Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104793 articles
Browse latest View live

NAHISI ZIWEZI KUENDELEA KUWA MPWEKE, NAHITAJI PENZI

$
0
0
Toka niachane na boyfiend wangu ni mwaka sasa nimejitajidi kuwa mwenyewe kwa muda lakini naona sina sababu na mimi nahitaji kupendwa, nahitaji mtu wa kuwa karibu nae na kumwambia yaliyo moyoni mwangu. Nimechoka na upweke jamani.!! tatizo ni kwamba Kila atakaye nitongoza naona kama ndio wale wale tu hakuna jipya...Ila sasa nimeamua Acha number au e-mail mwenye Bahati Ntampigia tuongeee....

UNA KILA SABABU YA KUOGA NA MPENZI WAKO..SOMA HII UTANIELEWA.

$
0
0
Unapo kuwa nyumbani , tena ni vizuri ikiwa weekend mkiwa wote mko nyumbani, hakikisha unapata nafasi ya kuoga pamoja na mpenzi wako, hivi ni vitu vidogo dogo sana vinavyoweza kufanya mapenzi yenu yawe mapya kila siku.
Wakati wa kuoga fanya mbwe mbwe kidogo msugue mwenzako, mgongoni hata sehemu nyingine hii sio kwa wanawake tu hii ni kwa wapenzi wote wawili tena hususani zaidi kwa wanaume hili ndio zoezi lao, mkimaliza kuoga chukua taulo na mfute mke wako vizuri kisha, chagua yale mafuta anayoyapenda zaidi mpake huku mkipiga story mbili tatu.

Inabidi tufahamu kuwa kunavitu unaweza kuviona ni vya kipuuzi sana kwenye mapenzi lakini, ndio vinavyokukosesha maksi kila siku. Usipomfanyia hivyo kuta watu wengine watafanya halafu utaonekana huna maaana..!! Kantagaze Nimekwambia

MAMA AMSAMEHE NA KUMFUNGUA KITANZI MFUNGWA ALIYE HUKUMIWA KUFA KWA KUMUUA MWANAE

$
0
0
Wanasema uchungu wa mwana aujuae mzazi! Na kutokana na uchungu huo wa mama, ni vigumu kumshawishi akae meza moja na mtu aliyemuua mwanae kwa makusudi tena kwa kumpiga hadi kuhakikisha anakata roho.

Lakini imekuwa tofauti na jambo lililowaacha mdomo wazi umati wa watu uliohudhuria kushuhudia kunyongwa kwa mwanaume aliyemuua kijana mwenye umri wa miaka 18 nchini Iran ambako hukumu ya kunyongwa hadharani ni kawaida kwa mtu aliyepatikana na hatia ya kuua kwa kukusudia, pale ambapo mama mzazi wa marehemu alipoingilia na kumfungua kitanzi muuaji huyo sekunde ya mwisho.

Kwa mujibu wa The Guardian, mwanaume huyo aliyejulikana kwa jina la Balal alikuwa tayari amefungwa kitambaa cheusi na kuvalishwa kitanzi akisubiri amri ya kitanzi kufyatuliwa, ghafla mama huyo alimzaba kibao usoni na kuanza kumfungua kitanzi akisaidiana na mumewe!

“Mimi ni mtu wa imani.” Alisema mama huyo aliyefahamika kwa jina la Samereh Alinejad. “Nilipata ndoto ambayo mwanangu alikuwa ananiambia kuwa yuko katika sehemu nzuri na yenye amani…baada ya hapo, ndugu zangu wote, hata mama yangu, wakaanza kunihimiza nimsamehe muuaji huyu.”

Balal alihukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kumpiga vibaya Abdollah Hosseinzadeh (18) hadi kumuua katika ugomvi uliotokea mtaani kati yao mwaka 2007.

WENGER, RODGERS WAGOMBEA KUMSAJILI MCHEZAJI MKENYA

$
0
0
KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger na kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers wameingia katika vita ya kumuwania mtoto wa staa wa zamani wa timu ya taifa ya Kenya, Mike Okoth Origi, Divock Origi anayekipiga klabu ya Lille ya Ufaransa.

Origi alizaliwa nchini Ubelgiji katika mji wa Ostend nchini Ubelgiji ambako baba yake alikuwa akicheza soka la kulipwa katika klabu mbalimbali za Oostende KV, KRC Harelbeke na Racing Genk.

Katika msimu huu, Origi, 18 amefunga mabao matano katika mechi za Ligi Kuu ya Ufaransa na tayari ameanzisha mgogoro miongoni mwa timu kubwa za England huku Liverpool na Arsenal zikianza kimbelembele.

Aweka rekodi Ufaransa

Akiwa na umri wa miaka 17 na miezi tisa tu, Divork aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa pili mdogo zaidi kufunga bao msimu huu wa Ligi Kuu Ufaransa huku wa kwanza akiwa kinda Neal Maupey, 16, wa klabu ya Nice.

Lakini kabla ya hapo, katika msimu wake wa kwanza Origi alifunga bao katika mechi ya kwanza dhidi ya Troyes katika sare ya 1-1. Kutokana na bao hilo, Origi alisifiwa vilivyo na kocha wake pamoja na wachezaji wenzake kutokana na kiwango kizuri alichoonyesha.

Kocha wake, Rudi Garcia, alimwelezea Origi kama muunganiko mzuri katika timu na tishio kubwa mbele ya lango, lakini alimtaka asivimbe kichwa kutokana na mwanzo huo mzuri. Garcia alisema kwamba ana kazi kubwa ya kufanya katika masuala ya mbinu.

“Amefanya mazoezi na sisi mara kadhaa. Ana nguvu na ni mzuri mbele ya lango, lakini lazima afanye kazi kubwa. Kuna kazi kubwa mbele yake sana sana katika suala la mbinu. Njia bado ndefu kwake.”

Kabla ya kutua Ufaransa, Origi alikuwa akikipiga katika klabu ya Racing Genk ya Ubelgiji ambayo baba yake pia aliwahi kuchezea. Mpaka sasa bado hajaamua timu ya taifa ya kuichezea lakini tayari ni staa wa timu ya vijana ya Ubelgiji chini ya umri wa miaka 19.

Amewahi kukipiga katika timu ya taifa ya Ubelgiji chini ya umri wa miaka 15, 16 na 17. Lakini mpaka sasa amefunga mabao manne katiak mechi tisa za timu ya chini ya umri wa miaka 19 ambako ana nafasi ya kudumu kikosini.

Harambee Stars yaanza kumtolea macho

Wakati Wabelgiji wakimtaka aichezee timu ya wakubwa ya nchi hiyo kwa kumuunganisha na mastaa wengine kama Eden Hazard, Marouane Fellaini, Romelu Lukaku, Christian Benteke na wengineo, Wakenya wanamuhitaji katika timu yao ya taifa kwa ajili ya kuimarisha safu yao ya ushambuliaji.

CHEKA KIDOGO-POMBE SIO SUPU JAMANI...MWANGALIE HUYU JAMAA

$
0
0
Leo siku nzima nilikuwa sijacheka ila baada ya kuangalia hii video imebidi nicheke ..Jamaa anapiga mbizi kwenye maji ya mvua ...Kweli Pombe sio Supu..
Bonyeza Hapa Kuangalia hiyo Video:

POMBE SI CHAI ...HIVI HUYU MFANO ANGEKUWA MITAA YA MANZESE INGEKUWAJE

$
0
0
Mwanadada Akiwa Amelala Pembeni ya Barabara Baada ya Kuzidiwa na Pombe ...Nawaza tu kwa Sauti huyu Angekuwa yamemfika haya akiwa Mitaa ya Manzese Ingekuwaje?

DODOMA UPDATES:BIDII ZA KUWATAFUTA VIONGOZI WA UKAWA ZIMEGONGA MWAMBA

$
0
0
DODOMA UPDATES.
• Bidii za kuwatafuta viongozi wa UKAWA zimegonga mwamba ,ila wakati haya yakifanyika, wabunge wa UKAWA wakiongozwa,na Mwenyekiti Ibrahim Lipumba walikutana,African dreams na kuweka mikakati ya pamoja.
• Wabunge wa UKAWA wafikia maamuzi ya kuzunguka Nchi nzima na kueleza wananchi sababu za wao kutoka ndani ya Bunge la Katiba.
• Mkutano mkubwa wa uzinduzi utafanya Zanzibar kesho katika uwanja wa Kibanda maiti
• Mkutano wa uzinduzi wa UKAWA wa kuzunguka Tanzania nzima utahutubiwa na viongozi wote wa vyama vinavyounga ukawa, pia Mtikila, Makaidi na vyama vingine wamejiunga rasmi UKAWA.
• Wajumbe wa UKAWA wamelaani upotoshwaji unaofanywa huku uongozi Ukiwa kimya

KUNDI LA MUZIKI LA P-SQUARE LAVUNJIKA

$
0
0
Now there are fears that there's real big trouble in PSquare's camp. Their elder brother, manager and director Jude Okoye just tweeted this "After 10 years of Hard Work, Now its Over , Am Done..." No full details or statement yet from them.But according to Linda, Peter and Paul Okoye of P-Square have been reportedly having issues for a while now. That the twin brothers practically disagree on everything now...songs, videos, ideas etc. That things even got out of hand last Wednesday April 16th, the brothers physically fought each other during rehearsals. They had to be separated by their dancers. Then that there are stories that one of the wives is the one causing some of the problems between the brothers. Real scary! Add all that to this tweet Jude just shared an hour ago. I hope all is well o?

CHAGGA BARBIE ATUPIA PICHA INSTA KUONESHA MAKALIO YAKE...NICE

$
0
0
 Baada ya Diva wa clouds Fm kuachia picha tata kupitia mtandao wa instagram (kama hukuiona bofya HAPA) Alifata Lulu michael kuachia picha yenye mitego (kama hukuona ya Lulu bofya HAPA) sasa ni zamu ya Chagga Barbie ambaye alikuwa mpenzi wa Prezzo kuachia picha tata, Tazama hapo chini

NIMEAMUA NIACHE SHULE..NINACHOPATA TOKA KWA WANAUME WENYE PESA ZAO NI ZAIDI YA SHULE

$
0
0
Admin Hide My Name...Mimi ni Msichana wa Miaka 22 Niko Chuo Kikuu Hapa Mlimani Dar es Salaam , Nipo Mwaka wa Pili sasa ...Mimi ni Mzuri kwa Umbo na Sura kiasi kwamba nimekuwa nikitafutwa na watu wenye Pesa zao nikawape kampani hasa wafanya biashara wa ndani na wa nje na siku moja moja wanasiasa , Toka mwaka wa Kwanza nafanya hii Biashara kwa usiku mmoja bei yangu huwa ni milion moja na saa zingine nikitoa huduma nzuri napewa zaidi ya hiyo ....huwezi amini mpka sasa kwenye account yangu nina zaidi ya Milion 80 na nyumba tayari nimeshajenga..Hapa najiandaa kwenda Nigeria Nimealikwa na Msanii mkubwa wa Huko Baada ya Kumpa Huduma nzuri alipokuwa Tanzania....Eti anataka Tena...Mimi sio malaya na wala sijiuzi mtaani ila wananitafuta wenyewe kwa uzuri niliyo nao ....Biashara imechanganyia sasa naona shule inanishinda hata assignment siku hizi sifanyi nalipa watu wanifanyie hivyo nafikiria kuacha chuo niwekeze katika mambo mengine..Kwa hela niliyonayo naweza fungua Biashara yoyote sasa....Ushauri Tafadhali 

JESHI LA POLISI LACHAFUKA..ASKARI WAKE AIBA MTOTO MCHANGA

$
0
0
Jeshi la polisi Mbeya limemkamata  Askari polisi mwanamke wa Dar es salaam kwa tuhuma za kumuiba mtoto  mchanga wa siku ambae aliibwa toka April 6 2014 kwa kushirikiana na baba mzazi.
Ahmed Msangi ambae ni kamanda wa polisi Mbeya amesema ‘tulimkamata huyu Mama na mtoto na hivi sasa Mwanamke huyu yuko mahabusu pamoja na baba mtu, tulichofanya niliagiza OCD wa Kyela amlete mama halisi wa mtoto ili aungane na mwanae na vilevile kukamilisha upelelezi, Mwanamke huyu anaitwa Prisca askari Polisi Tabata mwenye namba WP5367′

‘Sasa hivi yuko chini ya ulinzi, huu ni uhalifu kwa sababu ni wizi wa mtoto… nimeshaagiza mashtaka ya kijeshi na yanaendelea na tukishajiridhisha hatua stahiki za kitendo alichofanya zichukuliwe, ukifanya uhalifu adhabu yake ni kufukuzwa kazi ili tukupeleke Mahakamani ukashtakiwe, amefanya kitendo kibaya kinyume na mwenendo mwema wa jeshi la Polisi, kila mtu atachukua mzigo wake mwenyewe’

Kamanda wa polisi amesema Baba wa mtoto na askari huyo hawana uhusiano wa damu bali wa kibiashara hivyo wanaendelea na uchunguzi zaidi

MTANZANIA WA KWANZA KUDHIBITISHWA KUWA MMILIKI HALILA WA FACEBOOK ACCOUNT HUYU HAPA

$
0
0
Flaviana Matata amekua mwakilishi mzuri wa Tanzania kwenye nchi mbalimbali alizofanya kazi kama Ufaransa, Hispania na Marekani ambako anaishi sasa hivi New York.
Flaviana amethibitishwa rasmi na facebook kwamba hiyo account yenye hicho kitiki hapo juu ndio account yake pekee na halali hivyo ule utapeli ambao ulikua unafanywa kwa kutumia account nyingine feki za Flaviana utaishia hapa.
Flavvy anakua Mtanzania wa kwanza ninaemfahamu kuwa verified na facebook ambapo tayari kwenye account yake ya twitter yuko verified pia ambapo Watanzania wengine ambao wako verified twitter ni President Jakaya, Hasheem, Ay, mawaziri January Makamba na Lazaro Nyalandu.

TUNDU LISSU ADAI HATI ILIYOPELEKWA BUNGENI NI FEKI

$
0
0
Dodoma. Hata baada ya Wajumbe wa Bunge Maalumu kugawiwa nakala za Hati ya Muungano, Tundu Lissu, ameendelea kung’ang’ana kuwa haipo, ni feki.

Akizungumza kwenye Viwanja vya Bunge mjini hapa mara baada ya nakala kugawiwa bungeni, Lissu ambaye aliibua hoja hiyo alisema; “Hivi hawa wanamghiribu nani? Nasema hiyo hati haikuwahi hata kupelekwa Umoja wa Mataifa.”

Alisema saini iliyo kwenye hati hiyo ni tofauti na zilizo kwenye hati ya Mabadiliko ya Kwanza ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya 10 ya Juni 1965, Hati ya Muswada wa Sheria ya Udhibiti wa Fedha za kigeni na Sheria ya kugawa ardhi kwa Wazanzibari ambazo zote zinafanana.

Lissu alisema kwa miaka 50 haikuwahi kuonyeshwa, wala haikuwahi kuwa UN na hata Zanzibar hawana. Alisema walishuhudia Benard Membe (Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa) akisema iko UN, jambo alilosema ni kudanganyana tu.

Alisema nyaraka kama hizo, mkataba wa Uhuru zinatakiwa kuwekwa Makumbusho ya Taifa kwa kuwa ni nyaraka wazi zinazotakiwa kuona na kila anayetaka, kwa rahisi.

“Marekani ilipata uhuru zaidi ya miaka 200, lakini kila nyaraka za uhuru zinaonekana kwa rahisi siyo hapa...mambo yanafanyika chini kwa chini, utadhani biashara haramu,” alisema.

Baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu wamembeza Lissu kwa hoja hiyo wakisema hatua ya nakala zake kufikishwa bungeni ni sawa na kumfunga bao la kisigino na kuhoji watazungumza nini baada ya hati kupatikana.

JERR SILAA" YANGA HAKUNA KUJENGA UWANJA JAGWANI ..PALE NI MKONDO WA MAJI"

$
0
0
Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa amepigilia msumari wa mwisho kwa kuwataka Yanga kusahau kuhusu ongezeko la eneo la kujenga uwanja wake eneo la Jangwani kwa vile sehemu hiyo ni mkondo wa maji.

Akizungumza na gazeti hili, Dar es Salaam jana, Silaa alisema:

“Tumepata hasara kubwa (Serikali) hii yote imetokana na watu kujimegea maeneo na kujenga kwenye mkondo wa maji, mafuriko yote haya yanayotokea ni kwa vile maji yanakosa pa kwenda na kuishia kwenye maeneo mengine ndiyo maafa yote haya yanatokea.

“Hebu angalieni pale Jangwani sasa hivi kulivyo, maji yamefurika watu wengine wamepoteza maisha, halafu bado turuhusu watu waendelee kujenga kwenye mkondo wa bahari, waambieni wasahau hilo.”

Kauli hiyo ya Meya Silaa imekuja siku chache baada ya Baraza la Mazingira la Taifa (NEMC) kudai kuwa eneo ambalo wanaliomba Yanga ni hatarishi, hivyo watafute eneo lingine kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wao kama kweli uongozi uliopo chini ya Mwenyekiti wake, Yusuf Manji, una nia ya kuwajengea Wanayanga uwanja.

Eneo hilo la Jangwani, mbali ya kuwa ni bonde kubwa la Mto Msimbazi, ambalo ni mkondo wa upumuaji wa bahari, lakini pia kuna bomba kubwa linalopeleka maji Hospitali ya Taifa Muhimbili na lingine linalopeleka maji taka baharini.

Hata hivyo, licha ya Yanga kushauri kuondoka eneo hilo ambalo ni hatarishi, uongozi wa klabu hiyo chini ya Mwenyekiti wake wa

Ujenzi wa Uwanja, Francis Kifukwe, umezidi kusisitiza kuwa kuna masharti ambayo NEMC wamewapa na wakiyatimiza eneo hilo watapewa ikiwemo kubeba fidia za kuwalipa wakazi wa eneo hilo.

“Kuna masharti ambayo wametupa na sisi tupo tayari kuyatekeleza hawajatuambia chochote, huyo aliyekwambia tumenyimwa kujenga uwanja ni nani? Nitajie huyo mtu wa NEMC, ninachoweza kusema kuna masharti na maelekezo ambayo wametupa,” alisema Kifukwe huku akigoma kuzungumzia suala hilo kwa undani kwa kueleza masharti na mapendekezo waliyopewa.

Kamati ya Mipango Miji na Mazingira ya Manispaa ya Ilala ilikutana hivi karibuni kujadili suala hilo ambalo hata hivyo wameliacha  mikononi mwa NEMC.

Nayo Kamati ya Mipango Miji na Mazingira ya Manispaa ya Ilala ilifanya  ziara ya ukaguzi wa Jangwani hivi karibuni

Wakati huohuo; Mvua hizo zinazoendelea kunyesha zimesababisha ukuta mkubwa wa uzio wa uwanja wa Yanga, ambao umejaa maji kwa sasa kubomoka. Ukuta huo ni ule ambao upo upande wa bonde la Msimbazi chini ya uwanja huo.

SIMBA NA YANGA LEO UWANJA WA TAIFA NANI ATAIBUKA KIDUME?

$
0
0
Toa Utabiri wako hapa Nani atakalishwa Chini leo mchezo Baina ya Simba na Yanga Uwanja wa Taifa.........Kwa kila atakaye Tabiri Sawa atatumiwa Vocha ya Elfu 2000 baada ya mchezo kwisha

KIKWETE TANZANIA ITAKUKUMBUKA KWA LIPI ? SOMA JIBU LAKE HAPA

$
0
0

Mheshimiwa Rais wa JMT akiwa anahojiwa na mwandishi wa habari mwandamizi kutoka Nation media group aliulizwa swali je anategemewa utawala wake kukumbukwa kwa yapi ,Jk alijibu kama ifuatavyo:
  • The Tanzanians will decide but I consider ky term of office as a time of scalling up.We have scaled up on roads,on construction,on education,on health,and many other things. It is Tanzanian to judge but my biggest satisfaction is that we have done a tremendous job in the road infrastructure,expansion of primary and secondary education.
  • We had only 40000 students in universitu,now we have 180000,which is phenomena,we had 525,000 secondary school now we have 1.9 million.The important thing I want Tanzanians to appreciate is that I have made conttibution.I found them.somewhere and I leave them somewhere better than they were before when I took office.

CHADEMA INAPOTEZA MWELEKEO NA KUFA KIFO CHA MENDE KWA KUKOSA WASHAURI

$
0
0
Hakika kila mtu na kila kiongozi hasa mwenye mamlaka makubwa ni busara kuwa na WASHAURI ambao watamshauri na kumkosoa pia kabla ama baada ya kufanya maamuzi katika uongozi wake. Hili lipo wazi hata familia yenye baba, mama na watoto, baba anaweza kutafuta mshauri pembeni kuhusu namna ya kuiongoza familia.

Ni muda mrefu huwa najiuliza hili swali, hivi washauri wa Dr. Slaa na Mbowe ni kina nani maana nahc kama hawana ndio maana wanafanya maamuzi yasiyo sahihi kila wakati kwakuwa maamuzi hayo hayajengi wala kuleta maendeleo ndani ya Chadema. Mfano; timua timua za viongozi katika chama, kufanya utalii kwa chopa, kukataa kukaguliwa hesabu, kupanga maandamano yasiyo na tija, kususia vikao halali vya bunge, n.k. 

Haya yote yasingepelekea chadema kufa kifo cha mende kama wangekuwa na washuri wa chama. Wanawapuuza wazee kama Ndessa na Mtei, wanatumia halmashauri za vichwa vyao wenyewe, matokeo yake ndio hayo. Na kama wanao washauri, itakuwa hao wanaowashauri wanawashauri vibaya.

Kwani Mbowe akiwaza jambo lake, anawaita akina Lema, Lissu na wanachama wengine na waandishi wa habari wanaweka mikakati ya kulitekeleza pasipo kupingwa! Lifanikiwe, lisifanikiwe, akiota lingine anafanya vivyo hivyo.
Dr. Slaa nae hivyo hivyo, akiwaza kitu chake, fasta anaita waandishi wa habari na baadhi ya viongozi na wanachama isipokuwa Lema, maana lema wanadharauliana, wanaweka mikakati ya kutekeleza jambo hilo mara moja bila kupingwa!
Hawana team work ndo maana wanaishia kutimuana!

PENNY ATUPIA PICHA MTANDAONI AKIONESHA MAUNGO YAKE YA NDANI

$
0
0

Baada ya kuwa kimya katika akaunti yake ya instagram, Penny ambaye ni mtangazaji wa kituo cha DTV kilichopo Dar, amerudi kwa kasi katika mtandao huo baada ya kuachia picha yenye mitego ikionesha kitovu chake, Sasa sijui ndio kutaka Tension kwa Watu au ndio nini Hii. Tazama hapo chini picha hiyo.


STEVE NYERERE NA BATULI KIMENUKA

$
0
0
Staa wa sinema za Kibongo, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ na mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie, Steve Mengere ‘Steve Nyerere’ wameingia kwenye bifu zito baada ya kutofautiana katika makubaliano ya kikazi.

Kwa mujibu wa chanzo makini, hivi karibuni wawili hao waliingia kwenye mabishano wakati Steve Nyerere alipokuwa akiandaa .
 filamu yake mpya iitwayo Get Out ambapo alipaswa kumshirikisha Batuli.
Ilisemekana kwamba jamaa huyo alipompigia simu, mwanadada huyo alichomoa baada ya kuona makubaliano ya kifedha hayazungumziwi.
 “Batuli alipohoji kuhusu malipo, Steve hakuweka wazi ndipo mambo yalipoharibika, kikanuka kisha Batuli akamvaa kwa maneno kiongozi huyo na kudai hana sifa za kuwa kiongozi,” kilisema chanzo chetu.
 Ili kujiridhisha na madai hayo, mwanahabari wetu alimwendea hewani Batuli ambapo alipatikana na kukiri kuwa ametofautiana na Steve chanzo kikiwa ni filamu hiyo.


“Aliponipigia simu nilimwambia sitaweza kwenda kushuti kwa sababu hakuna makubaliano yoyote tuliyofanya ikiwemo gharama, usafiri, mavazi na vinginevyo ndipo akamaindi na kuanza kulaumu na kisha kukata simu,” alisema Batuli.
 Ishu haikuishia hapo, taarifa zinadai kuwa baada ya Steve kutofurahishwa na majibu ya Batuli, aliendelea kumtumia meseji za kumlaumu ndipo Batuli alipochachamaa zaidi kwa kujibu mashambulizi.
 “Steve anapaswa akasomee utawala na uongozi bora kwani hafai kuwa kiongozi, hana busara, kwa sababu kabla sijagombana naye nilikuwa nikisikia maneno na majungu ila baada ya ugomvi wangu na yeye nimegundua hafai,” alisema Batuli na kuongeza:
 “Ananiambia mimi ni msanii mchanga ilihali mimi kwenye kiwanda nipo kwa miaka kumi na nne na mwaka 2,000 wakati naanza yeye alikuwa anachekesha watu ili apate kula kwanza nimemdharau kwa sababu amekuwa akinichonganisha na wasanii wa Bongo Movie eti mimi nimewaambia wanajiuza.”
 Baada ya Batuli kufunguka, gazeti hili lilimgeukia Steve Nyerere na kumsomea madai hayo ambapo alifunguka:
 “Sipendwi na watu na sijui nini tatizo, nikiwa kama dairekta nina uwezo wa kumchagua huyu nifanye naye kazi na huyu kumuacha, yule (Batuli) kama analeta chuki basi zitakuja hivyo basi ni nyingi tu,’’ alisema Nyerere na kuongeza:
 “Kwa heshima niliyoitengeneza kwa miaka 32 alafu nije nigombane na mwanamke, kwanza nagombana naye nini? Nashukuru nimepata ushauri, naendelea na kazi ya kutetea maslahi ya Bongo Muvi kama ni filamu mimi nilishachezesha msanii mwengine.”


MASAI NYOTAMBOFU AJIONDOA KWENYE KUNDI LA VITUKO SHOW, SOMA KISA KIZIMA HAPA

$
0
0
MCHEKESHAJI maarufu hapa nchini katika swaga za kimasai ambaye pia ni mmiliki wa masainyotambofu.info Gilliady Severine Kahema 'Masai Nyotambofu' Ameamua kuitema kampuni aliyokuwa na mkataba nayo ya Al-Riyamy Pro ambayo hurusha kipindi chake cha VITUKO SHOW kwenye runinga ya CHANNEL TEN.
Akizungumza  leo, Masai Nyotambofu alisema kuwa ameamua kuachana na kampuni hio baada kugundua kuwa kuendelea kuwepo pale kwa muda mrefu ni sawasawa na kuididimiza sanaa yake kwani hamna mafanikio yeyote zaidi ya kuahidiwa kwamba baada ya kipindi fulani mambo yatakuwa mazuri huku siku zinazidi kwenda, ''Kiukweli nimeamua kuachana na Al-Riyamy Pro maana naona muda wote wa miaka mitano sijafikia malengo yangu niliotarajia na ahadi za kampuni hazionekani,

Pia kikubwa zaidi kilichoniondoa ni pamoja na kuchezeshwa na wasanii wasio na vipaji halisi wanaishia kuigaiga stile za watu tu hatima yake tunaonekana wote wabovu. Hapo mwanzo tulivyokuwa timu kamili tulifanya vizuri na kupokelewa vizuri lakini walivyoondoka baadhi ya wasanii wenye uwezo mkurugenzi akasema analeta wasanii wengine, Basi mimi nikaendelea kusubiri maana kila msanii alikuwa na mkataba wake hivyo kila aliyeondoka aliondoka kwa sababu zake binafsi mimi nikaendelea kukomaa nikihisi mbele ya safari kutakuwa na mabadiliko, Mara mkurugenzi akaaza kuwaleta watu tu from no whwre wasio na vipaji vya sanaa tucheze nao, Kila nikimuuliza kuwa mbona wengine wakisimama mbele ya Camera wakiambiwa Action hawajui itakuwaje? Jibu lake alinijibu nawasaidia maisha yao magumu. Nikamwambia huoni kuwa kazi ikiwa mbovu tutapoteza mashabiki? Akajibu we fanya kazi ntapitisha mchujo wasio na vipaji ntawaondoa watabaki wenye vipaji wachache tu niwatengenezee maisha ili muuone umuhimu wa kukaa kwenu hapa miaka mingi mimi nauona uvumilivu wenu, Cha ajabu mkurugenzi aliendea kujaza watu wasio na vipaji uongozi hakuna nidhamu kambini mbovu mimi siheshimiwi na mimi simuheshimu mtu basi tafrani kama kilabu cha komoni. Lakini nikaendelea kukomaa nikitarajia mabadiliko mwaka 2014, Kuna siku nikajaribu kumwambia mkurugenzi kuwa aniazime kiasi fulani cha fedha nikamilishe Video ya wimbo wangu alafu anikate akasema sina hela huoni mko wengi? kwanza kampuni hainilipi wewe unataka upate promo ili uzidi kuitwa kwenye Show utashuti saa ngapi na kwenye Show utaenda saa ngapi? Dah! Hapo ndipo nilipoona kuwa napoteza muda ukizingatia mwanzoni tulivyokuwa wakali watupu kipindi kikiruka hewani simu za wasanii zinaita mpaka kero lakini sasahivi kipindi kinaruka mwanzo mwisho hata hubipiwi..! Ni ishara tosha kwamba watazamaji wameanza kuingia mitini. Ni bora nikae pembeni nikinusuru kipaji changu kwani kama riziki yangu mwenyezi mungu hakuniandikia kuipata hapo hata nikomae vipi kamwe sitofanikiwa hapo. Nimeamua kurudi Nyumbani Jijini Dar kutuliza kichwa sina mkataba na kampuni yeyote kwa sasa najiandaa kuachia ngoma mpya baada ile niliyomshirikisha Rich Mavoko na Kitokololo (Yero Masai) Watu wangu kaeni mkao wa kula Uchekeshaji siachi mpaka mwisho wa uhai wangu, Kuondoka Al-Riyamy Pro Sio mwisho wa kampuni kufanya kazi wataendea wengine na wala sio mwisho wangu wa kuchekesha bado mtaendela kuzipata ladha zangu kupitia filamu zangu ambazo nipo katika mikakati ya kuanzisha Project. Namshukuru mwenyezi mungu kwa kunipa kipaji hiki kilichonifanya niwe na ukaribu wa hali ya juu na watu mbali mbali na katika show zangu napokelewa vizuri hicho kinanifanya nimuheshimu kila mtu wa kila rika, Nawapenda Mashabiki wangu One Love.


Viewing all 104793 articles
Browse latest View live




Latest Images