Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104799 articles
Browse latest View live

SITTA "UKAWA MILANGO IPO WAZI RUDINI MUELEZE MATATIZO YENU ALAFU TUENDELEE NA BUNGE"

$
0
0
Jana April 16 2014 UKAWA wakiongozwa na Profesa Ibrahim Lipumba wakati bunge likiwa katikati waligoma kuendelea nalo na kuamua kutoka nje kwa kile wanachosema ni ubaguzi na matusi pamoja na mapungufu mengine ambayo hawawezi kuyavumilia.
Baada ya hayo mwenyekiti wa bunge la katiba Mh. Samwel Sitta leo April 17 2014 akatumia sekunde kadhaa tu baada ya bunge kuanza kwa kusema ‘jana kumetokea jambo moja la kusikitisha na kwa hakika baadhi yetu tumesononeka sana na tukio la jana la wenzetu wanaitwa UKAWA kutoka nje ya ukumbu huu na hadi sasa hawajaniambia kama wametoka moja kwa moja au vp, kwa vyovyote vile jambo lile halikustahili’
‘Katika nchi yoyote kwa Mwananchi kuteuliwa kuwa miongoni mwa wale ambao wanaaminiwa na nchi kutunga katiba mpya ya nchi ni heshima ya kipekee kabisa, ni dhamana ambayo inatakiwa kuchukuliwa kwa uzito wowote kwa sababu utungaji wa katiba ni jambo la mara moja pengine kwa vizazi viwili vitatu’
‘Nilivyokua naangalia jana katika TBC1 maelezo yaliyotolewa na kiongozi wa UKAWA Prof. Ibrahim Lipumba kwamba wametoka kwa sababu ya lugha ya matusi na ubaguzi, kwa sababu ya Waziri mmoja wa serikali yetu amenukuliwa katika gazeti eti kasema mambo ambayo wao yamewaudhi yanadhihirisha ubaguzi bila hata Waziri huyo kupewa nafasi ya kueleza aliyoyasema’

‘Tumemuita Mh. Lukuvi alikua anaelekea Airport kwa matibabu, tumemuita arudi hapa na atatoa maelezo ambayo kama ni yale aliyoniambia mimi basi sijui watu walimnukuu vipi mpaka wenzetu kuona kwamba aliyoyasema yamewaudhi kiasi hicho lakini ukweli utabainika’
‘Wakati wote tumeushuhudia mwendelezo ambao tumeendelea kuuvumilia kwa nia njema kwamba tufikie mwisho mwema wa kutunga katiba, nyinyi nyote mnafahamu kanuni za bunge hili maalum zinapendelea wachache na tumefanya hivyo makusudi, ofisi yangu imekua wazi kupokea malalamiko ya yeyote ambae kaonewa’
‘Nimeitisha mkutano wa dharura wa kamati ya uongozi ili tuweze kuelewana namna ya kushughulikia jambo hili, ikiwa wenzetu wanatusikia na ikiwa bado wako Dodoma kwa sababu baadhi yao ni wajumbe wa kamati ya uongozi, waje watueleze kwa undani hatma ya vitendo vyao kwa sababu vina athari kisheria na kiutawala, wamejiuzulu au kutoka nje kuonyesha hisia zao alafu watarejea?’ wawepo ili tuzungumze tusaidiane’

‘Kazi iliyopo mbele yetu sio kazi ambayo unaweza kuisusa tu, mi sipendi niingie katika kauli matusi na ubaguzi lakini katika maeneo ya haki za binadamu, mtu anaedai kabaguliwa alafu anaondoka na kundi lake wanaimba Interahamwe, huu ni mwaka wa 20 toka mauaji ya Kimbari kule Rwanda, na neno iterahamwe hapa Afrika ni tusi la mwisho kabisa kwa sababu lina maana ya mtu mwenye chuki ambae yuko tayari kutekeleza mauaji tena ya Kimbari’
‘Sisi tumevumilia hata jina la mkusanyiko wao, (UKAWA) wao wanadai ndio umoja wa katiba ya Wananchi kama vile tunachokifanya humu sio cha Wananchi lakini tumevumilia tu manake hata jina hilo ni la kibaguzi, itakuaje kikundi kitoke nje chenyewe ndio kiseme ndio kinatunga au kinasimamia Wananchi kuliko sisi wengine wote tuliomo humu’
‘Sababu za kitendo chao jana hazitoshi, mlango wangu uko wazi na nimeongea pia na Waziri mkuu, yeye kama kiongozi pia wa chama cha mapinduzi pia mlango wake uko wazi, kama kuna jambo limejificha tujadiliane ili turudi kuendelea kutunga katiba ya Wananchi’


MASKINI:SOMA MESEJI ZA WATU WALIOKUWA KWENYE MELI KWENDA KWA NDUGU ZAO WAKATI MELI INAZAMA

$
0
0
Meli ya Korea Kusini iliyokua imebeba zaidi ya abiria 460 wengi wakiwa ni Wanafunzi, ilizama kusini mwa pwani ya nchi hiyo siku ya Jumatano asubuhi ambapo mpaka sasa wengi hawajapatikana huko Korea Kusini ilikozama na ni siku moja tu baada ya ajali ripoti zimeanza kutoka za msg zilizotumwa na wale waliokuwa wamekwama ndani ya meli hiyo.

Mwanafunzi:’huenda hii ndio mara yangu ya mwisho kukuambia kuwa nakupenda,’ndio ulikuwa ujumbe wa mwanafunzi mmoja kwa jina Shin Young-Jin kwa mamake.
Mama:”na mimi nakupenda mwanangu,” alijibu mama yake Shin kwa ujumbe wa simu bila kujua kilichokuwa kinaendelea.
Kulingana na jarida la Herald nchini humo, Shin alikuwa miongoni mwa watu 179 waliookolewa lakini wazazi wengine waliopokea ujumbe kama huo bado hawajaweza kuwaona watoto wao.
Mawasiliano mengine kati ya mwanafunzi mmoja na babake , yalinukuliwa na shirika la habari la AFP ni haya hapa chini
Mwanafunzi: “baba usijali,nimevaa boya la kujiokoa na niko na wasichana wenzangu. Tuko ndani ya meli na bado hatujaanza kuokolewa.”
Baba: Najua msaada uko njiani,lakini kwa nini hamjaanza kuelea, tafadhali jaribu kuondoka ndani ya meli kama unaweza.”
Mwanafunzi: ”Kuna msongamano mkubwa na meli tayari imeanza kuzama”
Mwanafunzi aliyetuma ujumbe huu bado hajapatikana.
Familia za abiria waliokuwa ndani ya meli hiyo walijawa na hisia wakisubiri taarifa zozote kuhusu wapendwa wao.
Katika ujumbe mwingine wa simu, mwanafuzni mmoja alimtumia ujumbe kakake mkubwa meli ilipoanza kuzama.
Mwanafunzi: “meli imekwama na haisongi walinzi wa baharini wameanza kuwasili kujua hitilafu imetokana na nini’
Kakake:” usiwe na wasiwasi fanya kila mnachoamrishwa kufanya na kila kitu kitakuwa shwari.’ baada ya hapo hakukua na mawasiliano mengine yaliyoendelea.

MAJIRANI WAMLALAMIKIA JIDE KWA UCHAFU

$
0
0
Gladness Mallya na Hamida Hassan
MAJIRANI wanaoishi karibu na mwanamuziki wa kizazi kipya Bongo, Judith Wambura ‘Jide’ wamelalamika kwamba mwanamuziki huyo ameiweka nyumba yake katika mazingira ya uchafu yanayohatarisha maisha yao.

Wakizungumza na Amani, majirani hao wanaoishi Kimara-Temboni jijini Dar, walisema mwanadada huyo ameacha vichaka vikubwa vinavyoizunguka nyumba yake hali ambayo ni hatari kwani nyoka wanaweza kufanya makazi hivyo kusababisha maafa kwa watoto na watu wazima.

“Yaani huyu mwanamuziki Jaydee ametuachia kichaka, yeye na mumewe hawataki kufanya usafi kuizunguka nyumba yao hali ambayo inatupa wasiwasi sisi majirani, tuna watoto wanaweza kung’atwa na nyoka kwani nyoka hupenda kuzaliana kwenye vichaka kama hivi,”

alisema jirani mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini.
Waliendelea kusema kuwa, Jide hana hausigeli wala ndugu yeyote anayeishi naye, inawezekana ndiyo maana anashindwa kufanya usafi kuzunguka nyumba yake.

“Lady Jaydee anaishi na mumewe (Gardner) tu labda ndiyo sababu ya kushindwa kutunza mazingira, majani yameota mpaka kero. Tumeshapeleka malalamiko yetu serikali ya mtaa lakini hajaitwa kuambiwa, tunashangaa,” alisema jirani huyo.

Baada ya kuzinyaka habari hizo, gazeti hili lilimtafuta Jide na mumewe Gardner ambapo mume huyo ndiye aliyepatikana na kusomewa madai hayo. Baada ya kusikiliza mpaka mwisho, Gardner alijibu:
“Kama wamesema hivyo mimi sina la kujibu (no comment)”.
Juzi, mapaparazi walifika kwenye ofisi ya serikali ya mtaa lakini ilikuwa imefungwa.
GPL

JOHARI: HARUSI YA RAY NITAKUWA MWANDAAJI CHAKULA

$
0
0
Na Erick Evarist
MKONGWE kwenye sanaa Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amefunguka kuwa endapo ikitokea mkurugenzi mwenzake, Vincent Kigos akaoa, yeye atajitolea kuwa mwandaaji wa chakula.

Akizungumza na mwanahabari wetu mwishoni mwa wiki iliyopita, Johari alisema yeye na Ray ni watu wa karibu kwa kuwa wameiongoza kampuni yao kwa muda mrefu hivyo katika jambo muhimu kama la ndoa, lazima ajitoe kinaga ubaga kufanikisha.

“Yani hata kama ikitokea kesho mkasikia Ray anaoa ujue kabisa nitakuwa muandazi kuhakikisha madikodiko yanawafikia waalikwa kwa wakati muafaka,” alisema Johari ambaye mara zote amekuwa akikanusha kuwa uhusiano wa kimapenzi na Ray.
GPL

NIMEMMISS MUME WANGU..MAMA MKWE KAJA ANA MWEZI NA HANA DALILI YA KUONDOKA TUNAISHI CHUMBA KIMOJA

$
0
0
Wana sisi wazima huku najua hakuna fujo sana.

Na kuna watu makini wa kunisaidia. 

Wapenzi nnamdogo angu ana kama 26 kaolewa na mtu wa Dodoma. Naishi nae karibu kama nyumba 5 kutoka kwangu amepanga chumba1 self containal.

Sasa kama mwezi mkwewe alikuja kumsalimu. 

Na alsema anakaa siku3 jamani had leo mumewake analala kwa marafiki zake juzi nasikia anaongea na ndugu zake kuwa atarudi hadi pasaka iishe jamani mwezi na siku kadhaa na analala kitandani bila aibu. 

Anaogopa kumwambia mumewe atahisi anamchukia mama yake na hivyo anataka jumamosi kuondoka kwenda kwao Morogoro ila mkwe haoneshi hata. Kuondoka kasema kama haukaisana utanikuta.
Hebu mshaurin mdogo angu jamani.

WAZIRI LUKUVI AWALIPUA CUF.."CUF WANASHIRIKIANA NA UAMSHO"

$
0
0
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, amesema, si makosa raia wa Tanzania kuhofia majeshi ya ulinzi kuchukua nchi ikiwa muundo wa Muungano wa serikali mbili ukibadilishwa na kuwa serikali tatu.

Aidha, amesema pia ana hofu kuhusu mwenendo wa CUF unaoshirikiana kisiasa na Taasisi ya kidini ya Uamsho, inayotekeleza majukumu yake Zanzibar kwamba umelenga kuua Muungano na kuhatarisha amani kwa mgongo wa dini ya Kiislamu.

Lukuvi alisema hayo bungeni, alipotoa ufafanuzi wa kauli zake alizozitoa katika Kanisa la Methodist, Jimbo la Dodoma wakati wa Ibada ya kumsimika Mchungaji Joseph Bundala kuwa Askofu wa Kanisa hilo.

Kauli hiyo ndio iliyodaiwa na Ukawa kuwa moja ya sababu ya kutoka nje ya Bunge kususia kikao.

Madai mengine ya Ukawa yalikuwa ni ubaguzi, matusi na vitisho vinavyoendelea bungeni. Katika ufafanuzi wake Lukuvi alisema kwamba mfumo wa serikali tatu unaweza ukasababisha nchi kupinduliwa na Jeshi na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inaweza ikaongozwa na CUF kwa Sera za Kikundi cha Uamsho jambo linalompa hofu ya udini na kuvunjika kwa amani.

Lukuvi ambaye jana alilazimika kukatisha safari yake ya kwenda India kwa matibabu, alisema alichoeleza katika hafla hiyo ya kumsimika Askofu ni hofu zake binafsi kuhusu muundo wa serikali tatu.

“Wote nikiwauliza hapa uamsho ni nani mtasema ni CUF, kwa nini sasa nisiwe na hofu ya kidini wakati kuna chama cha siasa ambacho kinamiliki taasisi inaitwa Uamsho lakini ina ladha ya kidini, hizo ndizo sera zao, unakuwaje na chama cha siasa kinachojipanga kutawala Zanzibar lakini kinaendeshwa na sera za Uamsho?

“Wanachosema CUF ndicho wanachosema Uamsho, wakisema serikali tatu ngangari, wakisema serikali ya mkataba sawa kabisa, wapi umeona vikundi kama hivyo, ukiona chama kinajitayarisha kuchukua madaraka na kinatumia taasisi hii kueneza sera zake ni hatari kwa mustakabali wa nchi,” alisema.

Akizungumzia hofu ya nchi kupinduliwa, Lukuvi alisema katika muundo wa Serikali tatu, Rais wa shirikisho hawezi kuwa Amiri Jeshi Mkuu, kutokana na kutokuwa na vyanzo vya mapato hivyo haiwezi kuendesha vyombo vya dola kama Jeshi na Polisi ambao mara nyingi bajeti zao ni kubwa na hazijawahi kutosha hata katika serikali mbili za sasa.

“Kwa mfumo huu wa serikali tatu, tusiwatafutie sababu wanajeshi wetu, mimi nilishasema sitashiriki kutafuta vyanzo kwa serikali ya tatu badala yake naukataa muundo huu,” alisema Lukuvi na kuongeza kuwa katika ukosefu mkubwa wa mapato, majeshi yahawezi kuvumilia lazima kutokee uasi na hiyo ndio hofu yake.

MADAKTARI WASHINDWA KUUNGANISHA UUME WA MWANAMUZIKI ALIYE JIKATA MAKUSUDI

$
0
0
Rapper mwenye uhusiano na kundi la Wu-Tang Clan, Andre Johnson hana tena kiungo kinachomfanya aitwe mwanaume kwakuwa madaktari wameshindwa kuunganisha.

Mtandao wa TMZ uliandika kuwa Johnson aka Christ Bearer aliukata uume wake jana Jumatano na kujirusha kwenye nyumba ya ghorofa mbili anakoishi huko North Hollywood kwa kile kinachodaiwa kutaka kujiua. Alikimbizwa kwenye hospitali ya Cedars-Sinai Medical Center lakini uume wako umedaiwa kukatika kabisa.

Johnson/Christ Bearer ni member wa kundi liitwalo Northstar, lilioanzishwa na rapper Wu-Tang Clan, RZA. Kulikuwepo na rappers wengine kwenye tukio hilo waliokanusha kuwepo na madawa ya kulevya kiasi cha kumfanya achukue uamuzi huo. Wanaamini kuwa Johnson/Christ Bearer anaweza kuwa na matatizo ya kiakili.

MKE WANGU ANAOMBA PENZI KINYUME NA MAUMBILE..SIELEWI JE ANACHEZEWA NA WENGINE ?

$
0
0
Admin hide my name , mimi ni kijana wa  kitanzania nina mke na mtoto mmoja kwa muda wa miaka miliwili sasa nimekuwa nikisoma UK Deree yangu ya pili , kwa sasa nimemaliza nimerudi Tanzania , sasa cha ajabu ambacho sikielewi ni kuwa kila nikikutana na mke wangu anataka nimwingilie kinyume na maumbile..yaani sometimes anaipeleka mwenyewe huko sehemu kwa siku kama mbili nimekuwa nafanya bila kujua imeingia huko...sasa nimejua nimemkalisha kikao lakini haeleweka hajanipa jibu la maana paka sasa...nahisi wakati mimi nipo uk kuna mtu alikuwa anamchezea sasa imekuwa hawezi sikia raha mpaka afanye hivyo ..mimi ninajua madhara ya huo mchezo siwezi kabisa kufanya kwa mke wangu ...swali linakuja hapa sasa nisipomfanyia ina maana ataendelea na hao jamaa zake wanao mfanyia ...sasa sijui nifanyaje ...naomba ushauri wa kina hapa 

VYAMA 10 VYA UPINZANI BADO VIMO BUNGENI..VYAGOMA KUJIUNGA NA UKAWA

$
0
0
ZAIDI ya vyama 10 vya siasa vya upinzani visivyo Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), vyenye wajumbe katika Bunge Maalum la Katiba wamegoma kuunga mkono Ukawa baada ya kuamua kubaki ndani ya Bunge hilo kuendelea na mjadala wa Rasimu ya Katiba.

Ukawa wakiongozwa na mmoja wa viongozi wake, Profesa Ibrahimu Lipumba, juzi walitoka bungeni kwa madai kuwa, mjadala unaoendelea umekuwa wa matusi, ubaguzi na vitisho huku wajumbe wakilazimishwa kuridhia serikali mbili zisizo mapendekezo ya rasimu.

Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta, leo alieleza kupata ujumbe wa uwepo wa wajumbe kutoka katika vyama hivyo na kuwatangazia wajumbe baada ya ombi kutolewa kwamba wajumbe walitaka kufahamu kama bungeni humo, wapo wanasiasa wa vyama vya upinzani.

Akithibitisha uwepo wa wajumbe wa vyama hivyo baada ya kukaribishwa kuthibitisha hilo na Sitta, Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha APPT-Maendeleo, Peter Mziray alivitaja vyama hivyo kwa majina na wajumbe waliokuwemo bungeni walisimama.

“Mheshimiwa Mwenyekiti nashukuru kupata fursa hii kwamba mtambue tupo, kwanza niseme tu kwamba tutahakikisha Katiba inapatikana na nimepokea ujumbe wananchi wanawataka warudi, mambo yote yanamalizwa mezani,” alisema Mziray.

Miongoni mwa vyama vilivyotajwa kuwepo bungeni ni pamoja na Demokrasia Makini, ADC, Jahazi Asilia, Wakulima AFP, Tadea, UPDP, TLP, CCK, Chausta, Sauti ya Umma (SAU), UND na chama cha DP kinachoongozwa na Mchungaji Christopher Mtikila ambacho mjumbe mmoja alikuwepo.

Mziray alisema vyama vyao vina usajili wa kudumu na havitaondoka bungeni mpaka Katiba ipatikane kwa mujibu wa sheria.

Naye kiongozi wa UDP, Gidion Cheyo alisema wapo bungeni kujadili mustakabali wa nchi ndio maana pamoja na kwamba wengine wao ni Ukawa, hawakutoka bungeni.

IMEBAINIKA NAHODHA WA MELI ILIYOZAMA HAKUWA KWENYE USUKANI WAKATI MELI INAZAMA

$
0
0
Taarifa bado zinazidi kutoka juu ya kile kivuko ambacho kilizama kikiwa na idadi kubwa ya wanafunzi,taarifa zilizopo ni kwamba msaidizi wa tatu wa nahodha wa kivuko kilichozama  anayeitwa Sewol ndiye aliyekuwa akiendesha kivuko hiko wakati kikizama.
Uchunguzi wa kina umebaini kuwa Nahodha mkuu haijabainika alikuwa wapi wakati wa tukio hilo ingawa inadhaniwa kivuko hiko kiligonga mwamba na kupinduka kwa haraka baada ya shehena yake kuegemea upande mmoja.
Wachunguzi sasa wanaelekeza juhudi zao kubaini kwanini Nahodha wa Sewol hakuwa kwenye usukani na pia kwanini baada ya tukio la kwanza abiria walikatazwa wasiruke baharini ili kuokoa nafsi zao kama ilivyo kawaida ya chombo kikipatwa na hali hiyo.
Leo asubuhi Waokoaji wamefanikiwa kuingia ndani ya kivuko hicho kilichozama baada ya kutoboa shimo upande wa juu wa kivuko hiko,kiongozi wa Mashtaka ya umma nchini Korea bwana Park Jae-Eok amesema kuwa nahodha mkuu Lee Joon-seok atakuwa na swali la kujibu.
Mpaka sasa abiria 270 waliokuwa ndani ya feri hiyo hawajulikani walipo asilimia kubwa kati yao wakiwa ni wanafunzi waliokuwa wakieleka katika kisiwa cha Jeju kwa safari ya masomo,watu 26 pekee ndio wamethibitishwa kufariki huku 179 wakitangazwa kuokolewa.
Imeandikwa na Bbc.

MASOGANGE, WAKISEMA UNAJIUZA UTAKATAA?

$
0
0

AGNES Jerald, binti anayetumika sana kunengua na pozi katika video za nyimbo za wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya, amejipatia umaarufu mkubwa sana baada ya kufanya kazi na mkali wa Morogoro, Belle 9 katika kibao chake cha Masogange.

Limegeuka kuwa jina lake na mwenyewe analitumia kikamilifu katika harakati za kimjini. Lakini aligeuka kuwa kipusa zaidi baada ya kukamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo jijini Johannesburg mwaka jana, akiwa na shehena kubwa ambayo Tanzania ilijulikana kama madawa ya kulevya, lakini Afrika Kusini wakasema ni malighafi inayoweza kutumika kutengeneza mihadarati.

Masogange ni msichana ambaye Mwenyezi Mungu amemjaalia uzuri wa asili wa Kiafrika. Ana sura nzuri ambayo bado hajaanza kuikoboa kwa mikorogo na mwili unaoendana na umbo lake maridhawa.

Sifa moja kubwa ya uzuri wa msichana huyu, ni maumbile yake ya nyuma, amejazia kiasi ambacho ni wanaume wachache, tena walio waadilifu kwelikweli, wanaoweza kupishana naye na wasigeuke nyuma kuhakikisha walichokiona!

Baada ya kuachiwa kutoka mahabusu nchini Afrika Kusini ambako alishindwa kesi ya kukutwa na shehena ile ya madawa ya kulevya, Masogange alijikuta akiwa gumzo kubwa jijini Dar es Salaam, kiasi kwamba pamoja na kuachiliwa, bado ilimchukua muda mrefu kurudi nyumbani.

Akiwa huko kwa Madiba, binti huyu alikuwa akiweka picha zake kila mara katika mitandao ya kijamii inayopatikana katika Internet, hasa Instagram. Ni utamaduni mpya kwa wasichana wa Kibongo siku hizi, wengi wanapenda kutupia picha zao humo na watu ambao huwaona, huwasifia kama wamependeza au huwaponda kama wamechukiza.

Lakini katika hali isiyotarajiwa kabisa, wiki kadhaa zilizopita, Masogange aliweka picha yake huko, ikionyesha sehemu kubwa ya mwili wake, ikiwa imepakwa hina.

Aliipaka kwa staili ambayo mtu akiitazama haraka haraka anaweza kudhani ni Tattoo, ile michoro inayochorwa kwa sindano mwilini ambayo hapo awali tulianza kuiona kwa wasanii wa Kimarekani.

Lakini kitu kibaya katika picha hiyo ni kwamba Masogange amepiga picha mguu wake akiwa amepaka hina hiyo hadi juu kabisa pajani.

Baadaye akapiga picha nyingine akiwa amevaa kimini, lakini kikionyesha sehemu ya paja hilo lililopakwa urembo huo ambao pia hutumiwa na wanawake wa Kiislamu wakati wa ndoa!

Ni picha ambayo mwanaume yeyote mkware akiiona, anavuta hisia za mahitaji ya kimapenzi. Na nieleweke, siyo Masogange tu anayetupia picha za aina hii, wasichana wengi hufanya hivi na baadhi yao, baada ya kuziweka, huweka pia na namba zao za simu, ukiwa na shida nao uwatafute!

Sitaki kuamini moja kwa moja kwamba msichana huyu ambaye amepata umaarufu bila ya kutarajiwa anajiuza, lakini ni vigumu sana kwa picha zile kuacha kusadiki jambo hili kama mtu mmoja atajitokeza na kutoa madai kama hayo.

Inakuaje mtoto wa kike, mwenye jina, tena na uzuri wako bomba kabisa wa asili, unapiga picha za namna ile na kuziweka hadharani? Nafikiri siyo sawa, zipo picha zinazopaswa kuendelea kubakia chumbani.

Kwa jinsi mambo yanavyotokea, unapata kabisa hisia kwamba kumbe dada zetu wanatafuta umaarufu kwa nguvu kwa malengo binafsi, yasiyo ya kimaadili na yenye kuchefua.

Wakishapata majina na bahati nzuri kuanza kufuatiliwa na vyombo vya habari, vikitanguliwa na magazeti, wanaanza makeke!

Kwa kutambua kwamba sura zao zinafahamika, badala ya kujistahi, ndiyo kwanza utashangaa kuona wanavaa mavazi yenye utata, kumbe tunaanza kuelewa kuwa wanafanya hivi ili kujitangaza, kama wanavyosema mabingwa wa uchumi, biashara matangazo.

Ndiyo maana nimejikuta tu nikijiuliza, hivi Agnes akiambiwa kuwa anajiuza kupitia mitandao ya kijamii, atakataa?
GPL

WEMA AMFUNGIA DIAMOND, ASHINDWA KUMZIKA MZEE GURUMO

$
0
0

Stori: Musa Mateja na Shakoor Jongo
HAYA yanaweza kuwa ni mambo ya malovee! Kuna madai kwamba Mbongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond’ alishindwa kushiriki zoezi la kuuaga mwili wa mwanamuziki mkongwe Tanzania, marehemu Muhidin Mwalimu Mohamed Gurumo ‘Maalim Gurumo’ kwa sababu alifungiwa asitoke ndani na mwandani wake madam Wema Sepetu, Ijumaa linakudadavulia.

Imedaiwa kuwa, Wema alimfanyia ‘umafia’ mpenzi wake huyo, Aprili 15, mwaka huu ambapo ilikuwa ndiyo siku ya mwili wa marehemu huyo kuagwa nyumbani kwake Mabibo jijini Dar na kwenda kuzikwa kijijini Masaki, Kisarawe, Pwani.

Itakumbukwa kuwa, Diamond ndiye msanii aliyewahi kumpa zawadi ya gari marehemu Gurumo kutokana na kuguswa na mchango wake katika tasnia ya muziki nchini.

Kwa mujibu wa mashuhuda, kitendo cha Diamond kutoonekana katika mazishi hayo ni kama amejishushia heshima kubwa aliyojijengea pale alipomthamini marehemu huyo kwa kumpa gari aina ya Toyota FunCargo.

“Tulitegemea tungemuona msibani lakini kwa kutokuwepo kwake ni kama mchango wake wa kumpa gari Gurumo hauna maana,” alisema shuhuda mmoja aliyekuwepo msibani hapo.
Mapaparazi wetu walidamka asubuhi hadi nyumbani kwa marehemu Gurumo na kujumuika na waombolezaji.

Baada ya mapaparazi wetu kufanya upekuzi yakinifu msibani hapo, walibaini kuwa, Diamond hakutia ‘maguu’ hivyo shughuli ya kumsaka ikaanza.
Breki ya kwanza kwa mapaparazi wetu ilikuwa nyumbani kwa Diamond Sinza-Mori jijini Dar ambako hawakumkuta.

Mapaparazi hawakuchoka, wakahamishia ‘majeshi’ nyumbani kwa mwanandani wake Wema, Makumbusho, Dar ambako mlinzi alibainisha kuwa, Diamond yupo na ‘bebi’ wake Wema.


Mapaparazi waliondoka na kurudi tena saa 8:37 mchana ambapo pia waliambiwa wapendanao hao bado wamejifungia ndani, wakaondoka hadi muda wa jioni baada ya shughuli za mazishi, walirejea na kuambiwa Diamond alitoka muda si mrefu pasipo kujulikana alikoelekea.

Waandishi wetu walimvutia waya Diamond lakini simu yake iliita kwa muda  mrefu bila kupokelewa.
Kusaka data zaidi, mapaparazi wetu walimtafuta meneja wa msanii huyo, Babu Tale ambaye alidai kuwa eti Diamond alikuwepo msibani Mabibo lakini hakwenda Kisarawe ambako mazishi yalifanyika.

“Tulikuwepo nyumbani kwa marehemu. Nilikuwa mimi na Diamond tena tumefika muda huohuo ndiyo mwili ukawa unapelekwa kwenye gari. Huwezi amini tulijumuika kuupandisha mwili kwenye gari na sisi tukarudi nyumbani kuendelea na shughuli zetu,” alisema Babu Tale.

Mapaparazi wetu baada ya kutoshibishwa na maelezo hayo, juzi Jumatano walimtwangia simu Diamond ambaye alizungumza kwa ‘kujikanyagakanyaga’.

“Mh! Nilikuwepo msibani ila sikwenda kuzika tu maana nilikuwa na Babu Tale pale na tulikuwa karibu kabisa na gari la Global Publishers, mara tu baada ya kumaliza kuupandisha mwili wa marehemu kwenye gari tuliondoka na kurejea kwenye majukumu yetu,” alisema Diamond.

Mapaparazi wa Global walikuwa jirani na gari alilotaja Diamond lakini hawakumuona staa huyo achilia mbali waombolezaji wengine ambao waliuliza kwa nini msanii huyo hakufika kwenye msiba wa rafiki yake mkubwa!
GPL


WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AZUIA MALIPO YA POSHO KWA WABUNGE WALIOKIMBIA BUNGE

$
0
0
Ikiwa ni Siku ya pili tangu Wajumbe wa Bunge la Katiba Kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo,Cuf na NCCR Mageuzi wanaounda kitu kinachoitwa UKAWA wasusie Shughuli za Bunge la Katiba kwa Madai wamechoka Kutukana na Kuburuzwa kwenye Bunge hilo.
Hii leo Naibu waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Nchemba ambaye kwa Sasa anakaimu Kuwa Waziri wa Fedha tangu Tarehe.10./04/2014 hadi 18/04/2014 kutokana na Waziri wa Fedha kusafiri Nchini Marekani Kikazi,amefuta Malipo ya wabunge waliosusia Mchakato wa Katiba.
Habari za Uhakika Kutoka Chanzo chetu ndani ya
hazina kinasema,Mwigulu Nchemba ameagiza Mabenki yote kurudisha Cheque za Malipo ya Posho na seating allowance zilizopelekwa na Bunge jana tar.16/04/2014 ili ziwekwe kwenye akaunti binafsi za Wabunge ikiwa ni Malipo ya Mpaka tar.30/04/2014.Pia ilikujiridhisha na taarifa hizo,Mwandishi wetu alizungumza na Wajumbe namna Mtiririko wa Malipo unavyofanyika ndani ya Bunge hilo,Mjumbe(Jina tunalihifadhi) alisema fedha zote zinapitia Benki na wakati wanajiandikisha siku za Kwanza walitakiwa Kuandika namba zao za Benki na Malipo yote hupitia huko,hivyo kama ni fedha zinazuiliwa Benki.

Baadhi ya wabunge wa CUF na Chadema wanaojiita UKAWA toka jana walijua wameshasaini fedha hizo hivyo zitaingia kwenye account zao Binafsi. Mambo yamekuwa tofauti baada ya Naibu Waziri wa Fedha(Sera) Mh:Mwigulu  kuagiza leo form zisainiwe upya leo na zitasainiwa pia tar 22 mpaka 25,Kwa madai ya asiyefanya kazi na asile. 
Mbali na hilo,Mh:Mwigulu amenukuliwa na clouds fm akisisitiza Rais kuwafuta wajumbe wakiojitoa na badala yake awateue watu waliotayari kutunga katiba hata bure kuliko hawa wanaokutana vikao lukuki kupanga njama za kususia mchakato. Aidha Mwigulu alisema fedha inayotumika ingeweza kulipwa Wazabuni wanaozidai halmshauri, wangeweza kulipa madeni ya walimu, au kuwapa mikopo watoto wa masikini waliofaulu ila hawajaenda vyuo kwa kukosa mikopo, au zingenunua madawa hosipitalini, au zingepeleka umeme, maji, vitabu au barabara lakini wamelipwa wajumbe badala ya kufanya kazi hiyo wanapanga njama ya kuhujumu mchakato usiendelee kwa kutafuta visingizio lukuki.
Bunge la Katiba linategemewa kuendelea Tar.22 Mwezi huu mara baada ya sikukuu za Pasaka Kupita na litaahirishwa tena Tar 25 mwezi huu kupisha Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

DIDA "HAPPY BIRTHDAY MY LOVELY HUSBAND EDZEN"

$
0
0
Mahaba mahabani watu wameongea na siku zinaendelea penzi lao ndio kwanza linaanza kumea, Happy Birthday Ezden ni bonge la party lilioshushwa nae mama DIDA wa ukwee, im happy for u Dida n God bless you n ya marriage jamani tunajitaji mtoto sasa lolest...

TANZANIA'S BEAUTY HAMISA MOBETO DOMINATING THE FASHION INDUSTRY IN KENYA

$
0
0
Most of us might know her but am pretty sure you have came across one of her photos somewhere. Well Hamisa Mobeto is a radio host and Model from Tanzania, she was featured on Pulse magazine sometime back and Inow fully understand why she is Tanzania’s favorite  celebrity.

Although Hamisa is not known that much in Kenya, she is a friend to most Kenyan beauties just like the Mdee sisters, she is also a friend and model to one photographer, buoart. As most complain about our half dressed socialites, Tanzanians are dressing decent and are still dominating the fashion industry with a bang! Hamisa is among the upcoming or should I say, have made it, in the tough world of juggling jobs when a celebrity.
Written by Niaje.com ,Kenya

HIYAAA...MR NICE NOW BLAMES GOD FOR HIS DOWNFALL

$
0
0
In a shocking move, Lucas Mkenda popularly known as Mr Nice, has come out to explain his miserable downfall in music terming it as God’s plan.

In a recent media interview, the Kidalipo hit maker said that he once had more than 1.5 billion shillings in his various bank accounts and he does not understand how and where all that money disappeared to.

"Kaka naweza kusema hii ni mipango ya Mungu tu kwani sikuwahi kumdhulumu mtu wala kuiba cha mtu pesa yote nilikuwa naipata kwa hali naweza kusema hii ni mipango ya Mungu tu wala si mkono wa mtu" he said

"Niliwahi kumiliki zaidi ya milioni elfu moja na mia tano kwenye bank tofauti hapa nchini pesa hizo zilitokana kufanya shoo nyingi za nje ya nchi kama Marekani, Uingereza, Ujerumani, Sweden, Holand, Dubai, Afrika Kusini na kwingineko na kila shoo nilikuwa napata pesa ndefu sana" he added during the emotional interview.

The star also talked about his numerous worldwide shows saying that the most memorable show he remembers and which makes him cry up-to today is a show in Rwanda when he found a Rwandese Minister waiting for him on the red carpet at the airport with a multitude of fans complete with a military escort just for him. The legendary singer has been making frantic efforts to bounce back into the music industry.

Is it right for Mr Nice to blame God for his down-fall?


MKAKATI MPYA WA BUNGE/CCM KUHUSU KATIBA MPYA HUU HAPA

$
0
0
Nilipotea kidogo kuwapa habari za ndani kuhusu yanayoendelea ndani ya Bunge maalum la katiba. Jana kulikuwa na kikao cha kamati ya uongozi kujadili kuhusu kujitoa kwa UKAWA ndani ya bunge hilo. Katika kukabiliana na matokeo ya UKAWA kujitoa na mustakhabali wa katiba mpya kikao cha kamati ya uongozi kimedhamiria kufanya yafuatayo kwa siri kubwa:

Imekubaliwa kuwa mara baada ya bunge kuahirishwa wiki ijayo, serikali itaandaa marekebisho mapya ya sheria ya mabadiliko ya katiba ili kuondoa kipengere cha maamuzi kufanywa na rheluthi mbili ya wajumbe toka Bara na theluthi mbili ya wajumbe toka Zanzibar.

Badala yake, kipengere hicho kitaeleza kuwa maamuzi yatafanywa na theluthi mbili ya wajumbe wa Bara watakaohudhuria kikao kitakachofanya maamuzi na rheluthi mbili ya wajumbe toka Zanzibar watakaohudhuria kikao kitakachofanya maamuzi. Ikumbukwe kuwa sheria kwa sasa inataka maamuzi yaridhiwe na theluthi mbili ya wajumbe wote (hata wasiohudhuria wanahesabiwa) toka bara na zanzibar jambo ambalo kujitoa kwa Ukawa kutaathiri maamuzi na hasa upande wa zanzibar.

Aidha kamati ya uongozi inaendelea na trick ambayo wapinzani walichelewa kuibaini hadi walipojitoa juzi ya kuweka 'majembe' yake kutoa hoja zao mwishoni mwa mjadala na kuwatanguliza wapinzani wote mwanzoni. Majembe ya ccm ni pamoja na Andrew chenge na Dr Migiro ambao ndio walioiandaa rasimu mbadala ya CCM. Hii inafanyika purposely jama alivyotangulizwa Warioba na JK akaja kufunga kazi huku UKAWA wakishindwa kubaini trick hiyo ya 'Save best for the last'. 

Ukawa na wapinzani sasa wakae tayari kwa marekebisho hayo ya sheria ambayo yamepangwa kuwasilishwa mwishoni kabisa mwa bunge la bajeti kwa hati ya dharula.

KAMA NI KWELI HUU NI WAKATI WA WAZANZIBARI KUDAI ABDU JUMBE AACHIWE HURU

$
0
0
Hili Bunge la Katiba kwa kweli limefichua Mengi sana hasa kwetu sisi ambao tumezaliwa miaka ya tisini..Nilikuwa sijui kuwa Tanzania kuna mfungwa wa kisiasa. Zipo taarifa kuwa Abdu Jumbe, aliyekuwa raisi wa Zanzibar ni mfungwa akizuiliwa huko Kigamboni na hatakiwi kutoka wala kutembelea Zanzibar kwa kosa la kudai mamlaka kamili ya Zanzibar. 
Kama huu ni ukweli basi huu ni wakati muafaka kwa Wazanzibari wadai kwa namna wanavyoona wao wanafaa uhuru wa mtu wao, aliyekuwa raisi wao na sasa yupo kizuizini nje ya mipaka yao kwa kutetea maslahi ya waliomchagua...

MKE/GIRL FRIEND WAKO ANAPOPIGWA MAKOFI NA JAMAA HUKU UKISHUHUDIA

$
0
0
Hebu fikiria, umetoka na mkeo kwa ajili ya mlo wa jioni. Mgahawa ni mzuri uko pembezoni mwa bahari. Upepo mwanana unazifurahisha nyoyo zenu. Mnakumbushana milima na mabonde mliyopitia. Mnacheka kwa furaha huku mkipongezana na kumshukuru Mungu kwa jinsi mnavyovumiliana na kupenda. 

Mnaongelea kuhusu mipango yenu kazini, na namna ya kuboresha miradi yenu binafsi. Mkiwa katikati ya maongezi, anatokea jamaa mmoja. Ghafla anaanza kumrapua vibao mkeo eti anaringa sana.

Humfahamu wala hujawahi kumuona. Siku hiyo ndio unamuonba kwa mara ya kwanza na hii ndio picha yake hali baada ya kumaliza kumpiga mkeo

Je utamfanya nini ili kumzuia asiendelee kumuumiza mkeo?

JADA PINKETT SMITH APOST PICHA FACEBOOK AKIWA MTUPU NA KUANDIKA UJUMBE MAALUM

$
0
0

Mama watoto wa muigizaji maarufu, Will Smith ambaye aliwahi kushiriki katika kampeni maalum ya kupinga tabia za kuuza mwili mwaka 2012 amepost picha ukurasa wake wa Facebook ikimuonesha akiwa mtu.

Jada Pink ambaye pia ni muigizaji mwenye mafanikio makubwa amepost picha ‘black ana white’ inayomuonesha akiwa amelala kitandani na kuandika ujumbe unahamasisha watu kutunza miili yao.

“The human body is beauty, art, creativity, expression, a vessel for the soul, our temple and a magnificent machine. We gotta take care of it. Love on your body today. It’s thee only body you got;”
PICHA HII HAPA

Viewing all 104799 articles
Browse latest View live




Latest Images