Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

RIDHIWANI 'Kukamilika kwa Uchunguzi Kuhusu Biashara ya Dawa za Kulevya ni Ukombozi Kwangu'

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Chalinze na mtoto wa Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Ridhiwani Kikwete aonyesha jinsi gani anaumizwa na tuhuma za muda mrefu zinazosambaa katika mitandao ya kijamii zikidai kwamba anahusika kwenye sakata la bishara ya dawa za kulevya.


Hivi karibuni mbunge huyo kupitia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio aliweka wazi namna ambavyo anaiunga mkono serikali katika vita ya dawa za kulevya.

Jumatano hii ameamua kurudi tena na kueleza jinsi navyoumizwa na kile kinachoendelea katika mitandao ya kijamii kuhusu tuhuma za kujihusisha na biashara hiyo.

“Ni jambo jema na la faraja kubwa kwangu kama uchunguzi unafanywa. Ni ukombozi kwangu, Ukweli utajulikana kuwa ni uvumi tu usiokuwa na chembe ya ukweli,” aliandika Ridhiwani Instagram.

Aliongeza,
“Ni maneno ya watu wasionitakia mema. Sina la kuficha. Sifanyi biashara hiyo haramu na wala sijawahi kufikiria kufanya. Ni bora kufa maskini kuliko kutafuta utajiri kwa njia hiyo,”

Uvumi huo umekuwa kwa kasi hivi karibuni baada ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kumkabidhi Kamisha wa kupambana na dawa za kulevya, Rogers Sianga majina 97 ya watu wanaotuhumiwa kufanya biashara hiyo.

Mkuu wa mkoa huyo wakati wa kukabidhi majina hayo alidai wako vigogo wa biashara hiyo pamoja na watoto wa viongozi.

KIBITI: Watu Watatu Wameuawa Akiwemo Afisa wa Upelelezi

$
0
0
Kibiti. Watu watatu akiwamo OCCID wa Wilaya ya Kibiti, Peter Kubezya wamefariki dunia kwa kupigwa risasi na watu wadhaniwa kuwa ni majambazi katika Kijiji cha Jaribu wilayani hapa.

Mkuu wa Wilaya ya Kibiti, Gullamuhusein Kifu amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kusema watu sita wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha za moto walikivamia kituo change Wiley's cha kukusanyia ushuru kilichopo kijijini hapo.

Taarifa za awali zimeeleza kuwa mauaji hayo yametokea usiku wa kuamkia leo Jumatano ambapo watu hao wanaodhaniwa kuwa majambazi wakiwa na bunduki walivamia kuzuizi cha maliasili kilichopo kijijini hapo na kukichoma moto kabla ya majibizano ya risasi na polisi wakiokuwa doria kwenye eneo hilo.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Misheni ya Mchukwi, Zakaria Lukeba amethibisha kufikishwa kwa mwili Kubezya ukiwa na jeraha la risasi tumboni pamoja na maiti mbili ambazo hazijajulikana majina.

ZITTO Kabwe Azidi Kuibana Serikali Kuhusu ufisadi wa IPTL....Amtaka Rais Magufuli Achukue Hatua

$
0
0
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, ameendelea kumtaka Rais Magufuli kuchukua hatua dhidi ya anachokiita ufisadi katika kampuni ya uzalishaji umeme ya IPTL, inayomilikiwa na Kampuni wa PAP.

Tangu Rais Magufuli alipoingia madarakani mwezi Novemba mwaka 2015, Zitto amekuwa mstari wa mbele kumsihi na kumuomba Rais Magufuli afanye maamuzi juu ya kampuni hiyo ambayo imekuwa ikilipwa milioni 300 kila siku bila kujali kama inazalisha umeme au la.

Kupitia mitandao ya kijamii, Zitto ameandika "Rais John Magufuli ana fursa ya kihistoria kumaliza kabisa huu mtandao wa wizi na utapeli uliodumu toka mwaka 1995. watanzania masikini na wanyonge tutakuwa nyuma yake kwenye hili. Atende sasa."

Mnamo tarehe 21, Septemba 2016 Mhe. Zitto Kabwe alimtaka tena Rais Magufuli aoneshe hasira zake dhidi ya hicho anachokiita ufisadi mkongwe wa IPTL huku akieleza masikitiko yake juu ya kutochukuliwa kwa hatua zozote hadi sasa.

Mhe. Zitto Kabwe ambaye amekuwa hachoki kulizungumzia sakata hilo la IPTL amehoji ni nini kipo nyuma ya pazia, na ni nani mfaidika hadi hatua zisichukuliwe, huku akitoa ushauri wa hatua zinazoweza kuchukuliwa na mahakama kwa sasa.

"Mahakama Ina uwezo wa kurejea maamuzi yake kwa kuitisha upya kesi zilizoamuliwa. Hivi hii Mahakama haioni suala la PAP kumiliki IPTL na kuchota mabilioni ya fedha zilizokuwa Benki Kuu na kuendelea kulipwa tshs 300m kila siku izalishe au isizalishe umeme? Ushahidi wote ulionyesha utapeli wa Kimataifa uliofanywa na Harbinder Singh Seth lakini kivuli cha uamuzi wa Mahakama umefanya matapeli hawa kuendelea kunyonya fedha kutoka TANESCO. Huu mrija wa PAP/IPTL upo kinywani mwa The Chato Inc? Ama ni jipu la mgongoni?". Alihoji Mhe. Zitto Kabwe

MBOWE 'Nina Mpango wa Kudai Fidia Kwa Kuchafuliwa Jina

$
0
0

Sakata la kutajwa kwa Mbowe Katika List ya Madawa ya kulevya iliyotangazwa na Paul Makonda lazidi kuchukua Sura Mpya baada ya Mbowe Kufunguka Haya:

"Nina mipango wa kudai fidia kwa kuchafuliwa jina, hilo liko wazi nilisema toka siku ya kwanza kwa hiyo mpango huo lazima tutautekeleza" Mhe. Freema Mbowe

Toa maoni yako

Wema Sepetu Atinga Maahakamani....Kesi Yaahirishwa Hadi March 15

$
0
0

Mwigizaji Wema Sepetu leo alienda tena  Mahakamani baada ya kuachiwa kwa dhamana kwenye sakata la dawa za kulevya baada ya kutajwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda.


Kesi hiyo imeahirishwa hadi  15 March 2017 baada ya upande wa Mashtaka kusema upelelezi bado  haujakamilika 

Wafanyakazi 14 wa Kampuni ya Quality Group ya Manji Wafikishwa Mahakamani

$
0
0

Raia  14 wa India ambao wanafanya kazi Quality Group iliyo chini ya Yusuf Manji leo wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka matatu likiwemo la kufanya kazi nchini bila ya kuwa na kibali.


Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha.


Hati ya mashtaka, iliyosomwa na mwendesha Mashtaka, wa uhamiaji Method Kagoma imewataja washtakiwa hao kuwa ni Rojat Surkar, Jagadish Mamidu, Niladri Maiti, Sivarar Raja Sekaran, Mohammed Taher Shaikh, Bijenda Kumar, Prasoon Kumar Mallik na Nipun Dinbandhu Bhatt.


Wengine ni Pintu Kumar, Anuj Agurwa, Varun Boloor, Arun Kumar Kateel, Avinash Chandratiwari na Vikram Sankhala.


Akisoma hati ya mashtaka, Kagoma amedai kuwa, Februari 13, mwaka huu, huko katika ofisi ya Quality Group Ltd iliyopo katika Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, washtakiwa hao walikutwa wakiwa na viza zilozoghushiwa za kufanyia kazi.


Katika shtaka la pili ilidaiwa kuwa siku na mahali hapo washtakiwa hao wakiwa raia wa India walikutwa wakiishi nchini Tanzania bila ya kuwa na kibali.


Kagoma aliongeza kuwa, Februari 13 mwaka huu, katika jengo la Quality Group washtakiwa hao wakiwa raia wa India walikutwa wakijihusisha na kufanya kazi katika kampuni hiyo kama washauri bila ya kuwa na kibali cha kufanya kazi nchini.


Hata hivyo, washtakiwa hao ambao wanatetewa na mawakili watatu, Alex Mgongolwa na Hudson Ndusyepo wamekanusha kujihusisha na tuhuma hizo na wako nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana.


Mahakama iliwaamuru washtakiwa hao kuweka dhamana ya milioni tano kila mmoja na kuleta mdhamini mmoja kila mtu atakayeweka  kiasi hicho cha fedha.


Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 7, mwaka huu.

HUKUMU ya Kesi ya Sheria ya Makosa ya Mtandao iliyofunguliwa na Jamii Media Yashindikana Kusomwa

$
0
0

Hukumu ya Kesi ya Sheria ya Makosa ya Mtandao iliyofunguliwa na Jamii Media yashindikana kusomwa. Sababu za msingi hazijaelezwa.

Jaji Koroso ambaye pia alikuwa akisimamia kesi hiyo amehamishiwa katika Mahakama ya Ufisadi.

Aidha mpaka sasa haijajulikana ni lini Kesi hii iliyofunguliwa tarehe 4 mwezi Machi mwaka jana itatolewa hukumu.

SIWEZI Kufanya Collabo na Gigy Money...Amber Lulu Afunguka

$
0
0
Hakuna mtu hapa Bongo ambaye hakumbuki urafiki wa warembo wauza nyago(Video Vixens)Amber Lulu na Gigy Money, waliokuwa karibu na vitu vingi walifanya pamoja.

Mwaka jana,urafiki wao ulivunjika baada ya Amber Lulu kusemekana kwamba alikamatwa na madawa ya kulevya huko Arusha,na Gigy Money akawa anamuua Shosti yake huyo kwenye vyombo vya habari.

Umepita muda sasa tangu kila mmoja achukue time yake, lakini time hii wamekutana kwenye fani nyingine tena. Gigy Money aliingia kwenye muziki mwaka jana,na Amber Lulu naye ameenda huko huko kwa kutoa pia ngoma yake.

Kwenye interview na Kipindi cha Supermega cha Kings Fm kinachoongozwa na Prince Ramalove, Amber lulu amedai kuwa japo wamekutana kwenye fani hii ya muziki tena,lakini hawezi kufanya collabo na rafiki yake huyo wa zamani.

“Am not ready,” amesema Lulu. “Nahisi kuna vitu vinatofautiana. Anachofanya yeye na ninachofanya mimi ni vitu viwili tofauti, kwahiyo sidhani kama inaweza ikatokea labda hapo baadaye sana,ila sio sasa hivi,” ameongeza.

Katika hatua nyingine mrembo huyo amewaomba mashabiki wake na wapenzi wa muziki mzuri waendelee kumsapoti kwenye ngoma yake hiyo ambayo kichupa chake kinapatikana Youtube tayari.



YUPI Anayefaa, Tajiri ila Hana Muda na Mimi au Mwenye Uwezo wa Kawaida ila yupo Nami Muda Wote

$
0
0
Kama kichwa cha Habari kinavyojielezea mimi ni binti mrembo tu Nina kaxi yangu nzuri Namshukuru Mungu, nimepita kwenye mahusiano kadhaa changamoto hazikosekani Nimekutana na wenye uwezo wanaoweza kanipa Nitakacho na wenye uwezo wa kawaida tu.

Nilichojifunza ni kwamba Unaweza kuwa kwenye mahusiano na mtu Anaejiweza akakupa kila utakacho ila hana muda na wewe hamna out wala muda wa kukaa mkayajenga hata mazungumzo ya kawaida maana mimi ni mpambanaji

Mkikutana ni show basi siku zinaenda mwaka umekatika hamna la maana na sio kwamba anamahusiano mengine Hapana ingawa Mwanaume huwezi msemea ila ni mtu ambaye uko nae huru ila yuko busy muda wote hawezi kujenga muda kwa ajili yako ila muda wa kufanya mengine kama kwenda Bar, karaoke nk anao

Pili Mwanaume Ambae hawezi kukuhudumia kwa chochote mnapata muda wa kuzungumza kushauriana kupanga Mambo ya maendeleo ingawa hamuwezi kwenda out nk kutokana na kipato ila mapenzi mnayafurahia hata kwa kukaa ndani tu coz mimi sio mtokaji na haijawahi kunipa chochote wala sijawahi kumuomba coz namjua Hali yake

Ingawa ana wasiwasi na mimi kutokana na uwezo wake na urembo wangu ila mimi sina tatizo coz najimudu kwa kila kitu. sasa huyo mwenye uwezo miezi4 hatuko vizuri na naona nimeshindwa mimi kwa moyo mweupe coz sijawahi kuenjoy nae hata siku moja nataka kumpokea huyu wa Hali ya kawaida kwa moyo mmoja tujenge familia maana kule naona utumwa naombeni Ushauri ndugu zangu

By Vantz

Thomas Ulimwengu kukipiga na kiungo wa zamani wa Arsenal timu moja huko Sweden

$
0
0


Kiungo wa kimataifa wa Ghana aliyekuwa akiichezea timu ya Arsenal ya England kuanzia Academy na mwaka 2011 kupandishwa kucheza timu ya wakubwa Emmanuel Frimpong, amejiunga na timu ya AFC Eskilstuna iliyopanda Ligi Kuu Sweden msimu huu.

Emmanuel Frimpong amejiunga na AFC Eskilstuna ambaye wiki kadhaa nyuma mtanzania Thomas Ulimwengu alijiunga nayo pia kwa mkataba wa miaka mitatu, baada ya kumaliza mkataba wake wa TP Mazembe na kutotaka kuongeza.

Frimpong anajiunga na AFC Eskilstuna ikiwa ni siku chache zimepita toka avunje mkataba na timu ya Arsenal Tula ya Urusi, ambapo katika msimu wake mmoja alikuwa hatumiki sana na alipata nafasi ya kucheza mechi tatu kwa mujibu wa mtandao wa ghanasoccernet.com

AFC Eskilstuna inaonekana kudhamiria kuleta ushindani katika Ligi Kuu Sweden inayotarajia kuanza mwezi March, Frimpong alikuwa nahodha wa timu ya taifa ya vijana ya England U 16 na amekulia katika Academy ya Arsenal kuanzia 2001-2011 alipopandishwa timu kubwa na kuichezea hadi 2014.

PAUL Makonda Ashindwa Kufika Clouds FM Kutoa Ufafanuzi Kuhusu Elimu na Mali Zake

$
0
0

Jana Redio ya Clouds kupitia kipindi cha Power Breakfast walitangaza kuwa siku ya Leo Atakuja mkuu wa Mkoa Paul Makonda kutolea ufafanuzi mambo mbali mbali kuhusu yeye ambayo yamekuwa yakiongelewa na kushutumiwa bila yeye kutoa majibu.

Sasa asubuhi ya Leo kipindi hicho kimeomba radhi kuwa Leo Mh Paul Makonda hata weza kuja kwenye kipindi hicho kutokana na majukumu ya kiserikali yanayomkabili siku ya leo

MREMBO Zari Hassan Atoa Ushauri Kwa Wadada Wanaopenda Kutembea na Waume za Watu

$
0
0

MREMBO Zari Hassan Atoa Ushauri Kwa Wadada Wanaopenda Kutembea na Waume za Watu

MREMA Aibuka Sakata la Madawa ya Kulevya..Ampinga Lissu Kutetea Watuhumiwa wa Dawa Hizo

$
0
0

MWENYEKITI wa Parole, Augustino Mrema amemshukia Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), kuwa anafanya makosa makubwa kutetea watuhumiwa wa dawa za kulevya.

Akizunguma na MTANZANIA kwa simu jana, Mrema alisema anamshangaa Lissu kuwatetea watu wanaojihusisha na dawa za kulevya na kumshauri atumie elimu yake ya sheria kuwatetea waathirika na wanaotaja wahusika wa dawa za kulevya akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Mbali na Lissu, Mrema aliigeukia  mahakama itambue kuwa pamoja na kutafsiri sheria, jukumu la kuzuia dawa za kulevya lipo mikononi mwao.

“Nashangazwa na hawa wanaotuhumiwa kukataa kwenda kupimwa na kuonyesha juhudi za kuzuia zoezi hilo, wakubali kwenda kupimwa kwani ndio itakuwa kusafishwa kwao kama majibu yatatoka kuwa hawatumii,” alisema Mrema.

Akizungumzia kauli hiyo, Lissu alisema Mrema anapaswa kujiuzulu cheo alichopewa cha Mwenyekiti wa Parole kwa sababu alipewa kinyume cha sheria.

Alisema sheria ipo wazi kwamba Mwenyekiti wa Parole awe jaji au alishawahi kuwa jaji na si mwanasiasa kama Mrema.

“Ninapoona Mrema anapiga kelele, anatetea chakula chake na si vinginevyo, kisheria Mwenyekiti wa Palore anapaswa kuwa jaji au alishawahi kuwa jaji,”alisema Lissu.

Aidha kuhusu kuwatetea watuhumiwa, Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema, alisema sheria ipo wazi kwamba                                                                                                                                                                                                                       wanachofanya mawakili kwa sasa ni kuwatetea watuhumiwa wote hata wanaotuhumiwa na dawa za kulevya, kwani sheria inamtaka wakili kutetea yeyote bila ubaguzi.

MAKANISA Yamekuwa Dili..Mrembo Irene Uwoya Atangaza Kuanzisha Kanisa lake

$
0
0

Msanii wa filamu Irene Uwoya amesema kuwa ana mpango wa kuwa Mchungaji pamoja na kumiliki kanisa lake yeye mwenyewe siku za usoni na kwamba anamuomba Mungu kila siku aweze kutimiza ndoto hizo.


Kauli hii imetoka kinywani mwa msanii huyo pindi alipokuwa akijibu maswali mubashara aliyokuwa anaulizwa na mashabiki zake kupitia katika ukurasa wa Facebook wa EATV katika kipindi cha Kikaangoni


"Nina ndoto ya kuwa mchungaji na kila siku huwa nina muomba Mungu anifanikishie suala hilo niweze kutimiza japokuwa sasa hivi bado nipo katika changamoto kubwa ila natumai ndoto zangu zitatimia. Natamani kuwa pastor ambaye ni mwalimu, niwafundishe watu Mungu anataka nini, lakini sitaki kuanzisha kanisa kama biashara, sitaki kucheza na Mungu, ndiyo maana najipanga kwanza sitaki kukurupuka, nataka niwafundishe watu Mungu anataka nini, na jinsi ya kumuomba Mungu". Alisema Uwoya


Uwoya pia amefunguka na kueleza kuwa kazi yake ya sanaa huwa inamtesa kiimani jambo ambalo linamfanya kila siku akiamka awe anatubu kwa ajili ya mambo anayoyafanya akiwa katika kazi zake za uigizaji .


Amesema katika tasnia ya uigizaji mara nyingi huwa wanaongea uongo na hata mambo mengi wanayoyafanya kufikisha ujumbe huwa ni vitu ambavyo havimpendezi Mungu.


"Mimi nina hofu ya Mungu sana pia napenda kusali linapokuja suala la kazi yangu ukweli naona kama inanisumbua imani yangu kwa sababu katika uigizaji mambo mengi tunayoyafanya siyo ya kumpndeza Mungu lakini ndiyo kazi sasa, kila siku asubuhi nikiamka huwa inabidi kumuomba msamaha mungu wangu ndiyo niendelee na kazi". Amesema Irene Uwoya.


Kwa waliotaka kujua kama Irene anatumia dawa za kulevya, amewajibu kuwa hatumii dawa za kulevya na hajawahi kutumia kwa kuwa ni mkristo na dini yake hairuhusu kutumia dawa za kulevya wala kushiriki katika ndoa za jinsia moja lakini pombe anakunywa


"Situmii dawa za kulevya lakini nakunywa bia, dini yangu haizuii kunywa, nina uwezo wa kumaliza hata kreti nzima, hata mapadre kwenye dini yetu wanakunywa, lakini hairuhusiwi kulewa"


Pia amefunguka kuhusu mapenzi yake ya kuvaa nguo fupi, ambapo amesema anapeda nguo fupi, kwa kuwa ana mzio 'allergy' na nguo ndefu, hivyo hawezi kuvaa nguo ndefu.

MREMBO Lulu Diva na Uhusika Wake Katika Madawa ya Kulevya..

$
0
0

Lulu Diva, mrembo anayefanya muziki wa Bongo Flava ambaye alitajwa kwenye orodha ya watu wanaodaiwa kuhusika na madawa ya kulevya amezungumzia alivyochukulia na jinsi wazazi wake walivyojisikia.

Akiongea na Bongo5, mrembo huyo amesema hakutarajia kutajwa kwenye orodha hiyo na ni kitu ambacho kiliwashtua mpaka ndugu zake kwa kuwa hajawahi kujihusisha na biashara hiyo haramu.

“Nilishtuka kwa sababu ni kitu ambacho sikuwahi kutarajia wala kutegemea kwa kuwa nilikuwa sifahamu chochote. Nilivyosikia vile nilikosa raha kabisa niliumia lakini namshukuru Mungu by the way,” amesema.

“Bado inaniaffect kwa kuwa ni itu ambacho hujawahi kutegemea, huhusiki wala hujawahi kufanya kwa hiyo kitu kama kile kinakuumiza pale unapokuwa unakutana na watu ambao hawafahamu halafu huwezi kusema unamkalisha mtu uanze kumpa somo umuelezee,” ameongeza.

Lulu amedai kuwa mpaka leo hii taarifa za tukio hilo hazijaweza kumfikia mama yeke kwa kuwa yupo mbali ambaye anaishi mkoani Tanga na kipindi alikuwa anajua mwanae kasafiri kwakuwa alishamuaga tangu muda mrefu.

“Mama yangu mpaka leo hakuwahi kufahamu kwa sababu the time niliyokuwa nimetajwa nilikuwa natarajia kusafiri kwahiyo akawa anajua mimi nimesafiri. Na vile kwa sababu yupo mbali hakuwahi kupata taarifa mapema lakini kwa ndugu zangu ndio iliniaffect sana kwa sababu wenyewe pia wanashangaa kwa sababu wapo na mimi muda mwingi na wanajua jinsi walivyonikuza na wananielewa vizuri mtoto wao. Kwa hiyo ilikuwa pia surprise na waliangalia vitu vingi kwa wao wenyewe kwa baadhi ya watu kuwalaumu.”

Kuhusu kulala rumande kwa siku tano, Lulu amesema, “Kipindi kile mule ndani sikuhitaji rafiki, yaani nilikuwa nasali nakesha nikiomba Mungu ili ukweli ujulikane ili nije kutoka mule ndani,” amesema.

KIMENUKA: Mwanafunzi akipata mimba mzazi jela miaka 30

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema serikali itatoa adhabu kali ya kifungo cha miaka 30 jela kwa wazazi wote wawili wa mtoto wa kike atakayekatishwa masomo na kulazimishwa kuolewa ama akipata ujauzito.


Aidha amesema Serikali itamfunga jela miaka 30 kijana anayetaka kumuoa msichana anayesoma pamoja na wazazi wake.


Amesema Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kumlinda mtoto wa kike katika kuhakikisha kuwa anapata haki yake ya msingi ya kusoma kufikia elimu ya chuo kikuu kwa kujenga mabweni na kuwachukulia hatua kali za kisheria watu watakaowapa mimba na kuwaozesha katika umri mdogo na kukatisha masomo yao.


Majaliwa aliyasema hayo jana wilayani Hanang, mkoani Manyara katika ziara yake ya kikazi ya siku sita kwa mkoa huo.


Alisisitiza kuwa kupitia sera ya kuboresha elimu nchini serikali imeondoa michango ya fedha za kulipia bili za maji, umeme, gharama za mlinzi na mitihani ili kumpunguzia gharama mzazi na mlezi na kuwaacha wazazi kushughulikia maeneo mengine muhimu kwa mtoto wao.


Alisema tayari kwa mwaka huu wa fedha, walimu 4,396 wa masomo ya sayansi wameajiriwa ambapo alisisitiza kuwa wazazi na walezi wanalo jukumu kubwa la kusimamia maendeleo ya shule ya watoto wao kwa lengo la kupandisha ufaulu wa elimu kwa wilaya,mkoa na taifa.


“Mtoto akiwa mtoro baba na mama wa mtoto huyo atashitakiwa,mtoto wa kike asiguswe,vijana waendesha bodaboda acheni kuwalaghai watoto hao kwa zawadi na usafiri, tutawasaka wote,” alisisitiza.


Akizungumza na watumishi wa umma katika halmashauri ya wilaya hiyo, aliwataka watumishi hao kujivunia serikali yao kwa kuienzi katika kufanya kazi kwa nidhamu katika kuwatumikia wananchi bila kujali uwezo wao, kabila wala rangi zao kwa kuwa wamepewa dhamana ya kusikiliza kero zao.


Majaliwa alifafanua kuwa wafanyakazi wana wajibu wa kuwatumikia watanzania kwa kuwa wao ni waajiriwa wa serikali hivyo ni muhimu wakatoka maofisini na kwenda vijijini kusikiliza kero na kuzitatua badala ya wananchi kungojea viongozi wa kitaifa kuja kusikiliza kero na malalamiko yao wakati wao ni watendaji wakuu katika maeneo yao.


“Utumishi wenu hauhitaji upendeleo ama ahadi za njoo kesho, utumishi wa awamu ya tano ni wa uwajibikaji zaidi na uwajibikaji ni pamoja na kuwa mwaminifu katika kulinda na kusimamia kikamilifu fedha za serikali zinazotengwa katika halmashauri husika kwa ajili ya maendeleo,” alisema.


Akizungumzia soko la kimataifa la Endagaw, aliwapongeza wananchi wa wilaya hiyo kwa kukubaliwa kujengewa soko kubwa la kimataifa ambako wakulima watapeleka mazao yao na kuyauza lakini pia wataweza kuingiza mapato kwa kukodisha makampuni makubwa yanayohitaji kukodi kuhifadhi mazao kama NRFA.


Aliwataka wakulima wa mazao mbalimbali wilayani Kateshi kulitumia soko la mazao la kimataifa la Endagaw lililojengwa na ofisi yake kuuza mazao yao kwa bei nzuri badala ya kuuza mazao majumbani ambako wamekuwa wakiuza kwa bei ya chini isiyowasaidia kukuza kipato chao.


Alieleza kuwa serikali itaendelea kjuimarisha miundombinu ya soko hilo kwa kujenga eneo la wazi la nje kudhibiti magari makubwa yanayoshusha na kupakia mizigo yasikwame kutokana na matope na kuwa na mizani ya kupimia mazao na magari.


Kuhusu kero ya maji katika mji wa Katesh, alisema marekebisho yanafanyika kurekebisha mashine ya kuvuta maji na kuhakikisha sera ya maji inatekelezwa kwa vitendo katika kumpatia maji kila mwananchi umbali usiozidi mita 400.


Awali katika taarifa yake Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Sara Msafiri alimweleza Waziri Mkuu kuwa changamoto kubwa inayoikabili wilaya hiyo ni migogoro ya ardhi, kuanzisha gereza la wilaya kupunguza usumbufu wa kuwapeleka wahalifu Babati, jambo ambalo alisema atalipeleka wizara ya mambo ya ndani lipate kushughulikiwa.


Msafiri aliomba pia kujengewa mahakama ya wilaya ambapo alisema ni mchakato uliopo wa mahakama kuu kujenga mahakama katika ngazi za wilaya hivyo jambo hilo nalo litashughulikiwa.


Mbunge wa Viti Maalum Mkoa, Ester Mahawe alibainisha tatizo la kuwa na shule ya kidato cha tano na sita moja kwa wilaya nzima ambapo alimwomba Waziri Mkuu kutoa kipaumbele katika bajeti zake za elimu ili shule zaidi zijengwe mkoani humo.


Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Manyara, Rose Kamili (Chadema) aliiomba serikali kufuatilia na kuyatolea maamuzi mashamba makubwa ambayo yamekuwa hayaendelezwi na wawekezaji kutoka Ngano Ltd wanayoyamiliki zaidi ya ekari elfu 45 ambapo wamekuwa wakilima ekari elfu 16 pekee na kuacha migogoro ya ardhi baina yao na wananchi na kukosesha mapato ya halmashauri.


Ziara hiyo ilipata baraka za mvua kubwa baada ya ukame wa muda mrefu ilishangiliwa na umati wa watu waliokuwa wakiimba kwa furaha kuashiria Waziri Mkuu kuja na baraka hiyo kuneemesha mazao yao.


Leo Waziri Mkuu anatarajiwa kuhitimisha ziara yake wilayani Babati ambapo pamoja na mambo mengine atafanya majumuisho ya ziara hiyo na kutoa maelekezo ya serikali kwa wananchi na viongozi ngazi ya mkoa.

POLISI aua mwenzake kwa Kumpiga Risasi na Kisha na Yeye Kujiua

$
0
0

Polisi  amemuua mwenzake kwa kumpiga risasi usiku wa kuamkia leo na yeye amejiua baada kutazama mechi ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya kati ya Manchester City na Monaco.


Kabla ya polisi huyo, Konstebo Constable Patrick Kihagi kujiua kwa kujipiga risasi kichwani, alimjeruhi polisi mwingine kwa kumpiga risasi begani.


Polisi aliyekufa ametajwa kwa jina la Konstebo James Makokha, na kabla ya kifo alikuwa akifanya kazi Jogoo House.


Inadaiwa kuwa Makokha alipigwa risasi wakati akitaka kumaliza ubishani kati ya Kihagi na Ng’etich.


Kabla ya tukio hilo saa saba na nusu usiku kwenye eneo la Tassia, Nairobi nchini Kenya, polisi hao watatu walikuwa baa wakitazama mpira na kisha wakaanza kubishana, wakatoka nje.


Mashuhuda wanadai kuwa, walipotoka nje walizidi kubishana, Kihagi akatoa bastola na kumjeruhi mwenzake, Konstebo Dominic Ng’etich kwa risasi.


Kihagi alikuwa akifanya kazi katika kituo cha Embakasi, Ng’etich anafanya kazi kwenye kituo cha polisi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta.

WEMA Sepetu Afanya Uamuzi Mgumu...Aamua Kuikimbia CCM na Kujiunga Chadema..

$
0
0

Mrembo Wema Sepetu Ameamua Kukikimbia Chama cha CCM baada ya Mh Paul Makonda Kumjumuisha katika watu wanaohusika na Madawa ya Kulevya na kufikishwa mahakani..

Picha kadhaa zimewekwa mtandaoni zikionyesha Wema Sepetu akiwa na Viongozi wa Chadema Akiwepo Muheshimiwa Mbowe....

Nini Maoni yako?

CCM Yaanguka kesi ya Ubunge Arusha

$
0
0


Mahakama ya Rufaa nchini imetupilia mbali rufaa ya kupinga hukumu ya kesi ya uchaguzi katika jimbo la Longido mkoani Arusha, yaliyompa ushindi Onesmo Ole Nangole (Chadema), iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa CCM, Dk. Stephen Kiruswa,


Uamuzi huo umesomwa leo (Alhamisi) na msajili wa Mahakama ya Rufaa nchini, Amir Msumi na kusema kwamba wakata rufaa waliwasilisha rufaa mpya badala ya kurekebisha baadhi ya vipengele kama walivyoagizwa na mahakama.


Msumi amesema badala ya kuwajumuisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali na  msimamizi wa uchaguzi kwenye rufaa hiyo, wakata rufaa walifanya kitu ambacho hawakuruhusiwa kukifanya na mahakama na hivyo rufaa hiyo imetupwa na wanapaswa kulipa gharama za uendeshaji wa kesi hiyo.

NAPE Atoa Mkwala Mkali Mechi ya Simba na Yanga...Adai Ukikasirika Nenda Kavunje TV Nyumbani

$
0
0

February 23 2017 wakati wa uzinduzi wa mfuko wa kuchangia Serengeti Boys Waziri wa habari, Sanaa, utamaduni na michezo Nape Moses Nnauye amezungumzia kuhusu mashabiki wataokwenda kutazama mechi ya Simba na Yanga Jumamosi hii February 25 2017 uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Waziri Nape amewashauri tu mashabiki ambao hawawezi kuwa na uvumilivu pale matokeo ya mechi yanapokuwa mabaya kwa upande wao “Jumamosi kuna mechi ya Simba na Yanga mtakumbuka mechi iliyopita kulikuwa na matatizo lakini nawaomba watanzania tuweke ustaarabu na uzalendo wetu mbele”

“Kama ukikasirika kunywa maji au nenda nyumbani, tunaomba tusiharibu miundombinu ya uwanja, Simba wanajua gharama waliyotumia kuukarabati uwanja ule, ukiona huna moyo wa kukaa uwanjani basi kaa nyumbani kwako angalia katika TV ukikasirika vunja TV yako” – Nape
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images