Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104793 articles
Browse latest View live

Hivi ndivyo Rais Magufuli Alivyoiwakilisha Nchi Kwenye Kikao cha Viongozi wa Afrika..!!

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Manuel Olveira Guterres wakati alipokuwa kwenye mojawapo ya vikao vya Umoja wa Afrika (AU) vinavyofanyika katika Makao makuu yake mjini Addis Ababa nchini Ethipia. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati alipokuwa kwenye mojawapo ya vikao vya Umoja wa Afrika (AU) vinavyofanyika katika Makao makuu yake mjini Addis Ababa nchini Ethipia. PICHA NA IKULU

Kutana na Maalim Hussein Mtabibu wa Nyota za Binadamu Africa na Dunia Nzima,

$
0
0

Kutana na Maalim Hussein Mtabibu wa nyota za binadamu Africa na dunia nzima,
Anatoa TIBA MAENEO YOTE NCHINI, KWA WALE WENYE KUHITAJI TIBA ANATIBU YAFUATAYO,
Husafisha nyota na kutoa Pete za bahati na kwa wale walia sumbuka kwaajili ya matiba na hawakufanikiwa njoo ujionee muujiza wa papo kwa papo-humpa mtu jini la mali kwa yule anaetaka kumiliki mali bila masharti yoyote,
Anatibu magonjwa yalio shindikana-Mpenzi/MUME/MKE Aliekukimbia Anakurudishia Ndani ya saa 72 tu, Pia tunatoa dawa za Nguvu za KIUME na Kurefusha kwa saizi unayo Taka-Anatoa Dawa za BIASHARA NA MVUTO-Tunatoa Dawa za Uzazi kwa kina Mama kwa wale wenye Tatizo Sugu-Anatoa Zindiko ya Nyumba,Mwili, na Mvuto kazini- Tunamaliza kesi zilizo kaa muda Mrefu bila kumalizika, Tung'arisha Nyota na Cheo kazini. Tunarudisha Mali zilizopotea au Kuibiwa na Mengine Mengi ya Siri tuwasiliane kwa Simu-Whatsapp +255674835107
+255 629254849

Ombeni Sefue Apata Shabu Jipya Umoja wa Nchi za Afrika,Hiki Hapa Ndio Cheo Chake Kipya..!!!

$
0
0

Mwanadiplomasia mahiri wa Tanzania aliyepata pia kuwa Katibu Kiongozi-Ikulu, Balozi Ombeni Sefue ameteuliwa kuwa Mtanzania wa kwanza kuingia katika Jopo la Watu Mashuhuri katika Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM).

Kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa APRM tawi la Tanzania, Rehema Twalib anayehudhuria mikutano ya Umoja wa Afrika na APRM mjini Addis Ababa, Ethiopia, Balozi Sefue ameidhinishwa kwenye kikao cha juu ya Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika ambao ni wanachama wa APRM kilichofanyika juzi Jumamosi mchana.

“Haikuwa kazi rahisi kupata nafasi hii. Nchi nyingi za Afrika zilileta majina ya watu wao mashuhuri ili kuingia katika jopo hili muhimu. Balozi Sefue licha ya kuwa na utumishi uliotukuka kama mwanadiplomasia mkongwe pia aliungwa mkono kwa nguvu zote na Serikali ya Awamu ya Tano ya Tanzania,” alisema Katibu Mtendaji huyo.

APRM ni Mpango wa Afrika uliobuniwa na Wakuu wa Umoja wa Afrika kwa lengo la kuwa na chombo kitakachosaidia kuhimiza nchi wanachama kuenzi utawala bora na utoaji wa huduma bora za kiuchumi, biashara na za kujamii kwa wananchi wao kupitia mfumo wa kujitathmini zenyewe na kukosoana.

Kwa mujibu wa tovuti ya APRM, Jopo la Watu Mashuhuri ni chombo cha juu cha kuwashauri Wakuu wa Nchi Wanachama wa APRM katika uendeshaji wa Mpango huo na husimamia mchakato mzima wa kujitathmini.

Wajumbe wa jopo hilo ambao hudumu hadi miaka minne hupendekezwa na nchi zao na baada ya mchakato mrefu wenye ushindani majina ya waliokidhi vigezo huwasilishwa na kuidhinishwa na na kikao cha juu katika APRM-Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali.

Tanzania ni miongoni mwa wanachama 35 kati ya nchi 54 wa Nchi za AU zilizojiunga na APRM na ilijiunga rasmi na Mpango huo tangu mwaka 2004.Tayari Tanzania ilishafanyiwa tathmini ya kwanza ya utawala bora na inaendelea kutekeleza mapendekezo yaliyotolewa.

Katika mkutano huo Mwenyekiti wa Wakuu wa Nchi za APRM Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya aliwapongeza wajumbe wa jopo hilo na kuwata kushiriki vyema katika kuihuisha APRM na kuwa chombo chenye thamani kubwa kwa Afrika kama walivyotarajia waasisi wake akina Thabo Mbeki, Olusegun Obasanjo, Benjamin Mkapa na wengine.

Balozi Sefue ataungana na wajumbe wengine wapya ambao ni pamoja na Prof. Ibrahim Agboola Gambari (Nigeria), Balozi Mona Omar Attia (Misri) Bi. Fatma Zohra Karadia (Algeria), Askofu Don Dinis Salomão Sengulane (Msumbiji) na Prof. Augustin Loada (Burkina Faso). Wajumbe wa zamani wanaoendelea ni pamoja na  Prof. Youssouf Khayal (Chad) ambaye kwa sasa atakuwa Mwenyekiti wa Jopo hilo na Brigitte Mabandla (Afrika Kusini) ambaye atakuwa Makamu Mwenyekiti.

Mkutano huo pia ulijadili Ripoti za tathmini za nchi katika maeneo anuai ya utawala bora kwa nchi za Kenya (ikiwa ni ripoti ya pili kuwasilishwa), Sudan, Chad, Senegal, Djibouti pamoja na ripoti ya utekelezaji ya Zambia.

Huenda hii ikakusaidia siku Moja ili Usiibiwe Hela Kwenye ATM

$
0
0

Endapo utavamiwa na majambazi na wakakulazimisha kuwatolea pesa kwenye ATM, ili kuokoa maisha yako, wala usitaharuki.

Unachopaswa kufanya ni kuingiza namba ya siri kinyume. Kwa mfano kama namba yako siri ni 1234, basi ingiza kama 4321.

Ukimaliza tu kuingiza tarakimu hizo, pesa zitaanza kutoka lakini zitakwama katikati. Ikitokea hivyo, taarifa kwamba kuna uhalifu unatendeka kwenye ATM hiyo itatumwa kwa Afisa Usalama wa benki husika na Kikosi cha Polisi bila ya 
m/wahalifu kujua.

Kila ATM ina mfumo huu, bahati mbaya ni kwamba mabenki hawawaelimishi wateja wao kuhusu tahadhari hii.

Wasambazie taarifa hii ndugu, jamaa na marafiki wote, huenda ukaokoa maisha ya mmoja wao.

Pichaa..Rais Magufuli Akihutubia Katika Umoja wa Afrika Leo,Tazama Hapa Livee..!!!

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na viongozi wa mataifa mabalimbali wakiwa katika picha ya pamoja katika jengo jipya la kituo cha  Amani na Usalama (JULIUS NYERERE) lililopo katika Makao makuu ya Umoja wa Afrika Addis Ababa nchini Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia Viongozi Wakuu wa Mataifa mbalimbali hawapo (pichani) katika Jengo jipya la Kituo cha Amani na Usalama kilichopewa jina Rasmi la Mwalimu Julius Nyerere, Addis Ababa nchini Ethiopia.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kutangazwa rasmi kwa Jina la Mwalimu Julius Nyerere katika kituo hicho cha Amani na Usalama.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Rais wa Rwanda Paul Kagame wakati wakielekea katika Kituo cha Amani na Usalama cha Makao Makuu ya Umoja wa Afrika kilichopewa jina la Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere, Addis Abba nchini Ethiopia. PICHA NA IKULU




Duh..!!! Vunja Mbavu na Kiingereza cha Mbwana Samatta Huko Ulaya Wakati Akihojiwa na Wazungu(Video)

Hatarii..Gigy Money Asambaza Video Yake Akipapaswa Sehemu Zake za Siri(+18 VIdeo)

$
0
0

Katika Hali Isiyo ya Kawaida,Video Queen wa Bongo Fleva Gigy Money amewaacha watu kinywa wazi ambapo alidhubutu kujirekodi video akichezewa sehemu zake za siri na bwana wake na kuiweka mitandaoni.

Katika pia huku na kule Hii hapa Video Yenyewe itazame

Picha: Treni ya Abiria Yapata Ajali ikitokea Kigoma Kwenda Dar

$
0
0
Treni ya abiria ya EXPRESS ikitokea Kigoma kuelekea Dar es salaam leo January 29 2017 imepata ajali maeneo ya Ruvu ndani ya mkoa wa Pwani ikiwa ni kilometa kadhaa kabla ya kufika kwenye jiji la Dar es salaam.
Shuhuda ambaye alikua ndani ya Treni hiyo amesema Behewa zaidi ya 10 zimepinduka na watu wanaendelea kuokolewa kwa kupitia Madirishani.



Huyu Ndio Faru Fausta wa Ngorongoro, Atimiza Miaka 54, Aishi Chini ya Ulinzi wa Kijeshi Masaa 24

$
0
0
FARU FAUSTA WA NGORONGORO ATIMIZA MIAKA 54
Ndio faru mzee duniani,sasa haoni
.Ngorongoro yampa ulinzi wa kijeshi

FARU Fausta ndio anayesadikiwa kuwa na umri mkubwa kuliko Faru wote duniani,mwaka huu amefikisha umri wa miaka 54.

Faru Fausta yupo katika mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro,lakini kutokana na uzee wake huo,sasa anakabiliwa na tatizo la macho la kutoona.
Kufuatia hatua hiyo,uongozi wa Ngorongoro sasa umemuweka katika makazi maalum ndani ya hifadhi hiyo.

Hatua ya mamlaka kuchukua hatua ya kumpa ulinzi maalum Faru Fausta inahofia kushambuliwa na wanyama wengine wakali na hususani fisi na Simba.
Hivi sasa gharama inayotumika kumlinda Faru Fausta ni kubwa,hivyo uongozi wa Mamlaka umeishauri wizara kuchukua
hatua juu ya Faru Fausta

Zari Rapper Aibuka: Rapa Mpya wa Kike Anayekuja Kuishika Bongo

$
0
0
Baada ya kuibuka kwa harmo rapper na chibu rapper sasa kaibuka rapper mpya wa kike aitwaye Zari rapper

Mwana FA: AY Alinitosa Kwenye Collabo ya Zigo Remix

$
0
0
Pamoja na urafiki au ukaribu uliopo kati ya Mwana FA na AY lakini kumbe inapofika kwenye kazi huwa inakua tofauti. Mwana FA amesema kuna kolabo ambayo aliomba kushiriki lakini nae ‘akatoswa’ na ameitaja wazi kolabo ambayo aliomba kuifanya ni 'Zigo Remix'.

"Kolabo niliyoomba ni Zigo. Kwanza mimi niliitaka mwanzoni kabisa nikamwambia eh bwana eh mi naomba hii. Sasa AY akaitoa halafu akanipa beat fanya hiyo kama unataka. Nikamwambia umeshatoa mimi sitaki tena". 

"Akaja akafanya Remix na Diamond halafu nilipoisikia nikasema eeh bwana ehe humu kama ningekuwa nimepitisha kumi na sita zangu ingekuwa fresh kweli lakini ikawa imeshatoka"

Miujiza ya Shekh Sharifu Rashid Kutoka Bagamoyo , Anarudisha Mapenzi na Kusafisha Nyota

$
0
0

MIUJIZA YA SHEKH SHARIFU RASHID KUTOKA BAGAMOYO PWANI, (RUDISHA MAHUSIANO YAKO NDANI YA MASAA 48 TU) ASANTE KWA KUENDELEA KUMPIGIA SIMU SHEKH SHARIFU RASHID KWA WALE WENYE MATATIZO NA WALE WANAOTOA SHUKRANI:

SHEKH SHARIFU RASHIDI ni mtaalamu wa tiba mbalimbali za asili, anatumia kitabu cha quran, dawa za asili, dawa za kiarabu na majini, anazo dawa za mapenzi, nguvu za kiume, chango, ngiri maji na n.k, anakuvutia mpenzi alie kuacha au alie mbali, pia anatoa pete za bahati zilizoambatanishwa na jini mali kulingana na nyota yako, anaouwezo mkubwa wa kutumia jina la muhusika kwa kutatua tatizo lako, anaouwezo wa kumrudisha mtu aliepotea kimiujiza, pia anatibu kwa njia ya simu popote ulipo,

WASILIANA NAE KWA SIMU NA WHATSAPP NO: 0718-668347. 0685-224047, 0767-204308 na 0627-251404 au follow@shekh_sharifu_rashid, Email:shekhsharifurashid@gmail.com

Tabia za Wanawake Kulingana na Maumbile yao

$
0
0

Inasemekana wadada wana tabia tofauti katika mapenzi kulingana na maumbo ya miili yao,


  1. Wasichana wafupi wanaongoza kwa wivu wa mapenzi na kuwajali wapenzi wao
  2. Wasichana warefu huwa hawawajali wapenzi wao na hawaogopi mahusiano kuvunjia hawajui kubembeleza hata kidogo
  3. Wasichana wenye DIMPOZ, MWANYA, MATEGE MBINUKO, MAHIPS NA KITHEMBE, hawa huongoza kwa kutokuwa WAAMINIFU katika mapenzi.
  4. Wasichana WANENE huongoza kwa MAPENZI YA KWELI yaani akipenda amependa kweli
  5. Wasichana WEMBAMBA hawa huwa ni WABISHI sana na hawa wanaongoza kwa kutendwa!
  6. Wasichana wenye NGOZI NYEUSI wanaongoza kwa KUTOA MIMBA na kupenda wanaume warefu na weupe
  7. Wasichana weupe wakiongoza kwa kuzalia nyumbani, na hawa weupe wengi wao huolewa wakiwa na watoto tayari huku wakipenda kuolewa na waarabu kuliko wanaume weusi.


Je kuna ukweli hapo?

Maalim Seif Ajipa Matumaini ya Kuwa Rais wa Zanzibar Siku Moja.Haya Ndiyo Aliyoenda Kuwaambia Marais wa Dunia Kuhusu Zanzibar..!!!

$
0
0

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad bado anaamini atakuwa Rais wa Zanzibar akidai kwamba nchi alizopeleka malalamiko yake zimefikia katika hatua nzuri.

Tangu kufutwa kwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 28, 2015, Maalim Seif amekuwa akitoa kauli za matumaini akisema: “Mambo yaelekea kuwa mazuri.”

Hata hivyo, Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein aliyeshinda katika uchaguzi wa marudio wa Machi 20, 2016 ambao Maalim Seif aligoma kushiriki, amekuwa akisema kwamba hakuna mtu yeyote anayeweza kumwondoa madarakani, awe wa ndani au nje ya nchi.

Akizungumza katika kipindi cha Funguka kinachoendeshwa na Tido Mhando kupitia Kituo cha Televisheni cha Azam, Maalim Seif alisema wananchi wasifikiri kuwa mataifa hayo yamenyamaza, bali suala hilo litapatiwa ufumbuzi na atapata haki yake hivi karibuni.

Inasikitisha Mnoo..Soma Hapa Alichokisimulia Mmoja ya Waliofukiwa na Kifusi Mgodini Jinsi Walivyokuwa Wanaishi Chini ya Ardhi Kwa siku Tano..!!!

$
0
0

Uji, biskuti na maji waliyotushushia jana ndivyo vilivyorudisha uhai wetu,” hayo ni maneno ya mmoja kati ya wachimbaji 15 waliookolewa katika mgodi wa RZ walikokuwa wamefukiwa na kifusi kwa siku tano.

Mchimbaji huyo, Mgalula Kayanda alisema hali yao ilikuwa mbaya na mwenzao mmoja alishakata kauli lakini maji yaliwafanya wawe na nguvu.

Na niliamini hata nisipotoka leo, sitakufa tena,” alisema baada ya wote kuokolewa jana.

Kayanda alisema waliingia mgodini saa nne usiku na kuanza shughuli za uchimbaji na saa nane usiku walisikia kishindo kikubwa huku wenzao wakiwaita watoke nje.

“Tukiwa chini tulisikia tukiitwa na waliokuwa nje, wakitueleza tusogee kunatitia, baada ya kusikia wote tukakaa sehemu moja na ghafla umeme ukakata, kukawa giza, hakuna mawasiliano na hewa ikawa haingii,” alisema.

Huku wakiwa hawajui majira kutokana na giza, mpira mmoja wa kupitisha hewa ulianza kufanya kazi na kuwapa tumaini, lakini changamoto kubwa ilikuwa njaa.

Mwenzake Jackson Lucas,  mwenyeji wa Tabora alisema walikua umbali wa mita 100 chini ya ardhi lakini walipopata taarifa kutoka kwa wenzao kuwa ardhi inatitia, walipanda na kukaa sehemu moja kusubiri muujiza wa Mungu.

Lucas alisema hali mbaya ya hewa iliyosababishwa na harufu ya kinyesi ilikuwa moja ya changamoto ya kukaa katika shimo hilo kwa siku nne.

Hata hivyo, juzi msemaji wa kampuni ya RZ, Francis Kiganga alisema shimo lililofukiwa na udongo lina urefu wa mita 38 kwenda chini na pembeni kuna njia yenye urefu wa mita nyingine 38.

Mgogoro Kanisa Anglikana Wachukua Sura Mpya,Askofu Mokiwa Atishia Kupasua Jipu..!!!

$
0
0

Askofu wa Kanisa Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam, Dk Valentino Mokiwa amesema ataweka hadharani vitu anavyodai vitaonyesha ukweli wa mgogoro uliopo katika dayosisi hiyo anayoiongoza.

Amesema baada ya siku saba, atawasilisha kwa waumini vitu vitakavyoeleza ukweli wa mambo kuhusu mgogoro unaondelea sasa.

Hivi karibuni, Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Dk Jacob Chimeledya alimtaka Mokiwa kujiuzulu kwa madai kwamba anatumia vibaya madaraka yake huku akimtuhumu pia kwa ubadhirifu wa fedha.

Hata hivyo, Askofu Mokiwa alikana madai hayo na kusema mgogoro huo unatengenezwa na adui zake jambo linawavunja mioyo waumini.

Jana, akiweka jiwe la msingi la Kanisa la Kigango cha Mtakatifu Simon na Yuda, lililopo Kimara Mavurunza ‘A’, Askofu Mokiwa alisema:

“Nipeni wiki  hii inayoaanza kesho (leo), nikichelewa wiki moja na nusu nitawaeleza ukweli; hakuna kitu kilichoibwa wala kukosewa, isipokuwa waliokosea wanataka kutuvuruga.

Radi ya Ajabu Yawaachia Vilio Wakazi wa Tukuyu...!!

$
0
0

Mtu mmoja amekufa na wengine wanne kujeruhiwa mjini Tukuyu wilayani hapa, baada ya radi kuupiga mti uliokuwa karibu na banda walipojihifadhi wakati mvua ikinyesha.

Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita karibu na vituo viwili vya mabasi ya daladala na  yaendayo mikoani kandokando  ya Barabara ya Mbeya-Malawi.

Mkuu wa Wilaya ya Rungwe,  Chalya Nyangidu alisema tukio hilo lilitokea juzi saa saba mchana   na kwamba aliyefariki dunia ni mkazi wa jijini Arusha, Freeman Swai (35) ambaye alifika mkoani hapa kununua ndizi.

Waliojeruhiwa na kupelekwa Hospitali ya Makandana ni Oliva Ipyana (45), Anna Jericho (30), Juliana Francis (32) na Stela Nsile (37) wakazi wa wilayani hapa.

Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Dk Marco Mbata alithibitisha kupokea mwili wa Swai na majeruhi wanne. Alisema baada ya uchunguzi ilibainika, Swai aliungua kwa moto wa radi na kusaidiana na simu iliyokuwa ikitumia kupiga muziki.

Duh..Rais Magufuli Awapasukia ya Moyoni Viongozi wa Afrika,Ataka Wayafuate ..!!!

$
0
0

JENGO la Amani na Usalama lililopo Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa nchini Ethiopia, limetangazwa rasmi kuwa litaitwa Mwalimu Julius Nyerere.

Jengo hilo limepewa jina hilo rasmi katika hafla ya chakula cha mchana, iliyofanyika jana na kuhudhuriwa na Rais John Magufuli pamoja na marais mbalimbali wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, mawaziri na mabalozi mbalimbali wanaohudhuria Mkutano wa 28 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika unaoendelea mjini humo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu, akizungumza katika hafla hiyo, Rais Magufuli aliwashukuru viongozi wote wa AU kwa kuamua jengo hilo liitwe jina la Mwalimu Julius Nyerere ikiwa ni kutambua mchango wake katika kupigania amani na usalama na alibainisha kuwa Mwalimu Nyerere alikuwa Mwafrika halisi na kiongozi mahiri na shupavu.

“Na kwa hakika naweza kusema kuwa alikuwa mmoja wa viongozi bora kabisa ambaye amewahi kutokea katika Bara letu, katika maisha yake yote Mwalimu Nyerere alipambana ili kujenga umoja na mshikamano miongoni mwa Afrika, alikuwa mmoja wa waanzilishi wa umoja huu, sisi Watanzania kwa hakika tunajivunia sana Mwalimu Nyerere kuwa Baba wa Taifa,” alisema Dk Magufuli.

Dk Magufuli aliongeza kuwa Mwalimu Nyerere alitoa mchango mkubwa katika kupambana na ubaguzi na unyonyaji wa kila aina, alisaidia ukombozi wa nchi nyingi za Afrika, na hata alipong’atuka katika hatamu za uongozi wa Taifa la Tanzania aliendelea kutoa mchango wake kupigania amani katika nchi za Afrika.

“Wito wangu kwenu, waheshimiwa viongozi ni kwamba, sambamba na kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa jengo hili, itakuwa ni jambo jema zaidi kama tutajitahidi kufuata nyayo zake pamoja na kuishi maisha ya viongozi wengine hodari wa Bara hili wakiwemo Kwame Nkrumah, Ahmed Ben Bella, Sekou Toure, Gamal Abdel Nasser na bila kusahau shujaa wetu mwingine Nelson Mandela,” alisisitiza Rais Magufuli.

Pitia Vichwa vya Magazeti ya Leo Jumatatu 30/1/2017..!!!

Maalim Seif Afunguka Aliyoyaona Gerezani Kwa Lema,Asimulia Haya Mazito..!!!

$
0
0

KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharifu Hamad jana alisema Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) ambaye yupo mahabusu tangu mwishoni mwa mwaka jana bado ana ujasiri ule ule.

Aidha, Maalim Seif ambaye alimtembelea Lema jana katika Gereza Kuu la Arusha la Kisongo, alisema amemkuta Mbunge huyo akiwa mwenye furaha kubwa.

Aidha, akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa kwenye uwanja wa ndege wa Arusha, Maalum Seif alisema Lema ameonyesha ujasiri mkubwa.

"Dhamira kuu iliyonileta hapa ni kimuona Lema, ambaye amewekwa mahabusu kwa zaidi ya miezi miwili, baada ya Mahakama mkoani hapa kumnyima dhamana," alisema.

Lema yupo mahabusu baada ya kushtakiwa tuhuma za kutoa taarifa za uchochezi na kumkashifu Rais Dk. John Magufuli.

"Dhamira kuu iliyonileta hapa ni kumtembelea Mbunge Lema, nimeweza kumuona na kuzungumza naye. Bado yupo na ujasiri ule ule na furaha kubwa."

Alisema jambo linalomtia moyo ni kumkuta Lema akiwa salama na bado hajavunjika moyo wa mapambano ya kutafuta haki na kuwa kwake gerezani kumempa nafasi zaidi ya kutafakari.

"Kama kuwekwa gerezani ndio njia pekee ya kumnyamazisha kuzungumza atakapotoka, basi wamekosea," alisema Maalim Seif ambaye aliwahi kukaa kizuizini.

"Tumaini languni atakuwa shujaa na jasiri (kuliko) hata kabla ya kukamatwa."

Lema alisafirishwa na polisi usiku kutoka Dodoma alipokuwa akihudhuria vikao vya Bunge mwishoni mwa mwaka jana mpaka hapa Arusha baada ya kukamatwa, na tangu Novemba 2 amekuwa ama mahabusu ya Kituo Kikuu cha Polisi Arusha au Kisongo.

Awali kabla ya kumtembelea Lema, Maalim alikuwa amefanya mazungumzo na kituo cha televisheni cha Azam na kudai kuwa tangu kumalizika kwa muda wake katika nafasi ya Makamu wa Kwanza Rais wa Zanzibar, hakuwahi kulipiwa na serikali gharama za safari zote alizokwenda nje ya nchi ingawa ana haki ya kulipiwa.

Maalim Seif, akizungumza jana katika kipindi cha Funguka, alisema kuwa licha ya kutambua kwamba ana haki ya kulipiwa na serikali gharama za matibabu, ameamua kujilipia mwenyewe.

“Nilisema hapana nitajipiga mwenyewe kwa kifua (changu). Na nina haki kikatiba kulipiwa na serikali," Maalim Seif alisema. "Kwa sababu nina haki kama viongozi wengine wastaafu (kupewa huduma) kama vile matibabu, walinzi, posho ya kila mwezi, matumizi ya VIP maeneo mbalimbali."

Alisema kuwa kwa sasa afya yake iko vizuri na kwamba safari zake za India zilikuwa kwa ajili ya kuangalia kama ana matatizo ya kiafya.

“Nipo ngangari kinoma, nilienda India kwa kucheki afya yangu, mara moja nilikwenda kwenye upasuaji na baada ya hapo nilikaa wiki moja nikarudi nchini na nikashauriwa kupumzika kidogo na baadaye nikarejea kazini," alisema.

"Kwa hiyo, mtu kuumwa ni jambo la kawaida hata angekuwa mtoto au kijana anaweza kuumwa," aliongeza na kukiri kuwa serikali bado inampatia baadhi ya huduma licha ya tishio la hivi karibuni la kumnyima msaada wa serikali kutokana na kitendo chake cha kumnyima mkono Rais wa Zanzibar.

"Ninaishi vizuri na familia yangu, nilipata marupurupu yangu baada ya kustaafu, lakini pia haki za viongozi wastaafu kama posho, walinzi matibabu napata, na wala serikali isidhani inafanya hisani bali ni haki yangu,” alisema.

UCHEPUSHAJI WA RUZUKU
Maalim Seif pia alisema wanashauriana na mawakili wao ili kuangalia uwezekano wa kulipeleka mahakamani sakata la ruzuku ya mamia ya milioni ya shilingi ya ruzuku ya CUF yanayodaiwa kuchepushwa na kuliwa na watu wachache.

“Kwanza sisi hatua tulizochukua tumemuandikia barua Msajili wa (Vyama vya Siasa), Gavana wa Benki Kuu na nakala tumempa kiongozi wa Takukuru (Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa. "Hatujui watachukua hatua gani, lakini sisi tunashauriana na mawakili wetu ili kuangalia uwezekano wa kuipeleka kesi hii mahakamani," alisema.

Alisema ameshangazwa na hatua ya Msajili kutoa fedha za ruzuku na kumpa Prof. Lipumba wakati awali alimuandikia barua kumuuliza sababu za kutokipatia ruzuku chama chao na kuelezwa kuwa amezuia kutokana na chama hicho kuwa na mgogoro wa kiungozi.

“Fedha zimekwenda kwenye akaunti ambayo bodi ya wadhamini wa CUF hawaijui na wala Katibu Mkuu, fedha za ruzuku ni za serikali na za walipa kodi na halafu zitakaguliwa na CAG (Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali). Sasa hizi milioni 290 ambazo msajili kampa (Prof. Ibrahim) Lipumba zitakaguliwaje wakati hazijaingizwa akaunti ya chama?" Alihoji.

Alisema pamoja na Msajili kudai kumtambua Prof. Lipumba, alipaswa kutambua pia kwamba katiba ya CUF inabainisha kuwa Katibu Mkuu ndio mwangalizi wa fedha na mali zote za chama na si Mwenyekiti wa chama hicho.

“Kwanini apewe fedha Mwenyekiti ambaye hahusiki na uangalizi wa fedha za chama, zile fedha ndio zimeshapotea, nani atazikagua?

Katibu huyo aliongeza: "Mimi - Katibu Mkuu bado natambulika na hajaniletea barua yoyote ya kwamba mimi si Katibu Mkuu tena.
Mimi ni Katibu Mkuu na najua dhamana ya ukatibu mkuu kumpelekea fedha mtu yeyote mwingine ni kinyume cha katiba.

“Msajili alikuwa na sababu gani kupeleka fedha kwenye akaunti ambayo bodi ya wadhamini na katibu mkuu hawaijui, hivyo hajui katiba ya chama inasema nini? Fedha hizi zilipelekwa kwenye akaunti mpya ambayo ni ya wilaya ya Temeke, sasa wilaya ya temeke hakuna watia saini. Msajili anajua mchezo alioucheza."

MGAWANYIKO CUF
Maalif Seif alidai kuwa yote yanayotokea ndani ya chama hicho kwa sasa yanaonyesha Prof. Lipumba anasaidiwa na nguvu ya dola.

“Profesa anasaidiwa na dola kama mkoa wa Lindi na Mtwara, taarifa ilitolewa polisi juu ya kuomba kibali cha kufanya mkutano wa ndani na polisi walikubali, lakini baadaye polisi hao hao alikuja OCD na kudai barua aliyotupa na akasema kikao hamna eti kuna Katibu kakataa, ni nani huyo wakati katibu ni mimi?” Alihoji.

KUGOMBEA 2020
Maalif Seif alisema anatarajia kuwa rais wa Zanzibar muda mfupi ujao huku akisema atafanya uamuzi wa kuwania au kutowania urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 baada ya kuangalia hali halisi ya kisiasa.

“Hilo suala tusubiri wakati wake tuonaje, tunafanikiwa au hatufanikiwi halafu baada ya hapo ndio tutafanya uamuzi, lakini kugombea 2020 tusubiri muda ufike na kuangalia hali halisi ya kisiasa,”alisema Katibu huyo.

SULUHU MGOGORO ZENJI
Katibu Mkuu huyo alisema hakuna dawa nyingine yoyote ya kumaliza mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar isipokuwa vyama vya siasa kushirikiana katika kujenga visiwa hivyo.

“Kama kila upande utakubali kwamba Zanzibar kuna tatizo, kila upande ukubali kwamba kuna haja kila kiongozi kupata ufumbuzi au uamuzi wa matatizo hayo na kwa kushirikiana pamoja. Kuwapo na meza ya mazungumzo kunawezekana, lakini kila mmoja akiri kwamba kuna tatizo na anaenda kuondoa tatizo,” alisema Maalim Seif.

KUACHANA NA CUF
Maalim Seif alisema hajawahi kufikiria kuunda chama kingine kwa kuwa yeye ni mmoja wa waanzilishi wa CUF na alivuja jasho na viongozi wenzake kukiimarisha chama hicho.

“Nitakuwa msaliti mkubwa sana, sijawahi kufikiria na kuwaza kuunda chama kingine, mimi ni mwana-CUF kindakindaki na nitaendelea kuwa mwanachama kindakindaki," alisema.

UCHAGUZI DIMANI
Maalim Seif alizungumzia uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani visiwani Zanzibar uliofanyika Januari 22 na kudai kuwa "ulitekwa na majeshi" kwa kuwa baadhi ya wapigaji kura walipelekwa kwenye vituo vya kupigia kura na magari ya jeshi.

Maalim Seif pia alisema hawezi kustaafu kwa sasa kwa sababu bado hajatimiza ahadi aliyowaahidi Wazanzibar.

“Ngoja kwanza nipate haki yangu, nikishapata haki yangu, CUF ikaongoza Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa uchaguzi unaokuja na hapo ndiyo nitafikiria, lakini kwa sasa ni lazima tupate haki yetu, niliwaahidi Wazanzibar kuwa nitawatumikia na kupata haki yao, tukishaipata haki na mimi nikawa Rais, na mimi naziona dalili hizo,” alisema.
Viewing all 104793 articles
Browse latest View live




Latest Images