikishie kuwa si rahisi kutetea mhaini, unapoona mtu anaamua kufanya hivi ni vyema kutafakari.

Askari wa Kituo cha Kati(Central) na wale wa Gereza la Keko – asanteni sana. Naelewa ni vigumu umma wa watanzania kuelewa namaanisha nini lakini ninyi kwa andishi hili mnaelewa vema ninachomaanisha. Wengi mliifanya kazi yenu kwa weledi mkubwa.

Viongozi wa kidini(wachungaji, ma-sheikh, maaskofu n.k) na wanasiasa wote(toka vyama vya upinzani na chama tawala) mlioshiriki katika hili – Asanteni sana. Hamkuingiza itikadi za kisiasa wala misimamo ya kidini bali mlitaka haki kutendeka. Nawashukuru!

Kuhusu kesi:

Ndugu zangu, ndio kwanza kesi inaanza kuunguruma tarehe 29 Disemba 2016. Si rahisi mimi kuongelea nini kilichomo kwenye kesi lakini naamini vyombo vingine vya habari kwakuwa tunayo sheria ya Haki ya Kupata Taarifa vinajua namna ya kuhakikisha vinaueleza umma nini kilichomo ndani yake (Mahakama Kuu na Mahakama ya Kisutu) ili watanzania waweze kuelewa mbivu na mbichi. Kuna ambao watajikuta kuwa walikuwa ndio walengwa hata hawakuguswa na kukamatwa kwangu, hapo ndipo watajua tunapigania nini.

Nipende kuwaomba tuendelee kuwa pamoja katika safari hii tunayoianza. Mimi ni sampuli tu, nasimama kwa ajili ya wale ambao naamini wana haki ya kutoa maoni na kufichua maovu (ili mradi hawajavunja sheria) na ninaamini wengi tunataka haki hii isipotee na iendelee kulindwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri wa Muungano.

Sina mengi kwa leo zaidi ya shukrani.

Wenu,

Maxence M. Melo

VIDEO:TAZAMA MAAJABU YA HUYU JAMAA

DOGO Janja Ajutia Kuikosa Shule...Adai Alifeli

$
0
0
Dogo Janja ambaye wiki kadhaa zilizopita amempoteza baba yake mzazi, alikiambia kipindi cha 'Ngaz Kwa Ngaz' kinachoruka kupitia EATV kuwa katika maisha yake anajutia kukosa shule na anasema katika kipindi ambacho alikuwa shule hakuwahi kupata experince ya mitihani ya kujipama jambo ambalo lilichangia yeye kufeli shule na kushindwa kuendelea na masomo.

"Unajua kila siku maneno yapo na yanasemwa lakini mimi katika maisha yangu mpaka leo kitu ambacho nakijutia sana ni kukosa shule, nakumbuka ilivyokuwa ni kipindi ambacho nilikuwa nimetoka Tip Top Connection kwa hiyo nilirudi Arusha ndiyo kipindi nilikuwa form two na ndiyo kipindi cha mitihani ya mock kilikuwa kimekaribia, kwa hiyo wenzangu walifanya mimi sikufanya hivyo sikupata experince ya mtihani iko vipi, inakujaje kujaje harafu nilikaa sana Arusha na niliporudi tu mjini wiki tatu tu mtihani wa taifa huu hapa kwa hiyo nilifeli, hata kufeli kwangu hakukuwa kwa maksi kubwa japo kuwa nilipitwa na vitu vingi" alisema Dogo Janja.

VIDEO:Maajabu ya Huyu Jamaa Anayetunza Maji Tumboni na Kuyatumia Kunawa na Kuoga

$
0
0

VIDEO:Maajabu ya Huyu Jamaa Anayetunza Maji Tumboni na Kuyatumia Kunawa na Kuoga

MAAFISA wa Nigeria Wamekamata Mchele wa Plastiki

$
0
0
Nigeria imekamata magunia 102 ya ''mchele wa plastiki'' yaliyokuwa yanaingizwa nchini humo na wafanyabiashara haramu ambao walitaka kuuza katika msimu huu wa sherehe, kulingana na afisa wa forodha katika mji mkuu wa nchi hiyo , Lagos.

Uchunguzi wa awali ulibaini kuwa mchele huo ulikuwa ni wa "plastiki'' ,baada ya kuuchemshwa, na kuoneka kuwa mkubwa zaidi ya mchele wa kawaida na ni Mungu tu anajua ni nini ambacho kingetokea kama ungeliwa na binadamu ", Haruna Mamudu aliongeza katika kauli yake juu ya tukio hilo.

Aliwawaonya wahujumu wa uchumi ambao wanangalia kipindi hiki cha sherehe kama njia za kupata mapato kwa udanganyifu kuwa watakabiliwa na mkono wa sheria.
Bwana Mamudu hakuelezea ni vipi mchele huo wa plastiki ulitengenezwa lakini ulikua na nembo iliyoandikwa "Best Tomato Rice".

Uchunguzi unaendelea kutambua ni kiwango gani cha mchele huo kimekuwa kikiuzwa na ni vipi unaweza kuondolewa sokoni ili kulinda afya za raia wa Nigeria waliokwisha utumia na kuwapeleka wahusika wa biashara hiyo haramu mbele ya sheria".

Nchini Uchina, kuliwahi kuwa na sakata ya chakula mwaka jana baada ya kubainika kuwa kuwepo kwa mchele uliotengenezwa kwa plastiki.

USHAURI Kwa Kina Kaka: Unapoanza Mahusiano Mapya Epuka Wanawake wa Aina hii

$
0
0
1.MSICHANA WAKO WA ZAMANI
Ni vizuri kutorudia mahusiano ya zamani na zaidi kama kwenye mahusiano yenu ya mwanzo mambo hayakuishia kwa uzuri. Sababu kuu ya msingi, kiukweli ni kwamba hakika mwanzoni mlikuwa hamuendani na ndio sababu ya iliyopelekea kuvunjika kwa mahusiano yenu, ndani ya hizo sababu kuna vitu vilivyopolekea kutokea kwa hayo, ukichunguza na kuziangalia kwa makini utagundua ni za asili na ambazo si rahisi kwa mmoja wenu kuzibadilisha sababu ni vitu au mambo ambayo yatakuwa ni ya damuni.

2.DADA WA RAFIKI YAKO KIPENZI
Epukana na kujiingiza kwenye mahusiano na dada wa rafiki yako. Si tu kwamba utaweza kujiingiza kwenye uhasama na chuki kama mambo hayatakwenda sawa, ila pia utaweza kujiweka kwenye mazingira ya kujikuta siku moja unapigwa hata ngumi za uso sababu tu ulimuumiza dada yake. Pia, utaweza kumkosa mtu ambaye ndie alikuwa ni kimbilio lako kwa mambo mbalimbali pale ambapo itatokea wewe na dada yake mambo kutokwenda sawa, sababu hapo patakuwa na mgongano wa kimaslahi kwa huyo rafiki yako.

3.WANAWAKE WENYE MAMBO MENGI
Kiukweli, kutoka na watu kama hawa kinaweza kuwa ni kitu cha kufurahisha, ila mwisho wa siku itakuingiza kwenye matatizo. Mara zote kumbuka ni vyema kuwa salama kuliko kujuta. Usijiingize kwenye majaribu ambayo utakuja kuyajutia kwa maisha yako yote.

4.WANAWAKE WANAOPENDA HELA KUPITILIZA (WACHUNAJI)
Kuwa mbali nao, labda kama unataka salio lako limalizike pasipo wewe kujifahamu. Naamini hili kila mmoja analifahamu na halihitaji darasa zaidi.

5.MSICHANA WA ZAMANI WA RAFIKI YAKO
Kama unathamini urafiki wako na mshikaji wako achana na habari ya kutoka na aliyekuwa demu wake. Mambo yanaweza kubadilika na kuwa kama au zaidi ya yaliyotokea kwa rafiki yako na ikaja kula kwako zaidi. Wakati mwengine inaweza tengeneza chuki kati yako na rafiki yako, huku akiamini kwamba ulikuwa unatoka au kumnyemelea msichana wake toka zamani.

Q Chief Atoa Siri ya Wasanii Kutoacha 'Ngada'

$
0
0
Msanii Q Chief amefunguka na kusema kuwa baadhi ya wasanii kushindwa kuachana na matumizi ya dawa za kulevya ni kutokana na wao wenyewe kutokubaliana na hali hiyo kutokana moyoni mwao.

Q Chief pia ametoa lawama kwa baadhi ya watu ambao wamekuwa wakijifanya kuwasaidia wasanii hao kuachana na madawa wakiwa na lengo la kutaka kunufaika nao kibiashara tu na si lengo la kweli kuwasaidia kuondokana na hali hiyo.

Q Chief anasema yeye alipitia kipindi kigumu zaidi kuachana na madawa hayo na alifanikiwa na mtu ambaye alimfanikisha kuachana na madawa hayo ni kijana kutoka mtaani ambaye aliweza kumbadilisha na kufanikiwa hivyo kijana huyo alifanya kazi kubwa ambayo serikali yake ilishindwa, mawaziri walishindwa na marafiki zake ambao walikuwa wakila bata na Q Chief walishindwa.

UJUE Ugonjwa wa Kisonono na Dalili zake Pindi Ukiupata

$
0
0

Kisonono ni ugonjwa wa zinaa unaoambukizwa, ugonjwa huu hutokana na wadudu aina ya Neisseria gonorrhoeae. Ugonjwa huu pia huambukizwa kwa tendo la ngono na hata kutoka kwa mama mjamzito anapojifungua huweza kumuambukiza pia mtoto endapo atakuwa alikuwa nao.

Ugonjwa wa kisonono kwa mara nyingi huwapata vijana na watu wazima. Waathirika wengi wa ugonjwa huu wa kisonono huambatana na magonjwa mengine ya zinaa, kwasababu kunabaadhi ya magonjwa mengine ya zinaa hujificha bila kuonyesha dalili, hivyo kukuta ukiugulia ndani kwa ndani.

Ugonjwa wa kisonono, unazuilika na kutibika pia, unaposikia dalili zozote za magonjwa ya zinaa, unashauriwa kumchukua mwenzi wakona kuwahi hospitali  kuchukua vipimo kwaajili ya matibabu.

DALILI ZA UGONJWA WA KISONONO.
Mara nyingi ugonjwa wa kisosnono huwa hauonyeshi dalili yoyote mwanzoni. Lakini ukionyesha dalili basi kwa mwanaume utasikia maumivu makali wakati wa kukojoa na kuambatana na usaha kutoka uumeni, kwa mwanamke pia dalili ni hizo hizo - maumivu wakati wa haja ndogo na kutoa usaha ukeni.

Usaha huo unaotoka uumeni au ukeni, huwa mzito na rangi ya kijani-njano, ambapo kwa mwanaume anaweza kuhisi maumivu katika korodani zake. Kwa Wanawake maumivu yanaweza  kuwa chini ya tumbo, uchungu wakati wa ngono, na damu Isiyokuwa ya kawaida kutoka kwenye uke.

Kama kisonono huenda kikakaa kwa muda mrefu mwilini  bila kutibiwa, inaweza kusababisha matatizo makubwa zaidi ya afya. Katika wanaume, inaweza kusababisha makovu ndani ya njia ya mkojo, ambayo inaweza kusababisha maumivu wakati wa kukojoa.

Katika wanawake, kisonono kinaweza kusababisha zaidi kutoka eneo la uke na kusababisha papo hapo ugonjwa mwingine wa "pelvic inflammatory" (PID) - maambukizi katika maeneo mbali mbali ya uzazi yanaweza kusababisha utasa.

Katika wanaume na wanawake, kisonono  kisichotibika kwa muda muafaka, huenda huweza kuenea kupitia damu katika sehemu za mwili ambazo ni mbali na viungo vya uzazi, na kusababisha uvimbe katika viungo, ngozi, mifupa, tendons, moyo, au hata eneo karibu na ini.

SIMBA, Yanga na Azam Marufuku Kusajili Wachezaji Toka Nje ya Nchi

$
0
0

Serikali imevipiga marufuku vilabu vya Yanga SC, Azam FC na Simba SC kutumia wachezaji wa kigeni hadi watakapokamilisha taratibu za uhamiaji nchini.

Vilabu hivi husajili wachezaji wengi wa kigeni kutokana na nguvu ya kifedha waliyonayo.

Mpaka sasa klabu ya Simba imeingia katika kashfa ya kuwatumia wachezaji wake wakigeni wasio kuwa na vibali.

MC Pilipili: Nimerudi Darasani Kujinoa Kimombo ili Kujiandaa Kwenda Kimataifa

$
0
0
Mchekeshaji maarufu nchini, Emmanuel Mathias aka MC Pilipili amesema amerudi darasani kujinoa zaidi katika lugha ya Kiingereza, kama sehemu ya mikakati yake ya kwenda kimataifa.

Kwenye interview niliyofanya naye, Pilipili amesema japo Kiingereza ni lugha anayoielewa, angependa kuifanya iwe laini zaidi mdomoni mwake. Amesema tayari amemaliza kozi ya kwanza pale British Council na tayari ameshaona mabadiliko.

“Nimepiga pale miezi yangu mitatu, naanza mingine January halafu nitapiga module yangu ya tatu,” amesema.

“Nafanya hivyo kwasababu naamini kwamba once the student is ready, teacher will appear. Kwamba nitakapokuwa tayari kwaajili ya kimataifa, kwahiyo hata gigs za kimataifa zitaanza kutokea kwasababu unaanza kufanania.”


 VIDEO:TAZAMA MAAJABU YA KIJANA HUYU

Viewing all 104809 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>