Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live

VIDEO: Cheki magari ya Messi, Baloteli, Ronaldo na Ibrahimovic


Huyu Ndio Msanii wa Kwanza Kusainiwa Kwenye Lebo ya Alikiba

$
0
0
Ni Abby Skillz aliyerudi rasmi kwenye muziki kwa wimbo wake Averina akiwa na Mr Blue pamoja na Alikiba amefunguka na kusema kuwa yeye ni msanii wa kwanza kusaini mkataba chini ya 'Label' ya msanii Alikiba inayofahamika kama 'Kings Music'.

Abby Skillz amesema hayo kupitia eNEWZ na kusema mpaka sasa label hiyo imeshasaini wasanii kama kumi ila yeye ni msanii wa kwanza kabisa kusaini chini ya uongozi wa Alikiba na kusema angeweza kuwataja wasanii wengine ambao tayari yameshadondosha wino lakini itakuwa si vyema hivyo muda utakapofika Alikiba mwenyewe ataweka wazi hilo.

"Alikiba amenitoa Kariakoo kule ni nyumbani kwa wazazi na saizi mimi niko kwake lakini nimekuja huku sababu ananisaidia mambo fulani katika muziki ambalo si jambo baya, lakini pia unapaswa kutambua mimi ni msanii wa kwanza kusaini mkataba chini ya label ya Alikiba 'Kings Music' ambayo mpaka saizi imeshasaini wasanii kama kumi hivi ila tunamsubiri Rais wetu Alikiba ndiye ataweka wazi jambo hilo" alisema Abby Skillz

Skendo ya Madawa ya Kulevya Kwa Hemedy...Mwenyewe Adai Alimuhofia Mama Yake

$
0
0
Baada ya hivi karibuni kusambaa kwa post kwenye mitandao ya kijamii ikitaja baadhi ya wasanii wa Bongo wanaotumia dawa za kulevya, miongoni mwa wasanii waliotajwa ni pamoja na Hemedy Suleiman.

Hemedy Suleiman kuzugumzia madai hayo……‘Nilipoiona hiyo post nilicheka kwa sababu mimi naujua ukweli, ila nilimfikiria zaidi mama yangu mzazi akisikia hizo habari itakuaje, na kweli alinipigia huku amepanic lakini ukweli ni kwamba mimi si mtumiaji wa dawa za kulevya’

Mwanamke Tajiri zaidi Afrika Dos Santos Atajirika zaidi

$
0
0
Bi Santos amechukua udhibiti wa benki hiyo ya BFA baada ya kampuni yake kununua hisa zaidi katika benki hiyo na kudhibiti zaidi ya asilimia 50 ya hisa katika benki hiyo.

Hatua hiyo imewaacha waangalizi kutojua ikiwa watamshangilia mama huyu mjasiria mali au kulalamikia mamlaka na ushawishi wa kiuchumi walio nao matajiri wachache sana barani afrika.

Isabel dos Santos mwenye umri wa miaka 43, amefanikiwa na angali na ari ya kufanikiwa zaidi katika kanda ambayo wanaume wanatawala katika ofisi nyingi za umma na za kibinafsi.

Bi Dos Santos, ni bintiye rais wa angola Jose Eduardo dos Santos, ambaye ameongoza taifa hilo tangu mwaka wa elfu moja mia kenda na sabini na tisa.

Angola ni moja ya mataifa masikini zaidi duniani.

Katika miaka ya hivi karibuni ilinufaika pakubwa kutokana na mapato yanayotokana na mauzo ya mafuta na uwekezaji kutoka uchina.

Hata hivyo ufisadi na umaskini vimesalia kuwa changamoto kubwa zaidi nchini humo.

Bi Dos Santos mara kwa mara amepuuzilia mbali madai kuwa familia ya rais inapewa nafasi zaidi kuliko raia wengine kuthibiti uchumi na masuala ya kisiasa ili kuhakikisha kuwa familia hiyo itaendelea kutawala Angola baada ya rais Dos Santos kustaafu, kama alivyohaidi hivi majuzi.

Kwa sasa Bi Dos Santos anasimamia shirika la mafuta la taifa na kampuni kubwa zaidi ya kutoa huduma za simu na sasa anadhibiti benki kubwa zaidi nchini Angola BFA.

Hii ikiashiria kuwa ushawishi wa familia ya rais dos santos itaendelea kuchukua nafasi kubwa zaidi katika masuala ya kiuchumi na kisiasa nchini Angola miaka zijazo.

Darassa Amtaja Prodyuza Aliyewahi Kumtosa Studio

$
0
0
Rapa Darassa amefunguka na kuweka wazi jambo ambalo katika maisha yake ya muziki lilimkwaza sana na hataweza kulisahau ni baada ya mmoja wa Producer wake kutoka AM Record Manecky kumkatalia kufanya kazi ambayo ndiyo iliweza kufungua zaidi milango

Darassa anakiri kuwa AM Record kwake ndiyo ilikuwa kama nyumbani kutokana na kazi alizokuwa akifanya lakini anadai aliweza kufanya kazi kwa Mr T Touch na siku hiyo studio ya T Touch kulikuwa na matatizo hivyo ilibidi ampigie simu Manecky na kumuomba waende studio ili waweze kupata sauti ya Mr Blue lakini mwisho wa siku Manecky alimkatalia.

"Sijawahi kusema hilo jambo sehemu yoyote ile ila nakumbuka siku hiyo nilikuwa nimefanya kazi kwa Mr T Touch ila studio kulitokea matatizo kipindi hicho mimi naunga unga hivyo nilimpigia simu Manecky nikiamini AM Record ni nyumbani kweli aliniambia niende nikaenda na Mr T Touch pamoja na Mr Blue lengo lilikuwa nipate tu sauti ya Mr Blue kisha ile kazi akamalizie Mr T Touch lakini huwezi amini Manecky alinikatalia". Alisema Darassa

Mbali na hilo Darassa anasema wimbo ambao ulimpeleka kwa Manecky ndiyo wimbo ambao uliweza kufungua milango zaidi katika muziki wake

Arosto ya Unga Humfanya Teja Awe Mwendawazimu, Yupo Tayari Kufanya Lolote – Fanani

$
0
0
Rapper wa zamani wa kundi la HBC, Terry Fanani ambaye ni mmoja wa mastaa waliowahi kuathirika na matumizi ya dawa za kulevya, amesema arosto anayopata mteja ni kitu chenye nguvu kinachompa uchizi teja.

Akiongea na Planet Bongo ya EA Radio, Fanani amesema teja akiwa katika hali hiyo, yuko tayari kwa lolote.

“Arosto inapokukamata unakuwa katika hali ya kama mwendawazimu,” amesema.

“Kwahiyo uko tayari kufanya lolote, uko tayari kumdanganya mtu ambaye anakusaidia ili ukapate pesa ukafanye, uko tayari kuchukua hata mama yako anaumwa umepewa hela ukanunua dawa hospitali la kwanza ni kujitubu wewe kwasababu tunakuwa na ubinafsi,” amesisitiza.

“Na inapofika wakati imefika jioni sijavuta halafu sina kitu niko na kampani za washkaji tunaweza tukaingia front sio, kaba mtu chukua hela ilimradi nitibu lile tatizo langu la msingi.”

Fanani amedai yupo kwenye kipindi ambacho ameacha kutumia madawa na anapambana ili asirudie tena kwasababu kuacha si jambo rahisi.

Serikali Inawajibika Kumtafuta Ben Saanane – Lissu

$
0
0
MWANASHERIA Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu, amesema serikali ndiyo yenye wajibu wa kumtafuta na kumpata raia wake, Ben Saanane,  ambaye amepotea kwa miezi ipatayo miwili sasa.

Lissu ameyasema hayo wakati akizungumza na Global TV Online inayomilikiwa na kampuni ya Global Publishers, wachapishaji wa magazeti ya Uwazi, Championi, Ijumaa, Risasi, Amani na  Ijumaa Wikienda.

Mwanasheria huyo alikuwa akijibu swali kuhusu ukimya wa chama chake kuhusu kada wake huyo ambaye amezua tafrani nchini akiwa hajulikani akiwa hai au amekufa.

Alikanusha uvumi unaoenezwa kwamba huenda chama chake kinahusika katika kupotea kwa  mtu huyo, ambapo alisema katika kukwepa kusema kitu kisichojulikana, wameitaka  serikali kutoa tamko iwapo inafahamu Mtanzania huyo aliko au haifahamu.

lissu-global-tv-10“Mpaka sasa serikali haijasema lolote kuhusiana na jambo hilo.  Tunafahamu Ben amepotea lakini wakati mwingine tunanyamaza kwa sababu tunachokifahamu sisi ni sawa na mnachokifahamu nyie (waandishi wa habari) ila nawahakikishia kwamba hatuhusiki kwa vyovyote na kupotea kwake,” alisisitiza mwanasheria huyo machachari.

lissu-global-tv-12Tundu Lissu katika picha ya pamoja na Mhariri wa Gazeti la Ijumaa Wikienda, Sifael Paul.

Akisisitiza msimamo wa chama chake, alizitaka mamlaka zote husika na usalama wa raia ziseme hali halisi inayozingira sintofahamu ya mahali alipo Saanane ikiwa yuko ndani au nchi za nje, au hata kama amefariki na kuzikwa kwa kutotambuliwa.


Akizungumza kuhusu kutoonekana kwake huko Arusha kusaidia juhudi za kumpatia dhamana Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, mwanasheria huyo alisema kuna wanasheria wengi wa chama hicho wanaoweza kufanya kazi hiyo lakini akasema suala hilo linaonekana gumu kwa vile linaendeshwa kisiasa.


Hata hivyo, alisema ataungana na wanasheria wenzake ili kulipatia ufumbuzi suala hilo linaloonekana kuendelea bila sababu za msingi.

Magari yenye taa za mwanga mkali yapigwa marufuku

$
0
0
POLISI Kikosi cha Usalama Barabarani kimesema kitaanza kukamata magari yote ambayo yamewekwa taa zenye mwanga mkali (spotlights) kwa kuwa uwekaji wa taa hizo, ni kinyume na sheria ya usalama barabarani.

Uwekaji wa taa hizo zenye mwanga mkali, umezuka kwa kasi katika maeneo mbalimbali nchini, jambo ambalo limetajwa linaweza kusababisha ajali kwa dereva atakayemulikwa na taa hizo.

Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Kikosi hicho, Naibu Kamisha Mohammed Mpinga wakati akizungumza na gazeti hili ofisi kwake jijini Dar es Salaam, ambapo alisema ukamataji wa magari hayo utaanza rasmi wiki ijayo.

Mpinga alisema wameshatoa maelekezo kwa askari wa usalama barabarani, kuhakikisha wanakamata magari, pikipiki na malori makubwa ambayo yamewekwa taa hizo.

“Ziko taa za aina fulani zinazowekwa kwenye magari na hata ukitembea usiku utaona mwingine ameweka taa moja mwingine anaweka nyingi sana, kiasi ambacho zimeleta matatizo kwa madereva wengine,” alisema Kamanda Mpinga.

Aidha, alisema kwenye barabara kuu kuna mtindo wa madereva wa magari makubwa, kuweka taa kubwa ambazo zinawekwa juu na kumulika mwanga mkali, kiasi ambacho dereva anayemulikwa anapata upofu wa muda na kushindwa kudhibiti chombo chake.

Kamanda Mpinga alisema kuwa walishatoa muda wa kutosha kwa wamiliki wote wa magari, walioweka taa hizo kuziondoa, hivyo kwa sasa wataanza kuwachukulia hatua wote ambao watakuwa hawajaziondoa.

Alifafanua kuwa uwekaji wa taa hizo ni kinyume cha Sheria ya Usalama Barabarani Kifungu cha 39 Sura ya 168, ambacho kinaeleza matumizi ya taa. Mpinga pia alisema magari yatakayokamatwa ni yale ambayo yameongezewa taa hizo.

Alisema magari ambayo yametoka kiwandani yakiwa na taa hizo, hayatahusika.

“Hapa nazungumzia taa za kuongeza. Lakini pia kuna magari kwa ajili ya uwindaji huwa yanawekwa taa, lakini wanachotakiwa kufanya waweke kava, wakati wote ziwe na kava,” alisema.

Alisema wamiliki wa magari hayo ya kuwindia, wanatakiwa kuondoa kava hizo wanapokuwa porini tu na kuongeza kuwa mtindo wa wamiliki wa magari makubwa kuweka taa nyuma ya magari ambayo inamulika, matokeo yake mtu anayemfuata anafikiri gari anakuja kumbe inakwenda mbele.

Upelelezi wakwamisha kesi ya Kitilya

$
0
0
KESI ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya na wenzake, imeahirishwa hadi Januari 20 mwaka huu kutokana na upelelezi kutokamilika.

Wakili Mwandamizi wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi alidai jana katika Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Wilbard Mashauri kuwa kesi imekuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Cyprian Mkeha, hayupo.

Kishenyi alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo aliomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa. Hakimu Mashauri alikubaliana na ombi hilo na kuahirisha kesi hiyo hadi Januari 20 mwaka huu. Katika shauri lililopita, Hakimu Mfawidhi, Mkeha aliutaka upande wa mashitaka kueleza upelelezi wa kesi hiyo umefikia hatua gani.

Wakili Esterzia Martin alidai kuwa jalada la kesi hiyo lipo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kwa ajili ya kuendelea kuchunguza nyaraka.

Hivyo, aliomba apangiwe tarehe nyingine kwa ajili ya kueleza upelelezi umefikia wapi. Mbali na Kitilya, wengine ni mshindi wa Mashindano ya Urembo (Miss Tanzania) mwaka 1996, Shose Sinare na Mwanasheria wa Benki ya Stanbic, Sioi Solomon. Kwa pamoja, washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka manane, likiwemo kutakatisha fedha, dola za Marekani milioni sita.

Wanadaiwa kutenda makosa hayo katika tarehe tofauti kati ya Machi 2013 na Septemba 2015 wakati wa mchakato wa mkopo wa Dola za Marekani milioni 550 wa Serikali ya Tanzania kutoka Benki ya Standard ya Uingereza.

Majaliwa acharuka, kumtuma CAG kukagua Tancoal

$
0
0
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa atamtuma mara moja Msajili wa Hazina, aende kufanya uchunguzi wa kina na wa kijinai (forensic investigation) ili kijiridhisha kama mapato na matumizi ya kampuni ya TANCOAL ni halali.

Alitoa kauli hiyo jana mara baada ya kupokea taarifa na kutembelea mgodi huo ili kuona shughuli za uzalishaji zikoje.

Waziri Mkuu alisema atamuagiza pia Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu ya Serikali (CAG) ili apitie mahesabu ya kampuni hiyo tangu mwaka 2011 walipoanza uzalishaji.

“Mbali na CAG, itabidi Gavana wa Benki Kuu naye aangalie utumaji wa fedha uliokuwa ukifanywa kama ulifanyika kwa halali,” alisema.

Katika maswali aliyoyauliza Waziri Mkuu, alitaka kufahamu ni kwa nini kampuni hiyo haijalipa gawio kwa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) ambao ni mbia (asilimia 30) na kampuni ya Intra Energy Limited (asilimia 70), licha ya kuwa imekuwa ikifanya uzalishaji wa makaa ya mawe na kuyasafirisha kwenye viwanda hapa nchini na nje ya nchi.

“Taarifa zenu zinaonyesha kuwa mmepata kila mwaka, lakini rekodi nilizonazo zinanionyesha kuwa mwaka 2013 mlipanga kuzalisha tani 50,000 na mkauza zaidi ya hapo. Mkaguzi wa Hesabu anasema kampuni imepata, hii itawezekanaje?” alisema wakati akimhoji Mkurugenzi Mtendaji wa NDC, Mlingi Mkucha.

“Desemba 2013 mliuza tani 39,000 kwa wamiliki wa viwanda vya nguo, pia mliuza tani 2,000 kwa Kampuni ya Saruji ya Zambia, Novemba 2013 mliingia makubaliano ya kuuza tani 165,000 kwa kampuni ya saruji ya Tanzania na ziliuzwa. Mbona ‘financial statement’ zenu zinasema mwaka huo nao mlipata hasara?” “Mnasema gawio (dividend) hutolewa baada ya mtu kutangaza faida. Mbona mlivuka lengo lakini mkatangaza kuwa kampuni imepata hasara katika mwaka huo wa fedha?” alihoji Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu alimbana Mkucha aeleze ni kwa nini akiwa mwanasheria wa NDC, aliruhusu kuwepo kwa mkataba unaotoa mwanya kwa kampuni ya TANCOAL kulipia gharama za menejimenti kwa wakurugenzi ambao wako Australia, wakati hawahusiki na utendaji wa kila siku wa TANCOAL hapa nchini.

Alihoji pia kwa nini aliyekuwa Mkurugenzi wa NDC, Gideon Nassari alikuwa ni mjumbe wa Bodi ya TANCOAL na mjumbe wa Bodi ya Intra Energy Corporation ya Australia huku akiwa ni Mtendaji Mkuu wa NDC.

“Wewe ulikuwa mwanasheria wa NDC na ulilijua hilo, lakini hukuona taabu ya kiutendaji katika hilo? Au ulishindwa kusema kwa sababu alikuwa ni bosi wako?” Waziri Mkuu alihoji.

Alimtaka Mkucha apeleke mkataba huo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili aupitie upya, na hasa kipengele cha kufungua akaunti za NDC kwa kutumia kanuni za Australia na suala la utaratibu wa gawio kwa wanahisa, ambapo kifungu kilichopo kinaipa Bodi ya TANCOAL mamlaka ya kuamua kutoa au kutokutoa kwa wanahisa.

“Kipengele kama hiki kwenye mikataba kinazuia ninyi kupata gawio, na ndiyo maana hesabu za kila mwaka zimekuwa zinasoma hasara na ninyi mnaona sawa tu huku Serikali ikiendelea kukosa mapato yake,” alisema.

Waziri Mkuu aliutaka uongozi wa kampuni ya TANCOAL, uongeze uzalishaji ili uweze kukidhi mahitaji ya ndani, kwani makampuni mengi yamebaini gharama kubwa iliyopo kwenye matumizi ya mafuta ya dizeli na sasa yanahitaji makaa ya mawe kwa uzalishaji.

“Nimetembelea mgodi na kujiridhisha kuwa makaa ya mawe yapo ya kutosha. Uongozi wa kampuni mmesema mashine ziko bandarini Mtwara, lipieni mkamilishe taratibu ili mashine na mitambo yenu vije kusaidia kuongeza uzalishaji,” alisema.

Waziri Mkuu alisisitiza kuwa serikali haitaruhusu uagizaji wa makaa ya mawe kutoka nje ya nchi na kwa maana nyingine, imeongeza wigo wa soko. Lakini, alisema anaona wanakosa teknolojia uchimbaji makaa kwa wingi na kuwataka wafanye haraka kuleta vifaa hivyo vilivyoko bandarini.

SINGIDA: Basi la Mohammed Trans Lapata Ajali, Watu Kadhaa Wafariki Dunia

$
0
0
Nimepita hapa kidogo kabla ya kufika Manyoni nimekutana na hii ajali mbaya. Inadaiwa watu 3 wamefariki na majeruhi ni 6. Aidha, inasemekana ni walimu ambao walilikodi basi kutoka Tanga.

Chanzo cha ajali ni gari ndogo lililokuwa limeegesha barabarani bila tahadhari, mbele ya basi kulikuwa kuna lori la mafuta hivyo dereva wa lori alipoona mbele kuna gari imepaka na yeye akatanua kwa haraka.

Wakati huo basi nalo lilikuwa linataka ku-overtake hivyo dereva wa basi akashindwa kulimudu kutokana na mwendo kasi na akaligonga roli la mafuta kwa nyuma na kutoboka kitu kilichopelekea kumwagika mafuta barabarani.

Tushukuru Mungu havijatokea vifo zaidi kwa sababu mafuta yaliyotapakaa ardhini hayakushika moto.

Mungu awaweke mahala panapostahili marehemu wote, amina.

By karume kenge/JF

Utafiti: Watu 550,000 waathirika na matumizi ya dawa za kulevya nchini

$
0
0
Tatizo la matumizi ya dawa za kulevya nchini ni kubwa ambapo utafiti uliofanywa mwaka 2014 unaonyesha kuwa watu elfu hamsini wameathirika kwa kutumia njia ya kujidunga sindano na watu laki tano kwa njia ya uvutaji.


Daktari bingwa wa magonjwa ya afya ya akili wa hospitali ya taifa Muhimbili Dk Kassian Nyandindi amesema utafiti uliofanywa mwaka 2014 umebaini na idadi hiyo ni kwa wale wanaotumia dawa aina ya heroin na cocaine lakini kuna wengine ambao hupatiwa huduma katika kliniki zao wanaotumia bangi,mirungi na pombe.

Aidha Dk Nyandindi amesema ingawa idadi ya watu walioathiriwa na dawa za kulevya nchini kwa sasa ni 25,000 waliojitokeza kupatiwa huduma katika kliniki nne zinazotoa huduma hiyo ni 3,500 tu na kuongeza kuwa kiwango cha HIV kwa kundi hilo ni asilimia 20 hadi 50 huku akitaja changamoto zinazoikabili idara hiyo.

Source: ITV

Max Rioba Adai Ameshindwa Kufanyakazi na Young Dee Kwa Kuwa Hana Nidhamu

$
0
0
Uongozi wa label ya Millian Dollar Boys ‘MDB’ iliokuwa unamsimamia rapper Young Dee, amedai hawafanyi tena kazi na rapper huyo kwa madai rapper huyo hana nidhamu.

Max Rioba ambaye ni mkurugenzi wa label hiyo, wiki moja iliyopita alionekana kulalamika katika mitandao ya kijamii akidai rapper huyo amerudi tena katika matumizi ya Madawa ya kulevya.

Akiongea Ijumaa hii katika kipindi cha FNL cha EATV, Max amedai habari za rapper kurudia matumizi ya Madawa ya kulevya na yeye anaziona katika mitandao ya kijamii kuhu akikiri kutofanya kazi tena na rapper huyo kwa madai ya kuwa hana nidhamu.

“Kwa sasa Young Dee hayupo tena kwangu,” alisema Max. “Sikumfukuza Young Dee kutoka kwangu, nilimwambia aondoke, kuna tofauti kati ya kumfukuza na kumwambia aondoke, sababu ni nidhamu.,”

Pia Max alidai kama rapper huyo atahitaji msaada wa pesa kutoka kwake ataendelea kumsaidia lakisi sio tena kuwa pamoja kama zamani.

“Young Dee akihitaji msaada wa kifedha nitamsaidia, hata binti aliyezaa naye akikwama kifedha mimi nitamsaidia, simchukii Young Dee,” alisema Max.

Katika hatua nyingine Max amedai kwa sasa hadhani kama atakuwa na nafasi tena ya kupokea msanii yeyote na kumsimamia.

Picha: Billicanas Ya Mbowe Yabomolewa Rasmi

$
0
0
Shirika  la Nyumba la Taifa (NHC) limeanza kubomoa jengo la iliyokuwa Klabu Bilicanas na ofisi za Free Media inayomiliki gazeti la Tanzania Daima zinazomilikiwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, Freeman Mbowe, lililopo makutano ya barabara ya Mkwepu na Indira Gandhi lenye kitalu namba 725-726/24 na hati namba C. T No. 186018/15 and C. T No. 186018/10.

Ubomoaji huo ulioanza jana unafanyika wakati Mbowe ameingia katika mgogoro na NHC baada ya kampuni ya udalali ya Poster and General Traders kumtolea vyombo nje mwanzoni mwa Septemba, mwaka jana kwa kudaiwa Sh bilioni 1.2 ambayo ni deni la pango ya miaka 20.

Mwanzoni mwa Septemba, mwaka jana NHC kwa kushirikiana na Kampuni ya Poster and General Traders, ilifika katika jengo hilo kwa maelekezo ya kutoa  thamani mbalimbali zilizokuwa katika ofisi za jengo hilo na kumpa Mbowe siku 14  kulipa deni analodaiwa na kuweza kugomboa mali hizo.

Mpango huo ulisimamiwa na Meneja wa Ukusanyaji Madeni wa NHC, Japhet Mwanasenga na alisema Mbowe alikuwa na muda wa wiki mbili kwa wakati huo kulipa fedha hizo kabla ya vifaa vyake kupigwa mnada.

Mwanasenga alisema taratibu zote zilifuatwa kabla ya kumwondoa mteja huyo ikiwamo notisi na kwamba vifaa hivyo vitashikiliwa kwa muda huo na endapo akishindwa kulipa jengo hilo atapangishwa mtu mwingine.

Alisema shirika hilo linahitaji fedha kwa ajili ya ujenzi na uendelezaji wa majengo yake hivyo mteja anayedaiwa ajiandae kuondolewa wakati wowote huku baadhi ya watu wakilihusisha tukio la Mbowe kuondolewa katika ofisi hizo na masuala ya siasa.

Hata hivyo, Mwanasenga, alisema uamuzi wa kumwondoa katika ofisi hizo hauna uhusiano na masuala ya siasa.

Kutokana na hali hiyo, Mbowe kupitia Mawakili wake, John Malya na Peter Kibatala, walifungua shauri la kupinga kuondolewa katika jengo hilo Mahakama Kuu ya Tanzania na kutaka kurudishwa katika jengo hilo.

Hata hivyo, maombi hayo yalitupiliwa mbali Oktoba 17, mwaka jana na Jaji Sivangilwa Mwangesi na kusema kuwa mahakama hiyo imechukua uamuzi huo baada ya kujiridhisha na hoja kuu tatu kuwa hakuna mkataba wa ubia uliopo baina ya NHC na Mbowe Hotels Limited na kuwa uhusiano pekee uliosalia ni wa mpangaji na mpangishaji.

Pia Jaji Mwangesi alisema mahakama imejiridhisha kuwa NHC imefuata taratibu zote katika kuiondoa Mbowe Hotels Limited kwa kutoa ilani ya siku 30 na baadaye siku 14 kabla ya kumtoa mteja wao huyo.

Kuhusu kusajiliwa au kutosajiliwa kama dalali rasmi wa mahakama wa kuendesha mchakato wa kumhamisha Mbowe katika jengo hilo, alisema hiyo nayo haikuwa hoja yenye mashiko na kwamba waombaji walitakiwa kuwasiliana na Msajili wa Mabaraza ya Ardhi.

Katika shauri hilo, NHC iliongozwa na Wakili Kiongozi, Aloyce Sekule na Ipilinga Panya na mawakili wake wengine waliojikita katika kujibu hoja zilizokuwa zikitolewa na wateja wao.

Aunt Ezekiel: Tununue Bongo Movie, Movie za Mbele Hazituhusu

$
0
0
Msanii wa Bongo movie aunt ezekiel amedai bongo movie bado ina uhai ila soko limedorora kidogo, lakini kudorora huko ni kutokana na watanzania kutopenda vitu vya kwao
Amesema ni bora kununua bongo movie kuliko kununua movie za nje ambazo haziwahusu na za kutafsiriwa

Kutana na Harmo Rapper Msanii Anayefanana na Harmonize na Kutumia Fursa Hiyo ipasavyo

$
0
0
Kutokana na kufanana huko amesema amejiingiza kwenye muziki na inamsaidia, hata wasichana mtaani anawang'oa sana kwa sababu ya mfanano huo na kuna label ya muziki imemchukua kutokana na mfanano wake

TEMBELEA Blog ya Tiba za Asili Kwa Maswala ya Tiba Asilia, Kusomewa Dua na Visomo, Kusafisha Nyota na Kumvuta Mpenzi

$
0
0
Tembelea  tovuti  pendwa  ya ASILI ZETU inayohusiana na masuala ya tiba asilia, kusomewa dua na visomo, kusafisha nyota,  kumvuta mume au mpenzi aliyekuacha, tiba ya magonjwa mbalimbali yaliyoshindikana,  mvuto wa biashara.

Pia tunatoa dawa za uzazi kwa wale kina mama wenye matatizo ya uzazi walio angaika kwa muda mrefu bila kupata mafanikio yoyote, kupandishwa cheo kazini, mali isiyohuzika kama vile kiwanja, shamba, nyumba, gari n,k.  Ingia HAPA

Ali Kiba Anavyoishi Mtaani Kwao: Majirani Wasema Haongei Nao na Anajificha

$
0
0
Majirani wa msanii Ali Kiba huko Tabata wamesema msanii huyo anaishi karibu nao lakini hawamuoni kwa kuwa kila akipita amefunga vioo tinted na wala hasalimii
Wamesema wanahisi kuwa anajificha ndio maana amekuwa kifanya hivyo, wamekuwa wakiona magari ya aina tofauti tofauti yakiingia anapokaa wala hawajui gari lake ni lipi..ila wamemsifu kwa muziki mzuri

Picha 8: Muonekano wa sasa wa Jennifer na Patrick walioibuliwa na marehemu Steven Kanumba

$
0
0
Watu wengi watawakumbuka Jennifer na Patrick kwa jinsi walivyoweza kutikisa tansia ya filamu Tanzania kipindi cha nyuma walipoibuliwa na marehemu Steven Kanumba.

Watoto hawa wawili walicheza kwa ustadi mkubwa katika filamu za Uncle JJ na This is It zote za marehemu Kanumba.

Kwa sasa Hanifa Daud ‘Jennifer’ na Othman Njaidi ‘Patrick’ si watoto tena. Wawili hawa hawajaonekana sana kwenye filamu baada ya Steven Kanumba aliyewatoa kufariki.

Jennifer ambaye amehitimu kidato cha nne mwaka jana mara ya mwisho alionekana kwenye filamu ya Zena na Betina ya Salma Jabu a.k.a Nisha mwaka 2014. Kwa upande wake Patrick, yeye alisema kuwa hana shauku ya kuigiza tena kama ilivyokuwa awali.

Zitto Kabwe Aitaka Serikali itangaze Baa la njaa

$
0
0
KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, ameitaka Serikali itangaze rasmi baa la njaa kwa mujibu wa sheria.

Zitto alitoa kauli hiyo jana katika mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea udiwani wa Kata ya Nkome mkoani Geita kupitia ACT-Wazalendo.

“Hali ya chakula nchini si nzuri. Wananchi mmeshuhudia namna bei za vyakula zinavyopanda kila siku. Bei ya sembe sasa kilo moja imefikia shilingi 1,600 pale Morogoro, kilo moja ya mchele ni shilingi 1,500, maana yake leo ugali na wali imekuwa bei inafanana. Gharama za maisha zitaendelea kupanda kutokana na uhaba wa chakula kuwa mkubwa.

“Kwanini hali ya chakula inazidi kuwa mbaya? Ni kwa sababu ya uamuzi mbovu wa Serikali kuhusu hifadhi ya chakula. Serikali zote zilizopita huko nyuma zilikuwa zinanunua chakula cha akiba ili wakati wa ukame kama sasa chakula hicho kiingie sokoni na hivyo kushusha bei na kuwezesha wananchi kumudu gharama za chakula.

“Rais wetu kawaambia wananchi wa Kagera kwamba Serikali haina shamba hivyo hakuna chakula cha njaa. Hii kauli si ya uongozi. Ni kauli ya kuficha uamuzi wa Serikali uliotusababisha kukosa akiba ya chakula,” alisema.

Zitto alisema Ghala la Taifa la Chakula (NFRA) lina tani 90,000 tu za chakula wakati kwa kipindi kama hiki mwaka juzi lilikuwa na tani 450,000.

Kwa mantiki hiyo, alisema chakula kilichopo kwa sasa ndani ya ghala hilo kinatosha kwa wiki moja kwa mujibu wa takwimu katika taarifa ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa mapitio ya uchumi ya Novemba, mwaka jana.

“Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dk. Charles Tizeba, alijibu hoja hizi kwa wepesi kabisa na kusema kwamba Tanzania ina chakula cha kutosha. Alipoulizwa ataje kiasi kilichopo NFRA, alijibu kwa sababu za kiusalama hawezi kutaja,” alisema.

Zitto alikwenda mbali kwa kumpongeza  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kwa kuamua yeye mwenyewe kutembelea NFRA na kujionea hali halisi.

Alisema alichokifanya Majaliwa ndio uongozi na si viongozi kukanusha habari ambazo ni za kweli na zilishathibitishwa na taasisi za Serikali kama BoT na alimtaka kuwachukulia hatua viongozi wa Serikali wanaoficha ukweli kuhusu baa la njaa.

“Waziri wa Kilimo anasema kama wananchi wanaona ugali ni ghali wale wali. Anasema kuna mchele mwingi nchini, lakini umeshikwa na watu binafsi. Waziri anataka kuwaambia Watanzania kuwa hivi sasa Serikali inategemea chakula cha watu binafsi ambao haijui idadi ya tani zilizopo kushughulika na suala la njaa.

“Hii ni ajabu kubwa sana, nchini Ufaransa alitokea mke wa mfalme mmoja. Wananchi walikuwa wanalalamika kuwa hakuna mikate. Malkia yule akiitwa Marie Antonnoite, alimwambia mumewe, hawa watu wako kama hawana mikate si wale keki? Hii ndio hali ya sasa nchini. Waziri anasema kama sembe imekuwa ghali, wananchi wale wali. Anasahau kuwa hata mchele umepanda bei. Maharage yamepanda bei na mafuta ya kupikia yamepanda bei,” alisema.

 Kauli ya Majaliwa

Katikati ya wiki hii, Majaliwa, akiwa mkoani Ruvuma alitoa agizo la kusisitiza kutunza chakula kwa kusema akiba ya mahindi iliyopo iendelee kutunzwa hadi msimu ujao wa mavuno.

Alitoa agizo hilo baada ya kukagua maghala ya nafaka yanayomilikiwa na NFRA Kanda ya Songea.

Alisema kawaida mwezi huu mvua za kutosha huwa zinanyesha na huwa kuna baridi lakini mwaka huu imekuwa tofauti kwa sababu kunashuhudia kuwapo joto kali.

“Kama mvua haijanyesha hadi leo ni lazima tuchukue tahadhari, hata mvua ikija hatujui itaendelea kunyesha hadi lini na kwa kiasi gani,” alisema.

Majaliwa aliwataka wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi wa halmashauri kutoa elimu kwa wananchi juu ya utunzaji wa akiba ya chakula.

Source: Mtanzania
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live




Latest Images