Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live

Mbowe Aingilia Kati Agizo la Magufuli Juu ya Mabilion ya UDA

$
0
0

MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amekutana kwa dharura na mameya, manaibu meya na viongozi waandamizi kutoka vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wa Dar es Salaam kwa ajili ya kujadili suala la Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA).

Hivi karibuni, Rais John Magufuli wakati akizindua Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka jijini Dar es Salaam (DART) alitoa siku tano kwa uongozi wa Jiji kuhakikisha Sh bilioni 5.8 zilizolipwa na Kampuni ya Simon Group zinapangiwa matumizi baada ya kuuzwa hisa asilimia 51 kati ya 100 kwa kampuni hiyo.

Jiji la Dar es Salaam kwa sasa linaongozwa na Ukawa chini ya Meya kutoka Chadema, Isaya Mwita. Katika kikao cha baraza Halmashauri ya Jiji hilo chini ya Meya Mwita kilichofanyika wiki iliyopita, kilishindwa kufikia mwafaka wa kuzipangia matumizi fedha hizo kutokana na madai ya wajumbe wa baraza hilo kuwa kitendo hicho ni kubariki ufisadi wa kuuza hisa kwa Simon Group.

Kikao hicho cha Baraza kilifanyika ili kuitikia agizo hilo la Rais Magufuli alilolitoa wakati wa uzinduzi wa mradi wa Dart.

Hata hivyo, pamoja na siku tano alizotoa kuisha bado halijapatiwa ufumbuzi. Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alipozungumzia suala hilo nje ya ukumbi wa Bunge, alikiri kuwaita viongozi hao wa jiji la Dar es Salaam ili kuzungumzia suala hilo la UDA.

“Nimewaita ili tuzungumze sintofahamu ya suala hili ili tupate msimamo wa pamoja.Tunahitaji kupata suluhisho la suala hili ili wakazi wa Dar es Salaam wanufaike na Uda,” alisisitiza.

Katika jiji la Dar es Salaam lenye halmashauri sita, Ukawa ilishinda halmashauri tatu ikiwemo halmashauri ya jiji hilo inayoongozwa na Mwita, Ubungo ikiongozwa na Boniface Jacob na Ilala chini ya Charles Kuyeko.

Baadhi ya viongozi hao wa Ukawa wa Dar es Salaam walionekana wakirandaranda katika viwanja vya Bunge jana na baadhi yao walikiri kuitwa na mwenyekiti huyo wa Chadema huku wakidai kuwa hawafahamu wameitiwa nini.

Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene akizungumzia kushindwa kugawanywa kwa fedha hizo alitaka watendaji wa jiji hilo wapewe muda ili waweze kuja na suluhisho la suala hilo.

Alisema kwa sasa hawezi kuzungumzia maagizo ya Rais Magufuli kuhusu matumizi ya fedha hizo, lakini endapo atapewa maelekezo kuhusu fedha atayatekeleza.

Harufu ya Ufisadi Yaibuliwa Mradi Ofisi ya Mama Samia...!!!

$
0
0

MAKALI ya Wabunge wa Bunge la 11 dhidi ya ufisadi yalijidhihirisha mjini Dodoma jana baada ya kamati yao inayoshughulikia Katiba na Sheria kueleza ilivyoingiwa hofu ya kuwapo harufu ya vitendo hivyo katika mradi wa ukarabati wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu.

Katika taarifa yake iliyowasilishwa bungeni mjini Dodoma jana, kamati ilidai kubaini kuwa ukarabati huo kwenye Ofisi ya Makamu wa Rais iliyopo Mtaa wa Luthuli jijini Dar es salaam, umefanyika chini ya kiwango na hivyo imeagiza uchunguzi ufanyike ili kujiridhisha na matumizi ya fedha zilizotumika kwa kazi hiyo.

Akisoma taarifa bungeni jana, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mohamed Mchengerwa, alisema kuwa katika fungu la 31 la ofisi hiyo, kwenye mradi namba 6389 ambao kamati ilifanya ziara zake imebaini kuwa jengo hilo limejengwa chini ya kiwango.

Alisema kamati imebaini kuwa kulikuwa na matumizi yasiyoridhisha ya fedha za umma katika baadhi ya miradi na kuagiza mamlaka zinazohusika kufanya uchunguzi maalumu kuhusu matumizi ya fedha na ubora wa miradi hiyo na kutoa taarifa kwa kamati.

Mchengerwa alisema katika mradi huo, wameagiza ufanyike uchunguzi na hatua kali zichukuliwe kwa watendaji wote waliohusika.

Tangu Serikali ya awamu ya tano iingie madarakani Novemba, 2015, chini ya utawala wa Rais John Magufuli na makamu wake Samia Suluhu, kasi ya vita dhidi ya vitendo vya rushwa na ufisadi imeongezeka huku ikielezwa kuwa hakuna atakayesalimika pindi ikibainika kuwa anashiriki vitendo vya aina hiyo vinavyokwamisha ufanisi wa miradi mingi ya maendeleo.

OFISI YA MWANASHERIA MKUU
Katika hatua nyingine, Mchengerwa alisema kuwa kamati yao ilibaini pia kuwapo kwa miradi mingi isiyofanikishwa kama ilivyotarajiwa kwa sababu ya kutolewa kwa kiasi kidogo cha fedha kisicholingana na mahitajhi.

Akieleza zaidi, Mchengerwa alisema Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imekuwa ikiomba fedha kiasi cha sh. bilioni moja kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi hiyo kwa miaka mitatu mfululizo bila ya mafanikio.

Alisema kwa mwaka 2014/15, 2015/16 na 2016/17, pamoja na kuomba fedha kwa kipindi hicho haikupokea fedha yoyote kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

MRADI WA NSSF DEGE ECO
Mwenyekiti huyo alizungumzia pia ripoti ya uchunguzi wa miradi ya NSSF ukiwamo wa Dege Eco, akisema kuwa ipo katika hatua za mwisho kukamilishwa na taasisi zinazofanya uchunguzi huo.

“Kamati ilitoa muda kwa Serikali kukamilisha ripoti hizi na inategemea kupewa taarifa kamili ya uchunguzi huu,” alisema Mwenyekiti huyo

Alisema katika ziara ya kamati ilikagua mradi wa nyumba za NSSF za Kigamboni- Mtoni Kijichi lakini imebaini kulikuwa na haja kwa Serikali kwa upande mmoja na NSSF kwa upande mwingine kujiridhisha na ukweli au upotoshaji wa ukweli kuhusu tuhuma zinazoelekezwa katika kufanikisha miradi hiyo.

Mchengerwa aliutaja mradi wa Dege Eco Village uliopo Kigamboni ambao ni wa ubia kati ya NSSF na kampuni ya Azimio Holdings.

Aliongeza kuwa katika kikao cha kamati na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Novemba 17, mwaka huu kamati iliarifiwa kuwa taasisi za serikali kama Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru) na vyombo vingine vya usalama, vinaendelea na uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za miradi ya NSSF.

Siri Gomvi la DPP, AG Sasa Hadharani...!!

$
0
0

HATIMAYE siri kuhusiana na mvutano baina ya Mwansheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju na Mkurugenzu wa Mashtaka (DPP), Biswalo Mganga,

Zimeanza kufichuka ikiwa ni siku moja tu baada ya Rais John Magufuli kuwataka vigogo hao kutafuta suluhu baina yao kwa nia ya kufanikisha vyema shughuli za Serikali.

Uchunguzi uliofanywa na Nipashe kupitia vyanzo mbalimbali vilivyo karibu na wawili hao na pia kwa baadhi ya wabunge wa kamati inayoshughulikia sheria na katiba, umebaini kuwa mvutano uliopo kati yao ni wa masuala mazito yanayohusiana zaidi na majukumu yao.

Chanzo kimoja cha uhakika kilisema jana kuwa mgogoro wa wawili hao ulianza kitambo na kwamba, chanzo kimojawapo kikubwa ni mamlaka aliyo nayo kikazi kila mmoja wao na pia, lipo pia suala la safari za kikazi. Juzi, akizungumza katika sherehe za Siku ya Sheria jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli aliwataka wawili hao kutafuta suluhu ya mgogoro uliopo baina yao huku akiwakumbusha kuwa wote wana nguvu kubwa kwa sababu wameteuliwa naye.

Ohh..Mnyika Arudia yale Makali Yake Anapokuwa Bungeni,Aaanza Kuichachafya Serikali Kupitia Hili...!!!

$
0
0

MBUNGE wa Kibamba (Chadema), John Mnyika, ameiomba serikali kuhakikisha inawalipa fidia wakazi wa Mloganzila ambao waliacha maeneo yao na kupisha ujenzi wa Chuo Kikuu cha Tiba na Afya Muhimbili (Muhas).

Akiuliza swali kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mnyika alisema baadhi ya wakazi wa eneo hilo walilipwa lakini miongoni mwao walipata kiasi ambacho hakilingani na maeneo yao, hivyo kuonekana kupunjwa.

Aidha, Mnyika alitaka kufahamu kwa jinsi gani serikali inashughulikia madai ya mapunjo ya fidia ya maendelezo kwa wakazi hao waliotakiwa kuondoka kwa ajili ya kupisha ujenzi wa Muhas.

Hata hivyo, Naibu Waziri wa wizara hiyo, Angelina Mabula, alisema ahadi ya kuwalipa fidia ya kihisani yaani mkono wa heri iliyotolewa na serikali Mei 20, mwaka juzi, itafanyika baada ya kupatikana fedha.

Mabula alisema malipo hayo hayajafanyika kwa muda kutokana na ukosefu wa fedha kwenye bajeti, lakini pale zitakapopatikana hakuna atakayeshindwa kulipwa.

Alisema tayari serikali ilishalipa Sh. 8,067,904,700 kwa ajili ya fidia ya maendelezo ya ardhi kwa wananchi 1,919 katika kipindi cha 2008 mpaka 2010.

Aidha, alisema 2011 serikali ilitenga Sh. 1,610,374,700 kwa ajili ya fidia ya wananchi 619 waliosalia katika malipo hayo ya fidia, wakiwa wamewekeza ndani ya shamba mali ya serikali.

Hata hivyo, Mabula alisema mpaka sasa serikali haidaiwi mapunjo ya fidia kwa kuwa fidia ilikwishalipwa kwa mujibu wa sheria.A

Inasikitisha..Kiungo Yanga Taabani Iringa,Aomba Huruma ya Wadau wa Soka ...!!!

$
0
0

KIUNGO wa zamani wa kimataifa wa Tanzania aliyewai kuichezea Yanga, Geoffrey Bonny (37) imeelezwa yupo mahututi nyumbani kwao Iringa akisumbuliwa na maradhi ya homa ya matumbo na Malaria.

Dada wa mchezaji huyo ambaye pia aliwahi kuichezea Prisons ya Mbeya, Neema alisema jana hali ya kaka yake ni mbaya na anahitaji msaada ili apelekwe hospitali kubwa akapatiwe matibabu kuokoa maisha yake.

Neema alisema Bonny aliyewahi kuichezea Taifa Stars chini ya kocha Marcio Maximo, alifanyiwa vipimo katika hospitali ya Makandana Wilayani Rungwe na kuambiwa Bonny anasumbuliawa na Malaria na homa ya matumbo.

"Kwa sasa anapatiwa matibabu nyumbani kwa sababu hatuna tena uwezo wa kifedha wa kumpeleka hospitali kubwa," alisema Neema.

Aidha, alisema anaomba wadau wa soka wenye moyo wa kumsaidia kuwasiliana naye kwa simu ya mkononi (0 765 359 290).

Bonny aliichezea Yanga chini ya kocha Dusan Kondic na hata alipoondolewa kocha huyo, aliendelea kuichezea timu hiyo chini ya Kocha mpya Kostadin Papic.

Kiungo huyo anakumbukwa kuwa miongoni mwa wachezaji walioiwezesha Taifa Stars kufuzu na kushirki fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) zilizofanyika Ivory Coast mwaka 2009.

Mange Kimambi Amuomba Wakili Albert Msando Akamtoe Wema Sepetu

$
0
0
Mange kimambi ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram huku akiwa ameambatanisha picha ya Wakili Alberto Msando:

" Mkuu wananchi tunaomba uchukue kesi ya Wema probono.
Tena sio kumtoa ndani tu, tunaomba umfunze Makonda adabu by during him and the city for defamation wamlipe Wema mabilioni kama Yale Togo waliambiwa walipe.... 

Please please Albert tunaomba, Wema kutoka ndani sio solution kabisa, wameshamwalibia maisha yake, hawezi kufanya Kazi na kampuni yoyote ile kubwa,

Please please tunakuomba au kama vipi tujichange tukulipe".

Hadi sasa wasanii walioitwa kuhojiwa bado wanashikiliwa na jeshi la polisi

Roma Atolewa Bonge La Povu na Mkewe Mama 'Ivan' Kisa Hela ya Madee

$
0
0
Rapper Roma Mkatoliki ameonekana kukerwa na mkewe mama Ivan.

Mkewe huyo ambaye kwenye mtandao wa Instagram anatumia jina la @mrs_roma2030 amepost kwenye mtandao huo kipande cha video akiimba wimbo wa ‘Hela’ wa Madee na kuandika,
“Mengi nimepitia nikiwaadisia wengine mtalia sana/inamengi dunia usipoangali watawakatisha tamaa..heeee/laaa @madeeali.

Kitendo hicho kimeonekana kumuumiza Roma ambaye aliamua kutoa dukuduku lake kwa kuandika comment iliyowashangaza mashabiki,
“Shobo hilo mxiuuuuuu kwa wimbo gani basi nawe ukaenda kujiiimbiiishaaaa!!!??? MXIUUU wajitia kuuvalia na Ushungi mwana mkosa kazi wewe!! Kwa msanii gani basi….Msanii Maandazi huyo. Nyote namiona washamba tu. Mxiuuuuuu.”

Gigy Money Akanusha Madai ya Kuwa Anataka Kuokoka

$
0
0
Mtangazaji wa kipindi cha Lavidavi cha Choice FM, Gigy Money amekanusha uvumi ambao ulizagaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa anataka kuokoka.

Taaifa hizo zilidai kuwa video queen huyo anataka kuokoka ili kufuta mabaya aliyoyafanya katika kipindi cha nyuma.

Akiongea katika kipindi cha Star News cha Star TV wiki hii, mrembo huyo amedai hana mpango huo huku adai labda abadili dini kumfuata mpenzi wake wa sasa Mo J.

“Kusema kweli Gigy kama Gigy Gigy hana mpango wa kuokoka, niokoke kwanini labda nibadili dini kwa sababu ya mpenzi wangu wa sasa lakini sio kuokoka,” alisema Gigy.

Pia video queen huyo amedai kwa sasa anapata deal za matangazo mengi ya nguo kutokana mwonekano

CCM kama Chadema,wabadili Gia Angani kwa Staili hii..!!!

$
0
0

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema chama hicho siku ya kesho tarehe 5 mwezi wa pili kitakuwa kikitimiza miaka 40 toka kimezaliwa, kimefanya mabadiliko katika kusherehekea siku hiyo kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii

Akiongea na EATV Humphrey Polepole amesema toka chama hicho kimeanzishwa kimekuwa ni chama cha wananchama na chama ambacho kinashughulika na masuala ya watu watu pamoja na matatizo yao, hivyo mwaka huu wameamua kushurehekea siku hiyo kwa namna tofauti kwani hawatukuwa na sherehe kama desturi yao bali watasherehekea kwa kushiriki shuguli za kijamii.

"Maadhimisho ya mwaka huu yatakuwa tofauti kidesturi kama ambavyo yamefanyika hapo mwanzoni hivyo hatutakuwa na sherehe kama ilivyodesturi ya mikutano mikubwa ya hadhara , kwa maana ya uzinduzi na kilele isipokuwa mwaka huu tutafanya shughuli za maadhimisho ya CCM kwa namna kuu mbili, moja ni kwa kushiriki shughuli za kijamii, shughuli ambazo moja kwa moja zinagusa maisha ya watu wetu, jambo la pili ni mikutano ya ndani na hapa wanachama wote wa CCM watashiriki mikutano ya ndani kuanzia mikoa, ngazi ya wilaya, ngazi za majimbo, ngazi za kata na ngazi za matawi kwa kushirikisha mashina yetu kote nchini Tanzania.

Mbali na hilo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema kuwa maadhimisho ya miaka 40 ya CCM kwa mwaka huu yatafanyika kwa mwaka mzima huu wa 2017.
Ikumbukwe kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kilizaliwa tarehe 5 Februari, 1977 kutokana na kuvunjwa kwa vyama vya Tanganyika African National Union (TANU) na Afro-Shirazi Party (ASP).

IGP Mangu Awasimamisha kazi Askari Polisi Waliotajwa na Makonda Kuwa Wanahusika na Madawa ya Kulevya..!!!

$
0
0

Zikiwa zimepita siku mbili toka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda kutaja majina ya baadhi ya askari polisi pamoja na wasanii mbalimbali wakituhumiwa kuhusika katika ufanyaji wa biashara za madawa ya kulevya na matumizi ya madawa hayo

IGP Ernest Mangu leo amewasimamisha kazi askari 12 

Kufuatia sakata hilo la madawa ya kulevya, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu amewasimamisha kazi askari 12 kupisha uchunguzi baada ya askari hao kutajwa kushirikiana na wauza madawa ya kulevya.

Yafuatayo ni majina ya askari hao 12 ambao wamesimamishwa kazi le kupisha uchunguzi dhidi yao 

Ben Pol Anatoka na Tunda ...!!!?

$
0
0

Msanii Ben Pol amefunguka na kuweka sawa juu ya tetesi ambazo zipo mtaani kuwa anatoka na video queen Tunda ambaye sasa inasemakana anatoka na rapa Young Dar es Salaam.

Ben Pol alipokuwa kwenye kipindi cha Friday Night Live (FNL) alisema yeye alikuwa na urafiki wa mbali sana na Tunda na kusema hizo tetesi hazina ukweli kwani Tunda alikuwa rafiki wa karibu wa mdogo wake na si yeye.

"Siyo kweli sijawahi kuwa na mahusiano na Tunda nachojua mimi Tunda alikuwa karibu na mdogo wangu mimi yaani rafiki yangu wa karibu anaitwa Tonny Dagi, ndiyo alikuwa naye karibu sana, sijawahi kujua kama Tunda anajihusisha na mambo ya madawa ya kulevya sababu sijawahi kuwa karibu naye kivile, kusema nimekaa naye hata masaa sita au manne sijawahi kukaa naye karibu" alisema Ben Pol 

Mbali na hilo Ben Pol alizungumzia suala la video Queen huyo kuhusishwa na madawa ya kulevya, anadai kama ni kweli anajihusisha na mambo hayo si jambo zuri sababu tayari yule amekuwa kioo cha jamii kuna mabinti wengi wanamuangalia na wengine wanatamani kuwa kama yeye hivyo si jambo jema yeye kuwa huko.

"Kama ametajwa kweli na anafanya hivyo vitu, kiukweli siyo kitu kizuri haileti picha nzuri yeye ameshakuwa na impact kubwa, mabinti wengi wanamuangalia, wengine wapo mashuleni huko wanatamani kuwa kama yeye, kuwa ma models, wanajulikana kwa hiyo haiwezi kuleta picha nzuri kama ni kweli inabidi aache" alisema Ben Pol  

Wasafi Hawaponi Sakata la Dawa za Kulevya - Afande

$
0
0

Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kutaja majina ya kadhaa ya wasanii na polisi mbalimbali ambao wanajihusisha huku wengine wakituhumiwa na matumizi na uuzaji wa madawa ya kulevya.

Afande Sele amefunguka na kusema kama jambo hili litafanywa kwa haki na umakini basi huenda hata wale wasafi wakaonekana  ni wachafu.

Afande Sele ameonyesha wasiwasi juu ya sakata hili la madawa ya kulevya ila amesisitiza kuwa kama kweli litafanyikwa kazi kwa umakini mkubwa basi kuna kundi kubwa la watu ambao wanaonekana ni wasafi kuchafuka kutokana na sakata hili.

"Katika hili sakata la MAPAPA na MAPUNDA ya unga kama kweli braza Paul yupo 'serious' na sio 'Matango Pori'kama tulivyoona katika masakata mengine, huenda hata wale WASAFI wakaonekana wachafu...kila la kheri Mr Paul....RiP dada Amina...wacha party ianzeee" aliandika Afande Sele 

Kauli hii ya Afande Sele imekuwa ni kauli tata na imeibuka mjadala kwa baadhi ya mashabiki katika kuitafsiri wengine wakisema Afande Sele amezungumzia wasanii ambao wapo chini ya label ya WCB Wasafi chini ya Diamond Platnumz huku wengine wakisema amezungumzia watu ambao wanaonekana ni wema katika jamiii kumbe si wema bali ni wachafu kwa matendo yao kwa kujihusisha na biashara za dawa za kulevya.

Pichaa:Harmo rapaaaa....... Kama Mfalme

Tundu Lissu: Kuwataja Vidagaa na Kuwaacha Nyangumi/papa si Ajabu ni Moja Kati ya Mambo ya Hovyo

$
0
0
Anaandika Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu.

Kuwataja Vidagaa na kuwaacha Nyangumi/papa si ajabu ni moja kati ya mambo ya hovyo katika awamu ya 5

Ushauri wangu kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paulo Makonda Vita ya madawa ya kulevya ikiendelea kuwa ya one man show itafika mahali itamshinda, hii vita si ndogo ni kubwa sana hata raisi mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete analifahamu hilo.

Simba Wamebahatisha Tu - Kevin Sabato

$
0
0

Mshambuliaji Kevin Sabato wa klabu ya Majimaji FC baada ya timu yake kufungwa bao 3-0 dhidi ya Simba amefynguka na kusema kuwa Simba wamebahatisha katika mchezo huo kuwafunga goli hizo tatu kwa sababu wao waliwazidi Simba kimchezo.

Kevin Sabato amedai kuwa makosa waliyofanya uwanjani ndiyo yamepelekea Simba kushinda mchezo huo na kuchukua ushindi pamoja na point tatu, lakini kwa upande wake Mzamiru Yasini kiungo wa Simba amesema kuwa timu yake ilikuwa vizuri kila kona ndiyo maana imeweza kuchukua pointi tatu kwa kupata magoli matatu.

"Sisi tulijianda vizuri tukafanya vizuri kila sehemu ndiyo maana tumeweza kuwafunga goli tatu Majimaji FC, unajua ligi ya mwaka huu ina ushindani mkubwa sana hivyo ikitokea umepata nafasi unaitumia vizuri. Na sisis tumepata nafasi ndiyo maana tumewapiga goli tatu hivyo naweza kusema tuliwazidi sehemu zote" alisema Mzamiru Yasini 

Jack Pemba Afanya Birthday ya Kufuru…

$
0
0

Mfanyabiashara maarufu nchini aliyehamishia makazi yake nchini Uganda, Pedeshee Jack Pemba, jana alifanya birthday ya kufuru nchini Uganda, huku mwanamuziki mahiri kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Koffi Olomide akiwa ndiye mgeni rasmi.

Vipande vya video zilizosambaa mtandaoni, vinamuonesha Koffi akipafomu live wimbo wa Ekotite (Selfie) akiwa na bendi yake, ambapo Jack Pemba anamtunuku noti kibao za dola miamia, na kushangiliwa na ukumbi mzima.

Kabla ya kufanyika kwa birthday hiyo, awali video ya Koffi aliyojirekodi akiizungumzia birthday hiyo na kuahidi kwamba atakuwepo nchini Uganda, ilikuwa gumzo kubwa mitandaoni na tukio la jana limewaacha wengi midomo wazi kwani si rahisi kwa msanii kama Koffi, kukubali kwenda kupafomu kwenye birthday na hata akikubali, dau lake huwa si la mchezo.

Kamanda Sirro: Wema Sepetu, Nyandu Tozzy na TID bado wanashikiliwa na jeshi la polisi

$
0
0

Wakati macho na masikio ya Watanzania wakisubiri kusikia hatma ya wasanii wanaodaiwa kujihusisha na dawa za kulevya, wasanii wanne waliofika Kituo Kikuu cha Polisi bado wanashikiliwa na jeshi hilo kwa mahojiano zaidi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema kuwa bado wasanii hao Wema Sepetu, Dogo Hamidu, Khalid Mohamed (TID), na mtangazaji maarufu wa Clouds TV Babuu wa Kitaa bado wanashikiliwa na jeshi hilo.

“Bado tunawashikilia kwa mahojiano zaidi,” amesema Sirro kwa kifupi.

Wasanii wengine waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambao wanatakiwa kufika kituoni Jumatatu ni Vanessa Mdee, Tunda na watu wengine Halidali Kavila, Amani, Kashozi na Omry Sanga.

Kwa Wanawake tu..Fahamu Mbinu Kuntu za Kummaliza Mumeo Ndani ya Sita kwa Sita Hadi Akapagawa ..!!!

$
0
0

Weekend hii nimeona ni vyema tuzungumzie kidogo kuhusu masualaya mahusiano pia kutokana na sekta hiyo kuwa na umuhimu wake pia katika maisha ya mwanadamu.


Katika masuala haya ya mapenzi nimeona ni vyema niaanze kuongea na wanawake kuhusu namna ya kuweza kufanikisha kummaliza mwanaume katika sita kwa sita.

Jambo la kwanza wanamke unapaswa kuwa jasari na mwenye kuamini katika kile unachofanya katika mapenzi, ambapo wewe mwanamke unatakiwa mkishafika katika uwanja wenu wa zoezi husika katika sikiu hiyo, Hakikisha unajitahidi wewe kuanza kumvua nguo mwanaume, huku ukimshika baadhi ya sehemu mbalimbali za mwili wake ambazo unaamini zitamsababishia msisimko mkubwa.

Baada ya zoezi hilo nawe pia (mwanamke)unaweza kutoa nguo zako kisha mkumbatie mmeo , huku mkigusanisha ngozi za miili yenu. Tambua ya kwamba ngozi huwa na mishipa midogo midogo yenye ufahamu ambayo hutoa taarifa mbalimbali za mwili kwenye ubongo, hivyo kitendo cha miili yenu kugusana huchangia kuibua hisia za kimapenzi zaidi.

Unapoona tayari mwanaume yupo tayari katika hali ya hisia kali za kimapenzi kabla ya kumruhusu akuingilie unaweza kuendelea kumshika baadhi ya sehemu za mwili mfano ndevu, sehemu zake za siri na mkune kwenye viganja vyake na mapaja na nk.

Fahamu ya kwamba mapaja ya mwanaume huwa na hisia kali, hivyo unaweza kuyashika zaidi kwa ustadi mkubwa, huku ukitumia vidole vyako na utaona akisisimka zaidi.

Sehemu nyingine ambayo itakusaidia wewe mwanamke kuweza kumsisimua vizuri mwanaume ni kwa kumshika maeneo ya kifuani kuelekea tumboni maeneo hayo huwa na msisimko mkubwa kwa wanaume walio wengi.

Eneo jingine lenye hazina kubwa na ya msisimko wa mapenzi kwa wanaume ni sehemu ya uume ambapo mwanamke huweza kushika ile sehemu ya mbele (kichwa cha uume) ambapo humfanya mwanaume kupata msisimko wa kimapenzi kwa haraka zaidi.

Uwapo katikati ya tendo hakikisha unkuwa serious na zoezi hilo, huku ukijitahidi kuepuka kucheka kwa jambo lolote lile hata pale mwenzi wako anapotoa sauti za kufurahisha wakati wa katikati ya tendo.

Pamoja na hayo, mwanamke uwapo katikati tendo hilo na mwenzi wako jitahii sana kujiachia maungo yako kwa mmeo, kwani kwenye tendo hilo la ndoa huwa hakuna uheshimiwa hivyo ni vyema ukajiachia.

Katika tendo la ndoa pia sauti na maneno  ya kimahaba ni muhimu sana wakati wa tendo la ndoa kwani huongeza hamasa katika tendo hilo.

Baada ya kumaliza tendo hilo kumbuka kusema asante na mpe pole mwenzi wako kwa kazi pevu, kisha chukuwa kitambaa na mkaushe kijasho cha utamu wa penzi kwa taulo uliloandaa maalum.

Wema Sepetu, Asiyefunzwa na Mamaye Hufunzwa na Ulimwengu..!!!

$
0
0

Nakumbuka miaka ya zamani lulu nae alikua hivi hivi hashikiki, kila club yeye, kila rafiki yeye, mtoto alikua hashikiki mpaka mama yake akainua mikono, lulu anatoroka kwao usiku wa manane anaenda kwa wanaume, maisha yake yalikua kwa mashosti, shule akaikacha, umaarufu ukampa kichwa akajiona yeye ndio yeye, siku ya siku ikatokea ajali ( wote mnajua yaliyotokea) akawekwa rumande miezi kadhaa, Lulu akawa lulu machozi, alikonda ,maisha yake kila siku vilio, mashost wote wakamkacha, hakuna aliyekua na habari nae alipokua rumande, kila mtu alimkashifu kwa style yake, lulu akawa lulu machozi, rafiki yake akawa BIBLIA na rosali, lulu akamgeukia Mungu, Mungu si athumani akasikia kilio chake akatoka kwa dhamana, akawa HURU, tokea hapo hatukuwahi kumsikia lulu na marafiki wa ajabu ajabu, lulu club akawa haonekani,familia yake ndo ikawa rafiki yake pamoja na muna love na baadhi ya mastaa wachache, sasa hivi huwezi kukuta picha za lulu akilewa hovyo kama zamani (kuna tetesi aliacha pombe) , lulu akabadilika kabisa akawa mpya, sasa hivi katulia na boyfriend wake.

Back to wema, nadhani ni wakati wa mashabiki wa wema waache kushabikia upuuzi, hivi karibuni wema amekua na scandal chafu za kubadili wanaume na kuongozana na mashoga wasio na focus na maisha, wema kampani yake wanaume mashoga, mashangingi na wauza madawa (pengine hii imemcost) inawezekana mdada wa watu hata hausiki ila kwa kuwa anaongozana na wezi na yeye lazima wamuhisi mwizi, nadhani hili litakua ni funzo kwake, mama yake kashalia sana na wema mpaka wamegombana ila wema hasikii,anaishi maisha anayotaka yeye, pengine ni hao hao marafiki zake wa karibu wamemchomea, MIMI NADHANI WEMA AKIWEKWA NDANI KAMA MIAKA MIWILI AU MITATU nadhani atabadilika, najua watu watafikiria vibaya ila SIO KILA JAMBO BAYA LINATOKEA KWENYE MAISHA YETU KWA NIA MBAYA,mengine yanatokea kama funzo au baraka, mi nadhani ni wakati wa wema kukubali matokeo na kukaa ndani, im telling you akitoka wema atakua anaimba GOSPEL, huruma zenu zitamponza, jela hapaui ni sehemu ya kujifunza.

Burkina Fa­­so Mshindi wa Tatu Afcon 2017..!!!

$
0
0

Timu ya Taifa ya Burkina Faso imekuwa mshindi wa tatu wa mashindano ya Afcon yanayoendelea nchini Gabon, baada ya kuifunga Ghana 1-0 katika Uwanja wa Port-Gentil.

Mkwaju wa adhabu ndogo uliopigwa na Alain Traore katika dakika ya 89 uliomshinda kipa wa Black Stars, Richard Ofori ulitinga kimiani na kuifanya Burkina Faso kutwaa nafasi hiyo, ambayo Ghana imekuwa ikiitawala kwa muda mrefu.

Ghana ilitolewa na Cameroon katika hatua ya nusu fainali baada ya kukubali kipigo cha 2-0, huku Burkina Faso ikiondoshwa na Mafarao wa Misri kwa njia ya mikwaju ya penalti.

Leo usiku macho na masikio yataelekezwa Gabon kushuhudia fainali ya kukata na shoka baina ya miamba ya Cameroon na Misri, mechi ambayo itaamua bingwa wa mashindano hayo makubwa zaidi barani Afrika.

Misri ni mabingwa wa kihistoria wa Afcon kwa kuwa wametwaa taji hilo mara saba, huku Cameroon maarufu kama Indomitable Lions wakitwaa ubingwa huo mara nne.
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live




Latest Images