Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

Kwa Heri Obama,Lakini..!!!

$
0
0

ZIMESALIA siku nne tu Rais wa Marekani, Barack Obama, kung’atuka madarakani.


Rais huyo anatarajia kumkabidhi Ikulu ya Marekani Rais mteule, Donald Trump, Ijumaa wiki ijayo.

Kabla ya tukio hilo kufanyika hivi karibuni Rais Obama alitoa hotuba ya kuaga taifa hilo akiwa mjini Chicago, nchini humo.
Kama kawaida yake, aliongea kwa pozi, sentensi moja na nyingine zilitawaliwa na tuo, alivuta pumzi, akatuliza kichwa.
Midomo yake ilitamka maneno yanayowavuta wapigakura, wanasiasa, viongozi na zaidi kuvuta usikivu miongoni mwa wanajamii.

Obama alikuwa yuleyule wa mwaka 2004 alipotikisa nchi hiyo alipokuwa Seneta Illinois. Obama alikuwa yuleyule wa mwaka 2008 akiomba ridhaa ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Marekani.

Alikuwa Obama yuleyule jasiri na mwenye nguvu za hoja zilizomshinda John McCain wa Republican wakati wa midahalo ya kuwania urais. Alionyesha uimara wake wa kuivuta hadhira, maneno yake yalijaa hekima, kiunganishi na kujenga umoja.

Na pengine ndiyo desturi ya Chama cha Democrat kuunganisha wananchi na hata viongozi wa ulimwengu kuliko Republican wenye taswira kama ya Donald Trump, George W. Bush mkubwa na George W. Bush mtoto au kina Henry Kissinger na wengineo.

Ni Obama yuleyule aliyemshinda Mitt Romeny wa chama cha Republican mwaka 2012 katika kinyang’anyiro cha urais.

Alikuwa Obama aliyesimama imara, akajenga hoja, aliongea kama kiongozi thabiti na mwenye kufurahia maisha binafsi ya kifamilia, uongozi na jeuri ya kuzaliwa Marekani. Na huo ni upande wa mwonekano wa mhutubiaji katika kuwasiliana na hadhira yake.

Katika hotuba yake kulikuwa na mambo mengi ambayo tunaweza kuyagawa katika makundi ya vilio, furaha yenye kutia moyo, kusikitisha na mafunzo kadha wa kadha katika anga za masuala ya siasa ulimwenguni hususani uongozi na demokrasia.

Ni mafunzo ambayo yamekuwa adimu kutolewa kwa baadhi ya wanasiasa, lakini Obama amedhihirisha kuwa bado kinara wa kuhamasisha, kutia moyo, uwezo mkubwa wa ushawishi kwa wapigakura na zaidi anakuwa kiongozi wa kwanza wa Marekani mwenye asili ya Afrika kumaliza kipindi cha miaka 8 

madarakani. Obama anaondoka akiwa na rekodi mbalimbali za kiutendaji, ikiwemo mazuri na mabaya yake.
Mathalani kwenye hotuba yake alisema: “Baada ya miaka nane ya kuwa rais wenu, bado naamini kwamba na ieleweke si suala la imani pekee bali mapigo ya mioyo yetu Wamarekani, tumekumbatia uzoefu na mtindo wetu wa kuunda Serikali ya kipekee kila mara.”

Nini tafsiri ya nukuu tuliyochukua? Ni dhahiri Obama anathibitisha kuwa muundo wa Serikali na sera za Marekani zimekuwa za kipekee na dunia imeshuhudia yote hayo.

Katika upande wa furaha Marekani imeleta mambo mengi yenye kuheshimika kuanzia viunga vya Umoja wa Mataifa, hisa zake katika Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani ni miongoni mwa mashirika makubwa ambayo yamekuwa yakitumiwa na mataifa mbalimbali kujipatia mikopo.

Aidha, muundo wa kipekee wa Marekani ni pamoja na kuileta dunia katika ardhi yao. Wanaweza kuweka mikakati katika masuala ya ulinzi, kulinda masilahi yao, kushikamana na mataifa rafiki na hata kuwa tayari kupambana kwa silaha za moto ili kuhakikisha masilahi yao yanakuwa kwenye mikono sana.

Anadhihirisha kuwa nchi yao imekuwa kwenye mkondo wa kuendesha mambo inayoyataka kwa wengine bila bughudha na kuhakikisha mawazo yao ya Kimarekani yanatawala dunia.

Hakuna biashara kubwa ambayo Marekani inafanya kama kuuza mawazo yake. Biashara hii imekuwa muhimu na ndio msingi wa sera mbalimbali, tangu ilipoiga hayo kutoka kwa wakoloni wa jamii za Ulaya hususani Uingereza. Tukumbuke pia jamii za Uingereza nazo zilijikita kwa jamii za Italia.

Sehemu nyingine anasema: “Kwa miaka 240, suala la ukazi wa wananchi katika taifa letu limetupatia kazi na umuhimu wa kukiachia mafunzo kizazi kimoja hadi kingine. Ni hicho kinachotuongoza, ni uzalendo wetu tuliochagua kama taifa, kuanzia chipukizi hadi wakongwe, toka zama za utumwa hadi ushujaa wa kutengeneza reli ya mafanikio ya nchi.”

Tafsiri ya nukuu hiyo ni kwamba, utaifa wa Marekani umeundwa Kimarekani, ndio maana katika mitaala ya elimu hapa nchini tuliwahi kufunzwa juu ya ubeberu wa Kimarekani (America Capitalism) ambayo ilielezwa kuwa tofauti na ubeberu wa Uingereza (British Capitalism). Sababu kubwa ni moja; Marekani walitafuta uhuru wao, wakatengeneza mawazo yao, wakayauza kote duniani.

Kisha wakabuni silaha na vita kama bidhaa muhimu kwenye soko la biashara. Maeneo mengi ambayo Wamarekani wapo yanakuwa na bidhaa mbili kuu; silaha na vita.

Kwa wataalamu wa masuala ya siasa ya kimataifa wanaelewa ninachosema kuwa silaha na vita ni miongoni mwa bidhaa muhimu mno kwenye mafanikio ya nchi kama Marekani.

Mifumo yao ya uchaguzi ya kura za moja kwa moja za wananchi (Electoral Vote) na kura za wajumbe wa majimbo (Electoral College) ni wa kipekee ambapo iwapo mgombea hajapata kura nyingi za wajumbe anaangushwa hata kama alipata kura nyingi za wananchi.

Ni mfumo wa kipekee wa Kimarekani, ndiyo ufahari wa Obama anaozungumzia kwenye hotuba yake juu ya miaka 240 ya fikra za Kimarekani.

Aidha, tumejionea vilio ambavyo Obama anaviacha duniani. Obama anaondoka akiwa hajatatua suala la Afghanistan. Anaondoka akiwa Marekani hajatatua suala la Irak.

Obama anaondoka akiwa ameshindwa kukamilisha mradi wa kuwakabidhi wapinzani wa Rais Bashar Al Assad wa Syria. Katika mgogoro wa Syria tumeshuhudia malumbano makali baina ya Urusi na Marekani, lakini mwishowe Obama akaweka ‘silaha’ chini na kumwacha Vladimir Putin akiibuka mshindi.

Obama anaondoka akiwa ameacha wingu la jeuri huko Libya, ambapo Serikali yake ilishirikiana na majeshi ya Kujihami ya Nchi za Magharibi (NATO) kumwangusha Rais Muammar Gaddafi.

Katika kipindi hicho, Obama alikaribia kuvunja sheria za nchi badala ya kusubiri kuidhinishiwa jeshi la kwenda vitani kwa siku 60 kutoka bungeni, lakini alikuwa tayari kuivunja.

Obama anaondoka katika kiti chake akiacha kilio cha Ukraine, ambao wametibuana na jirani yake Urusi kutokana na sakata la Jimbo la Crimea. Tumeshuhudia mapigano baina ya Ukraine na Urusi ambapo jimbo la Crimea lilitaka kujiunga na kuwa sehemu ya Shirikisho la Urusi kuliko kuwa sehemu ya Ukraine.

Obama ametuliza tu mgogoro wa silaha za nyuklia baina ya Iran na Marekani pamoja na nchi za Magharibi. Mgogoro wa Georgia uliolipuka zaidi Agosti mwaka 2008 dhidi ya Urusi haijamalizika.

Migogoro ambayo hajaimaliza licha ya kuingilia kati ni baina ya Israel na mataifa ya Asia hususani Iran, Irak, Mamlaka ya Palestina na Lebanon kwa kuzitaja chache. Ni mambo muhimu ambayo hakupaswa kuyaweka kiporo.

Na sifa kuu ya mwisho ya Marekani itakuwa kumkabidhi madaraka, Donald Trump kwa amani, tofauti na Yahya Jammeh wa Gambia anavyoshindwa kutekeleza matakwa ya kisheria kumkabidhi Adama Barrow. Lakini je, ufahari wa Obama kiuongozi na chozi lake juu ya hali ya Libya ni furaha au kilio?

Kama Unabisha Shauri yako: Miaka 10 ya Ustaa na Jinsi Wema Alivyotoboa Kimafanikio..!!!

$
0
0

SHINDANO lenye umri wa miongo miwili na tayari limeshatoa warembo kibao, lakini ukweli usio na shaka ni lile shindano la mwaka 2006 lililokuwa na mvuto wenye ladha iliyobeba msisimko wa kipekee.


Ni fainali zilizompa Wema Sepetu heshima ya kuwa Miss Tanzania. Lakini pia ni mwaka ambao umewatoa mastaa wengi wa Bongo. Mbali na Wema, wapo Jokate Mwegelo, Lisa Jensen na Irene Uwoya.

Kipimo cha ukubwa wa jina na hadhi yake unaweza kupimwa kwa mambo mengi ila wingi wa mashabiki wanaomfuata katika mitandao ya kijamii inaweza kuwa ni kipimo sahihi.

Instagram pekee ana watu zaidi ya Milioni 2.5 idadi ambayo hakuna staa yeyote wa kike Bongo ameifikia.

Katika kipindi hiki cha miaka kumi ya ustaa wa Wema, amefanya mengi makubwa na ya kujivunia. Ukiacha kutunza ustaa wake, jambo ambalo wengi wameshindwa, hapa chini Swaggaz inakuchambulia mafanikio yake akiwa staa wa Bongo katika fani mbalimbali ndani na nje ya urembo.

 FILAMU

Baada ya kupata ushindi mnono kutoka kwenye shindano la Miss Tanzania, Wema Sepetu aliitazama fursa iliyopo kwenye kiwanda cha filamu Bongo.

Kipaji kilichomuwezesha kuvaa uhusika wa kile kilichopo kwenye script kiliifanya Kampuni ya Game 1st Quality ya jijini Dar es Salaam, ikampa nafasi ya kucheza filamu yake ya kwanza iitwayo A Point of No Return, ambapo mhusika mkuu alikuwa ni marehemu Steven Kanumba, hiyo ilikuwa mwaka 2007.

Kazi hiyo ilimtambulisha vyema kwenye ulimwengu wa filamu. Zikafuata nyingine kama Family Tears (2008) Red Valentine, White Maria na nyinginezo zilizotolewa na Game, chini ya Mtitu Game.
 
Baadaye wadau wengine wakamshirikisha kwenye sinema zao, akiwemo staa wa Bongo Muvi, Jacob Stephen ‘JB’ kwenye 14 Days, Dj Ben, Chungu cha Tatu, Lerato, Basilisa, House Boy, It Was Not Me, Mapenzi Yamerogwa, Saa Mbovu na nyingine nyingi.

Idadi ya sinema alizoshiriki ni kubwa na kwa sehemu kubwa amefanya vizuri, akishirikiana na washiriki wengine, ambapo mara nyingi hucheza kama mhusika mkuu au mhusika mkuu msaidizi.

 AZINDUA ENDLESS FAME FILMS

Hakuishia kucheza filamu za watu pekee, bali alikuwa na kiu kubwa ya kuzalisha filamu zake mwenyewe.

Februari, 2013 mrembo huyu alifungua Kampuni ya Endless Fame Films, akiwa na dhumuni la kuzalisha filamu zake na za wasanii wenzake, kuibua na kukuza vipaji vipya na kuongeza ubora kwenye kazi za sanaa kwa ujumla.

Kupitia kampuni hiyo aliweza kulitikisa soko la filamu pale alipoachia filamu yake ya kwanza iitwayo Madame.

Filamu hiyo ilimpa nguvu ya kuvuka mipaka ya Tanzania na kutua Accra, Ghana kukutana na staa wa filamu mwenye heshima kubwa Afrika, Van Vicker.

Lengo la kumsaka Van Vicker ni kulitanua soko la filamu Tanzania hasa pale filamu yao inayoitwa Day After Death itakapoingia kitaa.

Hakuishia kwenye filamu pekee bali amewahi kumiliki wasanii wa Bongo Fleva, Mirror na Jordan waliokuwa wanaunda Kundi la Danger Vuu lililokuwa linapewa sapoti na marehemu Albert Mangwea.

‘IN MY SHOES’ YAMPA HESHIMA

Mwaka 2014  ulikuwa na neema kwake kwani aliamua kuweka hadharani kila hatua anayoipiga kwenye maisha yake. Alimua kutuletea In My Shoes, kipindi cha runinga kinachoonyesha maisha yake kama staa.

Watu wengi walipata kumfahamu zaidi na kiukweli alijiweka karibu zaidi na mashabiki hasa wale ambao walikuwa wanapenda kazi zake.

 ‘KISS BY WEMA’ NI BALAA KITAA

Wema si mwepesi wa kukubali kushindwa licha ya ukweli kwamba maadui anao wa kutosha, Novemba Mosi, 2015 kwa mara nyingine alionyesha jinsi anavyoweza kunyumbulika, hapa sasa alitutupa kwenye ujasiriamali.

Aliingiza mzigo wa lip stick zenye jina la ‘Kiss by Wema’ na kwa muda mfupi zilisambaa kitaa kufuatiwa kugombaniwa na warembo wenye mapenzi ya dhati na mnyange huyu.

AJISONGEZA ZAIDI KWA MASHABIKI

Mei 22, mwaka jana alijiongeza kibiashara ili kuwa karibu na mashabiki ambao mara kwa mara wamekuwa wakipokea taarifa zilizopotoshwa juu yake.

Akawaletea mashabiki huduma ya kupata habari zake kupitia simu za mkinoni inayoitwa ‘Wema Sepetu Mobile Application’.

MAFANIKIO NI YAKE

Hivi sasa ana miaka kumi kwenye tasnia ya burudani. Hakuna aliyeweza kuvunja rekodi ya kuubeba ustaa kwa muda wote huo bila kupungua.

Kwa maana hiyo, Wema bado ana nafasi kubwa ya kuendelea kutengeneza fedha zitakazomfanya aishi kistaa kulingana na hadhi yake ilivyo.

Bado ana nafasi zaidi, ni suala la ubunifu zaidi na kutambua thamani yake kama staa mwenye heshima Bongo. Kazi ni kwake.

Wiki ijayo tutawaletea maoni ya wadau mbalimbali wa sanaa Bongo, wanavyozungumzia mafanikio yake.

Zlatan Aaanza Kuipa Masharti Man United

$
0
0

Wakati United  ikijianda kuivaa Liverpool leo saa moja jioni, mshambuliaji wake mwenye maajabu Ibra Magic raia wa Sweden Zlatan Ibrahimovic amesisitiza kuwa Manchester United bado inaweza kutwaa ubingwa Ligi Kuu Uingereza msimu huu. 


Man United imehaha kuendeleza kiwango bora katika hatua za awali msimu huu, lakini mashetani hao wekundu wameshinda mechi tisa mfululizo katika michuano yote, sita zikiwa ni Ligi Kuu.

Kikosi hicho cha Jose Mourinho bado kipo katika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi lakini wamepunguza pengo la pointi dhidi ya vinara Chelsea hadi kufika pointi 10 na Ibrahimovic anaamini timu yake inaweza kupambana kutwaa ubingwa wa ligi iwapo wataifunga Liverpool katika uwanja wa Old Trafford siku ya leo.

"Ligi haitabiriki. Hakuna timu ambayo unaweza kusema itashinda na ikafanya hivyo," Ibrahimovic alikiambia Sky Sports News. "Chelsea imekuwa ikifanya vizuri, wanacheza mara moja kwa wiki, wana hali nzuri na nguvu nyingi kila wanapocheza, lakini walikuwa na wakati mgumu mwanzoni lakini walizinduka.

"Kama tutapanda pale na kuwasumbua, kila timu ina kipindi chake cha mafanikio. tumekuwa na wakati mzuri, tukishinda, tukipoteza na sasa tunashinda tena. Natumai tutaendelea hivyo na tunasubiri wengine wafanye makosa.

Mhh: Kwa Mipango Hii ya Joti Kwa Mwaka Huu Asipokuwa Bilionea ,Hata Fanikiwa Tena

$
0
0
UKUMUANGALIA tu lazima ucheke kwani ni kipaji na sio ngekewa, amefanikiwa kuteka watoto, vijana, watu wazima na wazee hiyo yote ni kutokana na kuigiza nyanja zote tena bila wasiwasi wowote ule, Lucas Mhavile maarufu Joti alitamba na Original Comedy kundi ambalo lilitoa burudani kwa muda wa miaka 11 bila kuwa na mpinzani katika angaza za uchekeshaji wenye mafundisho.


Kwa sasa kampuni yao imepumzika na kila mmoja kufanya shughuli zake ili  kutoa fursa kwa vizazi vipya kuonyesha kazi zao,  Kwa upande wake Joti ameamua kutumia mapumziko yake kwa kuanzisha Yotube Tv akiamini sasa hivi dunia iko kwenye kiganja.

“Nimeamua kuanzisha Yotube Tv kwa sababu dunia iko kwenye kiganja watu wanakosa muda wa kuangalia Tv, ila akiwa na simu yake ya mkononi anawez kuona chochote kile anachotaka hata kama ni saa sita usiku akiwa kitandani uwezo wa kumuangalia Joti upo.”

Tv  hiyo imelenga nyanja zote na imeangalia sana watoto kwa sababu kitu akikipenda mtoto basi na mzazi atakipenda, pia kutoa elimu kwa watoto katika uchekeshaji wangu huo nitatoa elimu  kwa watoto na mambo mengine mengi makubwa ya watoto yanakuja.

Watoto ni watu ambao wanaupendo wa kweli hawana unafiki na ndio vipaji ambavyo vinatakiwa kuendeleza kwa kuliona hilo nikaona hamna haja ya kuacha vipaji vyenye upendo wa kweli vipotee ni bora niwe navyo bega kwa bega.

“Licha ya kuegemea zaidi katika vipindi vya watoto, nitakuwa na vipindi vya watu wa rika zote pia nitatoa ajira kwa  vijana wenzangu kwa sababu sita weza kufanya kazi peke yangu.

Hata hivyo Joti alifafanua kuwa Chaneli yake itahusika na shughuli zake pekee mtu asitegemee kuona taarifa za habari na mambo mengine kama chanel za watu wengine.

Aidha Joti alisema kuna wachekeshaji wengi chipukizi wanafanya vizuri ila hawataki ushauri, wala hawana mtu waliyempenda ili kuingia katika hiyo kazi hili nitatizo na mtu kuwa staa lazima uwe na historia huwezi kukurupuka na kuwa staa.

“Mimi nimepitia analogi na digital na nimejua vitu vingi  kwa kuwa nilipitia kote ninauwezo wa kuutunza ustaa wangu hata miaka 15 ijayo kwa sababu najua kwenda na wakati, tatizo liko kwa vijana wanaochipukia wanataka kuwa Digital tu, pia hawana historia, hawashauriki ndipo tunapowaangalia na kwa sababu najua vurugu zake zote lazima akutane na ukuta na mimi simu yangu iko wazi muda wowote kwa anayetaka ushauri kutoka kwangu.”

Sikufahamu kama ninakipaji ila King Majuto ndio sababu amenipotezea sana muda, na amekula sana hela zangu wakati huo nilikuwa nikiona kuna onyesho lake shuleni basi lazma niingie, pia kumuangalia kwenye tv, lazima nipoteze muda kumuangalia hadi linikuwa nikipigwa sana na wazazi wangu kumbe ni kitu ambacho nilikuwa nakuja kukifanya ndio maana nilikuwa nakifuatilia sana ila bila kujua kama nitakuja kuwa mchekeshaji.

“Napita kwenye ugumu mwingi sana, kwa sababu unaweza ukapita sehemu mtu mmoja akakuomba kupiga picha ukakubali basi wataibuka wengine hapo hata 30 na huwezi kukataa ukikataa hata kama unachelewa utasikia wanasema supa staa Bongo neno ambalo naliogopa sana katika maisha yangu kwani hao wanaosema hivyo ndiyo mashabiki wangu wa wanaweza kunipandisha au kunishusha.’

“Mimi nimepitia analogi na digital na nimejua vitu vingi  kwa kuwa nilipitia kote ninauwezo wa kuutunza ustaa wangu hata miaka 15 ijayo kwa sababu najua kwenda na wakati, tatizo liko kwa vijana wanaochipukia wanataka kuwa Digital tu, pia hawana historia, hawashauriki ndipo tunapowaangalia na kwa sababu najua vurugu zake zote lazima akutane na ukuta na mimi simu yangu iko wazi muda wowote kwa anayetaka ushauri kutoka kwangu.”

Sikufahamu kama ninakipaji ila King Majuto ndio sababu amenipotezea sana muda, na amekula sana hela zangu wakati huo nilikuwa nikiona kuna onyesho lake shuleni basi lazma niingie, pia kumuangalia kwenye tv, lazima nipoteze muda kumuangalia hadi linikuwa nikipigwa sana na wazazi wangu kumbe ni kitu ambacho nilikuwa nakuja kukifanya ndio maana nilikuwa nakifuatilia sana ila bila kujua kama nitakuja kuwa mchekeshaji.

Alichokiandika Idris Sultan kwa Diamond na Watanzania Kwa Ujumla Kuhusu AFCON

$
0
0
Mtanzania Diamond platnumz alipata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania kwenye upande wa burudani kwenye ufunguzi wa mashindano ya AFCON ambapo alikabidhiwa bendera ya Tanzania na Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo, Nape Nnauye.

Baada ya hapo kulikuwa na maoni tofauti pamoja na maswali kwanini amepewa bendera ile. Idris Sultani ametumia ukurasa wake wa Instagram kumpongeza Diamond kwa kuiwakilisha nchi vizuri huku akiwasii watanzania kusupport wasanii wa nyumbani kwani wanapopata nafasi kama hizi ni dhahiri kuwa Tanzania inazidi kujulikana.

‘Sometimes watanzania tunasahau kama Mond anavyokula ruti, Idris anavyokula ruti, Vanessa Mdee anavyokula ruti huwa inamaanisha Tanzania imeenda mbali na yoyote kati ya watanzania anakua amefunguliwa ile njia’.-Idris Sultan
‘This is 2017 tukiacha kushushana na kulogana labda tunaweza kuwa mbali sana, na kimoja ambacho tunadharau sana ni Kiingereza na tunakua na maneno kama mbona wachina hawaongei ila wameendelea’Idris Sultan
‘(Niambie vifaa vitano unavyovijua vinavyotengenezwa Tanzania maana hata toothpick tu tunaagiza). WE NEED TO LEARN ENGLISH WE HAVE NO WAY OUT. As for Diamond mi na wewe tunaongea na kuzinguana daily ila hata tutaniane vipi siwezi kusahau kukupa your credit nikaenda kukupea kwenye simu (unaponipigaga mabango) ’-Idris Sultan

Nakupa hapa ili na wewe uache kunipaga hongera kwenye simu 😂 haya great show na Tanzania is well represented ningekuita Simba ila utashindwa kunywa juisi za Azam na ukirudi waelezee kwanini upewe bendera ya kupeperusha we ukashonee sare za madensa wako  #ThatIsKrezi –Idris Sultan

Lowassa - Kama Rais Hataki Kutoa Chakula ,Chadema Tutaoa Chakula kwa Wenye Njaa...!!!

$
0
0

Mjumbe wa kamati kuu Chadema, Mhe Edward Lowassa akiwa na mbunge wa Bukoba mjini wameudhuria ibada katika kanisa la KKKT. Akiwa kanisani Mhe Lowassa ametoa kauli.


''Mh rais amesema hatatoa chakula. Mimi nimewasiliana na chama changu tumeona tuwape chakula watanzania. Naamini dunia itasikia'', alisema Lowassa.

Uuuwii: Umemuona Mama Diamond Akiwa Amevaa Kimini na Kutembea Kimiss?Tazama Hapa Video Livee..!!!

$
0
0

Mama Diamond leo kupitia ukurasa wake wa Instagram amuonesha hawavumi lkn wamo ,ni baada ya kutupia kijivideo flan hivi amaiziiiiiiing ambapo mwenye anaonekana ametupia kiblauzi kimoja matata na juu akaweka kisweta flan hivi chepesi huku akiwa amevaa kimini watoto wa mjini wanaita full kipupwe huku akitembea mwendo wa kimiss.

Mashabiki wa mama huyo kizaa chema kama kawaida yao waliruka kwenye page ya Lundenga nakumtaka awe makini linapokuja suala miss Tanzania maana kuna watu wanaweza kutufikisha mbali kama taifa kwenye mashindano hayo

MO Dewji Akanusha Kuzungumza Kuhusu Pesa za Tetemeko la Ardhi Kagera

$
0
0

MO Dewji akanusha kuzungumza kuhusu pesa za tetemeko la ardhi Kagera

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji amekanusha taarifa ambazo zimesambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa amefanya mahojiano na kituo cha Redio cha Times FM kuhusu pesa zilizochangishwa katika Tetemeko la Ardhi la Kagera lililotokea mwezi Septemba, 2016.

 

Dewji amesema hajafanya mahojiano na kituo chochote cha habari kuhusu tetemeko la Kagera na habari hiyo haina ukweli wowote zaidi ni mbinu ambayo imetumiwa na baadhi ya watu kwa ajili ya kuchafua jina lake na kampuni yake ya MeTL Group ambayo mpaka sasa ina wafanyakazi zaidi ya watu 28,000.

 

Aidha Dewji amesema ana imani na Serikali ya awamu ya tano na kuwatoa hofu Watanzania kuwa ataendelea kushirikiana na Serikali kusaidia jamii yenye uhitaji ikiwa ni sehemu ya ahadi yake ya kutumia nusu ya utajiri wake kusaidia watu wenye uhitaji.

 

“Nitumie nafasi hii kuwajulisha Watanzania wenzangu kuwa hii habari ambayo inasambazwa na watu katika mitandao ni ya uongo na haina ukweli wowote, sijafanya mazungumzo na media yoyote na mimi nilichangia pesa kwa nia nzuri, nina imani na Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli kuwa inafanya kazi kwa faida ya watu wote bila kufanya ubaguzi,” amesema Dewji.

 

Katika ujumbe ambao unaonekana kusambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwepo Facebook, Instagram na WhatsApp imeandikwa kuwa MO Dewji amefanya mahojiano na Redio Times FM na kusema kama angejua mapema kuwa wahanga hawatopatiwa pesa hizo asingechangia

Tazama Video Highlight ya Magoli Wakati Man City Ilivyochezea Kichapo cha Goli 4-0 Kutoka kwa Everton...!!!

$
0
0

Leo Klabu ya Man City imekiona cha mtema kuni mara baada ya kucharazwa goli 4-0 na klabu ya Everton katika muendelezo wa ligi kuu soka Uingereza .

Chini ni video ya magoli ya mchezo huo ,unaweza kutazama

Zitto Atoa Tamko la Kumsulubisha Rais Magufuli Bungeni,Ampa Onyo Juu ya Njaa..!!!

$
0
0

Watanzania wakifa njaa tutamwajibisha Rais kwa mujibu wa Katiba ibara ya 46A
(Sehemu ya Hotuba ya Kiongozi wa Chama katika Mkutano wa Kampeni za Udiwani - Kijichi) 15/1/2017


Pamoja na masuala haya ya uchaguzi mdogo hapa Kijichi ninaomba nizungumzie masuala machache ya kitaifa. Nafanya hivi kwa sababu baada ya siku saba hatutakuwa tena na nafasi ya kuzungumza majukwaani kama viongozi wa vyama vya siasa kwa sababu ya zuio lisilo la kikatiba ambalo limewekwa na Rais dhidi ya mikutano ya hadhara. Hivyo, sisi tuliamua kutumia majukwaa haya ya kampeni za uchaguzi mdogo kuzungumzia mambo ya kitaifa pia. Hatujui chaguzi ndogo nyengine zitakuja lini.

Tulitumia mikutano hii ya kampeni kuelezea hatari ya njaa ambayo inaikabili nchi yetu hivi sasa. Nikiwa katika kata ya Kiwanja cha Ndege, Manispaa ya Morogoro nilieleza kuhusu kupanda kwa bei za vyakula na kiwango kidogo cha akiba ya chakula kwenye maghala ya Taifa (NFRA).

Tunashukuru kwamba suala hili limekuwa ni ajenda ya Taifa hivi sasa na tunawapongeza sana viongozi wetu wa dini kwa kutoa matamko ya kuhamasisha watanzania kuliombea Taifa kuepukana na adha ya njaa. Viongozi wa dini wameonyesha utu na uwezo mkubwa wa uongozi wa kutafuta jawabu la mwenyezi mungu kuhusu adha hii.

Serikali kupitia kwa Rais imewaambia watanzania kuwa hali ni shwari kabisa na kwamba Serikali haitatoa chakula cha msaada kwa sababu "Mzee Bure" ameshatoka madarakani. Lakini Rais pia alituhumu wanasiasa na wafanyabiashara kwamba ndio wanachochea hali ya njaa kwa kupitia vyombo vya habari kadhaa. Na akaenda mbali zaidi kwa kufikia hatua ya kutisha vyombo vya habari na kusema siku zao zinahesabika, kosa lao kubwa likiwa ni kuandika yale ambayo yeye hayapendi.

Sisi ACT Wazalendo tunamsihi Rais awe msikivu. Hii ni nchi ya kidemokrasia na watu wana uhuru wa mawazo. Haiwezekani kila mwenye mawazo tofauti awe ni mtu anayehongwa au mpiga dili. Kazi yetu sisi kama chama cha upinzani ni pamoja na kuikosoa Serikali iliyopo madarakani na kuonyesha sera mbadala kwa wananchi.

Tutaendelea kuichokonoa Serikali mpaka ianguke, maana ndio kazi yetu ili kuondoa sera mbovu zilizopo na kuweka sera bora.
Tumesema hili la njaa katika kutekeleza wajibu wetu, Rais na Serikali wamejibu na kufunga mjadala. Wakati utaamua na kuonyesha mkweli nani na mpiga propaganda nani.

Jambo moja ni muhimu sana, Rais anapaswa kujua kuwa anafanya kazi kwa mujibu wa Katiba ya nchi. Na Katiba imetoa wajibu wa lazima kwa Serikali kulinda watu. Ndio kazi ya Serikali – kulinda wananchi pale ambapo yanatokea majanga ambayo yanazidi kimo wananchi hao.

Tunamwambia Rais kwamba, Mtanzania yeyote akifa kwa njaa kwa sababu Serikali imeshindwa kutekeleza wajibu wake Watanzania tutapaswa kuchukua hatua, Katiba inatulazimisha kumtoa Rais madarakani ikiwa yeye na Serikali yake watashindwa kutimiza wajibu wake wa kulinda uhai wa raia wake.

Tunamkumbusha Rais kuwa yeye sio mungu mtu. Yupo chini ya Katiba na kwa idadi ya wabunge wa upinzani waliopo Bungeni, na wakiamua kusimama na wananchi na kulinda Katiba, Rais wa sasa atakuwa Rais wa kwanza wa nchi yetu kutolewa hoja ya kutokuwa na imani naye bungeni. Katiba inahitaji asilimia 20 tu ya wabunge kuwasilisha hoja hiyo bungeni.

Ninatoa wito kwa Watanzania wote nchini, bila kujali vyama vyao, kuweka rekodi ya hali ya chakula popote walipo na kuweka takwimu ya maafa yeyote yanayotokana na njaa. Mtanzania yeyote akifa kwa njaa ni lazima tuchukue jukumu la kumwajibisha Rais kwa kusema waziwazi kwamba hajatimiza wajibu wake kama Mkuu wa Serikali kulinda wananchi wake.

Tunamkumbusha Rais kwamba kwa mujibu wa ibara ya 46A ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo yeye amekula kiapo kuilinda, kuihifadhi na kuitetea, Bunge laweza kumshataki yeye Rais kwa kosa la mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais.

Wananchi wanaona lugha za ubabe, vitisho, kuonea watu, kudhihaki waliopatwa na majanga kwamba ni mambo yanayodhalilisha kiti cha Rais. Hivyo Rais achague maneno ya kusema mbele ya wananchi wake, atumie lugha ya kujenga matumaini badala ya kujenga hofu kwenye jamii, aache kuonea watu kwa kutumia madaraka yake, na akumbuke cheo ni dhamana.

Tunayasema haya kwa Uzalendo mkubwa kwa nchi, sisi kama chama, ACT Wazalendo, tulimwunga mkono Rais toka mwanzo wa utawala wake na kumkabidhi Ilani ya uchaguzi ya chama chetu kama ishara ya kwamba uchaguzi umekwisha na sasa tujenge nchi yetu. Hatujutii kumwunga mkono kwa sababu kuna mambo mazuri amefanya kuhusu nchi yetu.

Rais amefanya kazi nzuri ya kupambana na rushwa na ufisadi nchini. ameondoa hali ya ‘impunity’ iliyokuwa imeshika mizizi nchini. Hatua kubwa alizochukua za kuwajibisha watendaji na Waziri aliyekiuka maadili ya kazi tunaziunga mkono.

Hata hivyo, nchi huendeshwa kwa zaidi ya kutumbua majipu. Kuna uchumi unapaswa kuendeshwa ili watu waweze kujenga maisha yao. Rais anaelekea kushindwa kwenye eneo hili la 'Menejimenti' ya Uchumi kutokana na matamko yake ambayo yanakimbiza uwekezaji na hata mahusiano yetu na mataifa mengine duniani.

Rais bado anahutubia kana kwamba bado tupo kwenye kampeni. Huu ni mwaka 2017, ni muhimu, ajielekeze katika kujenga uchumi wetu ili kutengeneza ajira kwa wananchi wake.

Vile vile, sisi tunaona Rais anahangaika na majipu madogo na kuacha majipu makubwa yanayoathiri uchumi wetu na kupoteza fedha nyingi sana za nchi yetu. Kwa mfano, Rais ameacha kabisa kushughulika na ufisadi mkubwa wa IPTL ambapo kila mwezi TANESCO inalipa shilingi bilioni 8 kwa kampuni ya kitapeli ya PAP. Moja ya sababu za TANESCO kutaka kupandisha bei ya umeme ni kwa ajili ya kupata fedha za kulipa PAP.

Rais amemfukuza kazi Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO akijua kuwa Mkurugenzi huyo alikuwa anatekeleza mpango wa Serikali. Barua ya Waziri wa Nishati na Madini kwenda kwa Waziri wa Fedha kuhusu kupandisha bei ya Umeme imenukuliwa kwa Rais. Hivyo Rais alikuwa anajua kuwa bei ya umeme itapanda na Serikali imeijulisha hivyo IMF katika barua yake ya Disemba 20, 2016, siku 10 kabla ya Tamko la EWURA la kupandisha bei ya umeme.

Jambo hili kubwa la IPTL ambalo lilihusisha mabilioni ya fedha kuchotwa Benki Kuu Rais analiacha na hataki kabisa kulizungumzia, maana yake ni kwamba Rais anaogopa wakubwa na kuonea wadogo, amemtumbua Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO kwa sababu tu EWURA imetangaza bei mpya ya umeme ambayo Serikali yenyewe iliagiza kupandishwa toka mwezi Septemba mwaka 2016.

Lakini Rais huyu huyu anaendelea kutetea mkataba unaowalipa matapeli shilingi bilioni 8 kila mwezi. Rais wa wanyonge anawalinda matapeli wanaoiba fedha za umma.

Lingine ambalo Rais anaonyesha woga kwa wakubwa ni lile la mkopo wa Hati Fungani kutoka Benki ya Standard ya Uingereza. Serikali ilikopa dola milioni 600 mwaka 2013 kwa ajili ya miradi ya maendeleo. Licha ya mkopo ule kugubikwa na ufisadi katika upatikanaji wake, Serikali imeanza kuulipa na deni litakapokwisha baada ya miaka 6 itakuwa imelipa dola milioni 983.

Lakini sheria zote za kimataifa zinaibeba Tanzania kwamba kama mkataba na kampuni za kimataifa umepatikana kwa rushwa, nchi inaweza kukataa kulipa deni. Niliiambia serikali Bungeni kuhusu jambo hili na nimepeleka maswali kama manne bungeni kuhusu jambo hili lakini Serikali inaogopa hata kujibu maswali husika. Kwa sababu gani? Serikali inaogopa makampuni ya kigeni.

Najua kuna kesi mahakamani na sitaki kuingilia kesi hiyo. Lakini hiyo kesi iliyopo mahakamani na hao waliopo rumande ndio wangekuwa mashahidi wa Serikali kwamba Benki ya Standard ya Uingereza ilitoa rushwa kupata biashara nchini na hivyo Serikali ingeishitaki Benki hiyo na kukataa kulipa mkopo huo. Rais na Serikali yake hata kujibu maswali ya bunge wanaogopa. Sisi tunamtaka Rais ahangaike na mambo haya makubwa na aachane na watu wadogo. Rais ni mtu kubwa sana na akitumia ujasiri wake vizuri anaweza kuokoa nchi dhidi ya deni kubwa la kifisadi la Standard Bank ya Uingereza.

Lingine nataka kuongea nanyi ni suala la Bajeti ya Serikali na Utekelezwaji wake. Serikali ilileta Bungeni Bajeti ya matumizi ya shilingi 29.5 trilioni mwaka 2016/17. Katika hiyo, ilitarajia kupata mikopo na misaada kutoka nje pamoja na mikopo ya kibiashara ya shilingi 5.7 trilioni. Kutokana na mahusiano mabaya kati ya Serikali na nchi marafiki, mpaka sasa nusu ya mwaka wa Bajeti imekatika na Serikali haijaweza kupata hata thumni katika matarajio hayo. Vile vile Serikali imeanza kukusanya chini ya matarajio kwenye kodi na mapato yasiyo ya kikodi.

Miradi ya Maendeleo imechelewa kutekelezwa kwa sababu Serikali inafanya kazi ya kulipa mishahara na kulipa madeni tu. Ndio maana miradi mingi inayozinduliwa hivi sasa hakuna mradi mpya bali ni miradi iliyoachwa na Serikali ya Awamu ya Nne. Serikali hii inahitaji kurekebisha mahusiano yake na nchi marafiki zetu ili uchumi wetu usisimame. Masuala haya Rais hawezi kuambiwa na Mawaziri wake kwa sababu amejenga hulka ya kuogopwa. Sisi wa Upinzani ni lazima tumwambie maana ni wajibu wetu.

Katika Barua (letter of intent) ambayo Waziri wa Fedha na Gavana wa Benki Kuu wameandika kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Serikali inasema inataka kukopa mikopo ya kibiashara (syndicated loans and Eurobond) ili kupata fedha. Hata hivyo Mabanki ya Dunia yanataka kujua 'Credit Rating' ya Serikali yetu.

Hiyo pekee itachukua miezi mingi iwapo mfumo wa kawaida wa zabuni utapaswa kufuatwa. Hata hivyo IMF wameiambia Serikali kuwa soko la mikopo ya dunia hivi sasa ni baya maana Serikali itakopa kwa gharama kubwa, mpaka riba ya 9% kwenye fedha za kigeni.

Serikali inataka kuiingiza nchini kwenye madeni ghali kwa sababu tu ya kutaka kufanikisha Bajeti isiyotekelezeka, iliyotungwa kwa sifa bila kuzingatia uhalisia wa nchi yetu. Kwa maoni yetu sisi ACT Wazalendo, Bajeti ya Serikali haikupaswa kuzidi shilingi 24 trilioni. Ushauri wetu kwa Serikali ni kuitaka ikae chini na kuleta Bajeti ndogo Bungeni ili kurekebisha Bajeti iliyoko kulingana na uwezo wetu kama Taifa ili kujiepusha na mikopo ghali itakayoumiza wananchi.

Serikali ilitangaza kuwa ujenzi wa Reli ya Kati ya kisasa utaanza mwezi Disemba mwaka huu kwa msaada kutoka nchi ya China. Leo ni mwezi Januari hata zabuni ya kampuni iliyoshinda kutekeleza mradi huo Serikali haijatangaza. Hata hivyo tumesikia kuwa kampuni kutoka Uturuki imeshinda zabuni hiyo na China (ambao ndio watoa mkopo wa mradi husika) wamekasirika na wamegoma kutoka fedha zao.

Tumesoma kwenye vyombo vya habari kuwa Rais wa Uturuki anakuja nchini wiki ijayo. Hatukatai kuimarisha mahusiano na Uturuki, lakini ni muhimu Serikali ijitazame upya kuhusu mahusiano yake na China. China ni rafiki wa Tanzania wa misimu yote. Tanzania imekuwa na China muda wote na China imekuwa na Tanzania muda wote. Maamuzi ya Serikali ya kutozingatia taratibu za China katika masuala ya mikopo yanaweza kugharimu sana mahusiano yetu ya zaidi ya miaka 50.

Tunamsihi Rais awe makini sana na mwenendo wake wa kutojali misingi imara ya Sera yetu ya mambo ya nje. Serikali ikae chini na China kutazama upya suala la Reli ya Kati vinginevyo hatutajenga Reli hiyo, ama itachukua miaka mingi sana kuijenga Reli hiyo. Madhara ya kuchelewa kujenga Reli ya Kati ni makubwa mno kwani washindani wetu wa kibiashara, Kenya, wanamaliza Reli yao sasa kuunganisha na nchi za Rwanda na Mashariki ya Kongo.

Namkumbusha Rais na Serikali namna ndani ya mwaka mmoja tangu aingie madarakani walivyovunja misingi yetu kadhaa ya Sera ya Mambo ya Nje, hasa kuhusu Sahara Magharibi na Mashariki ya Kati. Tumeikumbatia Moroko kwa ahadi ya viwanja vya mipira na misikiti na kuwaacha wananchi wa Sahara Magharibi ambao Mwalimu Nyerere aliwalinda kwa gharama zote. Juzi juzi kwa mara ya kwanza tumewasaidia Israel kwenye Umoja wa Mataifa bila ya kujali msimamo wetu wa 'Two States Solution' kati ya Palestine na Israel.

Sasa tunakwenda kuweka nyufa kwenye mahusiano yetu na China. Serikali ijitazame upya. Tanzania haikuanza na awamu ya Tano, nchi hii imekuwapo na itaendelea kuwapo. Hatuwezi kukaa kimya tukiendelea kuona misingi ya nchi yetu inavunjwa vunjwa. Lazima tukemee.

Mwisho ni haya masuala ya Demokrasia. Juzi nilipokuwa Kahama nimezungumzia suala la ubinywaji wa demokrasia na kuwaweka ndani wawakilishi wa wananchi kwa makosa yanayodhaminika. Nilionya kuhusu tabia ambayo imeanza ya kuitumia mahakama kutekeleza matakwa ya kisiasa ya Serikali.

Wakati mbunge wa Arusha Mjini bado angali kizuizini, Mbunge wa Kilombero amehukumiwa kwenda jela miezi 6 kwa kosa ambalo lina adhabu ya faini. Kuna maamuzi ya mahakama ya rufaa kuhusu kwamba kosa lenye faini, faini ndio adhabu stahili na sio kifungo. Lakini kwa kuwa lengo ni kukomoa wanasiasa wa upinzani Mbunge wa Kilombero ameswekwa jela.

Narudia kutoa wito kwa Serikali kuwa makini sana na chuki inazozijenga kwa wananchi kutokana na uonevu huu. Ninaamini kuwa vyama vya siasa vyenye wabunge hao pamoja na taasisi za kutetea haki zitashiriki kikamilifu kuchukua hatua za kisheria dhidi ya matendo yanayoendelea nchini mwetu hivi sasa.

Tusiache kuinua mikono yetu kupinga uonevu kwa sababu uonevu wa dola ni mtego wa panya. Tukemee kabla hatujafikiwa pia.

Watu wa Kijichi, ninawatakia Uchaguzi mwema hapo Januari 22, 2017. Nina imani kwamba mwaka 2017 tutaweza kupata haki yetu ya kikatiba ya kufanya mikutano ya hadhara ili tuendelee kuwaelimisha wananchi ubaya wa Sera za CCM na ubora wa sera zetu za ACT Wazalendo. Tunawaomba wanaKijichi mumchague ndugu Edgar Mkosamali awe Diwani wenu ifikapo jumapili ijayo. Na tunawaomba WanaKijichi pamoja na Watanzania wote waichague ACT Wazalendo, ifikapo mwaka 2019 watupe mitaa mingi na mwaka 2020 watupe Serikali ili tuweze kuwaongoza kwa kuzingatia Utu, Uadilifu na Uzalendo.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo
Kijichi - Dar es salaam
Januari 15, 2015

Askofu Katoliki Ataka Viongozi Wanaoamini Taifa Halina Uhaba wa Chakula Waombewe Ili Waijue Kweli..!!!

$
0
0

Askofu mkuu wa jimbo la Mwanza Mhashamu Thadeus Ruwaichi amewataka waumini wafunge lovena kuliombea taifa juu ya baa la ukame na njaa pia kuwaombea viongozi watambue kuwa BAA HILO LIPO NCHINI KWA SASA.


Amesema hayo katika Parokia ya Pansiasi katika ibada ya kutoa kipaimara kwa vijana wa kikristo.

Kauli hii inatutaka waumini na raia kuwaombea wale viongozi wanaosema hakuna ukame wala njaa kwa vile wameona majani ni ya kijani.

Hii ni Zaidi ya Komoa:Mfanyabiashara Marekani Alipa Kodi kwa Kutumia Matoroli 5 Yaliyojaa Sarafu..!!!

$
0
0
kodi-2 MAREKANI: Mfanyibiashara mmoja nchini Marekani ambaye amezozana na idara ya magari nchini humo DMV amelipa kodi yake ya dola 3,000 kwa kutumia mikokoteni mitano iliojaa sarafu 300,000.


Nick Stafford kutoka Cedar Buff, Virginia, aliwasilisha sarafu nyingi hatua iliolazimu mashine ya kuhesabu sarafu hiyo ya Idara hiyo kushindwa kuzihesabu. Hatua hiyo imekuja kufuatia mgogoro kati yake kuhusu kuwasiliana na wafanyakazi wa mamlaka ya mapato nchini humo kuwauliza kuhusu kodi yao.

Iliwalazimu wafanyakazi kutumia saa saba wakihesabu sarafu hizo hadi usiku. Walimaliza kazi hiyo ya kuhesabu mapema siku ya Alhamisi.
kodi-1Bwana Stafford aliwasilisha pingamizi yake kwa sababu alizitaka idara za serikali kuangazia na kutoa majibu kwa maswala yanayowakumba raia.

“Haijalishi iwapo utalipa dola 300 kwa mwaka kama kodi au dola 3000 kwa mwaka kama mimi kwa sababu uti wa mgongo wa taifa lililo na demokraisa huru ni sharti liwe na serikali ilio na uwazi,” alisema.

Bwana Stafford ameelezea katika mtandao wake kwamba mgogoro wake na DMV ulizuka kwa sababu idara hiyo haikutaka kumpatia nambari za simu za moja kwa moja kuhusu afisa wa kuwasiliana naye ili kusajili magari matatu na kulipa ushuru kwa kuwa anamiliki nyumba tatu katika maeneo 3 tofauti.
kodi-3Aliwasilisha ombi la kutaka kupewa nambari ya moja kwa moja kulingana na Bristol Herald Courier na akapewa nambari ya simu ambayo angepiga. Lakini alipoitumia aliambiwa kwamba haingeweza kuitumia kuuliza maswali.

Bwana Stafford alitaka kujua nambari hizo za moja kwa moja za maafisa wengine tisa ijapokuwa Idara hiyo tayari ilikuwa imemshughulikia swala lake. Na ombi lake lilipokataliwa alienda mahakamani kuwasilisha malalamikoi yake.

Mapema wiki hii jaji mmoja alipinga maombi yake matatu aliowasilisha, akikataa maombi alilowasilisha kwa DMV na wafanyikazi wake wapigwe faini.

Hata hivyo wafanyikazi wa idara ya magari baadaye walimpatia nambari hizo alizotaka na tayari amezichapisha katika mtandao wake.

Bwana Stafford anasema kuwa idara ya magari ililazimika kukubali malipo yake kwa sababu sheria ya Marekani kuhusu sarafu mwaka 1965 inasema sarafu ni fedha halali na zinaweza kutumika kulipa madeni, kodi na mishahara

Jitofautishe na Wengine ili Uwe na Mafanikio Endelevu kwa Kazi Hiyo Hiyo Uliyonayo..!!!

$
0
0
 
Kufikia mafanikio makubwa kwa mujibu wa tafiti nyingi zinaonyesha ni matokeo ya kufanya jambo lilelile ambalo pengine  kila mtu analifanya lakini kwa njia tofauti. Hakuna uchawi tofauti na huo wa kufanya jambo lilelile lakini kwa utofauti.
Kama unajidanganya unasema mazingira mabovu ndiyo yanayokufanya uwe na hali ngumu unajidanganya. Katikati ya hayo mazingira mabovu kuna watu waliofanikiwa sana, na bila shaka hata wewe ni shahidi wa hilo na unawajua.
 
Kama unasema ‘oooh mimi sijafanikiwa kwa sababu sina kipaji au uwezo wangu ni mdogo pia unajidanganya.’ Dunia ina watu wengi sana ambao wanamafanikio makubwa  lakini hawakuwa na uwezo kama huo mkubwa unaofikiri.

Kama pia unasema mimi sifanikiwi kwa sababu sifanyi biashara ya aina fulani pia unajidanganya. Hakuna biashara ambayo ukiifanya ni lazima uwe tajiri moja kwa moja, nasema biashara hiyo haipo.

Watu ni matajiri katika kila biashara. Kama unafikiri natania angalia mtaani upate ushahidi kamili. Ile biashara unayoidharau kuna mwingine ni tajiri kupitia hiyo biashara ambayo unaiona haifai.
Hakuna mtu ambaye ameshindwa kuufikia utajiri eti kwa sababu hana mtaji. Na hakuna mtu ambaye ana mtaji na akajihakikishia utajiri wa moja kwa moja. Kinachokupa mafanikio ni kwa jinsi wewe unavyofanya vitu kwa utofauti.
Haijalishi wewe ni maskini kiasi gani kama unafanya mambo yako kwa utofauti ni lazima kwa vyovyote vile utatoka huko kwenye dimbwi la umaskini na kuanza kuupata utajiri polepole.
Unataka kufanikiwa fanya mambo yako kwa njia tofauti. Unaweza ukawa ni mkulima sawa, lakini lima huku ukiongeza ubunifu na kujua ni kipi cha ziada ambacho kinaweza kuongeza mazao yako thamani.?
Kama wewe ni mfanyabiashara fanya biashara yako huku ukiongeza ubunifu wa hali ya juu sana kila siku. Jifunze kwa wafanyabiara wenzako na pia jifunze kupitia semina mbalimbali.
Utafika mbali sana kimafanikio na kuwa mtu wa tofauti ikiwa utajua na kujifunza kufanya mambo yako kwa utofauti. Kila wakati jifunze kutafakari na kutambua je, unafanya mambo yako kwa utofauti?
 
Kama ni mtu wa kuiga iga na kusahau kabisa kufanya mambo kwa utofauti  ni kuhakikishie kabisa sahau kitu kinachoitwa mafanikio makubwa. Mafanikio makubwa yanajengwa na wewe kwa  kuwa watofauti.

 Naomba usije ukanielewa vibaya simaanishi uanze kufanya jambo jipya kabisa hapana. Fanya jambo lilelile, lakini lilokubwa kwako kumbuka kufanya kwa utofauti. Hapo ndipo siri kubwa ya mafanikio ilipo.
Kwa hali yoyote uliyonayo unaweza kubadili maisha yako na kuwa mtu wa tofauti kabisa ikiwa utakuwa unatenda kwa utofauti. Kama ulikuwa huna mtaji, upo kwenye madeni vitu vyote hivyo utavipata na kufikia mafanikio yako.
 
Nimalize makala haya kwa kusema hivi, kupata utajiri hakutegemei sana mazingira, hali, kipaji au unafanya biashara ya namna gani. Bali kupata utajiri kunategemea sana je, vitu hivyo unavyovifanya una vifanya kwa utofauti?

Zingatia Mlo Huu kwa Kujikinga na Ugonjwa wa Kisukari kwa Mwaka Huu 2017..!!!

$
0
0
matunda Matunda
Kisukari ni ugonjwa ulioingia kwa kasi nchini. Ni hali inayotokea wakati sukari inapozidi ile inayotakiwa katika damu kwa sababu ya upungufu au ukosefu wa Insulin. Insulin ni kichocheo kinachotengenezwa kwenye kongosho na kwamba hutumika kusaidia mwili kutumia sukari inayotokana na vyakula tunavyokula.


Kuna aina kuu mbili za kisukari

Kwanza ni kisukari kinachotegemea Insulin. Kazi ya Insulin ni kurekebisha hali ya sukari kwenye damu, ikiwa ni nyingi inapunguzwa kurudi kwenye hali ya kawaida na ikiwa chache huruhusu irejee kwenye hali ya kawaida pia. Kunapokuwa na hitilafu kongosho likazalisha homoni hii kwa wingi, sukari hupungua mwilini, au isipozalishwa, sukari huongezeka mwilini. Hospitalini, aina hii ya sukari inatibiwa kwa kutumia sindano za Insulin na kurekebisha ulaji wa vyakula.

Pili ni kisukari kisichotegemea Insulin. Hospitalini hiki huthibitiwa kwa kutumia vidonge pamoja na kurekebisha ulaji wa vyakula au kwa kurekebisha vyakula peke yake. Watu wengi walio na aina ya kisukari kisichotegemea Insulin ni wanene kupita kiasi na ikiwa watapunguza uzito kasi ya ugonjwa hupungua au kwisha kabisa. Sukari inaweza kuwa juu au chini kupita kiasi cha kiwango kinachotakiwa.

Hali zote hizo mbili si nzuri kwa binadamu kwa sababu mgonjwa anaweza kufa haraka. Sukari inaweza kuwa juu bila dalili zozote zile kujitokeza mwilini mwa mgonjwa. Watu wanaojijua kuwa na tatizo la kisukari wanashauriwa kupima damu au mkojo mara kwa mara ili kufahamu kama sukari katika damu yao iko sawa au haiko sawa.

Dalili za mtu aliyepungukiwa sukari mwilini ni pamoja na mapigo ya moyo kwenda haraka haraka, kutokwa jasho kwa wingi, kujisikia kama mwenye homa, kuchoka kukojoa mara kwa mara na kuumwa kichwa. Ni vizuri mtu akihisi dalili hizo ahakikishe anapima sukari mwilini. Hadi sasa hakuna tiba ya kuponya ugonjwa wa kisukari.

Hata hivyo, wagonjwa wote wanaweza kuishi vizuri na kufanya kazi zao zote ikiwa watafuata maelekezo na masharti yanayotakiwa. Madhara ya kisukari ni kwamba mtu mwenye kisukari anaweza kupatwa na tatizo la kupungua uwezo wa macho kuona, figo kutofanya kazi zake ipasavyo na kupata vidonda vya miguuni visivyopona kwa wanaume kuwa na upungufu wa nguvu za kiume.

Pia mtu mwenye tatizo la kisukari mishipa yake ya fahamu ya miguuni na mikononi kutofanya kazi zake vizuri, matatizo ya moyo na kupatwa na magonjwa mbalimbali ya ngozi. Madhara hayo yanazuilika kwa kuzingatia kutozidi kwa sukari kwenye damu ya mgonjwa.

Ushauri kuhusu chakula kama una kisukari, vyakula vinavyofaa husaidia mwili kuwa na viwango vya sukari na mafuta vinavyostahili kuwepo damuni, hupunguza unene kupita kiasi, hutosheleza mahitaji ya mwili ya nishati, madini na vitamini ili kuuwezesha mwili kuwa na uzito unaostahili na kufanya kazi ipasavyo.
matunda1Matunda na mboga
Kila mwenye tatizo la ugonjwa wa kisukari anatakiwa kuepuka kula vyakula vilivyowekwa sukari kwa sababu sukari huyeyushwa upesi sana tumboni na kusababisha sukari nyingi kuingia kwenye damu katika muda mfupi. Vyakula kama sukari, glucose, asali, jamu, keki, pipi, ice cream, chocolate na soda zote zilizo tamu haviruhusiwi kwa mtu mweye tatizo la kisukari.

Chai, kahawa, maziwa na uji vinaruhusiwa kutumiwa iwapo vitakuwa havijaongezwa sukari. Madafu na club soda vinaruhusiwa kwa sababu havina sukari inayoweza kuyeyuka haraka na kukimbilia kwenye damu.

Mgonjwa wa sukari anaweza kuongeza utamu kwenye mchanganyiko anaoutaka kwa kutumia vidonge maalum ambavyo hupatikana kwenye maduka ya madawa.

Njaa nayo huchangia kumfanya mgonjwa wa kisukari kujisikia vibaya huenda kwa vile sukari inaweza kupungua kupita kiasi mwilini.Mgonjwa wa kisukari anatakiwa kutokaa na njaa, kula mara kwa mara na pia kula mara tatu au zaidi kwa siku na ikiwezekana anatakiwa kutafuna vitu vidogo vidogo katikati ya milo mikubwa.

Inashauriwa kuwa mgonjwa asipendelee kula milo mikubwa mchana au jioni. Mgonjwa huyo hatakiwa kuacha kula vyakula vyenye wanga kama vile ugali, viazi na wali. Anachotakiwa kufanya ni kuzingatia kiasi cha chakula cha wanga anachokula kwa mlo na pia anatakiwa kutumia zaidi nafaka zisizokobolewa kwa mfano dona kwa sababu huweza kumpatia mgonjwa vitamini na madini. Hakuna sababu ya mgonjwa kupikiwa chakula chake maalum kwa sababu anaweza kula chakula chochote kilichopikwa na familia isipokuwa vile vilivyowekwa sukari.
ice creamIce Cream
Mgonjwa anatakiwa kula matunda kwa wingi na kwamba anaweza kula matunda aina zote kwa siku. Anatakiwa pia kula mboga za majani kwa wingi au kachumbari kila siku. Mgonjwa wa kisukari anatakiwa kupunguza kiasi cha mafuta anachokula na pia kuepuka kula mafuta yenye asili ya nyama. Anatakiwa kutumia zaidi vyakula vilivyochomwa, kuokwa au kubanikwa kuliko vile vilivyokaangwa na kula samaki, maharage au kuku aliyetolewa ngozi.

Mgonjwa wa kisukari anatakiwa kuepuka kunywa pombe kwa wingi kwa sababu huweza kuathiri afya.

Vyakula vinavyoweza kumwongezea mgonjwa madhara ni sukari yenyewe, nyama yenye mafuta, figo au maini husababisha sukari kupanda kwa kiwango cha aina ya mafuta mabaya yanayosababisha damu kuganda kwenye moyo na mishipa ya damu na kuleta magonjwa ya moyo.

Vyakula vya kuliwa bila masharti ni mboga za majani, nyanya, matango, bamia, karoti, vitunguu, pilipili hoho, pilipili, viungo vyote vya vyakula bila kuweka chumvi nyingi, maji ya kunywa, chai na kahawa.Ikiwa mgonjwa wa kisukari anaumwa na hawezi kula vyakula vya kawaida anatakiwa kunywa uji, maziwa na maji ya matunda.

Mazombi Yavamia Ofisi za Cuf Znz,Yafanya Uharibifu Huu..!!!!

$
0
0

Ofisi ya Chama cha Wananchi (CUF) Jimbo la Dimani Wilaya ya Magharibi B imevamiwa na watu wasiojulikana maarufu mazombi.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Hassan Nassir Ali amesema tukio hilo lilimetokea saa 6.30 usiku wa kuamkia jana.

Amedai kuwa mazombi hayo yalipora mali, kujeruhi watu na kuwateka wengine wa nyumba jirani na ofisi hiyo.

“Ni kweli taarifa tunazo za watu kuvamia ofisi hiyo ya CUF na kuwapiga pamoja na kuwahujumu watu na huo ni uharamia unaoripotiwa mara kwa mara,” amesema Kamanda Ali.

Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma wa CUF, Salim Abdallah Bimani amesema, “Huu ni uvunjifu wa amani na tunataka Rais John Magufuli iwapo anayo nia ya dhati afuatilie hujuma hiyo ambayo watekelezaji wake wanajulikana lakini hawakamatwi.”

Inasikitisha Sana : Hivi Ndivyo Ugonjwa wa Homa ya Ini Unavyozidi Kuwamaliza Watanzania..!!!

$
0
0

Ugonjwa wa homa ya ini maarufu kwa jina la hepatitis B umetajwa kuwa maambukizi yake ni makubwa na haraka zaidi ya Ukimwi.


Takwimu za Shirika la Afya la Kimataifa (WHO) zinaonyesha kuwa kiwango cha maambukizi ya homa ya ini B kwa Tanzania ni wastani wa watu wanane katika kila watu 100.  Maambukizi ya VVU, ni wastani wa watu watano katika kila watu 100.

Takwimu za wachangiaji damu katika kitengo cha uchunguzi wa magonjwa cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, (MNH) kwa kipindi cha siku 14 za Desemba 2016, zinaonyesha kuwa kati ya sampuli 480 za damu zilizopimwa, 18 zilikutwa na VVU.

Lakini, katika sampuli 480 zilizopimwa katika kipindi hicho hicho, 56 zilikutwa na virusi vya homa ya ini B, huku watu 20 kati yao wakiwa na ini C (hepatitis C).

Katibu Mkuu wa Serikali, Dk Mpoki Ulisubisya amesema Serikali imeanza kuwatumia watafiti wake kuangalia kwa undani kasi ya maambukizi ya ugonjwa huo.

KKKT Nao Watoa Tamko Juu ya Hali ya Njaa Nchini,Waitaka Serikali Ifanye haya..!!!

$
0
0

Serikali imeombwa kufanya tathmini ya haraka kubaini upungufu wa chakula nchini uliosababishwa na ukame wa muda mrefu.


Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Frederick Shoo ametoa ombi hilo wakati wa ibada ya kumweka wakfu Askofu wa Dayosisi ya Meru, Elias Nassari katika Usharika wa Usa River, Wilaya ya Arumeru.

Amesema Serikali haitakiwi kungoja hadi watu wafe ndiyo waanze kutafuta chakula.

Dk Shoo ametoa kauli hiyo siku moja baada ya Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC), Tarcisius Ngalalekumtwa kuwaandikia maaskofu wote wa kanisa hilo kuwataka waumini wao wafanye maombi, hija, mfungo kwa lengo la kukabiliana na ukame unaolikabili taifa.

Vilevile, hivi karibuni Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) lilitoa wito kama huo kwa waumini wake, huku Serikali ikisisitiza kuwa hakuna njaa nchini na kuwa haitatoa chakula cha msaada.

AIBUU: Baada ya Kupigwa Talaka,Frola Mbasha Aamua Kujipooza kwa Mlinzi Wake Binafsi,Issue Nzima Iko Hivi

$
0
0
mbasha
Flora Mbasha na Emmanuel Mbasha.

DAR ES SALAAM: Siku chache baada ya kutinga mahakamani kudai talaka kwa mumewe, Emmanuel Mbasha, staa wa Gospo Bongo, Flora Mbasha anadaiwa kuchumbiwa na mwanaume aliyetajwa kuwa ni mwenyeji wa Kahama, Sinyanga, Daud. Chanzo cha kuaminika kimepenyeza ubuyu wa motomoto kuwa, tukio la Flora kuvishwa pete ya uchumba lilijiri hivi karibuni baada mwanamuziki huyo wa Injili kutofautiana
na ‘mlinzi’ wake aitwaye Peter Shelembi.

“Si unakumbuka baada yankutofautiana na Mbasha, Flora alikuwa ‘close’ na jamaa f’lani hivi anaitwa Peter, alikuwa akizurura naye sehemu mbalimbali kwa ajili ya kuwa kama mlinzi wake, akihofia Emma (Mbasha) anaweza kumletea fujo? Sasa nasikia mama’ke Flora alimshawishi bintiye aolewe na Daud, naye bila hiyana akakubali.
flora-mbasha2  frola-mbashaa
Flora Mbasha na Emmanuel Mbasha na mtoto wao.
frola-mbasha 

 “Ilikuwa rahisi maana hata pale kanisani kwa Josephat Gwajima (Kanisa la Ufufuo na Uzima) alipokuwa anaabudu Flora alishaasi. Akaenda zake kuvishwa pete ya uchumba bila hata waumini wenzake kujua,” kilidai chanzo hicho. Baada ya kuzipata ‘good news’ hizo, Wikienda lilianza kwa kumtafuta Daud ili kumpongeza kwa kupata ‘kifaa’ na pia kujua mipango ya harusi. Tofauti na matarajio ya Wikienda

 kwamba pengine atazipokea pongezi na kumshukuru Mungu kuianza safari ya ndoa, jamaa huyo alipokea simu, baada ya mwandishi kujitambulisha, alikata. Wikienda lilipiga tena ili kutaka kujiridhisha labda pengine simu ilikatika kwa bahati mbaya lakini safari hii alipokea na kusema yeye si Daud, mwandishi amekosea namba, akakata tena simu.

Licha ya kujiridhisha namba hizo zinamilikiwa na Daud, Wikienda likaona isiwe kesi, likamvutia waya Flora ili kumpongeza na kumsikia anazungumziaje safari yake hiyo mpya anayoianza mbali na ile ya Mbasha iliyotawaliwa na ‘sarakasi’ nyingi hadi kufikia hatua ya kuishi kama paka na panya.

Baada ya Wikienda kujitambulisha na kumpongeza kisha kumpa ‘full mchapo’ kutoka kwa chanzo, Flora hakutaka hata kuzipokea pongezi hizo badala yake alisema hataki kuzungumzia jambo hilo na kushauri gazeti
hili lizungumze na mwanasheria wake.

“Jamani mimi sipo tayari kuzungumzia chochote zaidizaidi kama mnataka niwape namba ya mwanasheria wangu,” alisema Flora.

Flora alimtumia mwandishi wetu namba ya mtu aliyedai ni mwanasheria wake lakini alipopigiwa simu alisema kuwa, kuna kazi anafanya, apigiwe baada ya muda. Hata hivyo, baadaye simu yake ilipopigwa, haikupatikana hewani. Flora aliishi kwenye ndoa na Mbasha kwa zaidi ya miaka kumi na kufanikiwa kupata mtoto mmoja, Elizabeth kisha mwaka 2015 walitengana kutokana na ugomvi wao uliofukuta chini kwa chini kwa muda mrefu na kuibuka hadharani baada ya Mbasha kupata msala wa kudaiwa kumbaka mdogo wa Flora. Hata hivyo, kesi iliunguruma kwa muda na baadaye Mbasha alishinda na kuachiwa huru.

Kwa Wanaume Tu:Kwa Hizi Tabia, Huwezi Kujiita Mwanamme Mkamilifu Hata Siku Moja..!!!

$
0
0
Huwezi kujiita mwanamme kama hujui wanao wanakula nini?


Huwezi kujiita mwanamme kama hujui kama nguo walizovaa wanao pesa imetoka wapi?

Huwezi kujiita mwanamme kama hujui nguo aliyovaa mkeo, nywele alizosuka na kila kitu chake kimetoka wapi?

Mkeo kufanya kazi sio tiketi ya wewe kugeuka kuwa mwanamme suruali?

Kuna watu wengine hujisahau eti kisa mke anafanya kazi basi unafurahia kula kuku kila siku. Hata hujiongezi ukatoa matumizi ya ndani?

Ungekuwa na akili kidogo ungejua kuwa mshahara wa mkeo hautoshi kufanya vyote hivyo anavyofanya na ungekuwa makini, sasa wewe unaridhika tu kwakuwa anafanya kazi unamuachia kazi ya kuwa mwanamme.

Nikuambia tu kitu kimoja mwanamke hata awe na pesa vipi bado anahitaji mwanamme wa kumtunza, yaani mtu wa kwenda kumlalamikia shida zake na kumsikiliza. Sio kwenda kulalamikia shida zake kwenye ATM.

Katika familia mwanamme unatakiwa kutoa na mke kuchangia kwamba, hata kama ana kipato kikubwa lakini usibweteke na kumuachia kila kitu, asipoweza kulalamika kwako atatafuta sehemu ya kulalamikia.

Mwanamke anatakiwa kuongezea kilichopungua na si kutoa kisichokuepo.

Rasmi: CIA Wamtaka Trump Achunge Mdomo Wake,Lasivyo Haya Ndiyo Yatakayompata...!!!!

$
0
0
atrump_putin_compo
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA), John Brennan amemuonya Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump kuwa makini na kauli zake na kuuchunga mdomo wake, hasa anapozungumzia suala la uhusiano wa kidiplomasia kati ya Marekani na Urusi kwa madai kwamba anahatarisha usalama wa Taifa la Marekani.


Brennan aliendelea kueleza kuwa, Trump bado hajaelewa nia ya Urusi kwa Marekani kwa hiyo badala ya kufurahia mipango ya siri inayoendelea, anapaswa kuwa makini na kuchunga kauli zake.

“Nafikiri Trump haelewi kwa sababu gani uhusiano wa Marekani na Urusi umekuwa suala tete kwa kipindi kirefu kilichopita, anatakiwa kuwa makini sana anapolishughulikia suala hili,” alisema na kuongeza kuwa CIA inazo taarifa za namna Urusi inavyojaribu kumtumia Trump kutimiza matakwa yake.
cia
John Brennan
Brennan aliyazungumza hayo wakati akihojiwa na Kituo cha Runinga cha Fox News, ikiwa ni wiki moja tangu alipotangaza ripoti kwamba wamegundua kuwa Rais wa Urusi, Vladimir Putin na vijana wake, walifanya ‘makeke’ ili Trump ashinde kwenye uchaguzi mkuu nchini humo, na kumuangusha kwa hila mpinzani wake, Hillary Clinton.
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live




Latest Images