Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

Kwa Wanawake Tu..Fahamu Njia Sita za Kumongoza Mwanaume Anayekuvutia Hadi Akawa Wako..!!!

$
0
0

WANAWAKE wakiwapenda wanaume hubaki na mateso mioyoni mwao. Hii ni kwa sababu ni vigumu kumtokea mwanaume moja kwa moja kumwaga sera kuwa unataka ‘akung’oe’.

Ni kweli kwamba, hata kama mwanaume akimkubali mwanamke awe mpenzi wake baada ya kutokewa, imani yake huwa hafifu kuhusu penzi la kweli la mwanamke huyo. Anaweza kumtumia kwa siku kadhaa kisha akamwacha. Huo ndiyo ukweli.
Wanawake waliowahi kuwatokea wanaume wanaweza kuwa na ushahidi mzuri zaidi juu ya hilo. Pamoja na hayo yote, bado mwanamke anabaki kuwa binadamu, mwenye hisia za upendo na kutamani baadhi ya vitu.

Anaweza kumpenda mwanaume na ni haki yake ya msingi kabisa. Kuwa katika uhusiano na mtu unayempenda kwa dhati ni jambo zuri. Moyo huridhia na kuwa huru katika uhusiano huo.
Hapa katika Let’s Talk About Love tunakupa dondoo zitakazokusaidia kumsogeza mwanaume ambaye ameuteka moyo wako na hatimaye kuwa wako moja kwa moja. Katika vipengele vilivyotangulia nilieleza kuwa, kwanza mwanamke ni vyema ajitunze na aweke mwonekano wake wenye kuvutia muda wote halafu pia nikaeleza kuhusu kumvutia mwanaume kwa mambo mbalimbali hasa mavazi na mambo anayopendelea. Sasa tunaweza kuendelea.

ASIWE KWENYE UHUSIANO
Jambo lingine la kuzingatia kwa mwanaume huyo wakati wa harakati za kumweka mikononi mwako ni kuhakikisha hayupo kwenye uhusiano na mtu mwingine. Kuna baadhi ya wanawake wapo tayari kuwa na mwanaume hata kama yupo na mpenzi mwingine; hilo ni kosa na naweza kusema ni umasikini wa kufikiri.
Kama kweli umempenda, itakuwa na maana kama utaweka makazi ya moyo wako kwake milele na siyo kwa muda mfupi tu.

JISOGEZE ZAIDI
Tayari umeshakuwa na uhakika kuwa hana mtu, sasa unatakiwa kujisogeza karibu yake. Jizoeshe kumsalimia mara kwa mara na kumsifia kuwa amependeza.
Kamwe usioneshe dalili kwamba wewe ni ‘maharage ya Mbeya’, ishia kwenye kujisogeza karibu yake kwa kumsifia na kufanya mambo mengine yanayofanana na hayo na siyo zaidi ya hapo.

JENGA URAFIKI
Ukaribu wenu sasa unaweza kuwafanya marafiki wa karibu. Kama uko naye ofisi moja au mnaishi mtaa/nyumba moja ni rahisi zaidi. Kuwa rafiki yake wa kweli mwenye kujadiliana naye mambo ya msingi.
Katika urafiki wenu, kamwe usiwe mzungumzaji sana (hasa wa mambo yasiyofaa), aidha usipende kukaa naye katika mazingira yenye vificho ambayo yataweza kusababisha kuingia kwenye mtego mbaya.

ZUNGUMZIA ZAIDI MAISHA
Kuzungumzia zaidi maisha na kumshauri juu ya mambo muhimu ya maisha, kutamfanya akuone wewe ni mwanamke makini mwenye malengo mazuri katika maisha yako. Wanaume wanapenda sana wanawake ambao vichwa vyao vinafanya kazi sawasawa.
Hii inaweza kuwa sababu itakayomfanya atamani kuwa karibu yako zaidi, jambo ambalo ndiyo shabaha ya moyo wako.

HAKUNA YEYE BILA WEWE
Kwa sababu tayari ni marafiki na mnashirikiana baadhi ya mambo, tengeneza mazingira ya kuwa naye karibu zaidi. Mshirikishe kwenye mambo yako, mfanye ajione si mkamilifu bila kuwa na wewe karibu.
Hili litawezekana kwa kuishika siku yake, kumtakia siku njema na kumjulia hali yake kazini na maendeleo yake kwa ujumla. Kwa kuwa ni marafiki, kwa ndani lazima hisia za mapenzi zitaibuka juu yako na utamuweka kwenye nafasi ya kufikiri kuanzisha uhusiano na wewe.

NI WAKO TU!
Ukipitia hatua zote, bila shaka mwanaume huyo ni wako tu. Ikiwa pamoja na vyote hivyo bado haonyeshi dalili au hajafunguka kuwa unamhitaji, basi mwache, siyo riziki yako. Kwa nini ung’ang’anie usipopendwa?

Mke Wangu Ataniua Jamani,Anataka Tufanye Mapenzi Kila Siku..Naombeni Ushauri...!!!

$
0
0

Mke wangu siku hizi mapenzi sijui niseme yameongezeka au sijui niseme ana nikomoa nasema hivi kwa sababu ndani ya wiki kama 3 zilizopita amekuwa akinilazimisha nile mzigo kila siku hapa nilipo kichwa kinaniuma kutokana na mabao nitoayo kila siku na jana nimeona nivunje ukimya baada ya kuniamsha usiku wa ma8 nile mzigo nikamueleza mke wangu utaniua naomba tupumzike hata siku 3 mbele target yangu ni kuwa baada ya siku 3 anatarajia kuingia kwenye siku zake so ntapata mapumziko ya kutosha,cha ajabu mke wangu kaanza kulia na kulalamika kuwa haamini kauli yangu ya kukataa kula mzigo, ilinibidi nimmbeleze kisha nikampoza na kamoja hapa nilipo nipo njian natoka job ameshanitumia sms ananiambia eti niwahi Anahamu ya dudu langu nimekaa kimya sikumjibu kanipigia simu anasisitiza alichokiandika kwenye sms yake tena kwa sauti ya majonzi.Nampenda mke wangu ila ananichanganya kwa vile tabia hii hakuwa nayo mi ndio nilikuwa initiator wa mchezo wetu.

Hebu wadau naombeni mnisaidie itakuwa kapatwa na nini hadi amekuwa hivi? Tabia hii kaanza tangu niliporudi kutoka safarini ambapo nilikaa kule kwa miezi 3 bila kushiriki nae..

Hii Hapa Sababu ya Kwa Nini Wanamitindo na Wabunifu Wengi wa Mavazi ni Mashoga..!!!

$
0
0

Bila shaka umeshajiuliza sana kwanini wabunifu wengi wa nguo wa kiume duniani ni mashoga. Haya ndio majibu:
Kwanza, tasnia ya mitindo (fashion industry) kiutamaduni imekuwa ikiwakubali zaidi mashoga wanaojulikana wazi (openly gay men) tofauti na fani zingine. Hata leo, ni changamoto kubwa kwa shoga kufikia level ya kuwa CEO ama Mkurugenzi kuliko wanaume wa kawaida.

Tofauti ni kwamba shoga kwenye fashion anaweza kuheshimika na kuenziwa kwenye fani hiyo na kufanikiwa binafsi na kifedha bila kudhihakiwa kama ambavyo anaweza kujikuta akifanyiwa kwenye fani zingine kama upolisi, jeshi na kwenye michezo.

Mifano mizuri inaweza kuwa kwa manguli wa fashion duniani kama Valentino Garavani, Yves Saint Laurent, Perry Ellis, Karl Lagerfeld, Alexander McQueen, Gianni Versace, Alexander Wang, Giorgio Armani, Marc Jacobs (Louis Vuitton) Domenico Dolce na Stefano Gabbana, Tom Ford na wengine. Na hata kwa Tanzania wapo wengi wanaofahamika wazi.

Japokuwa mambo yanabadilika na hasa kwa nchi za wenzetu na kukubalika kwa watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, kumefanya mashoga nao wafanikiwe kwenye fani zinazotawaliwa na wanaume wa kawaida, lakini mifano ya dunia halisi inabaki michache na hasa tu kwenye majiji ama nchi ambazo mashoga na wasagaji wanapewa heshima sawa na wengine.

Pia kihistoria mashoga kwenye fashion walikuwa wakipewa kipaumbele zaidi kuliko wanawake. Ni Coco Chanel pekee ndio alikuwa miongoni mwa wanawake wachache waliofanikiwa kwenye kiwanda hicho kilichokuwa kikitawaliwa zaidi na mashoga Christian Dior na Cristobal Balenciaga. 

Pili, inasemekana kuwa utamaduni wa ushoga huwapa nafasi watu hao uwezo wa ubunifu. Mashujaa kwenye jumuiya ya mashoga sio wachezaji wa soka ama wanajeshi- japo wapo. Lakini zaidi wapo kwenye muziki, uigizaji, utengezaji wa filamu, uandishi na sanaa zingine.

Hii ni kwasababu ya ukweli kwamba hizi ndio zilikuwa kazi ambazo mashoga waliweza kufanikiwa na kuendelea kuwa walivyo na kujivunia wanachokifanya. Uwezo wao wa ubinifu huongezeka na ile sense ya upekee ambayo mashoga huikuza ndani ya ulimwengu wa mapenzi ya jinsia mbili (heterosexual world).

Hatarii..Wasanii Waingia Vitani Kupambana na Rais Magufuli..Vichwa vya Magazeti ya Leo 29/3/2017..!!!

Noma Sana..Serikali ya Magufuli Yataka Trilioni 31.6 za Matumizi Tu...!!!

$
0
0

Serikali imewasilisha bungeni mapendekezo yake ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na ya kiwango na ukomo wa bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha 2017/18 na inatarajiwa kukusanya na kutumia kiasi cha Sh 31.6 trilioni.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango ameyasema hayo jana wakati akiwasilishwa mapendekezo hayo bungeni mjini hapa.

Pia, fedha za maendeleo zimeongezeka kutoka Sh11.8 trilioni mwaka 2016/17 hadi Sh11.9 trilioni mwaka 2017/18 sawa na asilimia 38 ya bajeti yote.

Duh..Spika Ndugai Atoa ya Moyoni Kuhusu Bajeti Mpya ya Serikali..!!!!

$
0
0

Spika wa Bunge, Job Ndugai ameionya Serikali juu ya ucheleweshaji wa uwasilishaji wa mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo waTaifa, kiwango na ukomo wa bajeti.

Akizungumza bungeni jana muda mfupi kabla ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango kuwasilisha mpango huo, Ndugai alisema kuwa kikanuni mpango huo unatakiwa kuwasilishwa Machi 11 ya kila mwaka.

“Kama ikiwa siku hiyo imeangukia siku isiyo ya kazi basi uwasilishaji huu hufanyika siku inayofuata. Mkija mwakani namna hii haitawezekana, hatutakuwa na mjadala,” alisema Ndugai.

Amewataka mawaziri, makatibu wakuu, maofisa wa Serikali na wabunge

kuhakikisha wanakuwapo mjini hapa kwa ajili ya kufanya uchambuzi wa mpango huo kisekta na kuhakikisha kuwa kazi hiyo inakamilika kabla ya kuanza kwa mkutano wa Bunge Aprili 4 mwaka huu.

Noma Sana ..Watuhumiwa wa Ugaidi Waitisha Mahakama,Watoa Masharti Haya Makubwa..!!!

$
0
0

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha jana imesikiliza malalamiko ya watuhumiwa 61 wanao kabiliwa na kosa la ugaidi, ambapo ni shauri lililofunguliwa mwaka 2014.

Wakizungumza  mahakamani hapo watuhumiwa hao wamesema kuwa jana ndiyo itakuwa mwisho wao kufika kwenye viwanja vya mahakama hiyo mpaka upande wa jamuhuri utakapo kamilisha upelelezi wao.

Wamesema wamekuwa wakifika mahakamani kwa muda ambapo wengi wao familia zinateseka na kusambaratika sababu ya kukaa mahabusu kwa miaka minne kwa makosa ya kusingiziwa.

Aidha wamesema wamekuwa wakipewa ahadi  hewa na mkuu wa upelelezi  kuwa angeshughulikia shauri hilo ndani ya miezi mitatu na kwamba suala la mahakama kushindwa kutekeleza wajibu wake  wa kikatiba linaleta ukakasi kwa wananchi.

Hakimu Mfawidhi Nestory Baro wa mahakama hiyo amewataka watuhumiwa kuwa na subira wakati wakishughulikia shauri lao ambapo kesi itatajwa April 11 mwaka huu na amewataka kufika mahakamani siku hiyo bila kukosa wakati akifanya utaratibu wa kumtafuta mkuu wa upelelezi na kuzungumza naye

Kashfa Faru John Kuwasomba Vigogo Wawili..!!!

$
0
0

KAMATI iliyoundwa kuchunguza utaratibu uliotumika kumhamisha Faru John kutoka Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Sasakwa Black Rhino Sanctuary iliyoko kwenye Hifadhi ya Grumeti Serengeti, imependekeza hatua za kinidhamu dhidi ya maofisa wawili wa serikali.

Kamati haikufafanua aina ya hatua ambazo zinapaswa kuchukuliwa kwa maofisa hao, lakini umakini uliopo katika serikali ya awamu ya tano unaashiria upo uwezekano mkubwa kwa maofisa hao kutumbuliwa.

Ingawa kamati hiyo iligundua kuwa Faru John alikufa kifo cha asili, imependekeza hatua za kinidhamu kwa sababu hakukuwa na kibali rasmi cha kumhamisha kwenda mazingira ambayo yalisababisha kifo chake.

Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyelle alitoa pendekezo hilo jana wakati akikabidhi ripoti hiyo kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa juu ya uchunguzi walioufanya kuhusu uhamishwaji na kifo cha mnyama Faru John.

Kamati hiyo imependekeza hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi ya Mkurugenzi wa Wanyamapori wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Profesa Alexander Songorwa na Daktari wa Shirika la Hifadhi la Taifa (Tanapa), Dk. Moris Kileo.

Imefichuka..Kutumbuliwa kwa Nape Nnauye Uwaziri Kumbe Bernad Membe Anahusika...!!!!

$
0
0

Duru za siasa kutoka maeneo mbalimbali ya nchi, zimeanza kutaja chanzo cha aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, kupoteza wadhifa huo.

Vyanzo mbalimbali vinaonesha kuwa vumbi la Uchaguzi Mkuu la Mwaka 2015 bado linaendelea kutimka ndani ya CCM. Baada ya chama hicho kumfukuza uanachama Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM, Sofia Simba, na wenyeviti watano wa CCM wa Mkoa katika Mkutano Mkuu wa Dharura mwezi uliopita mjini Dodoma, huku wengine wakipewa onyo, duru zinaonesha kuwa Nape Nnauye naye kawa mhanga.

Wakati wa mchakato wa kumpata mgombea wa CCM, Mbunge wa sasa wa Nzega (CCM), Hussein Bashe, alipata kumtuhumu Nape hadharani kuwa alikuwa akishirikiana na Mwenyekiti wa CCM (wakati huo), Jakaya Kikwete, kumbeba Bernard Membe.

Bashe alimtuhumu Nape kuwa katika kulipwa fadhila, Membe aliahidi kumwachia Jimbo la Mtama agombee, suala ambalo lilitokea Nape akagombea na kushinda. 

“Pamoja na kazi kubwa aliyofanya Nape kumnadi bwana mkubwa, bado wapo watu wamepenyeza maneno yaliyodhoofisha uhusiano wao. Mara kadhaa wamekuwa wakimwambia bwana mkubwa kuwa Nape ni wakala wa Membe ndani ya Serikali yake. Hili hakulipenda Mhe. Rais Magufuli, hivyo wakawa na mgogoro wa kimyakimya,” anasema mtoa habari wetu.

Vyanzo vya habari vinasema ushauri alioutoa Membe mara tu baada ya Rais Magufuli kuingia madarakani na kupiga marufuku safari za nje, Rais Magufuli hakuupenda. “Tanzania si kisiwa,” alisema Membe wakati huo na kushauri Serikali isijitenge na jamii ya kimataifa kwa Rais na maafisa wa Serikali kutosafiri nje ya nchi.

Kinachodaiwa kuwa ni uhusiano wa Nape na Membe kiliongeza msukosuko baada ya Nape kupingana na kiongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam alipoamua kutangaza hadharani majina ya watu wanaotuhumiwa kufanya biashara ya dawa za kulevya pale Nape aliposema, “Kutangaza majina ya watu bila ushahidi kunaweza kuharibu heshima na ‘brands’ za wasanii walizotumia nguvu na muda kuzijenga.”

Nape alitaka watuhumiwa wafikishwe mbele ya vyombo vya dola na wachunguzwe kisha watakaoonekana wana hatia wafikishwe mbele ya Mahakama kujibu mashitaka, ila si kutangazwa bila ushahidi kwani mbele ya safari inaweza kuthibitika hawauzi dawa za kulevya ikawa wameharibiwa heshima.

‘Kutia mafuta kwenye moto unaowaka’, Nape akaunda Kamati kumchunguza kiongozi kipenzi cha Mhe. Rais, pale kiongozi huyo alipovamia Kituo cha Radio na TV cha Clouds (CMG). Mkuu wa nchi alikwishasema ‘… chapa kazi. Usikwazwe na maneno ya mitandaoni.’ Kamati aliyoiteua Nape ikathibitisha kuwa hayakuwa maneno ya mitandaoni ni kweli kiongozi huyo alivamia Clouds, hili lilimkera mno Mhe. Rais akaona amtumbue,” kimesema chanzo chetu.

Gubu la kutoungwa mkono katika mchakato wa kisiasa linaonekana kuisumbua CCM kitambo sasa. Januari 30, 1984 aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Zanzibar, Aboud Jumbe Mwinyi, alivuliwa madaraka mjini Dodoma, alipobainika kuwa alitaka katika uchaguzi wa mwaka 1985 aipe madaraka zaidi Zanzibar. Hii ya mwaka 1984 ilipewa jina maarufu kama ‘Kuchafuka kwa Hali ya Hewa Ndani ya CCM’.

Mwaka 1985, Maalim Seif Shariff Hamad alituhumiwa kumhujumu  Idris Abdul Wakil asipate ushindi wa kishindo Zanzibar, na pamoja na kumteua aendelee na Uwaziri Kiongozi wa Zanzibar, wawili hao waliendelea kuishi kwa kutoaminiana hadi Januari 26, 1988 wakati Abdul Wakil alipotengua uteuzi wa Maalim Seif na kumteua Dk. Omar Ali Juma.

Mgogoro uliendelea na ilipofika Mei 1988, Maalim Seif alijiondoa CCM. Seif aliondoka na akina Shaaban Mloo, Maulid Makame, Ali Haji Pandu na Hamad Rashid Mohamed. Baadaye kundi hili lilifungwa jela miezi 30 na liliachiwa baada ya kuanza kwa mfumo wa vyama vingi ambapo wote hawa walikwenda kuwa waanzilishi wa Chama cha Wananchi (CUF). 

Mwaka 1995, Augustino Mrema alijiondoa CCM baada ya kutofautiana na Serikali ya Alhaj Ali Hassan Mwinyi kuhusiana na kashfa ya mashamba ya mkonge Tanga, ambapo mfanyabiashara P. V. Chavda alipokuwa amepewa mashamba kinyume cha utaratibu. Mrema alijiunga na Chama cha NCCR-Mageuzi ambapo alileta hamasa kubwa katika uchaguzi mkuu kwa kupata asilimia 27.7 ya kura zote.

Uchaguzi huo aliogombea na Benjamin Mkapa duru zinaonesha kuwa kama si nguvu ya Mwalimu Julius Nyerere, ilikuwa Mrema anaingia Ikulu. Ndani ya CCM yalibaki makovu na wengi walidhani CCM ingesambaratika baada ya wimbi hilo, ila baadaye ikajikusanya.

Februari 7, 2008, Edward Lowassa alijiuzulu uwaziri mkuu baada ya kuwapo taarifa za fitina kuwa alikuwa anajiandaa kugombea urais mwaka 2010. Ilielezwa kuwa Lowassa alikuwa na mkakati wa chini kwa chini kutenganisha kofia za Mwenyekiti wa CCM na urais, na kwamba Lowassa angetumia fursa hiyo kumwangusha Rais Kikwete.

Mgogoro huu wa chini kwa chini uliwagawa wafuasi wa viongozi hao ndani ya CCM, lakini ilipofika mwaka 2010 Lowassa hakujitokeza kugombea ubunge ikathibitika kuwa ulikuwa uvumi uliopenyezwa na wajanja waliokuwa wanajitafutia fedha.

Mwaka 2015, Rais Kikwete alipotangaza bayana kuwa Lowassa hawezi kuteuliwa kuwa mgombea ndani ya CCM na Chama kikampitisha Rais John Magufuli, Julai 30, mwaka huo Lowassa aliamua kujiondoa CCM na kujiunga na Chadema. Uamuzi wa Lowassa ulileta changamoto kubwa, hali iliyopunguza kura za CCM na kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii upinzani ukapata kura takribani asilimia 40.

Kutokana na hofu ya mgawanyiko uliotokea mwaka 2005, mwaka huu CCM imebadili kanuni yake baada ya kuwapo taarifa za chini kwa chini kuwa walikuwapo wana-CCM waliokuwa wanajipanga kugombea urais mwaka 2020, ambapo kwa sasa Rais aliyeko madarakani kwa CCM imepitishwa rasmi mwaka 2020 ndiye atakayekuwa mgombea wao.

“Mazingira haya unayoona hadi Rais anajiwekea kinga ya mwaka 2020 ndiyo yaliyomponza Nape. Wengi wanaamini Membe aliko huko nje ya ulingo wa siasa anafanya mazoezi ya kugombea urais. Kama vile hiyo haitoshi, wakubwa wameona wamwondoe hata Nape waliyedhani anawafikishia kila taarifa. Kwa hiyo, hata kama Nape asingekwaruzana na … bado wakati ungefika akaondolewa tu kwa nia ya kulinda siri za Serikali,” kimesema chanzo chetu.

Juhudi za JAMHURI kuthibitisha taarifa hizi kutoka kwa wasaidizi wa karibu wa Rais hazikuzaa matunda. Hata hivyo, Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM, Humphrey Polepole, ameliambia JAMHURI: “Si kweli kabisa. Wanaosema hivyo, wapuuzwe. Kwanza Nape hakufukuzwa uwaziri, uwaziri wake haujatenguliwa, bali Rais amefanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri.”

Polepole amesema si dhambi wakati wa mchakato ndani ya chama kila mtu kuwa na mgombea anayempenda, ila baada ya mchakato kukamilika anayeteuliwa anakuwa mgombea wa wanachama wote. “Huo ndiyo utaratibu wa CCM. Baada ya mchakato tunavunja makundi. Hivyo aliyesema hivyo si mkweli. Apuuzwe.”

JAMHURI limemtafuta Nape kuzungumzia sakata la kufukuzwa kwake, akasema: “Kaka naomba mniache nipumzike kwa sasa. Maneno niliyokuwa nayo niliyasema siku hiyo mbele ya wanahabari. Nimesema bayana kuwa naunga mkono juhudi za Rais wangu kujenga nchi yetu. Sina kinyongo na Rais wangu. Nampongeza kwa uteuzi alioufanya na nitaendelea kuwa mwanachama mtiifu kwa nchi yangu na CCM.

“Nimesema mimi ni mbunge na namshukuru Mhe. Rais kwa kunipa nafasi ya kutumikia uwaziri. Wapo wabunge wengi, hawakuteuliwa kushika wadhifa huo, na hawakuhoji nilipoteuliwa mimi. Vivyo hivyo, umefika wakati wa Mtanzania mwingine kushika wadhifa huo, mimi sina kinyongo kabisa. Naunga mkono hatua hii. Niache nipumzike kidogo nitumikie wananchi wa jimbo langu la Mtama. Nawashukuru wanahabari na Watanzania kwa kuendelea kunipa moyo.”

Nape amekuwa ni miongoni mwa vijana wachache wa CCM ambao waliaminiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete, baada ya kutumikia nafasi ya ukuu wa Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara, wilaya ambayo ni nyumbani kwa Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, alipata nafasi kubwa.

Nafasi ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM aliipata baada ya kupitia katika tanuri kipindi hicho akiwa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), baada ya kuwashambulia baadhi ya makada aliowatuhumu kuingia mkataba wa ujenzi wa jengo katika kiwanja cha Umoja huo kilichopo makutano ya barabara za Lumumba na Morogoro.

Nape alichukua nafasi baada ya kuachwa wazi na Mkuu wa Mkoa wa Tabora wa sasa, Aggrey Mwanri, ambaye wakati huo alikuwa Mbunge wa Siha, mkoani Kilimanjaro. Ni kipindi ambacho Nape, pamoja na watumishi wengine wa Sekretarieti ya CCM, walikichukua chama kikiwa kimezongwa na tuhuma za ufisadi zilizokuwa zinawakabili wanachama wake.

Katika harakati za kukisafisha chama na kukirejesha kwenye mstari, alipata fursa ya kuzunguka sehemu kubwa ya nchi kukinadi CCM. Atakumbukwa kwa aina yake ya kuishambulia Serikali, hasa pale wananchi walipoonekana kutoa lawama kwa baadhi ya mawaziri.

Katika harakati hizo za kukijenga CCM, yaliibuka majina kama vile “mawaziri mizigo”, huku ujumbe huo ukiwa maarufu katika majukwaa ya siasa.

Ndani ya CCM, ambako leo Nape si miongoni mwa wajumbe wa Kamati Kuu wala Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa, nafasi ambazo alikuwa akiingia kwenye vikao kwa nafasi yake, leo hana nafasi hiyo tena.

Lakini mbali na kutokuwa kwenye nafasi hiyo tena, CCM kina jambo lolote la kujifunza kutoka kwa aliyekuwa Katibu wake wa Itikadi na Uenezi? Jibu ni rahisi sana, ndiyo. Hakuna anayeweza kubisha kwamba baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2010, CCM haikuwa inatamanika tena, wananchi wakapoteza matumaini.

Chama hicho kilipoteza mvuto zaidi baada ya kuingia mikononi mwa Wilson Mkama, msomi mzuri, ambaye alitarajiwa kuleta mageuzi makubwa ndani ya CCM, hasa kupitia mkakati wa kujivua gamba.

Chombo kilipoonekana kwenda mrama, Nape alichukua unahodha na kukiendesha kwa ustadi mkubwa. Mwenyekiti wa wakati huo na Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, aliamua kumkumbuka rafiki yake wa muda mrefu, tangu wakiwa jeshini Abdulrahman Kinana, huku nafasi ya Itikadi na Uenezi akikabidhiwa kwa kijana mdogo wakati huo Nape akiwa na miaka 34 tu.

Hapo ndipo inapokuja historia ya kulala porini kwa siku zaidi ya 850, akijaribu kukijengea taswira mpya chama chake kwa wanachama. Jambo hilo amelisema hata baada ya kutishiwa bastola, akisema “Wakati ninahangaika na chama hiki, ninyi mlikuwa mnakunywa bia tu… nimezunguka nchi hii miezi 28, nikijenga chama changu CCM.”

Tazama Katuni Tano Bora za Leo Kuhusu Siasa

Vita vya Madawa ya Kulevya Vyaamia kwa Mawakili wa Serikali ya Rais Magufuli,Huu Ndio Mchezo Wanaoufanya Kupiga Pesa Ndefu Kupitia Madawa ya Kulevya ..!!!

$
0
0

MAWAKILI wawili wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), wanashikiliwa na kuhojiwa na Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya yenye kifupisho cha lugha ya Kiingereza cha DCEA, kwa tuhuma za kuharibu kesi za 'unga' siku za nyuma.

Kukamatwa kwa Mawakili wa Serikali hao ni matokeo ya ahadi ya mapema mwezi uliopita ya Kamishana Mkuu wa DCEA, Rogers Sianga.

Akikabidhiwa majina ya watuhumiwa 97 wa biashara ya dawa za kulevya na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda Februari 13, Sianga alisema kuna majaji, mahakimu na Mawakili wa Serikali ambao walivuruga kesi zinazohusiana na dawa za kulevya kwa makusudi siku za nyuma.

Alisema kutokana na kuwapo kwa hali hiyo, DCEA ingepitia kesi zote za nyuma ambazo Serikali ilishindwa licha ya kuwa na vidhibiti, ili kuwabaini na kuwachukulia hatua, ikiwamo kwa kupeleka orodha kwa mamlaka husika.

Akizungumza na Nipashe jana iliyotaka kujua idadi ya watuhumiwa wanasheria hao na jinsi walivyohusika kupindisha kesi hizo, Sianga alisema:

“Hili jambo ni lazima ukae vizuri kwa kuweka ushahidi vizuri, (lakini) wanasheria wawili kutoka Ofisi ya Mwansheria Mkuu wa Serikali (tayari) tumeshawakamata.

"Hatua inayofuata ni kukamata mahakimu na majaji.

"Tunakwenda hatua kwa hatua kuhakikisha taratibu za kisheria zinafuatwa.

Kamishna Sianga ambaye aliiambia Nipashe kuwa alizungumza wakati akiwa safarini, aliahidi kutoa ufafanuzi zaidi wa hatua hiyo baadaye.

"Lakini kimsingi majina tunayo tayari na kuna mwanasheria atakayesimamia zoezi hilo anayejua namna ya kuchukua hatua kwenye suala hilo.”

Kamishna Sianga aliteuliwa Februari 12, na siku iliyofuata alikabidhiwa ripoti yeye majina ya watu 97 ambao ilidaiwa na Makonda kuwa wafanyabiashara, vigogo wa serikali ya awamu ya kwanza hadi ya tano, watoto vigogo na wananchi wengine.

Kamishna huyo alisema watapitia kesi zote za madawa ya kulevya zilizowahi kuamuliwa miaka ya nyuma, ili kuweka wazi zilizoharibiwa kwa makusudi.

Akitolea mfano wa kesi ambazo amedai zilivurugwa na mahakimu, alisema ni kesi iliyokuwa na ushahidi uliokuwa wazi kuwa mtuhumiwa amemeza dawa za kulevya, lakini hakimu akasema kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa na matatizo ya vidonda vya tumbo.

Aidha, Machi 6, wakati Sianga akikabidhiwa ripoti ya dawa za kulevya kidunia iliyoonyesha robo tatu ya waathirika ni wanawake na watoto, alisema DCEA inawahoji vigogo watano.

Tangu hapo, iligundulika, mtoto wa Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete, ambaye ni Mbunge wa Chalinze (CCM), Ridhiwani Kikwete, ni mmoja kati ya watu waliohojiwa na mamlaka hiyo.

MSUKUMO MPYA
Vita dhidi ya dawa za kulevya nchini imepata msukumo mpya tangu Makonda ataje orodha ya watu 65 ambao alitaka waisaidie polisi kuhusiana na biashara ya madawa ya kulevya Februari 8.

Kabla ya kutaja orodha hiyo iliyokuwa na viongozi wa dini, wafanyabiashara na wanasiasa, Makonda alikuwa ametoa orodha ya Polisi 12 na wasanii kadhaa ambao walitakiwa pia kufika Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa mahojiano.

Lakini harakati za kuwakamata watumiaji, wauzaji na watu wenye taarifa kuhusu biashara ya dawa za kulevya katika jiji la Dar es Salaam na nchini kwa ujumla zilipata msukumo mkubwa siku nne baadaye, baada ya Rais Magufuli kutaka zisiache mtu yeyote.

“Hakuna mtu maarufu, mwanasiasa, waziri au kiongozi yoyote au mtoto wa fulani, askari ambaye anajihusisha na dawa za kulenya aachwe, hata awe mke wangu Janeth... kamata wote weka ndani,” alisema Rais Magufuli.

Alisema biashara ya dawa za kulevya nchini imefikia katika hali mbaya na kwamba zinauzwa kama njugu nchini.

Alitaka vyombo vyote vya ulinzi vinavyoendelea kupambana na dawa za kulevya viendelee na mapambano.

Alisema biashara ya dawa za kulenya inapoteza nguvu kazi za Watanzania wengi haswa vijana, na kwamba vyombo vyote vya ulinzi vinapaswa kushirikiana ili kuwakamata hao.

Rais Magufuli aliwataka wahusika kuuwinda mtandao wote unaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

“Haiwezekani wauzaji wapo mtaani wanatanua tu, hawakamatwi," alisema Rais Magufuli.
"Kwa mfano kuna muuzaji mkubwa yupo mkoani Lindi, alishikwa na dawa za kulevya lakini sijasikia hata siku moja akitangulizwa Mahakamani.

"Ninajua kuna viongozi wanamtetea.”

Rais Magufuli alikuwa akimzungumzia mtu anayeaminika kuwa 'mzungu wa unga' aliyekuwa akitafutwa zaidi nchini na Marekani pia.

Ali Khatibu Haji (50), maarufu kwa jina la Shikuba, alikamtwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Machi, 2014 baada ya kuwindwa kwa miaka miwili kabla ya kuhamishiwa mkoani Lindi.

Anatuhumiwa kuwa kiongozi wa genge lenye makao yake Afrika Mashariki lakini likiwa na uhusiano wa kibiashara mpaka China, Brazil, Canada, Japan, Marekani na Uingereza.

Imefichuka... Hivi Hapa Vitu Vitano Vilivyokwamisha Bajeti ya Kwanza ya Serikali ya Rais Magufuli

$
0
0

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, amewasilisha kiwango na ukomo wa bajeti kuu ya serikali kwa mwaka 2017/18, akisema itakuwa Sh. trilion 31.6.


Aidha, waziri huyo amebainisha vikwazo vitano vilivyosababisha changamoto katika utekelezaji wa bajeti ya mwaka huu wa fedha ambayo ni ya kwanza kuidhinishwa chini ya uongozi wa Rais John Magufuli.

Akiwasilisha mapendekeza hayo ya serikali kuhusu mpango wa maendeleo ya taifa na kiwango cha ukomo wa bajeti kwa mwaka ujao wa fedha, Dk. Mpango alibainisha changamoto tano zinazowakabili katika utekelezaji wa bajeti ya mwaka huu wa fedha ambayo ilikuwa Sh. trilioni 29.539.

Alisema bajeti kwa ajili ya miradi ya maendeleo ambayo ni asilimia 40 ya bajeti yote ya serikali kwa mwaka huu wa fedha, ndiyo iliyoathirika zaidi kutokana na changamoto hizo.

Serikali ilipanga kutumia Sh. trilioni 11.82 kwa ajili ya bajeti ya maendeleo. Kati ya fedha hizo, Sh. trilioni 8.702 zilikuwa za ndani na Sh. trilioni 3.117 ni fedha za nje.

Dk. Mpango alisema hadi kufikia Februari mwaka huu, fedha zilizokuwa zimetolewa ni Sh. trilioni 3.975 ikijumuisha fedha zilizotolewa kwa Halmashauri, sawa na asilimia 34 ya bajeti yote ya maendeleo.
"Kati ya kiasi hicho, fedha za ndani zilikuwa Sh. trilioni 3.103 na fedha za nje Sh. bilioni 871.8," alisema.

VIGINGI VITANO
Akifafanua kuhusu vikwazo vya utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2016/2017, Waziri Mpango alisema mojawapo ya changamoto ni pamoja na sehemu ya fedha kuelekezwa katika kulipia madeni kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo.

Alitaja sababu nyingine kuwa ni kuchelewa kupatikana kwa misaada na mikopo kutokana na majadiliano na washirika wa maendeleo kuchukua muda mrefu.

Dk. Mpango alisema changamoto ya tatu ni kupanda kwa riba ya mikopo ya kibiashara katika soko la fedha kimataifa.

"Hata hivyo, ni vyema kutambua kuwa mwenendo huu wa kupungua kwa misaada na mikopo, haikuwa kwa Tanzania pekee. Nchi nyingine za Afrika zimekumbwa na hali hii hasa katika misaada ya maendeleo kama vile Zambia, Cote d’Ivoire, Bostwana na Algeria," alisema.

Mpango alitaja sababu nyingine ya kutotekelezwa kwa kiwango kikubwa kwa bajeti ya maendeleo na mpango wa maendeleo wa taifa wa mwaka huu wa fedha kuwa ni matayarisho hafifu ya miradi.

Dk. Mpango alitaja changamoto ya tano katika utekelezaji wa bajeti ya mwaka huu kuwa ni mwamko mdogo wa kulipa kodi kwa kuzingatia matumizi ya mashine za kielektroniki (EFD’s).

Aidha, alisema serikali imechukua hatua mbalimbali za kukabiliana na changamoto hizo, mojawapo ikiwa ni kuhakikisha fedha zinazopatikana zinaelekezwa kwenye miradi yenye tija na pia kuboresha mazingira ya uendeshaji biashara ili kuvutia uwekezaji nchini.

MAPATO, MATUMIZI KUFIKIA FEBRUARI
Akizungumzia mwenendo wa mapato na matumizi ya serikali hadi kufikia Februari mwaka huu, Dk. Mpango alisema mapato kutoka vyanzo vyote yalifikia Sh. trilioni 15.372, sawa na asilimia 79 ya lengo.

Alisema kati ya fedha hizo, mapato ya kodi yalifikia Sh. trilioni 9.306, sawa na asilimia 95 ya lengo la kukusanya Sh. trilioni 9.764, mapato yasiyo ya kodi yalifikia Sh. trilioni 1.305 sawa na asilimia 72.5 ya lengo la kukusanya Sh. trilioni 1.806.

Aliongeza kuwa mapato ya mamlaka za serikali za mitaa yalikuwa Sh. bilioni 310.6, sawa na asilimia 70 ya lengo la kukusanya Sh. bilioni 443.6; mikopo ya ndani ilifikia Sh. trilioni 3.506, sawa na asilimia 78 ya makadirio ya Sh. trilioni 4.479 na misaada na mikopo nafuu kutoka kwa washirika wa maendeleo ilikuwa Sh. trilioni 1.253, sawa na asilimia 40 ya lengo la Sh. trilioni 3.117.

MIKOPO KIBIASHARA YASHINDIKANA
Dk. Mpango alisema chanzo kingine ambacho kilitarajiwa kuipatia serikali fedha za utekelezaji wa bajeti ni mikopo ya nje yenye masharti ya kibiashara ambapo kwa mwaka huo ilipanga kukopa Sh.Trilioni 2.100 ili kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo.

Hata hivyo, mtaalamu huyo wa uchumi alisema hadi kiufikia Februari mwaka huu, seriklai haikuweza kukopa katika chanzo hicho kutokana na hali ya soko la fedha la kimataifa kutokuwa nzuri.

Katika kipindi hicho, alisema riba ilipanda kutoka wastani wa asilimia sita hadi wastani wa asilimia tisa, jambo lililoilazimu serikali kuahirisha mchakato wa kukopa kutoka kwenye masoko hayo.

Aliongeza kuwa gharama za ukopaji katika masoko ya Ulaya imeanza kuimarika na kwamba tayari serikali imesaini mikataba mbalimbali kwa ajili ya kupata fedha.

UPATIKANAJI WA FEDHA
Waziri Mapngo alibainisha kuwa kipindi cha Julai 2016 hadi Februari mwaka huu, jumla ya Sh. trilioni 16.152 zilitolewa kwa wizara, idara zinazojitegemea, sekretarieti za mikoa na mamlaka za serikali za mitaa.

Kati ya hizo, Dk. Mpango alisema Sh. trilioni 12.177 zilizotolewa kwa ajili ya matumizi ya kawaida, ikijumuisha makusanyo ya Halmashauri Sh. bilioni 126.3.

Aidha, waziri huyo alisema Sh. trilioni 3.975 zilitolewa kwa ajili ya matumizi ya maendeleo ikijumuisha makusanyo ya Halmashauri Sh. bilioni 177.6.

Kuhusu fedha za matumizi ya kawaida zilizotolewa, Dk. Mpango alisema zinajumuisha Sh. trilioni 4.266 kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa serikali, Sh. trilioni 6.135 kwa ajili ya mahitaji ya mfuko mkuu wa serikali na Sh. trilioni 1.775 za matumizi mengineyo.

VIPAUMBELE
Dk. Mpango alisema maeneo ya kipaumbele kwa mwaka ujao wa fedha ni miradi iliyobainishwa kuwa kielelezo na inatarajiwa kutoa matokeo makubwa kuendana na malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na mpango wenyewe.

Aliitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na ujenzi wa reli ya kati ambao mkandarasi wa kampuni ya Yapi Merkezi ya Uturuki kwa kushirikiana na Mota-Engil Afrika ya Ureno wamesaini mkataba kwa kusanifu na kujenga awamu ya kwanza na ujenzi unatarajiwa kuanza mwaka huu.

Mingine ni ukamilishaji malipo ya ununuaji ndege tatu za serikali, mradi wa chuma Liganga, makaa ya mawe Mchuchuma, uanzishwaji wa kanda maalumu za kiuchumi ambazo ni Tanga, Bagamoyo, Kigoma, Ruvuma na Mtwara.

Dk. Mpango alitja miradi mingine kuwa ni ya gesi asilia, shamba la kilimo na uzalishaji sukari Mkulazi.

Kadhalika, alisema serikali itaendelea kutekeleza miradi mingine ya kipaumbele ambayo ni ujenzi wa msingi wa uchumi wa viwanda ikiwa ni pamoja na uendelezaji wa eneo la viwanda Tamco, Kiwanda cha General Tyre mkoani Arusha, mradi wa magadi Soda, kuimarisha mfumo wa taifa wa maendeleo ya wajasiriamali, uendelezaji wa viwanda vidogo na ujenzi wa ofisi za Sido.

Waziri huyo pia alisema kipaumbele kingine ni kufungamanisha uchumi na maendeleo ya watu, mazingira wezeshi kwa uendeshaji biashara, kuimarisha mitaji na kutumia benki za ndani za maendeleo TIB na TADB, na kuhamishia shughuli za serikali kuu makao makuu Dodoma ambapo tayari wizara zimeelekezwa kutenga fedha.

VIHATARISHI VYA BAJETI
Waziri huyo alisema vipo viashiria mbalimbali ambavyo vinaweza kuathiri utekelezaji wa miradi ya maendeleo -- vya ndani na nje ambavyo ni mtikisiko wa kiuchumi kikanda na kimataifa, majanga ya asili, athari za mabadiliko ya tabia nchi, mabadiliko ya kiteknolojia na ufinyu wa rasilimali fedha na watu.

Kutokana na hali hiyo, aliseman serikali itachukua hatua kupunguza utegemezi kwa kuwianisha mapato na matumizi, kuongeza mapato ya ndani na kuboresha mazingira ya kibiashara.

SERA YA MAPATO 2017/18
Dk. Mpango alisema kuwa katika mwaka ujao wa fedha, mapato ya ndani ya serikali yanatarajiwa kuongezeka na hivyo kupunguza nakisi ya bajeti.

Alitaja malengo ya mwaka 2017/18 kuwa ni kuongeza mapato ya ndani hadi kufikia asilimia 15.9 ya Pato la Taifa, kuongeza mapato ya kodi kufikia asilimia 14.1 ya Pato la Taifa, kupunguza nakisi ya bajeti kutoka asilimia 4.5 ya Pato la Taifa mwaka 2016/17 hadi asilimia 3.8 mwaka 2017/18.

Alisema serikali imedhamiria kuimarisha ukusanyaji mapato ikiwa ni pamoja na kusimamia matumizi ya vifaa na mifumo ya kielektroniki, kupanua wigo wa walipakodi, kupunguza misamaha ya kodi isiyo na tija.

SURA YA BAJETI 2017/18
Dk. Mpango alisema katika bajeti ya 2017/18, serikali inatarajiwa kukusanya Sh. trilioni 31.6 ambazo zitatumika katika kipindi hicho, ambayo yatatokana na mapato ya halmashauri yanayotarajiwa kuwa Sh. trilioni 19.9 sawa na asilimia 63 ya bajeti yote.

Dk. Mpango alisema kati ya mapato hayo, mapato ya kodi ni Sh. trilioni 17.106, sawa asilimia 85.6 ya mapato ya ndani, huku mapato yasiyo ya kodi na mapato kutoka vyanzo vya Halmashauri yakiwa Sh. trilioni 2.1 na Sh. bilioni 687.3 kwa mtiririko huo.

"Ili kuhakikisha upatikanaji wa mapato hayo, serikali itaendelea kuimarisha usimamizi wa mapato na kuziba mianya ya uvujaji wa mapato," alisema.

Waziri Mpango alisema washirika wa maendeleo wanatarajiwa kuchangia Sh. trilioni 3.9 (sawa na asilimia 12.6 ya bajeti yote), ikiwa misaada na mikopo hiyo ikijumuisha fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo, mifuko ya pamoja ya kisekta na ya kibajeti (GBS).

Dk. Mpango alisema serikali inatarajiwa kukopa Sh. trilioni 6.1 kutoka masoko ya ndani, lakini kati ya kiasi hicho Sh. trilioni 4.9 zitatumika kulipia hati fungani na dhamana za serikali zinazoiva (rollover) na Sh. trilioni 1.208 ni mikopo mipya kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo.

“Ili kuongeza kasi katika ujenzi wa miundombinu, serikali iinatarajiwa kukopa Sh. trilioni 1.5 kutoka soko la nje kwa masharti ya kibiashara," alisema.

MATUMIZI
Dk. Mpango alisema katika mwaka 2017/18, serikali inapanga kutumia Sh. trilioni 31.6 kwa matumizi ya kawaida na maendeleo, kati ya fedha hizo, Sh. trilioni 19.7 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida ikuijumuisha Sh. trilioni 7.2 za mishahara ya watumishi wa serikiali na taasisi huku Sh. trilioni 9.4 za kulipia deni la taifa.

Alisema fedha zilizotengwa katika bajeti ya maendeleo zimeongezeka kutoka Sh. trilioni 11,820 mwaka huu hadi Sh. trilioni 11.999 kwa mwaka ujao wa fedha, sawa na asilimia 38 ya bajeti yote.

Mwaka 2015/16, Bunge liliidhinisha bajeti ya serikali ya Sh. trilioni 22.5, bajeti ya mwaka 2014/15 ilikuwa Sh. trilioni 19.85 na ya mwaka 2013/14 ilikuwa Sh. trilioni 18.2.

Credit - Nipashe

*Imeandikwa na Augusta Njoji na Daniel Mkate (DODOMA), Sanula Athanas (DAR).

Exclusive..Nay wa Mitego Afunguka Mazito kwa Saa 36 Alizokuwa Chini ya Ulinzi wa Polisi,Afunguka Mengi ya Kushangaza Aliyofanyiwa na Polisi..!!!

$
0
0

Siku moja baada ya Rais John Magufuli kuamuru msanii wa muziki wa kizazi kipya, Emmanuel Elibariki maarufu ‘Ney wa Mitego’ kuachiwa huru na baadaye kusema ameitwa Ikulu, rapa huyo amefunguka na kueleza kilichojiri katika saa 36 alizokuwa chini ya ulinzi wa polisi.

Ney wa Mitego alikamatwa Machi 26 alfajiri huko Turiani mkoani Morogoro, akikabiliwa na tuhuma za kusambaza wimbo wenye maudhui ya kuitukana Serikali. Hata hivyo, aliachiwa huru juzi alasiri katika Kituo cha Kati jijini Dar es Salaam.

Saa chache baada ya kuachiwa huru juzi, taarifa za Ney kuitwa Ikulu zilienea na kuthibitishwa na msanii huyo jana.

Pia, alihojiwa na kituo cha Televisheni cha Azam ambako alikiri kupata mwaliko wa kwenda Ikulu kesho kutwa kwa ajili ya mazungumzo na Rais Magufuli.

“Ni kweli kuna taarifa kama hizo, ila siwezi kuzungumza sana kwa sasa kwa kuwa masuala haya yapo chini ya sheria,”alisema.

Afunguka saa 35 alizoshikiliwa

Akisimulia tangu alivyokamatwa saa 10 alfajiri ya Jumapili hadi alipoachiwa Jumatatu ya Machi 27, Ney alisema alifuatwa na polisi katika hoteli ya Premier Lodge mara baada ya kumaliza shoo aliyokuwa akiifanya huko Turiani.

“Asubuhi nikapelekwa Kituo cha Dakawa, Mvomero huko nilikaa kwa saa chache kisha wakanipeleka kituo kikuu cha Morogoro mjini. Nilichoambiwa huko ni kwamba ninatakiwa kujibu tuhuma za kesi ya matusi kuhusu wimbo wangu mpya ‘Wapo’,” Alisema.

Alisema baada ya kukaa mahabusu kwa saa kadhaa walifika askari kutoka Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam na kumchukua akiongozana na polisi kutoka Morogoro saa nane mchana, tayari kwa safari ya Dar es Salaam.

“Jioni tulifika na hapa nilipokelewa na kuingizwa tena mahabusu, huko nilikaa na nikalala bila kuambiwa chochote,” alisema.

Hata hivyo, alisema alishangazwa na namna askari walivyokuwa wakiendesha shtaka lake, kwani hawakutaka kumuuliza chochote hata siku ya pili ndugu zake walipofika kumuulizia waliambiwa hayupo.

‘Mpaka sasa sijui ni kwanini ndugu, watu wa karibu na jamaa walipokuwa wakija kuniulizia waliambiwa sijafikishwa kituoni hapo, wakati huo wote mimi nipo mahabusu hapa Dar” alisema.

Alisema hata polisi walipoanza kumuhoji, walimuhoji kwa makosa ya mtandaoni huku wakidai kosa kubwa ni wimbo ulioikashfu Serikali.

Hata hivyo, alisema muda huo wote hakukuwa na Ofisa yeyote wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

“Nilihojiwa kwa takribani saa mbili na nusu hivi, wakati huo wote nilikuwa na maofisa upelelezi wawili pekee na baadaye nilirudishwa mahabusu,” alisema.

Licha ya mikiki hiyo yote, Ney alisema mpaka anaondoka Kituo cha Kati hakuambiwa kwa nini aliruhusiwa:

“Haya ni masuala ya kisheria zaidi hivyo siwezi kuhoji sana niliondoka baada ya wao kunishikilia kwa saa 30 na zaidi” alisema

Kuhusu kuboresha ‘Wapo’

Kuhusu kuboresha wimbo wake kama alivyoambiwa na Rais, Ney wa Mitego alisema amepokea maoni hayo na kwamba yupo katika mchakato wa kuuboresha na kuahidi hatavuka mipaka.

“Ninalifanyia kazi mheshimiwa amesema anaupenda wimbo wangu na anausikiliza, yeye mwenyewe amewekwa kwenye huu wimbo ni jambo ambalo hawezi kupuuzia na hiki kinachoendelea labda amefurahishwa, hivyo nitaifanyia kazi kwa kuongeza mengi makubwa na kwa mapana zaidi bila kuvuka mipaka,” alisema.

Alisisitiza kuwa yeye ni mwanamuziki na si mwanasiasa, hivyo kwa yeyote akitaka kumhukumu anatakiwa amhukumu kama mwanamuziki.

“Naona Rais ni mwelewa, tukimwambia tunahitaji nini atatuelewa ingawa inatakiwa tusivuke mipaka na wananchi pia wanatakiwa kuzungumza vikiwemo vyombo vya habari,” alisema.

Aliyeunguzwa na Mumewe Amshukuru Rais Magufuli..!!!

$
0
0

RAIS Dk. John Magufuli, amepongezwa kwa moyo wake wa kujitoa na kuwajali wanyonge hasa wagonjwa wasiojiweza na wenye mahitaji ya gharama za matibabu.

Neema Wambura, maarufu kama ‘Mgonjwa wa Magufuli’ alisema hayo jana alipotembelewa na waandishi wa habari katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alilazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu baada ya kupata majeraha ya moto.

“Ninamshukuru sana Rais Magufuli kwa msaada wake katika matibabu yangu. Hivi sasa nina maendeleo makubwa, naweza kuzungumza, kula na hata kugeuza shingo yangu.

Nitamwombea Rais Magufuli mpaka siku naingia kaburini, Mungu ambariki,” alisema.

Akisimulia mkasa uliompata, Neema alisema alimwagiwa maji ya moto na mumewe baada ya kuchuma mahindi mawili shambani bila ya ruhusa yake.

Mumewe huyo alitoweka na ndugu zake walihofia kumchukua kwa kuogopa kudaiwa mahali iliyolipwa na mumewe kama taratibu za kumuoa.

“Hakuna ndugu yangu hata mmoja aliyejitokeza kunisaidia kipindi chote cha matibabu.

Walihofia kama ningefariki dunia ingempasa huyo ndugu kurudisha mahali ambayo mume wangu alitoa. Nilikuwa nasaidiwa na majirani tu, nilikata tamaa ya kuishi na nilikuwa nasubiri siku yangu ya kufa ifike,” alisema.

Neema pia aliwashukuru watumishi wa Muhimbili wodi ya Mwaisela wakiwamo wauguzi na madaktari kwa upendo na msaada mkubwa waliompatia tangu siku walimpokea mpaka sasa wakati anatarajia kurudi nyumbani.

Akielezea maendeleo ya afya ya Neema, Mkurugenzi wa Upasuaji wa MNH ambaye pia ni Daktari bingwa wa upasuaji, Dk. Ibrahimu Mkoma, alisema mgonjwa huyo alipokewa hospitalini hapo Julai 6, 2015 akitokea Musoma mkoa wa mara huku akiwa na majeraha ya mwaka mmoja toka aunguzwe.

Alisema mpaka sasa ameshafanyiwa oparesheni tatu kwa nyakati tofauti, zilizohusisha kutenganisha baadhi ya viungo kwa kuwa shingo, kifua na mkono wa kushoto vilishikana.

Pia alisema ilibidi kutoa ngozi ya sehemu ya mwili ili kufunika sehemu zile zilizoathirika zaidi.

“Ni katika kipindi hicho cha matibabu, Rais alimwona Neema na kuguswa na hali yake na kuamua kumsaidia mpaka hivi sasa mnavyomwona. Neema sasa amepona na ataweza kuihudumia familia yake vizuri,” aliongeza Dk. Mkoma.

Nape Atoa Neno Hili la Busara kwa Rais Magufuli na Serikali Yake..!!!!

$
0
0

Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amesema ataendelea kuwa mtiifu kwa Rais John Magufuli, Serikali na Chama cha Mapinduzi tofauti na maneno yanayosemwa mitandaoni.

Tangu alipoachwa kwenye mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri, Machi 23, kumekuwa na taarifa nyingi feki kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kuenguliwa kwake zikidaiwa kutolewa na mbunge huyo wa Mtama ambazo hata hivyo, amekuwa akizikanusha.

Akizungumza jana wakati akikabidhi ofisi kwa waziri mpya wa wizara hiyo, Dk Harrison Mwakyembe katika ofisi za wizara hiyo mjini hapa, bila kutaja maneno hayo ya mitandaoni, Nape alisema ataendelea kumuunga mkono Rais katika dhamira yake njema ya kuleta mageuzi nchini.

“Heshima aliyonipa Rais ni kubwa mno na nitaendelea kumuunga mkono katika dhamira yake njema ya kuleta mageuzi nchini” alisema.

Alimshukuru Rais kwa kumpa dhamana ya kusimamia wizara hiyo kwa miezi 15 baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge kwa mara ya kwanza. “Nitaendelea kutoa ushirikiano kwa wizara hii kwa sababu mimi ni mdau mkubwa wa sekta hiyo,” alisema.

Waziri Mwakyembe alisema ataendeleza mazuri yote yaliyofanywa na Nape katika kuimarisha wizara hiyo na atahakikisha wizara hiyo inakuwa ya mfano nchini.

Alimsifu Nape akisema katika kipindi kifupi alichokaa katika wizara hiyo amefanya mabadiliko na watu wameanza kuifahamu.

Nape aliondolewa katika nafasi hiyo siku moja baada ya kamati aliyounda kuchunguza tukio la kuvamiwa kwa ofisi za Clouds kumkabidhi ripoti.

Mara baada ya kupewa ripoti hiyo, Nape aliahidi kuikabidhi kwa mamlaka zake za juu akizitaja kuwa ni Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na Rais lakini asubuhi ya siku iliyofuata aliondolewa katika nafasi hiyo.

Makabidhiano hayo yalishuhudiwa na viongozi wengine wa wizara hiyo, naibu waziri, Anastazia Wambura, katibu mkuu, Profesa Elisante Ole Gabriel na naibu katibu mkuu, Nuru Millao.

Zitto: NECTA Limesema hawana rekodi ya Albert Bashite wala Paul Makonda

$
0
0

Tumejulishwa kwenye Kamati kuwa NECTA hawana rekodi ya Albert Bashite wala Paul Makonda.

Yani wote hawapo kwenye kanzidata ya Baraza la Mitihani. Kwamba Tanzania haijawahi kuwa na wanafunzi wenye majina hayo 

Mwakyembe Atangaza Kipaumbele cha Kuwapatanisha Diamond na Ally Kiba...!!!

$
0
0

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk Harisson Mwakyembe amepokelewa na wafanyakazi wa Wizara yake Mjini Dodoma huku akiahidi kuwaweka pamoja wasanii Diamond na Ally Kiba.

Pia amefurahishwa na matokeo ya Stars ndani ya wiki kutokana na kuzifunga Botswana na Burundi.

Pamoja na hayo, ameahidi kuliondoa neno kichwa cha mwendawazimu katika Soka.

Facebook Nayo Yaja na Mtindo wa Snapchat..!!!

$
0
0

Baada ya Instagram kuanzisha Insta Stories, mtindo ulioipandisha chat Snapchat, Facebook nayo imekuja na mtindo huo kwenye app yake.

Kupitia app ya Facebook, sasa unaweza kushare matukio/stories na kuona kile marafiki zako wamekifanya kwa saa 24. Juu ya Facebook app, utaona picha za duara zinazowakilisha story walizoziweka marafiki zako na ukibonyeza, utaona picha, video ama michoro waliyoweka.

Baada ya saa 24, post hizo zitapotea na hazitaonekana tena.

Kwa maana hiyo Facebook sasa imeanzisha stories kwenye app zake zote, Facebook, Messenger, Instagram na Whatsapp. Hadi sasa Instagram stories zimekuwa na mafanikio makubwa.

Julius Mtatiro: Sophia Simba Anaweza Kumfukuza Kinana?

$
0
0

Na. Mtatiro J

Sofia Simba na wale wenyeviti wa CCM waliofukuzwa na Halmashauri Kuu ya CCM hawawezi kuitisha kikao chochote ndani ya CCM ila wanaweza kuitisha Vyombo vya Habari na kuvieleza kuwa kikao chao kimemfukuza Kinana. Kama ingehusu CCM, tamko hilo moja feki la Sofia Simba na wenzake lingelitosha kuwapa kesi ya jinai hata isiyo na dhamana. 

Lakini kwa CUF jambo hilo hilo linaleta maswali na hofu. Kwa ufupi, Baraza Kuu rasmi la CUF lilichaguliwa na Mkutano Mkuu mwaka 2014 na litakuwa madarakani hadi mwaka 2019 na ndilo lilimfukuza Lipumba uanachama mwezi Septemba mwaka 2016, na Baraza Kuu hilo hilo ndilo limekutana Zanzibar wiki moja iliyopita kwa mahudhurio ya asilimia 81 ya wajumbe wote na likafanya maamuzi mbalimbali ya chama. 

Baadaye Lipumba (aliyekwishafukuzwa uanachama) naye akaita kundi la watu wanaomuunga mkono (wanachama wa kawaida) pamoja na Wajumbe wa Baraza halali wasiozidi watano eti akadai hicho ni kikao cha Baraza Kuu la CUF. Akaenda mbele zaidi akaita vyombo vya habari na kuvisomea taarifa anayoiita ya Baraza Kuu la CUF, na vyombo haraka vikapata habari ya kuandika "SOFIA SIMBA AMFUKUZA KINANA....SOFIA SIMBA AMKALIA KOONI KINANA."

Maajabu ya namna hiyo yanawezekana kwenye vyombo vya habari na kwenye matamanio ya kifikra, katika uhalisia wa ndani ya Uendeshaji wa vyama hilo halipo. Vyama vya siasa vina mamlaka ya ndani ya vyama hivyo. Vikao vyote vya kitaifa vya CUF na mamlaka zake; Kamati ya Utendaji ya Taifa, Bodi ya Wadhamini, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa na Mkutano Mkuu wa Taifa - vilishamalizana na Lipumba tangu mwaka jana.

Vituko na matamko ya Lipumba ya sasa yataendelea kwelikweli, lakini hayawezi kubadilisha maamuzi ya vikao vya chama nilivyovitaja hapo juu. CUF imeingizwa kwenye mgogoro mkubwa wa makusudi lakini mifumo yake ya ndani haitatikiswa na Lipumba. Matamko yake hayawezi kubadilisha maamuzi halali ya vikao halali vya chama.

Tofauti ya CUF na CCM ni kuwa, Ofisi ya CCM ingelivamiwa na Sofia Simba na wenzake, Serikali ingelituma askari na silaha za kutosha wakawafurumushe kina Sofia Simba. Ila kwa CUF, serikali kwa saa 24 imempa Lipumba askari wa kutosha wamlinde ili aendelee kutoa matamko ya KIPUUZI kama hili la sasa.

CUF ina Baraza Kuu moja tu na lilipomsimamisha Lipumba na wenzake walikata RUFAA kwenda mkutano mkuu. Kwa hiyo Lipumba hawezi kuanzisha Baraza Kuu lake leo hii na likafanya maamuzi yoyote kuhusu CUF. 

Julius Mtatiro,
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi,
Safarini.
29 Machi 2017.

Breaking News..Makonda Atua Bungeni Kuhojiwa ...!!!

$
0
0

Napenda kuwajulisha kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo yuko mbele ya Kamati ya Maadili Haki na Madaraka ya Bunge.

Taarifa ya kamati itafikishwa kwenye Bunge zima na kusomwa.

Tuvute subira tujue mbivu na mbichi..
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live




Latest Images