Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

LIMBWATA YA KUMPA MWANAUME IPO....JE YA KUMPA MWANAMKE ILI AKOLEE NA MIMI IPO?

$
0
0
Kwa wale wanaotokea/waliopo mji mkuu wa limbwata (TANGA), na miji mingine midogo (upare, unyirambani,uzaramoni) naombeni majibu ya chapchapa sehemu ya kupata limbwata la kumlisha mwanamke (jimama) kama ipo...kama haipo niambie ''HAIPO'' ili nisihangaike

KAULI NANE AMBAZO MWANAMKE AKIZITOA JIHADHARI SANA

$
0
0
1. Mwanamke anaposema, 'sasa hivi' au 'dakika moja tu,' maana yake ni kwamba, ni nusu saa ijayo. kwa mwanamke sasa hivi ya kujiandaa ina maana sasa hivi ya muda mrefu mara sita zaidi kuliko ule anaoutaja. kama akisema , 'nusu saa tu, naja,' unapaswa kwenda kufanya shughuli nyingine kwanza, kwa sababu huenda ukiamua kuamini kwamba ni nusu saa kweli, utasimama au kukaa mahali kumsubiri hadi miguu iingie tumboni au makalio yaote ganzi.
2. Mwanamke anaposema, 'utajua mwenyewe,' ana maana kwamba amekasirishwa na kukatishwa tamaa na tabia yako na sasa hajali tena. maana yake ni kwamba kwa upande wake haoni sababu ya kujiumiza bure na huenda atachukua uamuzi ambao nawe pia hautaufurahia. Je, anaweza kuanza kutoka nje baada ya hapo? inawezekana ingawa siyo lazima.




3. Mwanamke anapopumua kwa nguvu, yaani kushusha pumzi kwa kishindo, hiyo pia ni kauli kwa upande wake. kama anashusha pumzi kwa nguvu wakati mkijadili au kuongea jambo, ni taarifa kwamba amekudharau. yaani amekuona mjinga nambari moja. ni kauli kwamba, haoni sababu ya kuendelea kuwepo hapo kubishana nawe, kwani huna jambo la maana unalomweleza.


4. Mwanamke anaposhusha pumzi polepole, ina maana kwamba, amekubaliana na wewe. Sasa hapo usifanye kosa kwani, ukibadilika kidogo au kuleta mambo mengine kinyume na na hayo yaliyomridhisha, ndipo hapo atashusha pumzi kwa nguvu , yaani kuanza kukuona huna maana kwa wakati huo. Kumbuka kwamba, mwanamke akishusha pumzi kwa nguvu kwa maana ya kukuona huna lolote, hukuona hivyo kwa wakati ule tu au kwa hilo jambo linalohusika tu, siyo kwamba, hukuona hivyo siku au muda wote. vivyo hivyo kwenye kushusha pumzi pole pole, hukuona 'babu kubwa' kuhusiana na na jambo mnalojadili kwa wakati huo tu.


5. Mwanamke anapotumia neno, 'sawasawa,' kwa kawaida kama kuna jambo umemfanyia, ina maana kwamba, 'ninachukua muda kutafakari, halafu utaona nitakachokulipa baadaye.' Kauli hii siyo nzuri na mara nyingi ni ya hatari. Wanaume ambao wamewahi kulipiziwa visasi kwa njia mbaya na ya hatari na wapenzi wao wamekiri kuambiwa,'sawasawa,' au 'sawa bwana,' kabla ya visasi hivyo.


6. Mwanamke anapotamka neno, 'we endelea tu,' anakuwa na maana ya kwamba, siku si nyingi zijazo, atafanya jambo ambalo hutalifurahia, kama hutaacha kufanya kitu au jambo lenye kumuudhi. hiyo ni kauli ya kukutahadharisha kwamba, usije ukashangaa pale ambapo utaona amefanya kitendo cha hatari dhidi yako kutokana na tabia yako au matendo yako mabaya dhidi yake.


7. Kuna wakati mwanamke anaweza kusema, 'sawa bwana fanya,' kama kuna jambo ambalo hamjafikia muafaka au amebaini umekuwa ukifanya jambo fulani baya au lenye kumkera. Hapa hana maana kwamba, amekuruhusu kwa moyo mmoja, hapana. Hapa anataka ubaini kwamba, hajakubaliana nawe, anakupa muda wa kujaribu kutafakari tena.


8. Je kama mmeshindana katika jambo au umemkera katika jambo au mambo fulani, kutokana na tabia au mwenendo fulani, halafu akakumabia, 'asante sana,' itakuwa na maana gani? Hii ina maana umemkera kupita kiasi na bado wala hajajua akufanye nini. Hii ni toafauti na 'asante' ya kawaida. Mwanamke anapoongeza neno 'sana,'ujue umemkera hasa, kuliko unavyoweza kufikiri. Halafu kama baada ya kusema, 'asante sana,' anashusha pumzi kwa nguvu, ujue hali ni mbaya zaidi, bora unyamaze kwanza, hata radhi usiombe kwa muda huo, subiri apoe kwanza

MPOTO AELEZA SABABU ZA YEYE KUTEMBEA BILA VIATU HATA AKIENDA ULAYA

$
0
0
Msanii wa muziki wa asili Mrisho Mpoto amedai kuwa ajisikii vizuri pindi anapo vaa viatu kutokana kudai kuvaa viatu kuna athiri utendaji wa kazi zake.

Mpoto ameiambia bongo5 kuwa amesemwa sana kuhusu tabia ya kuto vaa viatu lakini ameshindwa kubadilika.

“Beauty yoyote ipo kwenye jicho,unapozungumzi Mrisho Mpoto kuwa peku ,sehemu nyingi sana,mara nyingi sana watu wananiona peku, ni kwa sababu ya kutafuta energy ,unajua energy ya mimi kuendelea kuishi inapatikana kwenye udongo,yani ngozi yangu inapokutana na ardhi nakuwa so (confident) na nakuwa Mpoto, zaidi na nguvu na nakuwa na akili ,sasa sipendi wakati mwingine kuwa fake,najitaidi sana kuwa wakisasa ila nakuwa nasahau,kwamfano naweza nikanunu kiatu cha gharama alafu nikakisahau kwenye ndege au kwenye basi kwasababu siyo kawaida yangu kuvaa viatu, nisha jaribu lakini nimeshapoteza vingi,kwasababu siyo culture yangu kuvaa viatu ,viatu navaaga kwasababu watu wananisema.kwaiyo nikivaa ninakuwa kama inanisumbua, nikaona kama bora niache,alafu nakuwa siko huru,ukinikuta nimevaa viatu alafu tukaanza kufanya mazungumzo nakuwa siko huru kwasababu nakuwa nipo kama naelea hewani,yani kama sina chaji,kwaiyo kwangu mimi ardhi ni kama plug ya mwili wangu,nikikanyaga chini wewe niulize chochote nitakujibu niambie niandike shairi la haina yoyote,mimi ata nikiandika nyumbani kwangu lazima niweke miguu kwenye mchanga,ata nyumbani kwangu hakuna mchanga mimi ninabeseni kabisa la michanga,kwajili tu yakukanyaga yani nikiandika nakuwa confidant ata nikiandika nakuwa na amani”Alisema Mpoto

Pia Mrisho ataendelea kufafanua kwanini ataki kubadilika na kuchana na tamaduni ya kutembea mbila kuvaa viatu

“Nataka maisha yasiniendeshe mimi,mimi niyaendeshe maisha, kwasababu unajua speed ya utandawazi yani globalization ni kubwa sana kuliko speed ya mwanadamu kwa Tanzania,ukiangalia watu kama Marekani wamepata uhuru miaka mia mbili iliyopita,sisi tuna miaka mingapi tu ya uhuru na teknologia inakuja kwa kasi sana,ndiyo maana technologia inapokuta Tanzania watu wanaimasta sana,kwamfano facebook,instargam,twetter,whatsapp na mitandao mingine vimekuja kwa kasi sana na watu vimewabadilisha sana,ata Ngugi wa Thiong’o alisema huwezi kwenda kwa jirani kama ujatokea kwako,mtu kaka mimi ninapoigia kwenye technologia siwezi badilishwa kwasababu nimeshajijua mimi ni
nani”Alimalizia Mpoto

UGOMVI WA PETER & PAUL WA P-SQUARE, MKE WA PETER NA KAKA YAO INASEMEKANA NDIO CHANZO

$
0
0
Ni siku chache tu zimepita toka Paul Okoye wa kundi la P-Square afanye harusi ya kimila na mke wake Anita Isama huko Nigeria, lakini baada ya wote wawili (Peter & Paul) kukamilisha majukumu ya ndoa zao, kuna habari ambazo zimesambaa wiki hii kuwa umeibuka ugomvi baina ya mapacha hao wa kundi la P-Square ambao inasemekana sasa hawaelewani vizuri.

Mtandao wa Naija Gists umeripoti kuwa kwa mujibu wa chanzo, inadaiwa kuwa kumekuwa na kutoelewana baina ya kaka mkubwa wa mapacha hao Jude Okoye na mke wa mdogo wake Peter Okoye aitwaye Lola Omotayo, kitu kilichopelekea Jude kutohudhuria harusi yao mwaka jana.

Kama unakumbuka Jude hakuhudhuria harusi ya Peter na Lola mwaka jana, lakini alihudhuria ya Paul na Anita mwaka huu kitu kinachowafanya watu waamini kuwa kuna tatizo kubwa baina yao.

Chanzo hicho kimesema inadaiwa kuwa ugomvi huo unaomhusu Lola umesababisha Peter na Paul kugombana wakati wako kwenye rehearsle Jumatano wiki hii, mpaka walipoachanishwa na dancers wao.


Kaka mkubwa wa P-Square Jude alitweet kitu ambacho kinaaminika kuwa kinahusiana na ugomvi wao.
“After over 10 years of hard work, it’s over. (I) Am done.” ikiaminika kuwa alimaanisha amejiondoa kuli-manage kundi hilo japo kuwa yeye mwenyewe hakufafanua alichomaanisha katika maneno hayo machache.

After over 10yrs of hard work, it's over. Am done.

— IG: @Judeengees (@judeengees) April 18, 2014

Jude ndiye amekuwa akiwa-manage kwa miaka yote na kuproduce hits zao paomoja na kudirect idadi kubwa ya video zao zilizofanya vizuri.

Lakini kuna baadhi ya watu nchini Nigeria wamedai kubwa kuna uwezekano kuwa ugomvi ‘hewa’ unaoendelea na kuripotiwa katika vyombo vya habari ukawa ni ‘hype’ ya kuandaa ‘kiki’ ya album yao mpya.

HAWA NDIO WACHEZAJI WALIOITWA KWENYE TEAM YA TAIFA STAR

$
0
0
Kocha Msaidizi wa Taifa Stars Salum Mayanga ametangaza wachezaji wengine 23 watakaoingia kambini kesho Aprili 20 kuungana na 16 waliotajwa awali kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi ambayo itachezwa Aprili 26 mwaka huu.
Wachezaji walioitwa ni makipa Aishi Manula (Azam),Deogratias Munishi (Yanga) na Mwadili Ali (Azam) upande wa mabeki ni Abdi Banda (Coastal Union),Aidan Michael (Ruvu Shooting),Aggrey Morris (Azam),Erasto Nyoni (Azam),Hassan Mwasapili (Mbeya City),Kelvin Yondani na Said Moradi (Azam).
Upande wa Viungo ni Amri Kiemba (Simba),Frank Domayo (Yanga),Himid Mao (Azam) na Jonas Mkude (Simba)na Washambuliaji ni Athanas Mdamu (Alliance), Haruna Chanongo (Simba), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Khamis Mcha (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngasa (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Markhiya, Qatar), Ramadhan Singano (Simba), Simon Msuva (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).
Wachezaji walioitwa kutoka katika kikosi cha maboresho ni kipa Benedicto Tinoko Mlekwa (Mara), mabeki wa kati; Emma Namwondo Simwanda (Temeke) na Joram Nason Mgeveje (Iringa). Walinzi wa pembeni ni Omari Ally Kindamba (Temeke), Edward Peter Mayunga (Kaskazini Pemba) na Shiraz Abdallah Sozigwa (Ilala).
Viungo ni Yusuf Suleiman Mlipili (Temeke), Said Juma Ally (Mjini Magharibi), Abubakar Ally Mohamed (Kusini Unguja), Hashim Ramadhan Magona (Shinyanga), Omari Athumani Nyenje (Mtwara) na Chunga Said Zito (Manyara).
Washambuliaji niMohammed Seif Saidi (Kusini Pemba),Ayoub Kasim Lipati (Ilala),Abdurahman Othman Ally (Mjini Magharibi),Paul Michael Bundara (Ilala). Wachezaji wa U 20 niMbwana Mshindo Musa (Tanga) naBayaga Athanas Fabian (Mbeya).
Taifa Stars inategemewa kuingia kambini kwenye hoteli ya Kunduchi Beach.

JUMA KASEMA SASA NI KOCHA WA MAKIPA TEAM YA TAIFA UNDER 20

$
0
0
YANGA inashuka dimbani leo Jumamosi  kucheza dhidi ya watani wao wa jadi, Simba katika mchezo wa kufunga msimu wa Ligi Kuu Bara lakini katika kikosi chao  hatakuwepo Golikipa, Juma Kaseja ambaye  imefahamika kwamba amepata kibarua cha muda  kukinoa kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’.

Akizungumza na Mwanaspoti Kocha Mkuu wa Yanga, Hans Pluijm amsema kuwa walipokea maombi kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia benchi la ufundi la timu hiyo ya vijana wakiomba Kaseja aende kuwanoa makipa wao.

Pluijm alisema mara baada ya kupokea barua hiyo benchi lake lilimruhusu kipa huyo kwenda kufanya majukumu hayo kutokana na kutokuwepo kwenye kikosi cha wachezaji waanaotarajiwa kushuka uwanjani kuumana na Simba leo.

“Ni kweli Kaseja hayupo, tulipata taarifa rasmi kuwa Ngorongoro Heroes ina tatizo la kocha wa makipa, wakatuomba tuwapatie Kaseja ili akawafundishe makipa wa timu hiyo kwa muda,” alisema Pluijm.

“Hatukuwa na sababu ya kumzuia kwa kuwa hakuwa kambini tangu timu ilipokuwa Arusha, tuliona tumpe baraka za kwenda kuwafundisha vijana hao lakini siyo kwamba hakuwa anahitajika katika timu.”

HUU NDIO UKWELI JUU YA JOKATE KUPIGA PICHA ZA UTUPU

$
0
0
Jokate Mwegelo amekanusha vikali kuhusiana na picha za utupu zilizozagaa mitandaoni hivi karibuni kuwa si zake.

Akizungumzia ishu hiyo, Jokate ambaye pia ni mwigizaji alisema kuna mitandao imeanzisha uvumi huo kwa kuweka picha ya mtu mwingine na kudai ni yeye.


Mitandao ya kijamii inakera sana. Kila mtu anaandika habari itakayowafanya watu wafungue ‘blogi’ yake, siwezi kupiga picha ya utupu,” alisema Jokate.

WACHINA NOMA..MAKOMBE FEKI YA DUNIA ZAIDI YA 1000 YAKAMATWA CHINA

$
0
0
Wakati ziara ya dunia ya kikombe halisi cha kombe la dunia ikiendelea kabla ya kukabidhiwa kwa mmiliki wake mpya ambaye ni mshindi wa mwaka huu huko Brazil, maafisa wa China wamekamata makombe feki ya kombe la dunia zaidi ya 1,000, yaliyokuwa yamedhamiriwa kuuzwa katika kona mbalimbali za dunia.

Ikiwa zimebaki siku chache kabla kombe la dunia 2014 halijaanza kutimua nyasi huko Brazil , maafisa wa forodha wa China wamekamata makombe hayo ya dhahabu 1,020 huko katika mji wa Yiwu yakiwa tayari kusafirishwa kuelekea Libya kuuzwa, na kabla ya hapo makombe mengine feki 1,008 yalikamatwa.

TAULO LA KIPA IVO MAPUNDA LALETA KIZA ZAA SIMBA NA YANGA LEO..LAHUSISWA NA UCHAWI

$
0
0
Katika mchezo wa Simba na Yanga Leo Ambao wametoka droo kwa kufungana moja kwa moja palitokea kituko ambacho kimewaacha wengi huo...Kama Kawaida yake Ivo Mapunda akiwa langoni Huwa anakuwa na Taulo kubwa Jeupe la kujifutia Jasho Ambalo hulininginiza Kwenye Nyavu za Goli ..Leo Mchezaji Didie Baada ya Yanga kukosa Goli langoni Hapo aliamua kulichukua Taulo hilo na Kukimbia Nalo na kulitupa kwa Mashabiki ...Kwa kile kinachodaiwa ni Dumba inayozuia Yanga Wasifunge....Ilibidi mchezo usimame kwa muda baada ya kuanza kushikana mashati kuhusu hilo taulo, Mwishowe Taulo lilirudi kwa Ivo Mapunda na Mchezo Kuendelea....

SABABU YA MAREHEMU GURUMO KUPOTEZA JICHO LAKE MOJA HII HAPA

$
0
0
Marehemu Gurumo kwa maisha yake yote alikuwa na ulemavu wa jicho moja lakini hakuna mwanamuziki wala mdau  au mwanahabari aliyekuwa anajua sababu ya madhila hayo ya mzee wetu mpendwa.

Gurumo akaileza Saluti5 mbele ya mdau mkubwa wa muziki Juma Mbizo sababu ya jicho lake kupotea.

Ilikuwa jambo la kusisimua sana. Alitupeleka hadi mbele ya nyumba yake na kukutana na mti wa mwembe na kisha akasema: “Leo nataka niwaambie jambo moja ambalo sijui kama yupo mtu anayelijua.

“Huu mti una historia kubwa kwangu. Hapa ndipo nilipopoteza jicho langu nikiwa na umri wa miezi mitatu.

“Mama yangu alinilaza kwenye kivuli cha mti huu kisha akaenda kuendelea na shughuli zake. Bahati mbaya likaanguka tawi na kutua kwenye jicho langu.

“Nilisimuliwa kuwa juhudi za hospitali hazikusaidia kitu, nikapoteza jicho langu,” alimaliza Gurumo na kisha akataka arekodiwe kwa njia ya video ili tujipatie kumbukumbu adimu.
Baadae tutakuwekea video ya Gurumo akisimulia namna alivyopoteza jicho lake.


P FUNK AFUNGA NDOA NA MTOTO WA ARUSHA HIDAYA

$
0
0
Producer Mkongwe wa Music Aina ya Bongo Flava Anayejulikana kama P-Funk Ameamua Kufunga Ndoa Baada ya Kukaa Muda Mrefu akiwa Bachelor ..P-funk Ambaye Siku za Nyuma Alikuwa na Mahusiano na Mcheza Movie za Kibongo Kajala na Kuzaa nae Mtoto mmoja ....P-Funk Amemua Hidaya Kutoka Arusha..
Hongera sana P-Funk Majani

UKAWA"HATUJAMPIGIA MAGOTI ZITTO KABWE"

$
0
0
Habari inayoenezwa kuwa viongozi wakuu wa UKAWA na hata waandamizi nikiwemo mimi, eti tumembembeleza mhe. Zitto Kabwe ili aunge mkono mikutano ya UKAWA kuzunguka nchi siyo taarifa zenye ukweli wowote.
Mhe Zitto hajawahi kufuatwa na viongozi kuombwa ashiriki ktk shughuli za UKAWA. Na hadi sasa UKAWA haijatangaza shuguli zozote zile zaidi ya mkutano wa Zanzibar ambao pia polisi wamekataa usifanyike leo hadi mara nyingine.
Kwa bahati nzuri, wakati mhe. Zitto Z Kabwe akichangia sura ya 1 na ya 6 bungeni, alionesha njia sahihi kwa taifa na kwa asilimia mia moja aliunga mkono hoja za wananchi na hata mapendekezo ya UKAWA.....Kwa mfano Zitto Kabwe alisema, "hoja ya serikali tatu kuvunja muungano siyo ya kweli. Alisisitiza kuwa muungano unaweza kuvunjika ndani ya serikali moja, mbili, tatu na hata tano"

Ujumbe wa UKAWA ni HIYARI. Ndiyo maana baadhi ya wajumbe kama ISACK CHEYO wali-walk out pamoja na UKAWA bungeni lakini keshoye walirejea na kuendelea na bunge.
Umoja huu unaheshimu haki wajibu na maamuzi ya kila mtu. Msimamo wa UKAWA ni kulinda na kutetea rasimu ya maoni iliyoletwa na tume ya mabadiliko ya katiba kwa msingi wa kulinda mamlaka na maoni ya wananchi.
Tutafanya kazi na mtu yeyote ambaye anaamini yale tunayoyasimamia. Hatutamuomba mtu yeyote asiyeona uzito wa hoja zetu atuunge mkono, badala yake tutaendelea kuwaheshimu wote wanaotofautiana nasi kwa hoja huku tukiendelea kupigania kile ambacho tunakiamini.
J. Mtatiro,
UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI(UKAWA),
Zanzibar.

NAHODHA WA MELI ILIYOZAMA KOREA MBARONI

$
0
0
Nahodha wa kivuko cha Korea Kusini kilichozama na kusababisha watu zaidi ya 300 kutojulikana walipo amekamatwa Jumamosi (19.04.2014) kwa tuhuma za uzembe na kuwatelekeza watu waliokuwa kwenye shida ya kuhitaji msaada. Wapelelezi wamemkamata Lee Joon -Seok na wafanyakazi wenzake wawili mapema leo asubuhi na wote watatu wameshutumiwa kwa kuwatelekeza mamia ya abiria waliokuwa wamenasa ndani ya chombo hicho na kuhangaika wenyewe kujiokowa. Mahakama imesema imeamuru kukamatwa kwao ili kuzuwiya watuhumiwa hao kukimbia au kuharibu ushahidi.

Nahodha huyo mwenye umri wa miaka 68 yuko chini ya uchunguzi kwa kuwa miongoni mwa watu wa mwanzo kuitelekeza meli hiyo wakati abiria wake wakiwa bado wako hatarini.Lee amefunguliwa mashtaka ya uzembe na kushindwa kuhakikisha usalama wa abiria kinyume na sheria za bahari.Abiria waliambiwa kupitia vipaza sauti kwamba wabakie hapo walipo licha ya kuwa meli hiyo ilikuwa ikizama upande mmoja.
Nahodha atetea uamuzi wake
Watu 32 imethibitishwa kuwa wamekufa katika janga hilo na wengine 270 hawajulikani walipo wengi wao ni watoto wakiwa katikasafari ya shule ya upili.
"Naomba radhi kwa wananchi wa Korea Kusini kwa kusababisha janga hili na nainamisha chini kichwa changu kuomba radhi familia za wahanga" Lee amewaambia waandishi wa habari wakati akiondoka katika mahakama ya Wilaya ya Gwangiu Tawi la Mokpo kuelekea gerezani leo asubuhi. Lakini ametetea uamuzi wake ulioshutumiwa vikali wa kusubiri dakika 30 kabla ya kuamuru kuchukuliwa kwa hatua za kuondolewa kwa abiria.
"Wakati huo mawimbi yalikuwa makali sana, hali ya bahari ilikuwa ya baridi,na nilifikiri kwamba iwapo watu wataondoka kwenye kivuko hicho bila tafakuri inayofaa na ikiwa hawakuvaa majeketi ya uokozi na hata ingelikuwa wamevaa, wangelisombelewa mbali na maji na kukabiliwa na matatizo mengine magumu" Lee amesema na kuongeza kwamba meli za uokozi zilikuwa bado hazikuwasili na pia kulikuwa hakuna meli zozote zile za uvuvi au mashua nyengine karibu wakati huo.
Watu wengi wangeliweza kuokoka
Wataalamu wamesema watu wengi zaidi wangeliweza kunusurika ingelikuwa wameondoka kwenda vituo vya uokozi kabla ya meli hiyo kuegemea sana upande mmoja na maji kuanza kujaa ndani.
Msaidizi wake wa tatu mwenye umri wa miaka 26 ambaye alikuwa na uzoefu wa miezi sita katu hakuwahi kabla kuongoza meli hiyo kwenye njia hiyo na ndie aliekuwa kwenye usukani wakati meli hiyo Sewol ilipozama.
Kwa mujibu wa sheria Lee alikuwa akitakiwa awe kwenye sitaha ya meli ambapo nahodha hutowa amri zake ili kusaidiana na wenzake wakati meli ikipita kwenye maeneo ya bahari chafu.
Mwendesha mashtaka mwandamizi Yang Jung-jin amewaambia waandishi wa habari nahodha huyo alikimbia kabla ya abiria.Ukanda wa video uliorushwa na shirika la habari la Yonhap umemuonyesha Lee akiwa miongoni mwa watu wa kwanza kuwasili ufukweni kwa kutumia boti ya uokozi.
Yang amesema wafanyakazi hao wenzake wawili waliokamatwa walishindwa kupunguza kasi ya mwendo wakati kivuko hicho kikiwa karibu na visiwa na wameshindwa kuchukuwa hatua zinazohitajika kuokowa maisha.
Kulikuwa na abiria 476 na mabaharia kwenye meli hiyo ya tani 6,825 wakiwemo wanafunzi 320 na walimu 15 kutoka Shule ya Upili ya Danwon huko Ansan karibu na mji mkuu wa Seoul wakati ilipoanza kupinduka na kuzama ikiwa safarini kutoka Incheon kuelekea kisiwa cha kitalii cha Jeju kilioko kusini.
Afisa wa ulinzi wa mwambao Ko Myung-seok amesema meli 176 na ndege 28 leo zimewekwa kufanya msako kwenye eneo karibu na ilikozama meli hiyo na kwamba zaidi ya wapiga mbizi 650 wanajaribu kulifikia eneo la ndani ya meli hiyo iliozama Jumatano.

CHADEMA BADO ELIMU SI KIGEZO KIKUBWA CHA KUPATA UBUNGE...JE NI SAHIHI?

$
0
0
  
1) Godbless Jonathan Lema -- Diploma
2) Antony Gervase Mbassa - - Adv diploma - KCMC
3) Prof Kulikoyela Kanalwanda Kahigi --- Phd
4) Freeman Aikaeli Mbowe – Form six
5) Highness Samsoni Kiwia ---- Secondary education – O level
6) Simon Peter Msigwa - -- O level,
7) Yohana Israel Natse --- Diploma in Education,
8) Halima James Mdee --- Degree, UDSM
9) Zitto Zuberi Kabwe --- Degree (economic) UDSM, Masters degree (MLB)
10) Silvester Mhoja Kasulumbay – Primary,
11) John Magale Shibuda --- O LEVEL
12) Joseph Osmund Mbilinyi --- Form IV
13) David Ernest Silinde --- Degree(BCOM), UDSM
14) Mustapha Boay Akunaay – Degree in law, Open University
15) Meshack Jeremiah Opulukwa --- Not updated
16) Philemon Ndesamburo --- Advanced diploma in Shipping
17) Said Amour Afri --- Primary school
18) Vicent Kiboko Nyerere -- O level
19) Ezekia Dibogo Wenje --- Degree, St Augustine
20) Joseph Roman Selasini --- Degree, UDSM
21) Tundu Antiphas Mughwai Lissu ___ LLM – Masters degree
22) John John Mnyika --- CV not updated
23) Salvatory Naluyaga Machemuli ___ Degree – DIT
24) Joshua Samwel Nassari – Not updated


Msitari mwekundu kwa Uongozi wa juu nchini kama Ubunge unatakiwa uwe juu ya Advance diploma, Hili la Ubunge kwa chadema ni kama vile Mheshimiwa slaa alivyotangaza Kirahisi kuhalalisha gongo kwa lengo la kuvuna kura za wanywa gongo eti atakuza uchumi kupitia watengeneza gongo na wanywaji! Kasahau kwamba gongo hata kama sio sumu ila inaweza kutengeneza genge la wavivu kufanya kazi, Hawajali taaluma na wanazidi kujitetea na kutangaza kwamba elimu sio kigezo cha lazima kwenye uongozi kwani wasomi wa ccm wamechemsha tangu Uhuru!.

Ukweli ni kwamba ukiondoa wabunge wasomi wachache wa chadema wengine ni wapiga kelele tu Bungeni wanafanya kuonekana tu kwamba wanaongea lakini ni wabunge wasio na mtazamo wambali wanaona mwisho wa pua zao tu.

Taifa zima linapaswa kuamua sasa Kukataa kuongozwa na waigizaji wa Darasa la saba, na lazima tusitumie maneno rahisi kujenga jamii isiyothamini elimu Kama tunavyoaminishwa na wanasiasa rahisi hawa ambao kwasasa wanaonekana kivutio kwa wasiosoma kama akina afande sere, JB, Ray, Mzeemajuto ambao lengo lao kusaka ubunge nikuongeza umaarufu wao ila hawana vission yeyote kwa Watanzania.

Bungeni sio sehemu ya kuenda kufanya sanaa, Bungeni sio kwenda Kuchekesha Bali nikuenda kuwawakilisha watu milioni karibia hamsini sasa ambao asilimia 80 wanaishi katika umasikini wakutupwa, acha mwanamziki afanye kazi ya mziki, muigizaji aigize, mchekeshaji achekeshe nasio kukimbilia mambo mazito ya kitaifa kwa umaarufu rahisi walionao.

Tujiulize swali Tunajenga Taifa gani kwa kuongoza na Darasa la 7 au wasanii? 
Hivi mzee majuto anataka aende Bungeni Kufanya nini kama sio dharau kwa Bunge letu? 
Mtu kama Lema au Sugu Ufahamu wake unaweza kulitoa taifa letu toka katika umasikini? au ndio tunazidi kuongeza migogoro katika jamii? 

Tusitumie Kigezo rahisi Eti wasomi wameshindwa basi kilamtu awe kiongozi katika jamii, angalia ukweli Hivi mtu kama zitto au J Mnyika anaposimama bungeni unaweza kufananisha na sugu au Lema.

Taifa lolote lililoanza kupoteza Muelekeo linaanza kukumbatia wasio soma na wahuni kama akina lema na sugu na hii ni dalili mbaya Lazima Tujitambue na Tutambue athari za mfumo huu unaojongea Taratibu, Tusipokuwa makini Tutafanya kosakubwa sana kwa kuongozwa na Dicteta ambae kichwa chake ni sifuri kabisa.


Chadema Kama chama Mbadala talajali wa CCM, jitahidini kutujengea viongozi Bora, shawishini wasomi wagombee nafasi kubwa kama ubunge na msiangalie umaarufu wa mtu kwasababu baadaye mkipewa nchi mawaziri watabaki kunywa gongo, kuvuta bangi, kufanya maigizo, na kuimba bongo flever tu badala yakuwa serious kujenga Uchumi.

Wabunge ambao ni darasa la saba je wanajiendeleza kielimu au ndio wamebweteka wakijua chadema Hakuhitaji wasomi? au nadharia yenu ya kuogopa umaarufu wao ndio bado itawapa nafasi ya kugombea ubunge tena 2015?, Tuleteeni akina Mnyika, akina mdee, akina zitto wengi2015 nasio kutujazia watu waliokimbia umande eti wanaweza kwakuwa wapiga kelele wasiojua hata uelekeo.


Uchaguzi wa 2015 lazima Uwe uchaguzi utakaotuletea wasomi vijana wengi bungeni, Sugu, Lema, Majimarefu, Murugo, wote jiandaeni kugombea labda udiwani na hata baadhi yenu udiwani pia hauwafai gombeeni serikali za mtaa mwakani.

MARTIN KADINDA: ‘KUMMENEJI’ WEMA SHUGHULI PEVU

$
0
0
Stori: Musa Mateja
MENEJA wa Wema Isaac Sepetu, Martin Kadinda amekiri kuwa kumsimamia ‘kummeneji’ staa huyo ni shughuli pevu kwani ana tabia ya kubadilika.

Alisema Wema anahitahi hesabu kwani kuna vitu unaweza kupanga naye lakini akashindwa kutimiza kutokana na hisia zake binafsi.

“Kuna wakati unaweza kumwambia usitoke hadi nikuruhusu lakini cha ajabu unakuja kushtukia mwenzio yupo mtaani jambo ambalo hamkukubaliana, ni ngumu we’ acha tu,” alisema Martin Kadinda ambaye pia ni mbunifu wa mavazi.
GPL

KAJALA: NINA MACHOZI YA KARIBU

$
0
0
STAA wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘K’ amefunguka kuwa machozi yake huwa yapo karibu hivyo ukimuudhi kidogo tu lazimaali

Akipiga stori mbili-tatu na Bongowood, Kajala alisema: “Machozi yangu yapo karibu sana sijui kwa nini huwa nashindwa sana kujizuia yaani mtu akinikorofisha kidogo tu lazima nitoe machozi ndipo hasira zitulie.”

BREAKING NEWS:MELI ILIYOBEBA SUKARI HAIKUZAMA, SHEHENA IMEIBIWA NA KUUZWA KENYA

$
0
0
Ile meli iliyotangazwa imezama katika ziwa Victoria na tani 280 ya sukari siyo kweli. haikuzama ila umefanyika wizi na mmiliki wa meli hiyo Kitana Chacha wa Mwanza ambaye ikiwa njiani zilikuja boti kadha kutoka Kenya na sukari ikapakuliwa na kuingizwa kwenye hizo boti, na baada ya hapo meli ikazamishwa kwa kutobolewa chini ingawa haikuzama yote.

Inafaa vyombo husika vichunguze issue hii kwa kina na huyo Kitana na wafanyakazi wale wa meli wahojiwe kueleza ukweli.
Source:JF

KISA CHA KWELI KILICHONITOKEA..MASHEMEJI WENGINE NUKSI KWELI

$
0
0
Baada ya mke wangukunitambulisha yule shemejihisia za mapenzi zikaanzakunishika kwa kasi ya ajabu.

Nikajiapiza lazima nihakikishenampata kwa gharama yoyoteile.

Shem wangu yule kiukwelikaumbika maana guu guu hipshizoo na kwa upande waucheshi wake mimi sisemi kitu.

Basi nikaidaka namba yake nakuanza kumpa manjonjo nabaada ya muda mtoto akatiatimu na kuendana na matakwayangu yaaani kwa kifupiakasalimu amri.Akaniahidi tukutane hotel ilianipe furaha nami sikuwa na laziada zaidi ya kumpa fedha ilisiku ikifika nimkute kunakochumbani.

Siku ikafika mtoto akaniambiayuko kunako hoteli na mienikaenda na kabla ya kuingiahotel nikaona bora nipige vilobakwanza vinitoe nishai na kunipamaujasiri.

Nikavipiga weeee kisha nikaanzakuona naishiwa nguvunikamwomba twende tukajilievyetu.

Akanichukua na kunilazakitandani na akaniambiaanaenda kununua maji hotelnna kwa kuwa nilishajichokea namikonyagi nikalala nanakumbuka usiku nikaamkakumpa gemu moja tafu sana naakanisifia na tukaendelea kulala.

Asubuhi naamka niwashe taa nakwenda chooni nilishangaakuona kumbe pale hotelininililala na mke wangu.

Mke akashtuka na kusemambona umeduwaa nikakaakimya kwani nilimdanganyanaenda morogoro kikazi kwasiku moja ana nikaanza kuhisikuwa kuna ka mchezo pale.

Nimechanganyikiwa na sina chakusema maana naona wamenipawakati mgumu kwa kunitegeamtego huu.Sijui nifanyeje nimedata..i hatemashemu wote.

HATIMAE MSEMAJI WA P-SQUARE AONGEA KUHUSU TETESI ZA KUVUNJIKA KWA KUNDI

$
0
0
Wiki hii mitandao ya Nigeria iliripoti kuwa kulikuwa na ugomvi mkubwa kati ya mapacha wanaounda kundi la PSquare, Peter na Paul Okoye na kwamba walitaka kupigana wakati wakiwa mazoezini.

Habari hizo zilichochewa na tweet ya kaka yao mkubwa ambaye ni meneja wao, Jude Okoye iliyootafsiriwa na mitandao hiyo kuwa huenda ameachana na kundi hilo baada ya kuwepo ugomvi kati yake na ndugu hao kutokana na msimamo wake wa kutohudhuria ndoa ya kisasa ya mdogo wake itakayofanyika Dubai.

Mitandao hiyo iliandika kuwa Jude Okoye hapatani kabisa na mke wa Peter Okoye, Lola Omotayo.

“After over 10 years of hard work, it’s over. Am done.” Alitweet Jude Okoye.

Hata hivyo, msemaji wa kundi hilo anaejulikana kama Bayo Adetu amekanusha habari hizo wakati akiongea na Premium Times na kudai kuwa hafahamu habari hizo zimetoka wapi.  

“I am too busy to give some wanna be blogger traffic, I don’t know where that report is coming from. Maybe they just want to get traffic to their site. It’s baseless and untrue.” Amesema Bayo Adetu.

OMBI LA JUSTIN BIEBER KUFUKUZWA MAREKANI KWA KUWA ANA TABIA MBAYA LAGONGA MWAMBA

$
0
0
Hatimaye ikulu ya Marekani imejibu ombi lililotolewa na raia wa Marekani kwa Rais Barack Obama kumfukuza Justin Bieber nchini humo, ombi lililopata sahihi takribani 275,000 ndani ya siku 30 na kuvuka kiwango cha sahihi 100,000 zilizotakiwa kumfanya rais alifikirie.

Katika tamko hilo, Ikulu ya Marekani imeeleza kuwa haita-comment kuhusu ombi hilo linalojulikana kama ‘We ThePeople’.

Thanks for your petition and your participation in We the People. Sorry to disappoint, but we won’t be commenting on this one ...” Imeeleza katika tamko hilo.

Hata hivyo, imewashukuru watu hao kwa kuonesha kujali kuhusu suala la uhamiaji na kwamba suala hilo wamewaachia watu wengine walizungumzie.

“So we'll leave it to others to comment on Mr Bieber’s case, but we’re glad you care about immigration issues. Because our current system is broken."

Watu 275,000 walisaini ombi hilo kwa madai kuwa Justin Bieber amekuwa mfano mbaya kwa vijana wa Marekani kutokana na matendo yake mabaya ikiwemo uvutaji wa bangi, matendo ambayo yalikuwa yakiripotiwa mara kwa mara huku akiripotiwa kuwa kero kwa jirani zake.

Bieber amekuwa akikabiriwa na kesi kadhaa na nyumba yake kupekuliwa na polisi, huku akisimama kizimbani mara kadhaa kujitetea.  

Hii ni petition hiyo iliyopata sahihi 275,000:

"We the people of the United States feel that we are being wrongly represented in the world of pop culture. We would like to see the dangerous, reckless, destructive, and drug abusing, Justin Bieber deported and his green card revoked. He is not only threatening the safety of our people but he is also a terrible influence on our nations youth. We the people would like to remove Justin Bieber from our society."
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live


Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>