Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104808 articles
Browse latest View live

Waziri Mkuu Apiga Marufuku Madiwani Kupewa Fedha za Maendeleo Mikononi

$
0
0

Kassim Majaliwa amewataka Wakurugenzi wote wa Halmashauri na Manispaa nchini kuacha kutoa fedha taslimu na kuwapa madiwani ili zikafanye kazi za maendeleo.


Badala yake amewataka waandae mfumo maalum wa kutoa fedha hizo kama zinavyotolewa fedha za mfuko wa Jimbo ambazo ni maalum kwa wabunge lakini zinatumika kwa shughuli za maendeleo jimboni.


Ametoa kauli hiyo jana mchana (Jumatano, Januari 4, 2017) wakati akizungumza na viongozi na watendaji wa mkoa wa Ruvuma mara baada ya kupokea taarifa ya mkoa huo kwenye Ikulu ndogo Manispaa ya Songea.


“Nimepata taarifa kuwa fedha za maendeleo kwa madiwani zinakabidhiwa mkononi. Hapana. Msiwape fedha mkononi, bali zifuate mfumo wa utoaji fedha wa Serikali. Kama mlikuwa na matumizi ya aina hiyo, mwisho wake ni jana,” alisisitiza.


“Fedha za mfuko wa Jimbo ni za Mbunge lakini hapewi mkononi bali zinapelekwa kwenye Halmashauri na yeye anahusika kwenye kikao cha maamuzi. Anakubaliana na madiwani wenzake ni miradi ipi ipatiwe fedha, ambayo mara nyingi inakuwa imekwishaidhinishwa na vikao husika,” aliongeza.


Alisema makusanyo ya fedha yanayofanywa na Halmashauri hayana budi kuangaliwa pia na jinsi fedha hizo zinavyotumiwa. 


“Lazima tukishakusanya tuangalie tumepata kiasi gani, siyo kukaa na kuamua kutoa sh. laki tano tano kwa kila diwani. Suala la matumizi ni muhimu sana, ni lazima fedha hizo ziende kwenye miradi ya maendeleo,” alisisitiza.


Alisema kuna baadhi ya watu wanaamua kugawana fedha kwa kigezo cha maendeleo lakini wanaishia kutumia fedha hizo kwa kigezo cha kujengeana uwezo (capacity building).


“Hii si sahihi na jana nimepiga marufuku posho za aina hii pamoja na fedha za vitafunwa kwa sababu zinaishia kwa wakubwa wachache na waliozikusanya hawapati chochote,” aliongeza.


Akizungumzia kuhusu ukusanyaji wa mapato kwenye Halmashauri, Waziri Mkuu aliwataka waangalie baadhi ya makampuni ambayo yanajitokeza kutoa vifaa vya kukusanya ushuru lakini wanatumia software ambazo zinawanufaisha na wao pia.


“Tumieni watu wenu wa TEHAMA kukagua mifumo hii kwani kuna baadhi ya watu wanaoleta zile mashine siyo waaminifu. Watu wa TEHAMA wazikague na kujiridhisha kuwa hakuna mianya ya wizi. Tumegundua wako wanaokusanya fedha, lakini asilimia 80 inangia kwenye akaunti za Halmashauri na asilimia 20 inapelekwa sehemu wanayoijua wao. Ukiangalia unaona mapato yanaongezeka lakini kumbe pia unaibiwa. Jaribuni kuchunguza na mjiridhishe na hizo software zao,” alisisitiza.


IMETOLEWA NA

OFISI YA WAZIRI MKUU

Q-Chief Aeleza Namna Alivyoweza Kuachana na Madawa ya Kulevya 

$
0
0

Kuingia kwenye madawa ya kulevya ni rahisi sana, la kutoka ni ngumu,” ni maneno ya Q-Chief katika mahojiano na kipindi cha Amka na Choice FM.


Kwa mujibu wake mwenyewe, Chief ni miongoni mwa watu walioweza kujinasua kutoka kwenye matumizi ya madawa hayo yanayozidi kuwaangamiza vijana wa Tanzania.

Yeye aliwezaje kujinasua?

“Mimi I took my mind on a trip before making decision,” anasema msanii huyo.

“Ni kwamba nilikuwa nikiwatazama watoto wangu machoni naona maumivu, I saw tears wengine hawakuweza kuhandle ile situation nikajikuta nalia nao, tunalia pamoja. Lakini ikanifikia kipindi sasa nawakimbia kwa maana wakiniona wanazidi kulia, nikajiuliza nitaendelea kuwaumiza hawa malaika mpaka lini? Na niliwaleta duniani na wao wawe na faraja na kesho my father was one two, three.. ” anasema.

“Lucky me nilikaa nao chini na kuanza kuonesha mabadiliko mwenyewe. Changes starts with you. Kwasababu wewe unapobadilika, mtu wa jirani ataona mabadiliko yako. Lakini ukichukua muda mrefu kumuonesha jirani mabadiliko yako of course hatoamini sababu ukizungumzia unga naamini it’s very hard mtu kutoka,” amesisitiza Chief.

“Ndio maana wasanii wenzangu wanatoka, wanarudi.”

Anadai kuwa amepokea simu zaidi ya 100 wakiwemo BBC akiulizwa aliwezaje kujitoa kwenye matumizi hayo, na akadai kuwa aliamua mwenyewe kwa kuelewa umuhimu wake na wala hakwenda sober wala kufanyiwa counseling yoyote.

Q-Chief amesisitiza kuwa si rahisi kabisa kwa wasanii walioathirika na madawa ya kulevya kuyaacha kwa kushinikizwa na watu, bali ni wao wenyewe.

Msikilize hapo juu alivyozungumza kwa hisia na kutoa ushauri muhimu.

Kafulila Kupokea Kadi ya Chadema Jimboni Kwake Mwezi Huu

$
0
0

Aliyekuwa  Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, amesema atapokelea kadi ya Chadema jimboni mwake baadaye mwezi huu.


Kafulila alitangaza kuhama NCCR-Mageuzi na kurudi Chadema kwa alichoeleza kuwa ndicho chama kilichojipambanua kuelekea safari ya mabadiliko ifikapo mwaka 2020.


Kada huyo tayari amewasilisha barua kwa Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Mosena Nyambabe kumjulisha kuwa anajivua uanachama na  anarudi Chadema.


Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana, Kafulila alisema ameamua kuwa atapokelea kadi hiyo jimboni kutokana na mapenzi aliyonayo kwa wananchi wake.


"Nimepanga kuchukua kadi mwezi huu jimboni, kwa kuwa ilikuwa nichukue kadi mwanzoni lakini ilishindikana kutokana na siku kuu, hivyo siku yoyote kuanzia sasa nitachukua," alisema.


Wakati anajiuzulu NCCR-Mageuzi na kurudi Chadema, alisema hakufanya uamuzi kwa kukurupuka bali alitafakari na kushauriwa na wananchi wa jimbo lake, na kuridhika kurudi huko.


"Nilitafakari na kushauriwa sana jimboni na kuridhika kwamba Chadema ndiko sehemu inayojipambanua kwa mikakati ya kuleta mabadiliko yanayotarajiwa na Watanzania na ni vema kukusanya nguvu ya kila mwenye kiu ya mabadiliko ndani ya chama kimoja, ili kufupisha safari ya mabadiliko," alisema.


Alipoulizwa kwa nini amerudi Chadema wakati aliyekuwa Katibu  Mkuu wa Chama hicho, Dk Wilbrod Slaa alipata kumwita sisimizi kwa  alichoeleza kuwa hakuwa na imani naye, alijibu kuwa siasa ni malengo si uhusiano binafsi.


Kafulila aliongeza kuwa wanasiasa wanaunganishwa na malengo zaidi ya urafiki na kwamba malengo yake sasa ni kuendelea kupigania mabadiliko ya kimfumo yanayoenea zaidi kwenye chama hicho (Chadema) kuliko kingine.


Novemba 10, 2009 Kafulila alijivua uanachama wa Chadema na kuhamia NCCR-Mageuzi kutokana na kuondolewa kwenye nafasi ya uofisa habari wa chama hicho.


Pia akiwa NCCR-Mageuzi, alitimuliwa uanachama kwa kudaiwa kukiuka taratibu za chama hicho na tuhuma za kutaka 'kumpindua' Mwenyekiti, James Mbatia.


Hata hivyo, suala hilo lilipata suluhu baada ya Mbatia kuteuliwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete kuwa Mbunge. Wakiwa bungeni, Mbatia na Kafulila walikutana, kuzungumza na hatimaye kumaliza mzozo wao.

Jerry Muro aiandikia barua TFF ya kuomba kupunguziwa adhabu

$
0
0
Hatimaye msemaji wa Yanga Jerry Muro ameinua mikono juu na kuiangukia TFF kwa kuandika barua ya kuomba kupunguziwa adhabu ya kufungiwa kutojihusisha na masuala ya soka kwa muda wa mwaka mmoja.


Adhabu ya Muro ilianza Julai 7, 2016 hiyo inamaanisha tayari ameshatumikia adhabu yake kwa kipindi kisichopungua miezi sita.


TFF kupitia kamati ya maadili ilimfungia Jerry Muro kutokana na kutumia maneno ambayo si ya kiungwana michezoni hususan soka.

Source: Shaffih Dauda

Wasanii Wanaotumia Unga Wamtesa Harmonize, Afunguka Kinachomuumiza

$
0
0
Baada ya kuibuka kwa jinamizi kwa upande wa wasanii wengi kuingia kwenye matumizi ya madawa ya kulevya, Harmonize amefunguka yake ya moyoni.

Hitmaker huyo wa Matatizo, ameamua kutoa yake ya moyoni kupitia mtandao wa Instagram kutokana na kile kinachoendelea na kuwakumba baadhi ya wasanii ambao walikuwa wakikubalika kwa mashabiki.

Kupitia mtandao huo, Harmo ameandika:

Daaah Mungu tunusuru na hili janga la #Unga mana sisi tuna ushawishi mkubwa na tunatizamwa na watu wengi walio timamu na wasio timamu pia tunaigwa….!!! kwanini isiwe kwa watu wengine…..?? mbona kila siku sisitu…..?? #Muzi & #Muvie 🙏

Serikali ya Kenya Yasalimu Amri..Yaongeza Mshahara wa Madaktari Wake

$
0
0
Serikali ya Kenya imetangaza kuongeza 40% kwenye mishahara ya madaktari waliogoma nchini humo ili kumaliza mgomo uliodumu zaidi ya mwezi

Gigy Money Afunguka Suala la Kuwa Ana Ukimwi, Orodha ya Wanaodaiwa Kutoka Naye Yatajwa

$
0
0
Video queen matata ambaye pia ni mtangazaji wa kituo cha redio moja jijini hapa, Gift Stanford ‘Gigy Money’, ametema cheche akisema kuwa, watu wote wanaomsema kwamba kutokana na kuvaa nusu utupu na kujiachia na midume mbalimbali huenda ana maambukizi ya virusi vya Ukimwi, waache kwani kama ni kweli basi wengi wangekufa kwa sababu ameshatembea na mastaa kibao Bongo.


Gigy Money
Akizungumza na gazeti hili juzi, Gigy alisema kwamba amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na mastaa mbalimbali wakubwa Bongo akiwemo Mbongo Fleva, Ali Kiba na kudai kuwa, kama kuambukizwa virusi angeanza yeye na wengine wangefuata.

“Unajua watu wanashangaza sana. Kama mtu ana virusi vya Ukimwi hawezi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtu anayempenda, ningependa watu waache unyanyapaa. Ninachojua mimi sina Ukimwi kwa kuwa nilipima kwa shinikizo la mpenzi wangu wa sasa (Moulad Alpha ‘Moj’) na watu niliotembea nao wanaendelea vizuri tu, wengine wachumba zao wananyonyesha,” alisema Gigy.

Video queen huyo alikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa, kuvaa nusu utupu ni kitu anachopenda kufanya toka ndani ya moyo wake hivyo hakuna mtu wa kumwambia kitu au kumkataza hata siku moja na wala siyo mgonjwa wa akili bali anafanya kitu kujifurahisha nafsi yake si ya mtu mwingine.

“Mimi nasikilizaga moyo wangu unasema nini, si mtu anasema nini juu yangu hivyo kama kuvaa nusu uchi wana hofu na mimi waondoe hilo kwa maana kama ni Ukimwi wengi wangeondoka siku nyingi kwenye ramani ya dunia hii maana hakuna niliyemuacha kwa mastaa unaowajua,” alisema Gigy kwa kujiamini.

Gigy ameshatoka kwenye magazeti mbalimbali akidaiwa kutembea na mastaa kama Hemed Suleiman ‘PHD’, Richard Martin Lusinde ‘Rich Mavoko’, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Seif Shaban ‘Matonya’ na Omar Nyembo ‘Ommy Dimpoz’.
Mwingine aliyewahi kutajwa ni Mtangazaji Gardner G. Habash ‘Captain’ na Mshindi wa Big Brother Africa 2014, Idris Sultan.

Chanzo:GPL

Mifupa ya Mtu Yakutwa Katika Sandarusi Vingunguti

$
0
0
Siku ya tarehe 02/01/2017 mifupa ya bunadamu imekutwa na kwenye mfuko wa sandarus Vingunguti Dar es salaam. Kijana ambaye alikuwa anaokota chupa za maji katika jalala ndiye aliyeona mfuko huo na kuufungua kwa kudhani atakutana na machupa lakini ikawa tafauti baada ya kukuta mifupa ya binadamu mti mzima.

Pamoja na kwamba mwili ulibaki mifupa lakini, mwili huo umekutwa ukiwa na nguo zinazo ashiria marehemu ni mwanaume. Alivaa suruali ya kitambaa nyeusi, shati leupe lina mistari ya pundamilia meusi, na shati kifuani lilikuwa limejaa damu. Kwa jinsi nguo zilivyo inaonekana huyo mtu hakufa muda mrefu sana.

Taarifa ilitolewa polisi na wakauchukua mwili na kuendelea na taratibu zao

Hashimu Rungwe Amtolea Uvivu JPM, Ahoji Nchi imepinda Kuelekea Wapi?

$
0
0
Ahoji kauli ya Rais kuwa nchi imepinda kuelekea wapi, Kuelekea Ubungo au Temeke? Anahoji kila mara Rais anasema ufisadi wakati kapewa jeshi, polisi na kodi za kumsaidia, kwanini hakamati hao mafisadi, ahoji CCM kuhoji ufisadi wa Lowasa na kushindwa kumkamata, hivyo wanamsingizia.
Amesema ndani ya miaka 10 nchi imepiga hatua kubwa kwenye maendeleo kuna barabara nyingi zimejengwa kwa kiwango cha lami, vyuo vikuu vilikuwa vitatu leo kuna vyuo vikuu vingi, kuna viwanja vya ndege vimejengwa na vingine kupanuliwa usafiri wa boti za kisasa njia za majini lakini Rais Magufuli anadai nchi imepinda, anahoji maendeleo hayo ndio kupinda kwa nchi?
Anendelea kudai kuwa Magufuli hajafanya chochote cha kujivunia kuwa kainyoosha nchi na kuleta maendeleo tofauti na kununua ndege na kununua ndege unachukua fedha na kununua tu, sio kazi kubwa
Tazama mwenyewe hapa

Dr Slaa Afunguka Anapokubaliana na Kutofautiana na Rais Magufuli

$
0
0
AWALI ya yote, namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutulinda, kutupa uhai na afya njema hadi leo. Yote yamewezekana kwa kuwa amependa sisi wajoli wake tuwe hai na wenye afya.

Wako wenzetu wakati huu wako hospitali au vitandani kutokana na maradhi mbalimbali. Tuwaombee wote walio wagonjwa.

Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kujua kwanini wengine kawapa afya njema na wengine kawapa maradhi ya aina mbalimbali. Inawezekana kati ya mnaosoma makala hii sasa, wengine hamtaweza kuuona mwaka 2018.

Ndugu zangu Watanzania, ili tuweze kuwa na matumaini ya mwaka mpya wa 2017 tuliouanza, ni vema takatafakari mwaka tunaouaga wa 2016.

Huu ni mwaka wa kwanza tangu Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015, ambapo tulimpata Rais mpya, John Magufuli na kuunda serikali yake. Ni dhahiri kila tunapoingia kwenye uchaguzi, kila mmoja wetu huwa na matumaini ya matokeo ya uchaguzi kuleta unafuu katika maisha yetu ya kila siku.

Ndio maana wakati wa kampeni, tunasikiliza kwa umakini sera mbalimbali zinazoletwa kwetu. Hatimaye tunapiga kura kuichagua ile sera ambayo kila mmoja kwenye nafsi yake anaamini itamletea unafuu, itamtoa pale alipo kuelekea kwenye maisha bora.

Kwa wengine ni matumaini ya kutoka kwenye maumivu ya maisha kwenda kwenye unafuu. Kwa uzoefu wangu wa ubunge wa miaka 15 na miaka 20 kwenye siasa( active politics), ninaelewa kabisa kuwa wako ambao siku ya pili baada ya uchaguzi wanataka kuona kero zao zimeondoka.

Kama tatizo lilikuwa maji safi na salama, hawaelewi, baada ya kumpata kiongozi kwanini siku ya pili, ya tatu, mwezi na hata mwaka baadaye hakuna maji!

Hii ni hali ya kawaida kwa binadamu. Mimi nilichaguliwa na watu wa Karatu kutokana na kero kubwa ya maji wilayani Karatu. Maji yalidhalilisha utu wa binadamu hasa akinamama.

Maji yalifanya watoto wadogo kubakwa kwenye vituo vichache vya maji vilivyokuwepo. Maji yalifanya mahudhurio ya watoto shule za msingi yadorore kwa kuwa watoto walikesha usiku kucha kusubiri maji kwenye vituo vichache vya maji.

Nakumbuka kila nikipita mitaani, nilianza kuitwa tapeli kwa kuwa miezi sita baadaye, na kisha mwaka mmoja baadaye, maji yalikuwa hayajaonekana kwao. Mwananchi wa kawaida yeye hajui jitihada unazofanya kuleta maji.

Yeye kazi yake ilikuwa kupiga kura, mengine hayamhusu. Hajui kuwa maadui zako wanakuhujumu na kukuvuta chini ili usifanikiwe, kwani kufanikiwa kwako ni kuonyesha udhaifu wao.

Mwananchi haelewi kuwa mikakati ya utekelezaji wa mradi wowote haina budi kuandaliwa kwa umakini, fedha zitafutwe, kazi ya usanifu lazima ifanyike.

Kwa Karatu, maji yalianza kutoka kwenye mabomba mwaka 2000, wakati uchaguzi ulikuwa 1995. Tone la kwanza la maji lilipotoka, wananchi hata waliokata tamaa, waliodhani wametapeliwa walilipuka kwa furaha ya ajabu.

Walisahau matusi yote waliyokuwa wamenishushia. Sasa wakaanza kubaini kwamba kumbe hawakuwa wakidanganywa. Waliokuwa wavumilivu waliona na kushuhudia hatua zote za utekelezaji wa mradi.

Waliokuwa wepesi kukata tamaa nusura watukatishe tamaa sisi watekelezaji kwa kejeli, kebehi, matusi tuliyokuwa tukimwagiwa mitaani.

Uvumilivu ulizaa matunda. Wananchi takribani 30,000 walipata maji ya uhakika ndani ya nyumba zao, wengine katikati ya kitongoji chao, vitongoji vingine vilikuwa na DP ( Distribution Points) zaidi ya mbili au tatu.

Hivyo mama anaenda na sufuria na akirudi anabandika jikoni. Hili ni tunda la uvumilivu. Ndugu zangu nimeeleza kidogo kwa kirefu hadithi hii ambayo ilinipata mimi na wananchi wangu wa Karatu.

Ninafahamu pia kwamba mara baada ya ushindi wa Magufuli, makundi tofauti ya wananchi yatakuwa na matumaini tofauti kuhusu matarajio ya nini watakachokipata.

Wamachinga walijua mikopo midogo midogo itapatikana kwa urahisi, na hawatakimbizwa tena mitaani kama mbwa. Bodaboda waliozuiliwa kuingia katikati ya miji walijua sasa wamefunguliwa milango na hivyo biashara yao itakuwa rahisi.

Hali hii iko hivyo kwa takribani makundi yote ya kijamii. Kwa miaka mingi, wananchi wetu wameaminishwa kuwa nchi yetu ni tajiri na hivyo wana matarajio makubwa kwa viongozi wao.

Tuna rasilimali za kila aina kuanzia rasilimali chini ya bahari na maziwa yetu, magogo kwenye misitu yetu, rasilimali wanyamapori, ikiwa ni pamoja na “twiga wetu” aliyekunjwa shingo na kuingizwa kwenye ndege kutoroshwa.

Kuna kero nyingine pia kama vile maelfu ya tembo na faru waliokuwa wakiuawa bila huruma na majangili kwa manufaa yao binafsi, fedha zetu kwenye benki kuibiwa hovyo nakadhalika.

Wananchi haohao wamesahau kuwa mara baada ya uchaguzi, kazi kubwa ni mapambano dhidi ya “ wahujumu hao”. Kwa bahati mbaya “mpira usiocheza hujui si rahisi kujua ugumu wake. Kumbe hata ukiachiwa peke yako ufunge bao kwenye goli lililo wazi, unaweza kuupaisha juu kwa mshangao wa wengi!”

Hivi ndivyo ilivyo kwa serikali. Natambua kabisa watumishi wa umma walitegemea mishahara itapanda na kukidhi mahitaji yao, wanafunzi wa vyuo walijua mikopo sasa itakuwa rahisi na itatoka kwa wakati.

Wazazi walijua “ elimu itakuwa bure hadi kidato cha nne” na hawatasumbuliwa tena, hata kero ya madawati itatatuliwa bila mwananchi kuguswa kabisa! Natambua kuwa matamanio hayo si tu hayakutekelezwa bali maumivu yalikuwa makubwa zaidi kwa mwaka wote wa 2016.

Mitaji imepotea, mabenki hayakukopesha kwa hofu mbalimbali, mzunguko wa fedha ulikauka, hata wenye mitaji yao midogo ikaliwa. Hoteli nyingi kufungwa kwa kushindwa kulipa mikopo kutokana na kutokupata wateja.

Watumishi wa umma hawakupewa mishahara iliyotangazwa kupanda. Hii ni hali ngumu na ninatoa pole sana kwa wale wote, kwa makundi yao, walioumia kwa namna moja au nyingine.

Kazi ya kwanza ya kiongozi yeyote makini anaposhika dola ni kuangalia mianya mbalimbali ya wizi na uozo wowote katika usimamizi wa rasilimali za umma. Nadhani wote tunakiri serikali hii ilipoingia tu madarakani, jambo la kwanza lilikuwa kubaini wafanyakazi hewa.

Leo tunazungumzia wafanyakazi hewa takribani 20,000. Fikiria ni mabilioni mangapi kwa mwezi yalienda kwa wafanyakazi hewa? Ni dhahiri fedha hizi zingelitengeneza mzunguko wa fedha kama zingelikuwa kwenye mkondo sahihi. Hakuna shaka kwenye hilo.

Lakini ni wafanyikazi hewa, hivyo taifa halikuzalisha kutokana na wafanyakazi hao hewa. Ghafla uhakiki unaonyesha kuwa kuna siyo tu waalimu hewa, lakini wanafunzi hewa zaidi ya 60,000. Mungu atusamehe!

Sijui tumelogwa! Taifa la ajabu. Watu “wanatumbua” bila aibu. Hawa walikuwa wakitumbua fedha zetu kwa manufaa ya “ matumbo yao” na familia zao.

Hatujakaa sawa tukaambiwa kuwa hata fedha za TASAF zilizolenga kusaidia kaya maskini sana nazo zimeliwa. Kaya takribani 55,000 zilizokuwa zinufaike zimekosa huku baadhi ya viongozi wa serikali wa ngazi mbalimbali, wakiwemo maofisa wa TASAF wenyewe wakidaiwa kuhusika na wizi huo.

Hatujatulia mara maelfu ya wanafunzi ambao hawakuwa na sifa za kujiunga na elimu ya Chuo Kikuu walipewa nafasi! Ni dhahiri kuwa wazazi wa watoto waliofukuzwa wameumizwa na hatua hii.

Lakini ipi nafuu kuendelea kuwa nao na kuathiri ubora wa elimu hasa katika dunia ya leo ya ushindani. Wenzetu kila siku wanapambana na ugunduzi wa mipango ya kwenda kwenye sayari mbalimbali kwa lengo la kutafuta sayari yenye kufaa kwa maisha ya binadamu.

Sisi tutaendelea kuwa na mijadala ya kutafuta fefha kwa matundu ya choo. Hadi lini! Najua lilikuwa uamuzi Mgumu sana Mhe. Rais na Waziri wako wa Elimu. Lakini hapakuwa na njia.

Nashukuru kama wazazi mlifanya jitihada za kuwaelekezea vijana hao penginepo ili rasilimali watu za Taifa zisipotee na wao pia wanufaike na rasilimali za Taifa lao. Ni haki yao.

Haikuishia tu kwenye fedha. Bandarini Kontainer zaidi ya 11,000 zinaingizwa bila kulipiwa kodi na ushuru mbalimbali. Hii ikasababisha milango na mirija ya ukwepaji kodi kufungwa.

Na dhihiri waliokuwa wakinufaika na kupata “ super profit” kwa kukwepa kodi wataikimbia Bandari yetu. Kitendo cha kuikimbia Bandari, kwa muda athari yake ni kuwa bidhaa zitapungua, na makusanyo ya kodi za Serikali pia yatapotea.

Mzunguko wa fedha katika ujumla wako nao utapungua. Na hivyo hali ya maisha kuwa ngumu kwa kila kundi.

Ndugu zangu, kwa kiongozi yeyote jasiri, mwadilifu, mpenda Taifa lake anakutana na mtihani mkubwa sana. Aidha ni uchaguzi mgumu. Au aache uozo huo wote kuanzia “ hewa” hadi “ ukwepaji kodi uendelee au audhibiti kwa njia zote zinazowezekana.

Akiuruhusu maana yake nimkuwa mzunguko bandia wa fedha utaendelea kuwepo na kundi dogo linalofikiwa na mzunguko huo litaendelea kunufaika lakini umma mpana utaendelea kuumia, kama tulivyokuwa tukiumia kabla ya uchaguzi.

Kwa bahati mbaya walio wengi ambao walikuwa hawanufaiki na uozo uliokuwa ukiendelea hawakuwa na pa kusemea. Leo angalau wamempata Rais anayewasemea wao. Rais amekuwa akitumia neno “wapiga dili”.

Ni kweli waliokuwa wakinufaika ni hao wapiga dili waliotengeneza “ wafanyikazi hewa, hewa, hewa, kila sekta”.

Lakini kwa bahati mbaya wanaoathirika ni pamoja na mama lishe, na wafanyibiashara ndogo ndogo ambao kimsingi hawahusiki kwa lolote lile na kupiga dili.

Wao wanafanya biashara wakati hao wachache wakipiga dili. Lakini hapa ndipo palipo na msemo, “mtego wa panya kuwakamata wahusika na wasiohusika”. Hii ndio inayoitwa “Dilemma”.

Unachagua kipi? Uache uozo na ufisadi/ huu mkubwa uliofilisi nchi nzima uendelee kwa ajili ya kuwasaidia wenye biashara ndogondogo au funga njia, kwa muda tutaumia, rudisha nchi kwenye reli na baada ya muda fungua milango kwa biashara halali.

Kweli kwa uamuzi huu liko kundi litaumia sana. Lakini taifa likirudi kwenye reli, kundi hilo na wote tutanufaika. Taifa zima litanufaika.

Nina hakika tukiisha kurudi kwenye mstari ajira zitatoka kwa utaratibu unaotakiwa, fedha za miradi zitatoka na mzunguko wa fedha utarudi kama kawaida. Maamuzi magumu yanahitaji kushirikiana lakini pia uvumilivu mkubwa. Hakuna jambo jema linapatikana kirahisi.

Najua kuwa kuna wengi wanalalamika. Wako wasomi kati yao. Lakini kama wasomi hao wana dhamira njema, miaka yote nchi ilipokuwa inatopea kwenye dimbwi la ufisadi, uwizi huu; mbona walikaa kimya?

Mbona hatujusikia sauti yao. Wasomi hao wengine wao si ndio walikuwa pia wakikusanya mamilioni wakati mwingine kwa “Dola Za Marekani” kwa kilichokuwa kikiitwa kazi za kiushauri yaani Consultancies?

Wengine walikuwa wakiandika rasimu za sheria mbovu lakini wakiishia kujikusanyia mamilioni ya fedha. Kwa bahati nzuri sizungumzii nadharia. Ninayafahamu yote ninayosema kwa undani.

Mambo ya “ Watumishi hewa”, wanafunzi hewa Kamati ya Bunge ya Hesabu ya Serikali za Mitaa tulianza kuyazungumzia mwaka 2007. Mbona tangu wakati huo wakati huo hatukumwona msomi yeyote akifanyia utafiti ( hata baada ya kuwarahisishia kwa taarifa za LAAC).

Tuache kudanganyana. Hawa wasomi wetu hawakuona huo ufisadi , wizi na uozo huu wakati ulipoanza ? Leo ndiyo wanaona uchungu au kwa sababu kwa namna moja au nyingine na wao pia wameguswa? Japo si wasomi wote.

Watu wanalalamikia safari za nje kuzuiwa. Tena wanaihusisha na mgawanyo wa mamlaka na kuwa Rais anaingilia mamlaka zingine. Hivi mwaka 2014 nilipotaka Bunge kufanyiwa “Special Audit” kwa ziara za kibunge zilizokuwa zikitumbua fedha bila manufaa kwa taifa walikuwa wapi?

Ni sekta ipi katika nchi yetu ambayo haikuguswa na Ufisadi? Hatimaye mwajibikaji mkuu wa fedha za Umma ni Rais kwa mujibu wa Katiba. Iweje basi akichukua hatua ionekane kuwa ameingilia mamlaka zao?

Ni kweli siyo kila kitu cha Serikali ya Awamu ya Tano mimi naunga mkono. Mimi siungi mkono kujenga reli kwa fedha nyingi kwa Standard Gauge. Labda tuambiwe kuwa wakati inajengwa kwa Standard Gauge wanazungumzia pia Electrification.

Nilikwishasema “ we do not have to re- invent the wheel”. Leo unatoka Hamburg kwenda Munich Ujerumani takribani umbali wa kilomita 1500 kwa muda wa saa 3 tu. Sisi tunakwenda Dar- Mwanza na treni inachukua siku tatu hadi nne.

Hii ni karne ya sayansi, hatuhitaji kuwekeza fedha kama hatutaenda kisasa. Inatakiwa mtu alalale nyumbani kwake Mwanza anaenda kufanya kazi Dar na kinyume chake.

Tunataka bidhaa za viwanda na za kilimo zizalishwe kwa wingi Mwanza, Mbeya na Kigoma na zifike katika Bandari ya Dar es Salaam kwa muda usiozidi saa tatu na si baada ya wiki.

Nchi hii haiwezi kuendelea kwa namna ya kufikiri ya mwaka 1947. Wasomi wetu wana jukumu la kujitafakari na kubadilisha namna yao ya kufikiri na kutoa mchango kwa taifa kama wanahitaji tuwatambue kwa usomi wao.

Wanasiasa wetu nao ajenda isiwe kuingia Ikulu pekee. Ajenda iwe namna ya kuliondoa taifa kwenye “ mduara” ( Vicious Circle) tulioko na mkakati walio nao wa kulipeleka taifa tunakotaka.

Kwa ujumla nchi ilikosa mtu wa kusimamia rasilimali. Nchi ilikosa mtu wa kutoa maagizo na maamuzi. Nchi ilikosa usimamizi na mtu wa kukemea. Rais JPM amejidhihirisha kuwa anayo nia, anayo dhamira na anao ujasiri na uwezo wa kufanya.

Chanzo: Gazeti la Raia Mwema, JAN 05, 2017.

Mwandishi wa makala hii aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Chadema na Mbunge wa Jimbo la Karatu kupitia chama hicho.

Install APP ya Blog Hii ya UDAKU SPECIAL Kwenye Simu yako Kutoka Google Play Kusoma Habari Kirahisi

$
0
0
Download  Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu yako Kutoka Play Store Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi

Bonyeza Hapa CLICK HERE 


Au Kama Unayotayari Bonyeza Hapa Ku Update Uweze Kupata Ikiwa na Muonekano Mpya

Ilikuwa ni Lazima Tutoe Album - Navy Kenzo

$
0
0
Wasanii Aika na Nahreel ambao wanaunda kundi na Navy Kenzo wamefunguka na kusema kuwa album yao ya 'AIM' itawapa thamani zaidi kama wasanii hata kama haitaweza kurudisha au kuwapa pesa za kutosha lakini itawaongezea thamani kama wasanii.

Navy Kenzo walisema hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio na kusema huo ulikuwa ni moja ya mpango na kwamba wao waliona hawawezi kuendelea na 'career' yao kama wasanii ikiwa watakuwa hawana album.

"Sisi tunaona ni muhimu msanii kuwa na album hata kama hutapata pesa lakini ni muhimu kwanza inakupa thamani kama msanii, tuliona Navy Kenzo hatuwezi kuendelea na career yetu bila kuwa na album, hivyo tunajivunia. Huenda inaweza isiingize kitu sana ila itatuongeza thamani zaidi. Maana hata tunapokwenda kwa wenzetu huko unaona kabisaa msanii bila album anakuwa hana thamani kivile" alisema Nahreel

Mbali hilo Aika alisisitiza kuwa waliona umuhimu wa album yao ndiyo maana waliamua kuipa heshima kwa kufanya kazi kubwa nzuri ambazo nyiingine wameshiriakiana na wasanii wakubwa.
"Sisi Alikiba tunamuona ni mtu mwenye kipaji kikubwa uwepo wake kwenye album yetu unaleta baraka kubwa, na si Alikiba tu wapo wengine wasanii wakubwa wengine kama  Patoranking, R 2 Bees, Mr Eazi hivyo nadhani sisi tunaheshimu kazi ya sanaa lakini tuliiheshimu sana album yetu ndiyo maana tuliipa nguvu kama hivi" alisisitiza Aika

Crazy GK Aipa Serikali Ramani ya Kuwadhibiti Wauza Unga

$
0
0
Ikiwa sakata la madawa ya kulevya linazidi kuchukua sura mpya nchini kutokana na vijana wengi kuingia katika matumizi ya dawa hizo Rapa King Crazy GK kutoka East Coast Team ameitaka serikali kutowapuuzia watu ambao wanauza madawa ya kulevya

Gk ametoa neno hilo kwa serikali na kusema kuwa watu hao ni hatari kwani wanauza sumu ambazo mwisho wake zinaua vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa.

King Crazy GK ameitaka serikali isiwachekee hata kama ni watu maarufu au wanamuziki wanapaswa kupewa adhabu kali sana kwani hao ndiyo kioo cha jamii pia ametoa rai kwa vyombo vya usalama kuwashirikisha wananchi kwani wanajua ukweli juu ya sakata la madawa ya kulevya.
"Mtu anayebeba au kuuza unga ni kama mchawi, na nchi za watu wakikamatwa wananyongwa kwa sababu anauza sumu inayoua watu lakini kwetu hapa mtu anayeuza na kubeba madawa ya kulevya anaonekana ndiye mjanja. Inabidi serikali isiwachekee hawa watu hata kama ni wanamuziki inabidi wapewe adhabu kali sana sababu hao ndiyo kioo cha jamii, hivyo wanapoendelea kuchekewa wanalisha sumu kwa jamii na kuona hayo ndiyo maisha yenyewe watu wanapaswa kuishi kumbe siyo". Alisema King Crazy GK

Q Chief Ataja Sababu zilizomfanya Aache Unga

$
0
0
Msanii Q Chief amefunguka na kuweka wazi sababu kubwa zilizopolekea yeye kuachana na matumizi ya dawa za kulevya na kusema yeye alipitia njia ngumu zaidi ya kuachana na matumizi ya dawa hizo kwa kupambana na nafsi yake.


Amesema hiyo ni tofauti na wasanii wengine ambao wamekuwa wakilazimishwa kuacha ili hali wao bado wanaupenda unga na hawapo tarayi kutoka moyoni mwao.

Q Chief alisema hayo alipokuwa akiongea na EATV na kusema jambo la kwanza kabisaa lilimfanya apigane vita na nafsi yake kwanza aliwatazama watoto wake wa kike watatu na kuona hawana furaha kuona baba yao yuko vile.

"Kiukweli mimi nilianza kupigana na nafsi yangu mwenyewe nilianza kujiaminisha kuwa hiki kitu si kizuri kwa afya yangu nataka kuacha, nikasema sasa basi, nina watoto watatu wa kike, mimi ni baba wananihitaji, nina fani yangu na nina mambo mengi ya kufanya". Alisema Q Chief
Mtazame Q Chief hapa

Wanaume: Vijue Visa vya Michepuko Mjini...

$
0
0
Kila side chick anatamani siku moja awe main chick, tena hawa ambao uliwambia Iam married halafu wanajifanya mioyo yao imetengenezwa na maganda ya bamia, anakwambia "worry not darling mi sinaga hata wivu wala sitakubana ila tu nikikutaka unipe dyudyu yangu usijifanye bize na mkeo am ready for wateva"

Ndo wana balaa sio mchezo mkianza atajifanya anamheshimu mkeo kabla ya kupiga simu anakuuliza 'are u free nikupigie' ila baadae dyudyu ikikolea anasahau (baundary) basi anajikurupukia tu sa9 usiku anatwanga eti "nimekuota bebi i wish you were here"

Mhh saa hizii? Akiona hukolei sasa anakutengenezea balaa ili mkeo agundue, akikukosa kwenye lipstick kwenye kola ya shati basi siku hizi wana misabuni yao na viungo- mseto vya kuweka ndani ya uvungu kunogesha penzi vinanukia balaa vinaitwa mishki na shaibu.

Nyuchi zinawekewa pilipili hoho mixer na viungo vya pilau mzee ukichepuka ukirudi home mkeo lazima agundue maana unabakia na harufu ya biriani siku 3 hata uoge na OMO haitoki labda ujisugue na utomvu wa mpapai na steel wire

Madhara ya Kiafya Kuhusu Wanaojichora Tattoo

$
0
0
Tafiti nyingi za kitabibu pia zinaonesha kwamba, wino au rangi za tattoo zinaweza kusababisha uambukizo wa bakteria aina ya Mycobacterium cholonae.

Bakteria hawa wanaweza kusababisha magonjwa ya ngozi na nyama za mwili, matatizo ya njia ya mkojo, mfumo wa kupumua, magonjwa ya uambukizo kwenye mifupa na nyama za moyo.

Michoro hiyo pia huweza kusababisha homa ya uti wa mgongo na tatizo la macho.


Vilevile, vifaa vinavyotumiwa kuchora mapambo hayo hutumika kwa watu mbalimbali kwa wakati mmoja bila utaalamu sahihi wa kuvisafisha.


Hali hiyo huweza kusababisha vibebe vimelea vya magonjwa mbalimbali na kuyahamishia kwa wengine.

Hali hii inaweza kusababisha uambukizo wa magonjwa yatokanayo na virusi hatari kama vile virusi vya Ukimwi, virusi ninavyosababisha homa ya ini (Hepatitis B na C) au virusi vya malengelenge (herpes simplex virus).

Kumbuka, wakati wa kuchora tattoo, ngozi hutobolewa kwa mashine au sindano hadi kuifikia sehemu ya ndani kabisa. Hii ni hatari kwa afya yako.

Wafugaji 50 waponea chupuchupu kufa

$
0
0
WATU 50 wakiwa na watoto wadogo wamenusurika kufa, baada ya kupotea ndani ya Pori la Akiba la Selous kwa siku saba; huku wakikosa chakula na maji na kulazimika kula kinyesi cha ng’ombe, damu na mikojo ya binadamu.

Watu hao ambao ni wafugaji, walikuwa wakihama na mifugo yao inayokadiriwa kufikia 1,780 kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya ya Rufiji mkoani Pwani, yakiwemo Chumvi na Muhoro waliekea Morogoro, ambako walidai ndiko yalipo makazi yao.

Tukio hilo ambalo si la kawaida kutokea katika pori hilo, lilianzia Jumatano iliyopita wakati wafugaji hao, walipoanza safari ya kuelekea Malinyi mkoani Morogoro, wakiongozwa na mwenyeji wao, waliyemtaja kwa jina la Mzee Mzigua, ambaye hata hivyo wanadai aliwalaghai na kuwatelekeza.

Wafugaji hao walisema walitembea kwa siku tano ndani ya pori hilo, wakitarajia kufika Malinyi, yaliko makazi yao. Lakini hali ilikuwa tofauti, baada ya mwenyeji wao huyo, kuwalaghai kwa kuwapitisha njia sisizo sahihi.

Walisema waliishiwa chakula na maji ya akiba na mwisho walijikuta wanatokea ndani ya Pori la Akiba la Selous; huku hali zao zikiwa zimedhoofu kutokana na njaa na kiu cha maji. Wakiwa safarini, mwenyeji wao huyo, aliwataka kila mmoja alipe fedha ikiwa ni ujira wake kwa kuwaonyesha njia. Walidai kuwa walimlipa fedha nyingi.

Wengine walimlipa Sh milioni mbili, Sh milioni moja na wengine Sh 500,000, wakitarajia angewasaidia. Walitembea usiku na mchana ndani ya pori hilo, wakipishana na wanyama wakali kama simba na nyati, hivyo kuhatarisha usalama wa maisha yao na watoto wao.

Hali ilizidi kuwa mbaya zaidi, baada ya kutimia siku ya tano wakiwa ndani ya pori hilo, pale walipoishiwa chakula na maji, hivyo kuwalazimu kuanza kuchinja ng’ombe na kunywa damu kwaajili ya kukata kiu. Pia walikula kinyesi chao ili kupunguza njaa. Yule mwenyeji wao aliwatelekeza baada ya kuona hali zao zimekuwa mbaya.

Alitokomea kusikojulikana, akiwaacha wasijue pa kwenda, hivyo kulazimika kutelekeza mifugo yao ili kunusuru kwanza maisha yao. Halikadhalika, wengine walilazimika kunywa mikojo yao na mingine kuwanywesha watoto wao kunusuru maisha yao, hali iliyowafanya kuathirika kiafya na kushindwa kuendelea na safari.

Wengine walianguka na kupoteza fahamu. “Sisi tulikuwa tunataka turudi nyumbani kwetu Morogoro. Huku tulikuja wakati wa operesheni ya Morogoro, huku tulikuja kununua ng’ombe lakini miji yetu ipo kule Morogoro. Tukaambatana na huyo mwenyeji wetu aliyejitambulisha kwa jina la Mzee Mzigua na mtoto wake.

Lakini tunajua mpaka nyumbani kwake”alisema Kiongozi wa msafara wa wafugaji hao, aliyejitambulisha kwa jina la Lisesi Cherahani Bela na kuendelea, “Zilitimia kama siku nne tukiwa hatujanywa maji, jua lilikuwa linawaka, tukaanza kuanguka, tukaanza kuchinja ng’ombe na kunywa damu, tulijaribisha kula kinyesi cha ng’ombe, tulikuwa tunakojoa mkojo tunanywesha hata watoto. Mimi nilikunywa mkojo lita moja, ikaniathiri hapa kifuani, kumbe mkojo ni kitu kibaya.”

Akizungumza na waandishi wa habari waliofika katika eneo hilo, kiongozi huyo alisema baada ya kuona hali inakuwa mbaya zaidi, alitafuta eneo ambalo lina mtandao wa simu na kufanya mawasiliano na watu mbalimbali, ambapo alifanikiwa kuwasiliana na watu wa Kigoma na kuomba msaada wao.

Alisema kuwa watu hao, waliwasiliana na wahifadhi wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi na kuwasiliana na wahifadhi wa Pori hilo la Selous, ambao walianza kazi ya kuwasaka na hatimaye kuwakuta katika eneo la Mlima Luhombelo, lililopo katikati ya Pori hilo wakiwa tayari wameshadhoofika kiafya.

Askari hao wa wanyamapori wa Pori hilo, waliwapatia uji na maji na kuwapa huduma ya kwanza wale wengine ambao walikuwa na hali mbaya.

Baada ya taarifa hizo za kupotea kwa wafugaji hao, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Gaudence Milanzi alifika katika eneo hilo juzi, akiambatana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA), Martin Leibooki, Meneja wa Pori la Akiba la Selous, Henock Msocha na maofisa wengine wa wizara na pori hilo.

Milanzi alisema Serikali inaangalia namna ya kuwasaidia wafugaji hao, kurejea katika hali zao kiafya pamoja na kuwasaidia kutafuta mifugo yao ili waweze kurejea katika makazi yao na kuendelea na shughuli zao.

“Kwa upande wa Serikali kama Wizara hatuchukulii kama hawa wameingia kwenye hifadhi hapana, muhimu kwanza ni kuokoa maisha ya binadamu, na hicho ndicho tunategemea kukifanya sasa hivi, na baada ya hapo kutakuwa na masuala ya kutafuta hiyo mifugo, kwa sababu wamepata hasara kubwa”alisema Katibu Mkuu huyo.

Aliutaka uongozi wa wilaya ya Rufiji, kutoa ushirikiano na wizara ili kuwabaini waliowadanganya wafugaji hao, kwa kuwaingiza kwenye pori hilo na kuwatapeli kiasi hicho kikubwa cha fedha.

“Hawa waliowadanganya na kupita huko ndani ya pori kwa kweli tutaendelea kuwatafuta na tutaomba tuwe na ushirikiano na uongozi wa Wilaya kwa sababu inaelekea kuna watu kazi yao ndo hiyo, ukiangalia pesa walizowapa ni nyingi sana, sasa watu wamechukua pesa zote na wamewaacha katika hali kama hii, wengine wana watoto wadogo, kwa hiyo tutahakikisha tunashirikiana kuwatafuta ili tukomeshe hili tatizo moja kwa moja”alisema.

Katibu Mkuu huyo alimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa TAWA na Mhifadhi Selous kwa juhudi za haraka walizochukua. Alisema wizara yake itaendelea kushirikiana na Mamlaka mbalimbali, kutoa misaada ya haraka, endapo yatatokea tena matukio ya aina hiyo.

Kwa upande wake, Leibooki alisema TAWA ambao ndiyo wamiliki wa hifadhi zote za wanyamapori nchini, haitawachukulia hatua za kisheria wafugaji hao, kwa kuwa waliingia ndani ya pori kwa kudanganywa na watu wenye nia mbaya.

Lakini, alisisitiza kuwa mamlaka yake, itawashughulikia kisheria wawindaji haramu na wafugaji wanaoingiza mifugo yao ndani ya hifadhi zilizo chini ya Mamlaka yake.

Pia alisema Mamlaka yake, inaendelea na utaratibu wa kushirikiana na wananchi waishio pembezeni mwa hifadhi zote, kwa kuwapa elimu ya ufugaji bora kwa kushirikiana na wizara zinazohusika na kuendeleza miradi ya maendeleo, ikiwemo miundombinu ya maji.

Katibu Mkuu wa Chama cha Wafugaji chini (CCWT), Magembe Makoye aliwataka viongozi wa Halmashauri mbalimbali nchini, kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji mahali walipo, bila ya kuondoa watu wengine.

Alisema kuwa wao kama chama, wamesikitishwa na tukio la kuondolewa kwa wafugaji hao katika bonde hilo la Rufiji, kwa kuwaambia warudi walipotoka. Alisema tamko hilo lilitolewa na uongozi wa Halmashauri hiyo na ndilo lililosababisha matatizo hayo.

Makoye alisema kufanya hivyo, hakuondoi migogoro ya wafugaji na wakulima, badala yake ni kuendelea kuzalisha migogoro hiyo katika maeneo mengine, ambayo wafugaji watahamia.

“Tunalaani kweli vitendo hivi vya viongozi na watendaji wengine wa Halmashauri kuwafukuza wafugaji, tena wakati mwingine kwa kuwatisha na matokeo yake wananchi hawa 50 wangepoteza maisha, kama isingekuwa bahati ya mtu mmoja kuwa na simu kati yao” alisema Katibu Mkuu huyo.

“Kwa kweli kwa niaba ya wafugaji wote wa Tanzania naishukuru sana Wizara ya Maliasili kupitia kwa Katibu Mkuu, Gaudence Milanzi.” alisema Katibu huyo.

Alisema kuwa kungeweza kutokea majanga makubwa zaidi kwa kuwa kuwa wafugaji hao walikuwa wakisafiri na watoto wao wadogo katika mazingira hatarishi katikati ya pori hilo, ambalo lina wanyama wakali.

“Kwa kweli ni mazingira ya kusikitisha. Lakini niishukuru sana Serikali kwa maana ya Wizara ya Maliasili na Utalii, wamefanya kazi yao kwa namna ambavyo mimi ninawiwa kuwashukuru. Tangu jana tumewasiliana na Katibu Mkuu wa Wizara, leo watu wote wameweza kupatikana, kumefanyika doria ya ndege, doria za magari, doria kwa miguu, wamewatafuta hawa watu, wamewaokoa, wamewaleta kwenye huduma za afya, wamewapa chakula, wamewahifadhi, hawajawadhuru” alisema.

Aliiomba Serikali kuhakikisha tatizo la wafugaji nchini, linatafutiwa ufumbuzi wa kudumu, kwani jamii haiwezi kuendelea kubaki na tatizo hilo kwa miaka yote. Alitaka wafugaji watafutiwe maeneo ya kudumu ya kufugia, ikiwa ni pamoja na kupimiwa maeneo yao, badala ya hali ilivyo sasa kuafukuza kila kukicha.

5,219 wafa ajali za barabarani

$
0
0
AJALI za barabarani katika mkoa wa Dar es Salaam, zimeongezeka kutoka 3,710 kwa kipindi cha Januari hadi Desemba mwaka 2015 hadi kufikia ajali 5,219 kwa kipindi kama hicho mwaka jana.
Hilo ni ongezeko la ajali 2,009 ambazo ni sawa na asilimia 36.5. Aidha kuna ongezeko la vifo 9 ambapo kwa kipindi kama hicho mwaka 2015 vilitokea vifo 316 ikilinganishwa na vifo 325 vilivyotokea mwaka jana ambavyo ni sawa na ongezeko la asilimia 2.7.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya usalama barabarani kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Desemba 2016, ikilinganishwa na Januari hadi Desemba mwaka 2015.
“Pia kuna ongezeko la watu 654 waliojeruhiwa kwani Januari hadi Desembwa mwaka 2016 walijeruhiwa watu 4,066 ukilinganisha na watu 3,412 waliojeruhiwa kipindi cha Januari hadi Desemba 2015 sawa na asilimia 16” alisema.
Alisema kwa upande wa makosa yaliyokamatwa, kuna ongezeko la makosa 382,207 kwani katika kipindi kama hicho mwaka jana yalikamatwa makosa 769,170 yaliyoiingizia serikali maduhuli ya Sh 23,065,020,000 ikilinganishwa na makosa 386,963 yaliyoiingizia serikali maduhuli ya Sh 11,608,700,000 kwa mwaka 2015, ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 49.6.
Takwimu za ajali za pikipiki, zimeonesha kuna upungufu wa ajali 168. Kwa kipindi kama hicho mwaka jana zilitokea ajali za pikipiki1036 ikilinganishwa na ajali 1,204 zilizotokea mwaka 2015 ambazo ni sawa na asilimia 13.9.
Sirro alisema kwa upande wa vifo vilivyotokana na ajali za pikipiki vimepungua kwa idadi ya watu nane kwani Januari hadi Desemba mwaka jana watu 80 walifariki kutokana na ajali za pikipiki ikilinganishwa na watu 88 waliofariki mwaka 2015 sawa na upungufu wa asilimia tisa.
Pia alisema majeruhi wa ajali za pikipiki nao wamepungua watu 225 kwani Januari hadi Desemba 2016 walijeruhi watu 904 ikilinganishwa na watu 1,129 waliojeruhiwa mwaka 2015 ambao ni sawa na asilimia 20.

Ajinyonga kwa kunyimwa na mkewe samaki mbichi

$
0
0
MKAZI mmoja wa kijiji cha Kalundi kilichopo kata ya Kipande wilayani Nkasi, Vedast Kazumba (51) amejiua kwa kujinyonga kwa kile kinachodaiwa kuwa alighadhabika, baada ya mkewe kumnyima kitoweo cha samaki mbichi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando alithibitisha tukio hilo.
Alisema ni la usiku wa mkesha wa Mwaka Mpya na kwamba Kazumba alifikia uamuzi huo mgumu kwa kujinyonga akitumia kamba ya katani .
Alieleza kuwa hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa na polisi kuhusu tukio hilo na uchunguzi wake unaendelea . Habari kutoka kijijini humo, zinaeleza kuwa chanzo cha Kazumba kujinyonga ni kukasirishwa na kitendo cha mkewe, Antoniata Mwisua kumnyima kitoweo cha samaki mbichi.
“Mke wa marehemu aitwae Antoniata alimwandalia mumewe huyo chakula cha usiku, kitoweo chake kikiwa ni samaki mbichi alimkomba samaki huyo kisha akamwomba amwongezee kitoweo kingine cha samaki, lakini mkewe alimweleza kuwa kitoweo hicho kimekwisha. Ndipo mumewe alipokasirika akidai kuwa mkewe amemnyika kwa makusudi kitoweo hicho ndipo alipochukua hatua ya kuzira kula“ alieleza mmoja wa mashuhuda kwa masharti ya kutoandikwa gazetini.
Akizungumzia mkasa huo , Mwenyekiti wa Kijiji cha Kalundi , John Kalasa alidai kuwa marehemu wakati wa uhai wake alikuwa ni mtu mwenye kujawa na ghadhabu ambapo mara kadhaa alisikika akitishia kujinyonga.

VIDEO: Usipocheka utakuwa Mgonjwa

Viewing all 104808 articles
Browse latest View live




Latest Images