Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

Majaliwa Akiri Nchi Ina Uhaba wa Chakula,Atoa Onyo Hili..!!!

$
0
0

Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa wakati akizungumza na Wakuu wa Idara na sekta mbalimbali katika mkoa wa Njombe amesema kuwa Tanzania ina upungufu wa chakula katika baadhi ya maeneo na si maeneo yote. 

Waziri Mkuu anasema kitendo cha baadhi ya watu kusema Tanzania ina baa la njaa si sahihi kwani kufanya hivyo ni kuwatia hofu wananchi, maana tafsiri ya baa la njaa ni hali kuwa mbaya zaidi, kusema hivyo kutapelekea watu kushindwa kuwa watulivu.

"Tatizo tulilonalo ni katika maeneo yale, mikoa, wilaya ambayo hawakupata mvua kubwa msimu uliopita, utaratibu wetu ni kwamba tunaimarisha masoko ya ndani ili kuhakikisha kwamba maeneo yote yanakuwa na chakula angalau mtu aweze kwenda kununua, kwa hiyo neno baa la njaa ni jambo jingine. Naomba watanzania tusitiane hofu, tusiwatie hofu wananchi kwa kutamka maneno ambayo maana yake halisi kuwa ni hali mbaya zaidi tukafanya watu washindwe kuwa watulivu" alisema Waziri Mkuu

Mbali na hilo Waziri Mkuu amewataka wananchi kuwa wasikivu kwani katika baadhi ya hayo maeneo ambayo kuna upungufu wa chakula serikali imesema inaweza kuwatumia wafanyabiashara wakaleta chakula katika maeneo hayo, pia Waziri Mkuu ameeleza kupanda bei ya chakula katika maeneo mengi ni kutokana na watu wengi kuhifadhi chakula kutokana na hofu ya hali ya hewa ya sasa jambo lililopelekea chakula kupanda bei. 

Idrisa Sultani Aaamua Kuanika Kila Kitu Jinsi Wema Sepetu Alivyomkausha Milioni 500 Zake za Ushindi wa Big Brother..!!

$
0
0

Mshindi wa Shindano la Big Brother Africa Idris Sultan ameamua kukiri wazi kuwa kipindi yupo kwenye mahusiano na Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu alikumbwa na ukata.

Kupitia kipindi cha Clouds e cha Clouds Tv Idris Sultan amesema wakati yupo kwenye mahusiano yake yaliyopita na mrembo Wema Sepetu alikuwa kwenye Ukata hivyo nilijikuta sifanyi vitu vya maana kuliko
kipindi hiki ambapo yupo Single.

“ Wakati nipo kwenye mahusiano yangu yaliyopita niliyumba kidogo kiuchumi kwani sikuwa nafanya mambo mengi ya muhimu kuliko sasa hivi kwani hata watu wangu wa karibu watakueleza hivyo,nafurahi niko
single na naendelea kupambana“Alisema Idris.

Ikumbukwe idris alishinda tsh milioni 500 za kitanzania kwenye shindano la big brother Africa. Idris sasahivi ni mtangazaji wa choice FM 

Rais Magufuli Aaanza Safari za nnje ya Nchi,Aenda Ethiopia Kwenye Mkutano wa AU..!!!

$
0
0

Rais John Magufuli Mapema hii Leo amekwea pipa kuelekea nchini Ethiopia kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa viongozi wa Afrika unaotaraji kuanza rasmi kesho kutwa.

Zaidi Barua Rasmi ya Ikulu Hii Hapa..!!

Harmo Rapa Ang'ang'ania Jina la Harmonize ,Atoa Sababu Hizi Nzito za Kufanya Hivyo..!!!

$
0
0

Msanii wa bongo flava ambaye ndiyo anaanza kuchipukia, Harmo Rapa, amesema kuwa hana mpango na wala hawezi kubadili jina hilo lililompa umaarufu kwenye muziki kwa hofu ya kupoteza mashabiki wake. 

Msanii huyo anatamba na ngoma yake inayokwenda kwa jina la 'USIGAWE PASI'. ametoa msimamo huo kupitia eNewz ya EATV iliyomtafuta kuzungumza naye kuhusu mpango wa kubadili jina lake na kutotumia jina la 'Harmo Rapa'.

“Mimi sina mpango wa kubadili jina langu kwa sababu naogopa kupoteza mashabiki zangu na ukiangalia kwa sasa jina la Harmo Rapa limeshakuwa kubwa na tayari nimeshajitengenezea mashabiki kupitia jina hilo”

Pia amesema kuwa hana mpango wa kwenda WCB na wala hahitaji msaada wowote kutoka kwao huku akionesha jeuri kuwa angeweza kutoka hata bila kutumia jina hilo. "Hata bila kufananishwa na Harmonize mimi ningetoka tu"

Harmo Rapa ni moja kati ya wasanii ambao wamepata kiki ya kutosha kutokana tu na muonekano wake ambapo watu wengi wamekuwa wakimfananisha na Harmonize kutoka WCB.

Msanii huyo hivi karibuni katika kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio alijifananisha na Fid Q na kuwaacha watu midomo wazi.

Rais John Magufuli Aelekea Addis Ababa Kwenye Kilele cha Mkutano wa 28 wa Wakuu wa AU

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Mungano wa Visiwa vya Comoro Mhe. Azali Assoumani walipokutana kwenye ndege katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Januari 28, 2017 tayari kwa safari ya Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 28 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU). Rais Assoumani alikuwa akitokea Comoro kupitia Dar es salaam.

Matumaini ya Kuwapata Wahanga Waliofukiwa na Kifusi Yaonekana

$
0
0
Matumaini ya kuwapata watu walionasa chini ya mgodi Geita yameongezeka baada ya timu ya waokoaji kufanikiwa kuchoronga mwamba na kufikia wachimbaji hao ambao wametuma ujumbe mfupi kwamba wako 15 na wote wako hai ila wameomba chakula kwa kuwa wana njaa na mmoja wao sasa haongei kwa kuzidiwa njaa.

Tayari timu ya madaktari kutoka Hospitali ya Mkoa wa Geita na hospitali ya Waja wametuma glucose na maji ambayo yamepokelewa.

Wanaume Mnaojisifia Mnajua Mambo Sita Kwa Sita Mnaboa Sana

$
0
0
Umekutana na jamaa very Handsome... Very Smart..Kajazia misuli UKAMTAMANI...Yaani kila ukimwangalia Pichu inajaa udambwidambwi...Unampatia Picha Ukimpa Mzigo jinsi atakavyoimanua vizuri papuchi...SIKU YA SIKU UMEJIANDAA UMEMPA SHOO....Jamaa yuko bize anapiga mikelele ya shangwe kuita wazungu wakati wewe wala huoni anachofanya and ur wondering," WHAT IS THIS NIGGA DOING ON TOP OF ME "

Imewahi kukutokea ? 

Halafu MBAYA ZAIDI baada ya kukuru kakara zisizo na faida yoyote kwako na kupakwa shombo la maana na kuwa disappointed jamaa linashuka na kukuuliza
" BABE HOW WAS IT "..Teh teh,Hapa wanaume tunapewaga jibu la kisiasa tu IT WAS FINE...halafu ananyanyua gagulo lake anaenda bafuni akirudi utasikia
"I think we should go , Nimekuta Missed call za Mum"
HUPEWI TENAAAAAA....Wanaume ukiona umepewa mara 1 ukiomba tena unazungushwa kama unafuatilia TIN NUMBER ofisi ya TRA ujue ULIFELI DAY 1...Akupe tena ili iweje??
UKIPEWA PAKUA HASWA..Ukishuka mtu alale kama masaa2 hivi ndo akumbuke kumbe kuna mama home ... Sio mtu unashuka nae anabeba taulo..HUJAFANYA KITU BROTHER!

Mbinu Mpya za Wanawake wa Siku Hizi Wanaosaka Ndoa Kwa Nguvu..Ni Noma Sana

$
0
0
Siku ya kwanza atakuja na chupi 2, moja anaifua anaacha bafuni,nyingine anavaa asubuhi anaondoka...
Siku ya 2 anakuja na khanga,anaivaa usiku,asubuhi anaianika nyuma ya mlango anaondoka...

Siku ya 3 anasahau pete na hereni juu ya meza anakwambia 'Hny nitunzie nimesahau hereni zangu mezani

Siku ya 4 anakuja na nguo 2 na vipedo vya kubadilisha na viatu pea 2,anavua high heels anaweka kwenye Shoe rack,asubuhi anaondoka na flat shoes kwenda chuo. Baada ya mwezi chumba chako kinakuwa na vitu kadha wa kadha,na ole wako uvihamishe alipoacha,kesi zinaanza...

Hao ndo Wanawake wa kileo,akija na begi zima si utamuuliza Vipi mwenzangu na utamkimbiza...Anahamia taratibu.. Mwisho wa siku dressing table yako iliyokuwa ina perfume na mafuta ya Rays inakuwa imejaa hereni na 'Foundation'...

My Brother,huna haja ya kuuliza,NDO KASHAHAMIA HUYO....
Kifuatacho utaambiwa,''Honey I miss my days',Zamani nilijua ni Simu za mkononi tu ndo zina Missed Calls, Siku hizi kuna Missed days,ukiambiwa hivi tu jua imekula kwako, inawindwa ndoa hapo...

Magufuli Apanda Ndege Kwenda Ethiopia..!!!

$
0
0

RAIS John Magufuli ameondoka nchini na kuelekea Addis Ababa, Ethiopia ambako atahudhuria Mkutano Kilele wa 28 wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) unaoendelea nchini humo.

Ziara hiyo ni ya kwanza kwa Rais Magufuli kutoka nje ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) tangu aingie madarakani kuongoza Serikali ya Awamu ya Tano Novemba 5, mwaka jana.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu Dar es Salaam jana ilisema katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wa jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli aliagwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Wengine waliojumuika kumuaga Rais Magufuli ni viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda.

Kwa mujibu wa Ikulu ya Dar es Salaam, pamoja na kuhudhuria mkutano huo, akiwa Addis Ababa, Rais Magufuli anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa Bara la Afrika wanaohudhuria mkutano huo.

Waokoaji Geita wafanikiwa kuwasiliana na waliofukiwa

$
0
0
WAKATI imeelezwa kuwa waokoaji katika mgodi wa dhahabu wa RZ Union ulioko Geita , wamebakiza mita tatu kuwafikia waliofukiwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Medard Kalemani akizungumza na ndugu wa watu waliofukiwa amesema kwamba wanafanya mpango wa kuwapelekea chakula wachimbaji hao.

Amesema kwamba jana wamefanikiwa kufanya mawasiliano na wachimbaji hao na kwamba wapo kumi na watano na kuwa wanachohitaji kwa sasa ni chakula.

Alisema waokoaji walifanikiwa kuwafikishia kamba na kalamu watu hao ambao waliandika mahitaji yao na kusema kwamba wote wapo salama.

Awali akizungumza  akiwa eneo la tukio jana, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Ezekiel Kyunga alisema kuwa bado walikuwa hawajawafikia watu hao lakini wamefika chini sana na kukaribia njia hizo za Mlalo.

“Kinachofanyika sasa ni kuondoa udongo kwenye njia kwa kutumia watu kwa kufanya taratibu na kwa umakini mkubwa ili udongo usiporomoke tena katika eneo hilo,” alisema.

Alieleza kuwa matumaini yao ya kuwakuta watu hao wakiwa hai bado ni makubwa kwani uokoaji huo unafanyika kwa umakini lakini kwa haraka sana na sehermu iliyobaki kufikia njia hizo ni ndogo sana.

Watu hao akiwemo raia wa China mmoja walifukiwa na kifusi juzi usiku baada ya udongo kukatika na kuziba mlango waliokuwa wakitumia kuingia na kutoka na uokoaji unaendelea kwa kushirikiana na vyombo mbalimbali vya uokoaji.

Kyunga alieleza kuwa watu wengi wapo katika eneo hilo wakiwemo ndugu wa waliofukiwa lakini kwa juhudi wanazoziona za uokoaji wametulia na kufuata maelekezo wanayopewa ikiwemo kukaa mita 500 toka eneo la tukio.

Alisema wametakiwa kukaa mbali na eneo hilo la uokoaji ili wasisongamane na watu wanaoendelea na uokoaji ili kuwapa fursa nzuri ya vikosi vyote kujadiliana namna ya kufanywa kwa ajili ya kufanikisha uokoaji huo.

Jambazi Auawa Akijaribu Kuwatoroka Polisi..!!!

$
0
0

MTU mmoja mwanaume ambaye amejulikana kwa jina moja la Mungiki (35) ameuawa kwa kupigwa na risasi na askari polisi wakati akijaribu kuwatoroka baada ya kukutwa akiwa na silaha aina ya bastola yenye namba za usajili TZCAR 97076.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Januari 27, mwaka huu saa 6.30 usiku katika Mtaa wa Bwiru Kata ya Kitangiri katika Manispaa ya Ilemela.

Alisema bastola aliyokamatwa nayo aliipora kwenye tukio la unyang’anyi wa kutumia silaha mwaka 2013 mkoani Tabora. Alisema polisi walipata taarifa kutoka kwa raia wema juu ya kuwepo kwa kijana anayejihusisha matukio ya uhalifu wa kutumia silaha jijini Mwanza na mikoa jirani.

“ Polisi walifanya ufuatiliaji wa tukio hilo, na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa na baada ya kuhojiwa alikiri kuwa na silaha hiyo na ndipo alipowaongoza askari hadi maeneo ya Songambele mtaa wa Kabohoro kwenye mapango ya mawe na kuikuta bastola hiyo ikiwa imefichwa kwenye pango la jiwe,” alifafanua.

Alisema mtuhumiwa alikiri kupewa bunduki na mtu mmoja ( jina limehifadhiwa kwa sababu za kiusalama) ambaye walikuwa wakishirikiana kwenye matukio mbalimbali ya unyang’anyi wa kutumia silaha jijini Mwanza na mikoa jirani.

Alisema mtuhumiwa alisema walishirikiana na mwenzake huyo katika kuvamia kwenye maduka mawili yanayofanya miamala ya fedha katika maeneo ya Kilimahewa kwa Msuka na kupora vitu mbalimbali kwa kutumia silaha hiyo na kufunguliwa kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha yenye namba MZN/IR/632/2017.

“Askari waliongozana hadi kwenye alikokuwa ameficha silaha, lakini ghafla mtuhumiwa alikurupuka akiwa na pingu mkononi na kuanza kukimbilia upande wa pili wa barabara kwa lengo la kutoroka. “Askari walifyatua risasi kadhaa hewani wakimuamuru asimame lakini alikaidi na ndipo walifyatua risasi wakimlenga kwenye miguu lakini kwa bahati ilimpiga sehemu za juu za kiuno, ambapo mtuhumiwa alikufa akiwa njiani kuelekea hospitalini,” alifafanua.

Vyakula Hivi Vinasababisha Saratani ! Jihadharani Navyo

$
0
0

Ugonjwa wa saratani  ama  kansa  unatajwa  kuwa  ndio  ugonjwa  wa  hatari  zaidi  duniani  na  unaoua   watu  wengi  zaidi  duniani.  Ugonjwa  huu  unasababishwa  na  mambo  mbalimbali  ikiwa  ni  pamoja  na  ulaji  wa  vyakula   vya aina  mbalimbali. Vifuatavyo  ni  baadhi  ya  vyakula  ambavyo  vimetajwa  katika  tafiti  mbalimbali  kuwa  visababishi  vya  ugonjwa  wa  saratani.

VYAKULA VYA KUKAANGA
Vyakula vingi vinavyotayarishwa kwa kukaangwa kwenye mafuta yenye moto mkali huwa na madhara kiafya na miongoni ma madhara hayo ni pamoja na kusababisha kansa ya kwenye mfuko wa uzazi. Vyakula hivyo ni pamoja na chips na vyakula vingine vinavyopikwa kwa kukaangwa kwenye mafuta.

VYAKULA VYENYE CHUMVI NYINGI
Vyakula vyenye chumvi nyingi vimebainika navyo kusababisha kansa. Vile vile inaelezwa kuwa chumvi huwa kama chakula kwa bakteria wa kansa tumboni. Kansa ya tumbo inadaiwa kuua watu wengi nchini Japan kutokana na jamii hiyo kupenda sana vyakula vyenye chumvi nyingi. Miongoni mwa vyakula vyenye chumvi nyingi ni vile vya kusindika, kama vile nyama za makopo, maharage, n.k

SUKARI
Matumizi mabaya ya sukari yanaelezwa kusababisha kansa. Kama tujuavyo, kuna aina mbalimbali za sukari lakini sukari hatari zaidi ni zile zinazowekwa kwenye vinywaji mbalimbali, zikiwemo soda, juisi za ladha ya matunda ambazo huwa na kiwango kingi cha ‘fructose’ ambayo inaelezwa kusababisha saratani ya kongosho.

Vile vile sukari kwa ujumla wake hairuhusiwi kutumiwa na mtu ambaye tayari amegundulika kuwa na kansa kwa sababu chakula cha chembechembe za saratani mara nyingi huwa ni sukari. Kwa matumizi mengine ya kawaida, sukari inatakiwa kutumiwa kwa kiwango kidogo sana katika vinywaji au vyakula tunavyotumia, tofauti na baadhai ya watu wanavyoweka sukari nyingi ili kupata utamu zaidi.


NYAMA ILIYOIVA SANA
Upikaji wa nyama kwa muda mrefu na kwenye moto mkali (high temperatures) husababisha aina fulani ya kemikali inayojulikana kitaalamu kama ‘heterocyclic aromatic amines’. Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na Chuo Kikuu cha Utah (University of Utah), umeonesha kwamba watu wanaopenda kula nyama zilizoiva sana, wako hatarini zaidi kupatwa na saratani ya njia ya haja kubwa (Rectal Cancer). Hivyo inashauriwa unapopika nyama, usipike kwenye moto mkali na kuiva kupita kiasi.

POMBE
Unywaji wa pombe kupita kiasi nao unaelezwa kusababisha aina nyingi ya saratani, kwa wake kwa waume. Aina ya saratani zinazodaiwa kusababishwa na pombe ni pamoja na satarani ya mdomo, ini, utumbo na koromeo, ambazo ndizo zinazoua watu wengi hivi sasa nchini Marekani.

NYAMA NA MAFUTA
Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Havard nchini Marekani, umegundua kwamba watu wanaopenda kula nyama kila siku wako hatarini kupatwa na saratani ya utumbo kuliko wale wanaokula mara moja moja. Pia baadhi ya mafuta ya wanyama na yale yanayowekwa kwenye ‘baga’ au ‘cheese’ huweza kusababisha kansa.

Vile vile ulaji wa vyakula vilivyotengenezwa kwa kuchanganya na nyama zilizosindikwa au kuhifadhiwa kwa matumizi ya muda mrefu husababisha saratani pia. Vyakula hivyo ni pamoja na ‘soseji’ ambazo hupendwa na watu wengi. Pia mikate ya nyama ‘hot dogs’ nayo ni chanzo cha magonjwa ya saratani.

VYAKULA VYA UNGA MWEUPE
Vyakula vyote vinavyopikwa kutokana na unga uliokobolewa na kuondolewa virutubisho vyake vyote na kuwa mweupe, vinaelezwa kuchangia magonjwa ya saratani kwa kiasi kikubwa. Vyakula hivyo ni pamoja na ‘donati’ (doughnuts), maandazi, mkate mweupe, n.k

Mwisho, licha ya kuepuka ulaji wa vyakula vilivyotajwa hapo juu, unatakiwa kuzingatia ulaji wa vyakula asilia vitokanavyo na mimea, mboga za majani na matunda kwa wingi kila siku. Utaona kwamba adui mkubwa wa afya zetu ni vyakula vyote vya kusindika na vile vya kutengenezwa viwandani au vile ambavyo wakati wa utayarisjaji wake huondolewa virutubisho vyake vya asili.

Hivyo Ndivyo Wauza Mihogo Barabarani Wanavyojiuza! Dar

$
0
0

KUFUATIA madai kuwa, baadhi ya wasichana wanaofanya biashara ya kuuza mihogo, karanga na nazi kwenye foleni za magari na mitaani jijini Dar, wanajihusisha na biashara ya kujiuza, Kikosi cha Operesheni Fichua Maovu (OFM) kiliingia kazini na hiki ndicho kilichobainika.


MADAI YA AWALI


Baadhi ya mashuhuda walioongea na Risasi Jumamosi awali walidai kuwa, akina dada hao wawapo kwenye biashara hiyo, ukiwataka pia kwa huduma ya ngono wamekuwa ni wepesi kukubali kutokana na hali ngumu kimaisha. “Hawa akina dada unaowaona wanauza mihogo kwenye mabeseni wanapiga madili pia ya kujiuza, ukiwa kwenye gari au mtaani kisha ukamtaka unaweza kuondoka naye au anakupa namba yake kisha baadaye unamtafuta, mnamalizana,” alidai kijana mmoja anayefanya kazi ya umachinga kwenye mataa ya Ubungo jijini Dar.



Kamanada wa OFM na muuza mihogo.


OFM KAZINI


Kufuatia madai hayo kushika kasi, Kamanda wa OFM akiwa ndani ya gari lake maeneo ya Stendi ya Mawasiliano kuelekea Ubungo, alikutana na dada mmoja aliyejaaliwa shepu bomba akiwa anauza mihogo na mazungumzo yakawa hivi:


OFM: Shilingi ngapi mhogo?


Mdada: Kipande au mzima?


OFM: Kipande tu. Mdada: Kuna kipande cha 200, 500 na 1,000. Karanga na nazi pia zipo, si unajua tena! OFM: Nipe kipande cha mia tano na karanga lakini pia nakutaka na wewe, unasemaje?


Mdada: Aka! Sasa hivi niko kazini.


OFM: Basi nipe namba yako, nitakutafuta baadaye. Mdada huyo muuza mihogo huku akijichekesha akataja namba yake, OFM akaisevu.


MUUZA MIHOGO WA PILI


Siku nyingine kamanda wa OFM akiwa kwenye mizunguko yake maeneo ya Sinza-Mapambano jijini Dar alikutana na mdada mwingine muuza mihogo na mazungumzo yakawa hivi:


OFM: (Huku akionekana kum changamkia kana kwamba wanajuana) nataka kipande kidogo cha nazi na muhogo pamoja na wewe mwenyewe, unasemaje?


Mdada: Mh! Wewe ule kwanza mihogo na karanga zako kisha unitafute baadaye.


OFM: Baadaye tutaonana vipi sasa?


Mdada: Simu yangu imezima chaji, niachie namba yako basi halafu nitakutafuta. OFM akamuachia namba kisha wakaagana. Saa 2.30 usiku Katika kutaka kuthibitisha kama kweli akinadada hao wanafanya biashara hiyo ya kujiuza, ilipofika saa 2.30 usiku, kamanda wa OFM alimpigia simu yule dada wa kwanza, mazungumzo yakawa hivi;


OFM: Mambo?


 Mdada: Poa, nani?


OFM: Najua huna namba yangu, mimi tulikutana pale Ubungo mataa, ukanipa namba yako.


Mdada: Aaa! Nimekukumbuka, niambie, nakusikiliza.


OFM: Ni hivi, mimi nimevutiwa na wewe, nakutaka kimapenzi, nikuandalie shilingi ngapi?


Mdada: Mh! kwani uko wapi?


OFM: Hapa Mwenge. Vipi unaweza kuja?


Mdada: Saa hizi itakuwa ngumu maana naishi mbali, tufanye kesho. Mwingine aingia mzimamzima Katika utafiti huo, OFM ilifanikiwa kukutana na dada mmoja anayeuza mihogo maeneo ya Buguruni Chama na alipotakiwa kutoa huduma ya ngono aliweka wazi kuwa, kama ni kulala aandaliwe 20,000 lakini kwa ‘short time’ ni 5,000!


Chanzo: Global Publishers

Aunt Ezekieli Ahahaa Kufuta Skendo Zake Mbele ya Mwanaye..!!!

$
0
0

UKIGUSA ‘Top 5’ ya wasanii wakike wanaofanya vyema kwenye tasnia ya filamu nchini, jina la Aunt Ezekiel ni lazima liwemo ndani yake. Hii imekuja baada ya kuweza kuhimili mabadiliko makubwa yaliyotokea na kuwapoteza wasanii wengi wenye haiba kama yake.

Tulianza kumfahamu pale alipolitwaa taji la urembo jijini Mwanza na kufanikiwa kuliwakilisha Jiji hilo kwenye mashindano ya Miss Tanzania mwaka 2006. Fursa hiyo ilimpa tiketi ya moja kwa moja kuingia kwenye tasnia ya filamu.

Miss Bongo, ni filamu yake ya kwanza iliyodhihirisha ubora alionao pale anapokuwa mbela ya kamera. Chini ya mwongozaji Willium Mtitu anayemiliki kampuni ya 5 Effect tulianza kumuona Aunt Ezekeil akikua kisanaa.

APATA MASHAVU KIBAO

Baada ya kufanya kile kilichowashtua wengi kwenye filamu ya Miss Bongo, Aunt Ezekiel akaanza kupata dili za kushiriki kwenye filamu nyingine nyingi zilizoandaliwa na waongozaji wakubwa Tanzania.

Miongoni mwa filamu hizo ni Yellow Banana, Eyes On Me, Jungu la Urithi, Shoga Yangu, Siri Sirini, Signature, Nampenda Mke Wangu, Young Billionaire, Danger Zone na Mrembo Kikojozi iliyozidi kumpandisha chati.

SKENDO ZAMPA CHATI

Zaidi ya filamu 40 alizocheza mpaka sasa zimetosha kumpa umaarufu. Ustaa huo ulimfanya aanze kuhusishwa na skendo za hapa na pale ambazo zilifanya jina lake lisikauke kwenye midomo ya wapenda burudani.

Licha ya mazuri mengi aliyowahi kuyafanya lakini pale alipoteleza kama binadamu na kujikuta akiwa kwenye dimbwi la skendo, habari zilikuwa kubwa zaidi na hakika ustaa wake uliongezeka kufuatia kuzungumzwa sana.

Skendo kama kutoka na mume wa mtu, kuolewa na kuachika, kuishi kinyumba na mfanyabiashara maarufu ni matukio yaliyompandisha chati kipindi hicho ustaa wake umeshika hatumu.

HOFU YA SKENDO KUMFIKIA MWANAYE

Aunt Ezekiel amekuwa mtu mzima sasa. Ni mama wa mtoto mmoja anayeitwa Cookie aliyezaa na dansa wa Diamond Platnumz, Mose Iyobo, hivyo mambo aliyokuwa anayafanya kipindi cha nyuma ni lazima ayaache ili mwanaye aweze kujifunza mema kutoka kwa mama.

 “Kwa wakati ule nilikuwa sijui madhara yake ila kwa sasa naona  katika mambo ambayo yatanifedhehesha basi ni skendo nilizonazo, mwanangu Cookie akizisikia au kuziona hii inaniumiza sana kichwa,

“Sitahitaji mwanangu ayapitie maisha niliyopitia mimi, sikujua kama ningeweza kujulikana kwa kufanya kazi zangu pekee, nahisi akijua mabaya yangu nitakosa pa kuficha sura ,” anasema Aunt.

ADHAMIRIA KUFUTA MAKOSA

Aidha alifafanua kuwa hivi sasa ameamua kubadili mfumo wa maisha yake ili afute yale yote mabaya aliyowahi kuyafanya na ikitokea mwanaye Cookie akisikia skendo zake asiweze kuamini.

NENO KWA CHIPUKIZI WAPENDA KIKI

Staa huyo amewataka wasanii wachanga kulinda heshima zao kwa kupata sifa kutokana na kufanya kazi na siyo kutokana matendo machafu kwani baadaye matendo hayo yatakuja kuwasuta na kuwasumbua kwenye maisha.

“Sasa  hivi nimeamini na nitawafunza wasichana wengine wafahamu kuwa mbali na maisha ya usichana wanatakiwa wafikirie maisha yanayokuja na madhara yake, wakifanya hivyo watakuwa vioo vya kutazamwa na jamii,” alisema Aunt.

SKENDO ZAYUMBISHA SOKO

Kumekuwa na hali ya sintofahamu kwenye tasnia ya filamu, wadau wanalalamika kuyumba kwa soko la filamu nchini, hali hiyo Aunt Ezekiel anasema matendo machafu ya wasanii yamechangia kwa namna moja ama nyingine kporonmoka kwa soko.

“Kipindi hiki filamu zimepoteza mvuto na watu wamekuwa wakizungumza mengi ila ninachoona mimi ni matendo yetu machafu yanachangia, mbona wasanii kama kina King Majuto bado wanafanya vizuri? Skendo zinayumbisha soko la filamu na siyo kitu kingine,” anasema.

Pitia Vichwa cha Magazeti ya Leo Jumapili 29/1/2017..!!!


Diamond Awakomesha Ali Kiba na Wema Instgram...!!!

$
0
0

MREMBO asiyeishiwa matukio kila kukicha Bongo, Wema Isaac Sepetu na msanii wa Bongo Fleva anayewika kwa wimbo wake Aje, Ali Kiba, mwisho wa wiki hii wamenagukia pua katika mitandao ya kijamii na Diamond Platnumz ameendelea kuwaonyesha kuwa yeye ana nguvu kuwazidi wao mtandaoni.

Awali iliripotiwa kuwa Wema amefuta picha zake zote katika mtandao wake wa Instagram kwa shabaha ya kurudi kwa kishindo na kuwaonyesha watu kuwa yeye ndiye malkia wa mtandao huo hapa nchini. Jitihada zake ziligonga mwamba pale aliporejea na kutegemea mapokezi makubwa na haikuwa hivyo. Daimond aliweka video ya familia yake iliyowaonyesha laivu akiwa na mkewe na mwanaye Tiffa Dangote.

Video hiyo ilipata watazamaji 20,708 na wachangiaji zaidi ya 600 na kusababisha watu wengi kuacha kumzingatia Wema na kurudi kwa Diamond. 

Aidha Ali Kiba amekuwa akiendelea kushushiwa matusi na kupewa lawama na mashabiki zake baada ya kuonekana mahojioano kupitia vituo mbalimbali vya televisheni akisema kuwa yeye hapo alipofika ni juhudi zake.


Mashabiki zake hawakupendezwa na kauli hiyo na kuitafsiri kama majigambo. 

Alikiba, Yazingatie Malalamiko ya Mashabiki Wako..!!!!

$
0
0

Ali Saleh Kiba al maarufu kama Alikiba ni miongoni mwa wasanii wakongwe na wakubwa Tanzania, Afrika Mashariki na pengine Afrika kwa ujumla. Ni mshindi wa tuzo zaidi ya 14 kwa mwaka 2016 ikiwezo tunzo kubwa kabisa za MTV EMA kwa kipengele cha Best African Act.

Kwa mafanikio makubwa aliyoyapata mwaka jana ikiwemo kupata mkataba mnono wa kampuni kubwa ya muziki duniani yaani Sony Music na kushinda tuzo zote hizo ndani ya mwaka 2016 ni wazi kabisa kuwa thamani ya Alikiba imepanda maradufu barani Afrika na pengine kila mfuatiliaji wa muziki Afrika angependa zaidi kumfahamu Alikiba, kufahamu kazi zake, ni wapi ametoka na wapi anakwenda.

Sekeseke lilitokea mwaka jana kwenye show ya Mombasa rocks iliyofanyika mjini Mombasa, Kenya kati ya Wizkid na Alikiba ni moja kati ya mambo ambayo yalifanya jina la Alikiba lizungumzwe sana barani Afrika haswa Tanzania, Kenya na Nigeria ambapo mitandao mbalimbali ya Nigeria iliripoti kua Alikiba anatrend sana nchini Nigeria.

Ushindi wa MTV EMA pia ambao awali alipewa Wizkid kabla haujatenguliwa na kupewa Alikiba ni mambo yaliyofanya apate attention zaidi kwenye soko la muziki barani Afrika.

Kutrend ni kitu muhimu sana katika soko la muziki kwa sasa, wasanii wengi duniani kote hata mpaka Marekani wamekuwa wakitengeneza kiki kabla ya kuachia kazi zao mpya ili kupata attention. Nafahamu kuwa msanii Alikiba amekuwa sio muumini mzuri sana wa kiki, lakini kiki kama hizi ambazo zinajitengeneza zenyewe ni dhambi kubwa kuacha kuzitumia kibiashara sababu kuna wanaotamani kutrend hata kwa kutembea uchi lakini hawazipati.

Mapema mwaka huu Alikiba alitangaza ratiba ya World Tour yake itakayoanzia South Africa kisha America na kumalizikia barani Ulaya. Kwa mujibu wa ratiba kutoka kwenye posters zake alizozipost Instagram Tour yake inaanza February mwaka huu. Hivyo mpaka ninaandika makala hii zimebaki siku tatu kufikia mwezi February.

Kati ya sehemu ngumu sana kupenya kimuziki barani basi ni Afrika Kusini na hii imetokana na ‘wasauzi’ kuthamini sana muziki wao na haikushangaza licha ya jina kubwa alilojijengea Diamond Platnumz kwenye kiwanda cha muziki barani Africa aliwahi kaririwa akisema amefanya collaboration na AKA ili kupenyeza muziki wake África Kusini.

Sasa wasiwasi wangu ni je? Alikiba anategemea kujaza viti kwa kuitegemea nyimbo ya Aje pekee? Target yake kwenye hii tour ni kuifanya iwe ya kidunia au analenga waTanzania pekee wanaoishi kwenye nchi husika? Aliahidi atatoa Aje remix ambayo ni nyimbo aliyoimba na msanii kutoka Nigeria MI Abaga lakini mpaka zimebaki siku tatu kabla hatujaingia mwezi anaoanza tour hakuna dalili ya hiyo nyimbo?

Binafsi nilidhani ingekuWa sahihi sana kama angeachia nyimbo ambayo amesharekodi mama mkongwe Yvonne Chakachaka kwa lengo la kuiteka zaidi South Africa kibiashara zaidi ili jina lake liwe kubwa nchini humo hata wakati wa Tour yake angetumia pia na fursa hiyo kufanya media tour kuitambulisha zaidi hiyo ngoma.

Nadhani si Mimi ila asilimia 98 ya mashabiki hawaridhishwi na namna ambayo Alikiba amekuwa slow sana na kutojua namna soko la mUziki linavyoenda na nini linataka. Ni jana kupitia mtandao wa instagram msanii wa maigizo ambaye pia ni shabiki mkubwa wa msanii Alikiba alipost kipande cha screenshot kikionesha ujumbe aliotumiwa na shabiki mwingine wa Alikiba DM kua Ali atapoteza mashabiki wake sababu hawapi raha wanayoitaka, siku zote amekuwa mtu wa kujiamini na kuwasibirisha mashabiki wake ambao ukweli bila wao asingekua hapo halipo leo.

Mwaka mpya umeanza kwa kasi kweli kila mtu yuko kasi lakini naona Alikiba bado yule yule.

Mrirthi wa Kanumba Aunguzwa na Kemikali Usoni..!!!

$
0
0

Kumekuwa na tatizo kubwa katika mfumo mzima wa uandaaji wa filamu hapa Tanzania hasa katika suala la kuandaa wasanii ili kuleta uhalisia wa kazi husika.
Kiajana aliyetambuishwa na mama wa aliyekuwa nguli wa filamu hapa nchini, Steven Kanumba, Flora Mtegoa kuwa ndiye mrithi wa mwanane huyo kwenye tasnia ya uigizaji, Fred Swai amekumbwa na balaa ambalo ameeleza kuwa hatolisahau katika maisha yake baada kuunguzwa vibaya na kemikali usoni katika harakati za kuandaa filamu.
Akizungumza kwenye Kipindi maalum cha Exclusive Interview kupitia Global TV Online, Swai amesema kuwa siku hiyo aliitwa kwenda kucheza kipande cha muvi ambacho alitakiwa aigize kama mgonjwa.
Hivyo muandaaji alimtaja afungwe bandeji usoni ili kuonesha uhalisia wa mgonjwa, ambapo bandeji hiyo ililowanishwa na kemikali zinazotumika kusafishia vidonda, iodine solution.
Swai aliendelea kueleza kuwa, badala ya kulowanishiwa iodine ya kawaida isiyo kali (diluted solution) aliwekewa concentrated iodine ambayo ni kali zaidi hivyo kuunguza sehemu ya paji la uso.
Hii imekuja ikiwa ni siku chache tu baada ya Muigizaji wa Nigeria, Kuchomwa Moto wakati wakishuti video.

Picha: Dunia Yampinga Trump Baada ya Marufuku kwa Waislamu Kuingia Marekani Kuanza Jumamosi Hii..!!!

$
0
0


Uamuzi wa Donald Trump kupiga marufuku wahamiaji wa kiislamu kutoka kwenye nchi zenye raia wengi wa dini hiyo, umesababisha hasira kuu duniani kote na wahamiaji wakikataliwa kupanda ndege kuingia Marekani.

Raia waliokuwa na hati za kusafiria kutoka Iran, Iraq, Libya, Somalia, Sudan, Syria na Yemen walizuiliwa kwenye viwanja vya ndege, wakati wale waliokuwa wameshapanda ndege walishikiliwa baada ya kutua Marekani.

Katika tukio moja, abiria watano wa Iraq na mmoja wa Yemeni, waliokuwa na visa halali, walizuiliwa kupanda ndege ya EgyptAir iliyokuwa ikitoka Cairo kwenda New York na hatimaye kuelekezwa kwenye ndege zinazorudi kwenye nchi zao.

Mwanamke mmoja aliyekiambia mauaji ya Isis nchini Iraq mwaka 2014, alizuiliwa kupanda ndege mjini Baghdad, baada ya kusubiria visa kwa miezi mingi ili akaungane na mumewe ambaye tayari yupo Marekani. Rais Trump amepiga marufuku kwa miezi mitatu wakimbizi toka nchi saba duniani, ili kuchuja magaidi wa kiislamu wasiingie nchini humo.

Wakimbizi kutoka Syria wamepigwa marufuku kimoja.

Hata hivyo, jaji mmoja alitoa ruhusa Jumamosi kwa raia kutoka nchi hizio saba waliokuwa wameshaingia nchini humo, wale waliokuwa njiani, wenye visa halali kukaa Marekani. Waandamaji kadhaa walikusanyika kwenye viwanja vya ndege nchini Marekani Jumamosi hii kupinga uamuzi huo wa Trump. Maandamano zaidi yatafanyika Jumapili hii.


Breaking News: Waliofukiwa na Kifusi Mgodini Geita Waokolewa Wote

$
0
0

WATU 15 waliofukiwa kwa kifusi katika mgodi wa dhahabu wa Kampuni ya RZ Union Mining Ltd uliopo Kata ya Nyarugusu mkoani Geita, wameokolewa wote wakiwa hai kutokana na  jitihada zilizofanywa na wataalamu wa mgodi huo na mingine kwa kushirikiana na serikali.

 Habari zilizotufikia punde ni kwamba watu hao wameokolewa baada ya kukaa takribani siku tatu ndani ya mgodi bila kupata chakula na bila kuona mwanga wa jua.

Aidha, taarifa za awali zinasema kuwa baada ya kuokolewa watu hao  wamewekwa chini ya uangalizi wa 
karibu na wataalamu wanaendelea na uchunguzi huo ambapo baada ya muda itatolewa ripoti kamili.

Viewing all 104809 articles
Browse latest View live




Latest Images