Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104808 articles
Browse latest View live

Sugu: Mbunge Mlinga wa CCM Anatukana Mbona Naibu Spika Anamlinda Tukiomba Mwongozo..!!!?

$
0
0

Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi amehoji inakua vipi mbunge wa Goodluck Mlinga wa CCM amekuwa akitukana wapinzani mara kwa mara bungeni ila hachukuliwi hatua

Amesema walipoomba mwongozo wa matusi ya mbunge huyo naibu spika alisema tukio hilo lilitokea siku iliyopita hivyo halipaswi kuzungumziwa lakini Freeman Mbowe aliitwa kwenye kamati ya maadili kutokana na kauli iliyoombewa muongozo na Kangi Lugola ambayo Mbowe aliitamka na siku tatu zilipita

Ukweli Mchungu..Mbona Kama Diamond Anatuchezea Akili Zetu..!!!

$
0
0

Kwa siku nne zilizopita kumekuwa na taharuki baada ya ‘kutekwa’ kwa wasanii wa Bongo Fleva, Roma, Moni na wenzie lakini habari njema ni kuwa kwa sasa wamepatikana. Tukio hilo limezua mijadala mingi katika mitandao ya kijamii.

Wakati mijadala ikiwa inaendea na watu kuhoji wapi alipo Roma na wenzie, msanii anayesifika na kuheshimika nchini, Diamond Platnumz anatoa wimbo ‘Acha Nikae Kimya.’

Wimbo huo umekuja kukoleza mijadala iliyokuwa inaendelea, watu wanauhusisha tukio la kupotea wakina Roma. Binafsi nimesikiliza wimbo huo nikubaini kwa nini umezoa mjadala.

Mosi: Diamond ameshindwa kuficha hisia zake dhidi ya RC ambaye ni kipenzi chake, kuna mstari anasema ‘Napewa za chini ya kapeti kuna redio imevamiwa eti Ehh, napita kwenye magazeti nakuta lundo la watu wameketi Ehh, badala ya kutafuta senti wanabishana tu mambo ya vyeti’.

Kabla ya kuandika makala haya, kupitia account yangu ya twitter niliandika ‘Diamond asicheze na akili zetu….,’. Hata sasa naweza kurudia hivyo, Diamond asicheze na akili zetu.

Kwa tafsiri pana ya hiyo mistari hapo juu, ni kwamba yeye hajui kuhusu tuhuma za RC kuvamia kituo cha redio/TV pia ndani yake kuna kubeza tuhuma hizo, be intellectual.

Pia nimesikia amegusia kuhusu vyeti na kuwashangaa wanaohoji suala hilo badala yake watafute fedha, well in god. Nimpongeze kwa hilo maana hata mimi sipendi watu wanaokaa vijiweni/vibanda vya magazeti na kuongea udaku tu bila kufanya kazi.

Lakini tuhuma za kughushi vyeti tena kwa kiongozi ambaye anaongoza kundi kubwa la watu katika jamii ni wajibu wa wale anaowangoza kuhoji, wala hakuna ubaya, udaku au kupoteza muda wa kutafuta senti kama wewe unavyodai. Hapa mchezo ni simple tu kama kumsukuma mlevi, anayetuhimiwa ajitokeze akanushe na maisha yaendelee.

Jambo la pili linaloleta mjadala kuhusu wimbo huu ni suala la Roma, ‘ahh, ohh Tanzania Mara kimbembe Dodoma wabunge pinzani wamegoma juzi akapotea na Roma,’, ni moja lines. Nimejiuliza maswali mengi sana, kwanini huu wimbo utoke muda huu na si wiki iliyopita au mwezi ujao, Diamond asije akatudanganya alikuwa ameurekodi siku nyingi maana Roma na mwenzie ‘wametoweka’ wiki hii, ina maana wimbo umeandikwa na kurekodiwa wiki hii. Jaribu kuwaza kwa sauti, narudia tena, jaribu kuwaza kwa sauti.

Siukatai wimbo wake, kwani ameimba vizuri, melody nzuri, beat nzuri, ujumbe unahasisha uzalendo na kuwa na busara lakini kuna mambo ambayo yananipa ukakasi. Ila pongezi kwake

MAWAZO YANGU

Yeye kama msanii ambaye ni kioo cha jamii anatakiwa kusema shida za wengi, yaani kuwakilisha kundi kubwa la watu. Kujali maslahi binafsi ni kujiharibia.

Zitto Kabwe: Serikali Haijawasilisha Taarifa ya CAG Bungeni Leo, Imevunja Katiba..!!!

$
0
0

Amendika katika ukurasa wake wa facebook,kwamba serikali hutakiwa kuwasilisha taarifa ya CAG bungeni ndani ya siku saba tangu kuanzia kwa bunge la bajeti.

Anasema mpaka sasa taarifa hiyo haijawasilishwa hivyo kuvunja katiba ya jamhuri inayotaka iwasilishwe ndani ya Siku saba.

Yaani Hata CCM Wamshangaa Roma... Wahoji Anaficha Nini...!!!?

$
0
0

Na Thadei Ole Mushi.

Kutokana na Maelezo ya Roma na kutekwa kwake ni kwamba hajui waliomteka na wala hajui watekaji walikuwa wanahitaji nini.

Maswali ninayojiuliza....

#Roma anadai hajui kwa nini alitekwa ila anasema watekaji walipomchukua walienda kumhoji. Kama walimhoji moja kwa moja anawajua waliomteka. 

Aidha walimhoji kumuuliza labda kama anatembea na mke wa mtu, au walimhoji kuhusu kujihusisha na siasa, au walimhoji kuhusu nini??

Kutokana na mahojiano hayo moja kwa moja Roma anajua waliomteka ni kina nani kama hawajui atuambie walimuuliza maswali gani tutamsaidia kumwambia ni kina nani hao au na sisi tutaridhika kuwa kwa kweli maswali hayo yalikuwa hayaeleweki. 

Sitaki kuongea sana hili naweza kuvuka mipaka na kuzidi kuuweka ukweli upenuni.

#Raia wa Tanzania wana ulinzi kiasi Gani??? Kutokana na Issue hii??? Yaani mtu anatekwa na simu yake ipo hewani na sms anasoma ila bado polisi wetu hawajui alipo mtu huyo. Kama haya yanaweza kufanyika jeshi letu halioni linajiondolea weledi mbele ya raia? 

Mtu anatekwa Studio taarifa zinafikishwa polisi gari waliyoondoka nayo inajulikana ni Noah na hata number za Gari zitakuwa zinajulikana ila bado polisi wanashindwa kusema ni kina nani hao.... 

Ubaya mmoja haya mambo hayafuatiliwi na watanzania tu bali hata majirani zetu hamuoni mnawakaribisha wakidhani mu dhaifu kwenye maswala ya kiulinzi?

#TongweRecords hawana Mlinzi? Kama wanaye walimteka na yeye?? Maana kipengele hiki wamekisahau kwenye hili Tukio. Kama Mlinzi alikuwepo alikubalije watu kuingia ndani ya Studio na kuondoka na vitu? Je walipoingia Getini hawakujiandkisha?????

#Waliotekwa ni wanne kwa nn Roma aende peke yake kujieleza? Katika wote waliotekwa yeye ndiye aliyepigwa zaidi kwa maelezo yake kwa nn hao wengine hawakumsaidia kwenda kuongea na vyombo vya habari wakati yeye akiendelea kujiuguza?

Hawaoni kuwa kwa tafsiri ya kawaida kabisa watakayoipata wananchi ni kuwa kama wangeenda wote wangejichanganya kimaelezo? Tayari kina Roma wanajua kuwa mtaani kuna sintofahamu kuhusu wao hawaoni kuwa kwa kutokufika wote kutaruhusu wazo hili na kuongeza hii sintofahamu??

#Roma anadai kuwa walitupwa karibu na dimbwi wakajikokota wakapakia pikipiki wakaenda nyumbani kubadili nguo. Ila walipofika nyumbani hawakumkuta mtu hivyo walilazimika kuvunja mlango....

Ni boda boda gani iliwachukua toka hapo walipotupwa?? 

Roma bado alikuwa na simu yake kwa nini avunje mlango badala ya kumtafuta mkewe kwenye simu ili aje kumfungulia mlango?

Kama walimnyanganya simu ni kweli kuwa alikuwa hajui simu ya mkewe?? Si angelitafuta simu mahali ampigie?

Je majirani wa kina Roma ni nani walisikia vishindo vya kuvunja mlango?? 

Na kama walisikia walichukua hatua Gani?.........

#Hata eye contact ya Roma ina Mashaka asilimia 90 kashindwa kuamgalia waandishi anajishika usoni tena machoni. Wala hakuwa na hisia za mtu ambaye kweli alitekwa.

#Unatekwa unateswa unaumizwa halafu unaenda nyumbani kubadili nguo..... Si unapoteza ushahidi?? Kwa nn aende Polisi akiwa ameshabadili nguo? 

Sitaki uamini kama ninavyoamini tuendelee na story zetu za kawaida........nilishasema hutakiwi kufikiri sana ukiwa Tanzania.

Mwigulu Nchemba Ajibu Kuhusu Madai ya Bashe na Raia Kutekwa..!!!

$
0
0

Mwigulu anasema kuna vitu vingi, moja ni tofauti kati ya kukamatwa na kutekwa, kama serikali imekukamata itakuwa ni rasmi na njia za wazi itakupa sababu ya kukukamata
..Je Bashe alikamatwa au alitekwa?

Hizi Hapa Mbinu Chafu Watekaji Wanayotumia Kukunyamazisha..!!!

$
0
0

Hapa nazungumzia hawa watekaji wa Tanzania. Hii sio story za movie au kutunga.

Utekaji Tanzania haujaanza leo. Kuna awamu ya Rais Flani hapa Tanzania, wapinzani walitekwa sana. Sema sasa Mambo ya kidigitali yanasaidia kusambaza habari haraka sana. Kuna watu walikuwa madiwani/ wabunge ( siwataji) walifanyiwa mbinu hii na wapo kimya mpaka leo.

Hapa naongekea utekaji wenye malengo machafu ya kisiasa. 

Hawa watekaji wana mbinu chafu sana ya kumyamazisha mtekwaji kiasi kuwa hata wakimuachia huru, hawezi ongea yaliyomtokea na yote aliyofanyiwa.

Kwa kifupi ni kuwa, Hawa jamaa wanatabia za kuwaingilia kinyume cha maumbile watekwaji huku wanawapiga picha au wana warecord video. Pale wanapoamua kukuachia huru, wanakupa mashariti moja wapo ni la kukaa kimya. Endapo utakiuka mashariti, wanasambaza picha au video zinazoonyesha jinsi walivyokuwa wakikuingilia kunyume na maumbile.

Sasa wale mnao mtupia matusi Roma katika kipindi hiki kigumu anachopitia mjaribu kuangalia na upande wa pili. Hamjui kapewa mashariti gani mpaka anakuwa mgumu kueleza yote yaliyomkuta. Hawa jamaa wanamateso ni hatare. Usiombe yakukute siku moja. 

Wapo ambao waliharibiwa kisaikolojia kabisa kwa hii mbinu maana dah... hebu assume kesho mnakutana na kivideo clip mtandaoni Roma anafanyiwa vya sodoma. Yan hii ni mbaya sana. Hta mimi nakaa kumya milele.

Kwa mfano assume wewe ni msanii, umeandaa bonge ya li-single la kuichana serikal. Dena watekaji wanakudaka alafu wanakufanya yao. Na wanakuambia, ukijaribu kuichana tu serkal, wao wanareleaze your anal sex tape. Unadhani unaweza jarbu kwenda kinyume cha mashart yao?????

Mkuu wa Freemason Azikwa Kwa Kuchomwa Moto leo.

$
0
0

Dar es Salaam. Mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Freemason Afrika Mashariki, Sir Jayantilal Keshavji Chande maarufu kama Andy Chande, umeteketezwa leo Kijitonyama, jijini Dar es Salaam kupitia tukio lililodumu kwa takribani  saa moja.

Mwili huo umeteketezwa kwa moto kupitia ibaada iliyofanyika kwenye nyumba maalumu inayotumika kama sehemu ya maziko ya waumini wa dini ya Hindu.

Sir Chande alifariki dunia siku tano zilizopita wakati akipata matibabu katika hospitali ya Nairobi baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa ulitokana na matatizo ya utumbo mdogo kusambaza sumu mwilini.

Ukitaka Mafanikio Ya Kweli Acha Kulalamika Juu Ya Mambo Haya....!!!

$
0
0

"Hivyo ulivyo inatokana na mtazamo ulionao" usemi huu niliwahi kukutana nao siku moja katika pekuapekua zangu, usemi huu una ukweli ndani yake kwa asilimia zote uzijuazo wewe, kwa sababu maisha yako hivyo yalivyo yanataokana na mtazamo na imani ulizonazo.

Watu wengi ambao hawajafanikiwa wanaamini ya kwamba mafanikio yanapatina kwa baadhi ya watu fulani, lakini dhana hii si kweli kwa sababu kila mmoja mwenye pumzi na fikra ana wajibu wakuweza kufanikiwa kwa kiwango kikubwa.

Hivyo nikwambie ya kwamba mafanikio makubwa yatakuwa upande wako endapo utaacha mara moja kulalamka juu ya mambo yautayo;

1. Acha kulalamika juu ya elimu uliyonayo.

Mafanikio yatakuja kwako endapo utaacha kulalamika juu ya elimu uliyonayo. Watu wengi wanalalamika eti kwa sababu ya elimu walizonazo, wengi husema mimi sina mafanikio kwa sababu sina elimu ya kotosha, au nimesoma kidogo na sina elimu ya chuo kikuu.

Kiuhalisia, dhana hii haina mahusiano ya moja kwa moja na mafanikio yako, hii ni kwa sababu sio kila mwenye elimu amefanikiwa hivyo kwa elimu hiyohiyo ambayo unayo ni kigezo tosha juu ya mafanikio yako. Hebu tujiulize watu wengi ambao wamefanikiwa elimu zao ni kiwango gani?

2. Acha kulalamika eti hujafanikiwa kwa sababu huna bahati.

Kama nilivyoanza kueleza hapo awali ya kwamba mtazamo ndio kila kitu, imani hii ya kuendelea kuamini ya kwamba mafanikio ni bahati nakuomba uachane nayo mara moja, imani hiyo inaweza kukupoteza na ukashindwa kupata mafanikio kama utaishikilia sana.

Tambua imani kubwa juu ya mafanikio ni kwamba kila mmoja amezaliwa kwa ajili ya kufanikiwa na si vinginevyo jambo la msingi ni kwamba mara zote hakikisha unakuwa na mtazamo chanya, ubunifu, pamoja kufanya kazi kwa bidii haijalishi ni kazi ndogo au kubwa kiasi gani.

3. Acha kulalamika eti huna pesa za kutosha.

Hili ndilo kikwazo cha mafanikio ya wengi hii ni kwasababu watu wengi wamekuwa wanalalamika ya kwamba hawana pesa za kutosha ili wafanye jambo fulani, kuendelea na tabia hii ni kujiua mwenyewe kwani siku zote pesa huwa hazitoshi.

Jambo la msingi ni kuhakikisha kwa kiwango hicho cha pesa ulichonacho ni njia pekee ya kuanza kufanya jambo unalolitaka, kwani endapo utaendelea kusubiri ufikishe kiwango fulani cha pesa ndio uanze kufanya jambo fulani nakuhakikishia huwezi kufanya kamwe.

4. Acha kulalamika juu ya serikali kama kweli unataka kufanikiwa.

Maisha yako yapo mikononi mwako, hata hivyo kama kweli unaamini hili hakikisha unakuwa bora sana katika kutafuta kusudio lako katika dunia hii, nasema hivi kwa sababu watu wengi wanashindwa kufanikiwa kwa sababu wao kazi yao ni kuilaumu serikali tu.

Na watu hao wamekuwa wakifanya hivi huku siku sikizidi kwenda na wao maisha yao yamekuwa hayabadiliki,  jambo la msingi ambalo nataka kukuasa ni kwamba kila mmoja asimame kidete katika kuyapigania maisha yake ambayo yatamtengezea kesho yake bora.

Hivyo nikuache kwa kukuambia ya kwamba endapo utaendelea na tabia yako ya kulalamika ni kutengeneza maisha yako kuwa duni zaidi.

Nukuu ya siku inasema "kulalamika ni adui namba moja wa mafanikio yako"


Ongeza Uwezo Wako Wa Kupata Pesa Kwa Kufanya Mambo Haya...!!!

$
0
0

Upo uwezekano mkubwa wa wewe kuongeza uwezo wako wa kupata pesa zaidi ya hapo ulipo ikiwa utafuata misingi sahihi ya pesa jinsi inavyotaka. Kila kitu kina kanuni zake ikiwamo hata kanuni za kupata pesa.

Kama bado unashangaa kwa nini wengine wana pesa nyingi na wewe huna, hiyo yote ni kwa sababu wanazifanyia kazi kanuni za pesa bila kujali wanazitumia kwa bahati mbaya au kwa kujua.

Huna haja ya kuendelea kukosa pesa kila wakati. Umefika wakati wa kukubali kujifunza na kutumia kanuni za pesa ili zikusaidie kuongeza uwezo wako wa kupata pesa na kufanikiwa maishani mwako.

Kupitia makala haya, naomba nikuachie dondoo kadhaa zitakazoweza kukusaidia moja kwa moja kuongeza uwezo wako wa kupata pesa na kuwa mtu wa mafanikio. Karibu tujifunze kwa pamoja;-

1. Jifunze mambo ya pesa kila siku.

 Jifunze kwenye vitabu, pia jifunze kwenye semina. Huwezi kufanikiwa kipesa kama hujachukua hatua za kujifunza jinsi pesa inavyofanya kazi.

Unalazimika kujua jinsi pesa inavyoweza ikawekezwa na kudumu katika maisha yako. Yote haya hayawezi kuja kwenye upande wako kama uchawi bali ni kwa wewe kuweza kujifunza.

2. Tafuta mshauri (Mentors) atakayekuwa anakuongoza kwenye mambo yako ya pesa pale unapokwama au unataka kusonga mbele zaidi. Hili linaweza kuwa jambo ni dogo kwako lakini ni muhimu kwako.

Watu karibu wote ambao wana mafanikio kila siku wana watu ambao wanawafuata au wanawashauri kila mara katika mambo ya pesa. Hali hiyo hupelekea kuwaweka juu kimafanikio.

3. Kama upo kwenye madeni, tafuta namna ya kuondoka huko. Madeni  ni sumu kubwa ya mafanikio kama utakuwa nayo kwa muda mrefu. Kama una madeni mengi, upo uwezekano wa nidhamu yako ya kipesa ikawa mbovu.

Weka mpango imara ambayo itaweza kukutoa kwenye madeni na kuanza kuishi kwa uhuru wa kifedha. Hutaweza kufika mbali kimafanikio ikiwa kila wakati ni mtu wa kudaiwa, hutaweza kufanya kitu chochote.

4. Jilipe wewe kwanza kila ukipata pesa yoyote ile. Kila aina ya pesa unayoipata, tenga kiasi kidogo na ujilipe kama mtafutaji wake. Usiache kujilipa hata kama pesa uliyopata ni kidogo.

Pesa ile ambayo utakuwa unajilipa wewe kwanza, huna haja ya kuwa nayo na haraka kuitumia. Kama ambavyo tumekuwa tukisema iache iwe nyingi baada ya hapo iwekeze.

5. Tafuta namna pesa zako zitakavyoweza kukulinda pale unapokuwa umeumia au kufa na kuacha watoto wadogo. Kuwa na ulinzi wako kama bima vile, lakini wewe bima yako inaweza ikawa  pia vitega uchumi vyako mbalimbali.

Hapa unatakiwa ujifunze kuwekeza mapema wakati bado ukijana mwenye nguvu. Kwa kadri jinsi unavyozidi kuwekeza pesa zako zitakulinda hata pale utakopokuwa umeshazeeka au kupatwa na matatizo yoyote.

Hivyo ndivyo unavyoweza kuongeza uwezo wako wa kupata pesa kama utazingatia mambo hayo matano kama yalivyowekwa wazi kupitia makala haya. Naamini umejifunza kitu na chukua hatua.

Jinsi y Kupata Channel Zaidi ya 30 za Bure Kupitia Startimes

$
0
0

Naam ndugu zangu tuendelee tu kujuzana mambo mbalimbali maana hili ndio nimeonelea ndio jambo jema,  leo tugeukie kwenye kisimbuzi cha startimes lakini leo tuchungulie kisimbuzi kinachotumia dish.

Huenda ulikuwa hujui ila channel za bure zipo nyingi mno katika kisimbuzi cha startimes kinachotumia dish leo nakupa siri hii bure kabisa fuata njia hizi hapa.


chukua remote yako bonyeza button ya menu
kisha chagua DVBS Installation
kisha chagua single search
kisha search zitakuja channel kibao ambazo ni free on air

Muhimu

trick hii ni kwenye visimbuzi vya startimes vinavyotumia dish , haihusiki kwenye visimbuzi vinavyotumia antena.

Pia jambo muhimu zaidi kuliko yote sambaza makala hii kwa marafiki na kuniachia maoni yako kuhusu makala hii hapo chini kwenye coment box

Hatua Za Kumfanya Mwanamke Amuache Mpenzi Wake Aje Kwako..!!!

$
0
0

Wakati umekutana na mwanamke mrembo halafu ukapiga naye gumzo zuri, unaweza mwisho kugundua kuwa ana boyfriend. Ama labda una rafiki mwanamke mrembo ambaye tayari ana mpenzi. Kwa njia yeyote ile, kujua kuwa mwanamke amechukuliwa kunaweza kukatiza matumaini. Mwanzo, wanaume wengi hukatizwa tamaa wakati wamezungukwa na wanawake warembo aina hii ambao tayari wameshachukuliwa.

Kukatiza stori fupi, hapa utakuwa umebakishwa na uchaguzi miwili ambayo unapaswa kuchagua ikifikia hapa: unaweza kuamua kuachana naye, ama unaweza kuchukua hatua ya usoni. Sasa hii haimaanishi ya kwamba unapaswa huuvunja uhusiano ambao tayari yuko nao ama tayari anafurahia. Lakini, kama anaonekana kuwa hajapendezwa na mahusiano ambayo tayari yuko, ama umeingiwa na hamaki ya kumtaka awe girlfriend wako, basi kuna hatua kadhaa ambazo unaweza kuzitumia ili umfanye aachane na mpenzi wake na akufuate wewe.

Hatua #1 Chambua mahusiano yako
Kabla kuchukua hatua yeyote lazima uchambue mahusiano yake na wewe. Je anakuchukuliaje? Kama amekuingiza katika himaya ya urafiki, basi tatizo hapa halitakuwa kwa boyfriend wake bali uhusiano wake na wewe wa kirafiki. Wanawake huwa na fikra mbilimbili kabla hawajaanza kudeti marafiki zao wa dhati kwa kuwa hawataki kuharibu uhusiano wao wa kirafiki nao.

Katika kesi nyingine, wanawake wanakuwa marafiki wazuri na mwanaume kiasi cha kuwa hawaingiwi na mawazo ya kuwa wanaweza kuwadeti hata kama wako single. Hii inaweza kuwa kama kesi unayoipitia sahizi. Hili neno ‘friend zone’/himaya ya urafiki linatumika sana na wanaume wengi wanafanya makosa mpaka wanajikuta wameingizwa katika shimo hili ambalo ni vigumu kujinasua – hili jambo liko na linakera sana. Kama umenaswa katika hili jinamizi na ‘friend zone’ na mwanamke unayempenda, basi fanya hima hima ujinasue na ufuate mbinu thabiti ambazo zitakujeuza mwanaume tofauti ambaye anaweza kudeti naye.

Hatua #2 Jifanye kama uko single
Baada ya kuchambua mahusiano yenu, anza kufikiria mambo ambayo munaweza kuyafanya mkiwa pamoja na mambo ambayo hupaswi kufanya akiwa na wewe. Mfano hupaswi kuleta stori za kumhusu mpenzi wake, ili uweze kumsoma kiwango gani ambacho anacho ikija kwa kumpenda mpenzi wake.

Kama hamzungumzii kuhusu mpenzi wake mara kwa mara katika maongezi yenu, basi itakuwa ni ishara ya kwanza kuonyesha kuwa hayuko interested na yeye sana. Hii itakurahisishia kazi kwako kuweza kumnasa kiurahisi. Kile ambacho unahitaji kufanya nikumsuka zaidi, ongea na yeye vile ambavyo anataka uongee naye, na pia mfanye akuone kuwa unavutia kadri wakati unavyosonga.

Hatua #3 Linganisha ustadi wako wa mahusiano
Wakati huu, nni wakati wa kujilinganisha wewe na boyfriend wake kinjia fioa, yaani kujipima uwezo wako na boyfriend wake kichinichini. Kwa kuanza mambo, unapaswa kuongea kuhusu vile ambavyo unaweza kuwa boyfriend mbaya kwa sababu unapenda maisha sana. Mbinu hii ya maongezi ni ya viini macho ambayo tuliieleza kwa kina awali katika machapisho yenu. Huku kutamfanya mwanamke kutaka kujua ni kwa nini unapenda maisha, na ni kivipi utakuwa boyfriend mbaya kwake.

 Pia katika mazungumzo yako, muelezee ni kivipi unayapenda maisha yako na jinsi unavyoishi. Kufanya hivi kutamfanya mwanamke ajenge picha ya maisha yako akiwa na wewe. Utamsisimua na kumfanya akuone kuwa maisha yako ni ya furaha wakati wote.

Kwa kufuata hatua muhimu, unaweza kuiba atenshen ya mwanamke ije kwako, na kuweza kumuwini mwishowe hata kama tayari ana boyfriend – aminia hili. Pindi utakapofanikiwa, anaweza kukuonyesha hata dalili za kuwa ameanza kufall na wewe na kumuacha mwanaume aliyempenda 
awali  kabisa...

Upo!

Billnass afunguka sababu ya wasanii kuringa

$
0
0

Mzungu Mzee 'Billnass' anayesumbua na ngoma ya 'Mazoea' ameweka wazi kinachowafanya wasanii wengi waonekane wanaringa na kusema wengi wao hukumbuka mateso na manyanyaso ambayo huwa wanapitia kabla ya kutoboa lakini pia ni mbinu za kibiashara.

Billnass amefunguka hayo na kusema kuwa wasanii wengi siyo kwamba wanaringa bali huamua kukaa maisha ya mbali na wale watu kipindi walipokuwa wanatafuta misaada halafu wakawa wanawanyima, hivyo wanapotusua na wao wanakuwa hawataki mazoea.

"Mimi ni social sana ndo maana hata maneno mengi yananipata, wasanii wanaonekana wanaringa kwa sababu hawataki zile kujuana sana ndiyo kuharibiana CV so usinijue kama hauna plan B' ndo mazoea hawataki. Unajua visasi siyo vizuri lakini kuna watu wakiwa wana 'hustle' huwa wanawakariri nani na nani walinipa msaada nani alinikazia kwa hiyo akifanikiwa anaamua kuishi maisha yake binafsi ya kukaa mbali na watu wanafiki" Amesema Billnass.

Hata hivyo msanii huyo ambaye ni mwanafunzi wa chuo cha CBE amedai licha ya kuwa anachukua kozi ya manunuzi (Procurement) anampango wa kuwa mfanyabiashara mkubwa na kabla ya kujiajiri atataka kuajiriwa na kufanyia kazi elimu yake.

"Nina ndoto za kuwa mfanyabiashara mkubwa, lakini elimu yangu ambayo naichukua lazima niifanyie kazi hata nikajiriwa miaka miwili inatosha kabisa ili niweze kwenda kujiajiri peke yangu kwenye biashara ninazoplan kuzifanya", alimalizia  Billnass.

Fahamu tabia za wanawake wanaopenda sana pesa

$
0
0



1. Huwa na tamaa ya mambo yasiyo ya lazima.
Wanawake wengi wapendao pesa huwa na tamaa ya mambo yasiyo ya lazima, mambo ambayo hayagusi maisha moja kwa moja. Hata nilipokuwa chuo wanawake wengi waliokuwa wanapenda pesa Sana walikuwa na tamaa za kusikitisha ambazo zilipofusha fahamu zao.

Unakuta mwanamke anaomba laki tano kwaajili tuu ya kununua Simu nyingine kubwa wakati akiwa bado na simu mpya.

Katika maisha ni bora uingie jehanam kuliko kukutana na mwanamke mpenda pesa kwani utateseka Sana kwa ajili yake na bado hata ona msaada wako.

Sio rahisi kujenga familia bora na mwanamke mpenda pesa.

2. Wengi hutoka familia masikini.
Wanawake wengi Kama sio wote ambao hupenda pesa kuliko utu wao hutoka familia kame Sana. Ukame wa kiuchumi mpaka kiakili. Wengi wao huweza kutoa hata rushwa ya ngono ili tuu wapate pesa wasijue miili yao inathamani zaidi ya zile karatasi.

Mtu ni masikini unandoto za kuwa na mwanaume mwenye pesa nani alikuambia wenye pesa wanataka masikini.

Umasikini wako usikufanye ujidharau au mtu akudharau. Lipo kundi dogo la wanawake wanaojitahidi kutetea thamani ya jinsia yao lakini wengi wao ni wakuonewa huruma tuu.

3. Wengi wao hawana elimu ya kutosha.
Mwanamke aliesoma akaelimika hawezi hangaika na pesa ya mtu. Ndio maana wanawake wachache huhangaika kwajili ya kujitegemea na sio kumtegemea mwanaume.

Wanawake wengi wenye elimu na vipato vizuri huwezi msikie akiongelea pesa Kama kigezo muhimu kwa mwanaume anayemuhitaji awe mume wake.

4. Ni wavivu na wasio na mawazo.
Wanawake wote wanaopenda pesa ni wavivu kupita kiasi. Uvivu wao umeanzia akilini kiasi kwamba hawana mawazo ya maendelo. Utakuta mwanamke anawaza mambo mepesi kabisa Kama urembo, nguo, mtoko, n.k.

Wanawake wapenda pesa ni hatari kwa ustawi wa familia.
Huwezi kuwa na familia kubwa ukiingia katika bahari ya viumbe hawa.

5. Hawana shukrani wala uvumilivu.
Wanawake wapenda pesa huwezi msikia akikushukuru zaidi ya kujichekesha tuu na kubinua makalio.

Kwa mfano amekuomba milioni moja then ukampa laki tano basi utamsikia akisema sasa hii nitafanyia nini, au niongezee tena mume wangu huku akikushika kifua au ndevu.

Wanawake wenye hekima hushukuru mpaka mwanaume anasikia aibu.

Suala la uvumilivu halipo kwa hawa wanawake. Shida ikitokea ukishindwa kuitatua kwa wakati huo basi hesabu umeliwa. Yaani kwao kukusaliti ni jambo lisilo na mashaka.

RAIS Magufuli Awajibu Kiana Wabunge Wanaolalamika Kutekwa na Wanaotaka Mikutano ya Kisiasa

$
0
0
#NUKUU:"Wanasiasa tuiache serikali ya CCM ifanye kazi yake, mambo mengine tukutane mwaka 2020,Tutangulize Tanzania kwanza, siasa baadaye, watanzania wanataka maendeleo, hakuna Mtanzania anayekula siasa”Rais Magufuli.

"Ukiwa dereva wa lori, hutakiwa kusikiliza watu uliowapakia wanaimba nini au wanatazama wapi, wewe endesha lori uwafikishe salama. Dereva mzuri huwa hasikilizi watu aliowapakia wanasema nini, au haangalii kule wanapoangalia wao. Hili lori la maendeleo litafika.


Tunajua tunapokwenda, asitokee mtu anayetaka kubadilisha ajenda yetu tuanze kuzungumzia mambo ambayo hayapo kwenye ilani ya chama." - Rais Magufuli #UjenziWaReliYaKisasa

TABWE Atoa Ujumbe Mwingine Kwa Simba "Wasitegemee Ubingwa"

$
0
0
Baada ya kupona kwa mastraika wa Yanga, Donald Ngoma na kiungo Thabani Kamusoko, straika raia wa Burundi, Amissi Tambwe, ameibuka na kusema wapinzani wao Simba wasitarajie Yanga itapoteza mchezo wowote tena hadi wanachukua ubingwa.

Ngoma na Tambwe kwa nyakati tofauti walikuwa nje ya kikosi hicho kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya goti lakini kwa sasa wamepona na Jumamosi iliyopita Ngoma na Kamusoko, walidhihirisha hilo kwa kucheza katika mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya MC Alger ya Algeria.

Tambwe amesema kuwa uwepo wa nyota hao utawafanya wazidi kupambana na Simba kwenye mbio za ubingwa na hatimaye kuwapiku na kuwa mabingwa hata kwa tofauti ya mabao kama watalingana pointi.

Tambwe amesema tangu amewaona Kamusoko na Ngoma wameanza kucheza wikiendi iliyopita, hakika amepata nguvu ya kufanya vizuri zaidi ya hapo na kwamba kama hakitatokea kikwazo kingine basi Simba wao wajaribu kuelekeza nguvu mahali pengine tu kwani suala la ubingwa litakuwa gumu sana kwao.


“Najua wenzetu wapo mbele kwa tofauti ya pointi mbili baada ya kuifunga Mbao FC, juzi lakini naomba wajue tu kuwa kupona kwa Ngoma na mimi huku Kamusoko naye akiwa fiti, hii ni chachu kubwa ndani ya safu yetu ya ushambuliaji ambayo utaona kila mmoja atakuwa amepata nafasi kubwa ya kucheza na kufunga kwani sisi kila mmoja ana uwezo wa kumtafutia mwenzake na kufunga mwenyewe.
“Simba wasitegemee ubingwa kama sisi tupo hata kama wamekuwa na kasi nzuri, lakini wajue kuwa tutapambana hadi mwisho,” alisema Tambwe.

MWILI Wakutwa Umefukiwa Katika Msitu wa Mabwepande

$
0
0

Mkazi wa jijini Dar es Salaam, Onoratus Mwinuka aliyepotea wiki mbili, mwili wake umekutwa umefukiwa kwenye pori la Mlolo Mabwepande nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Mke wa Marehemu, Frida Msabi akizungumza na Nipashee juzi kwenye pori hilo ambalo mwili huo ulionekana alisema Machi 14, mwaka huu, mume wake alichukua fedha ambazo alitaka kwenda kununua gari aina ya Pick Up.

Alisema kabla ya kuondoka nyumbani alipopiga hatua chache alimwita mtoto wake Gweni na kumtaka achukue mfuko wa fedha hizo na ufunguo akazihifadhi chumbani kwake(kwa marehemu).

Alisema mume wake alimwambia mtoto kuwa ndani ya chumba hicho kwenye kabati kuna fedha zingine hivyo ahakikishe anafunga chumba hicho.

Alisema wakati akitoa maelekezo hayo ilikuwa ni saa 9:00 usiku muda ambao mume wake amekuwa akiondoka nyumbani kwenda Makumbusho kusambaza maziwa anayouza.

Baada ya kumkabidhi mkoba mtoto alisema aliondoka kwa baiskeli akiwa ameambatana na Ayub.

Mama huyo mfiwa alisema Ayub alidai kuwa walipofika kibao cha Shule ya Sekondari Mabwe Pande usiku huo ghafla ilitokea gari aina ya Noah na kusimama kisha kuwauliza kama wanakwenda.

Baada ya hapo alisema mume wake hakuonekana hadi siku ya nane alipokutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa katika pori hilo.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Kinondoni, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Suzan Kaganda alipotafutwa kwa njia ya simu hakupokea kwani iliita bila majibu.

UJUE Msitu wa Ajabu Japan Ambapo Maelfu ya Watu Wamekufa Kimiujiza

$
0
0

Aokigahara au msitu wa kujiua au bahari ya miti ni msitu ambao una ukubwa wa 35 square- kilomita ambao uko karibu na milima ya fuji huko japan

msitu huu ni msitu ambao mbali ya kuwa ni kivutio kikubwa cha watalii ni msitu ambao unasemekana kuwa una mambo ya ajabu, kutisha na kuogofya

ni kawaida kabisa ukiwa ndani ya msitu wa Aokigahara ukisikia unaitwa jina lako na mtu asiyeonekana iwapo ukiwa ndani ya msitu huo.

pia inasemekana kuwa unaweza kumuona mtu kwa mbali kwenye miti ya msitu huo ukifuatilia huoni mtu kwa maana watu hao wanapotelea kwenye miti 

Msitu huo unasemekana una mapepo ya kujapan kwani tokea uwepo wake ni maelfu ya watu wamekuwa wakikutwa wamekufa maeneo hayo haya kwa kujiua

ambapo kwa mwaka 2010 pekee watu 54 wamekutwa wamekufa ndani ya msitu huo

tafiti zaidi zinasema kuwa tokea mwaka 1988 walipoanza kufanya hesabu za watu wanaojiua msituni hapo ni watu 30 kila mwaka huenda msituni hapo na kujiua

In 2003, miili 105 ilikutwa msituni watu wakiwa wamejiua, ambapo iliizidi recodi ya watu 78 mwaka 2002 

mwaka 2010, it was estimated that watu 200 walijaribu kujiua na kati ya hao 54 walifanikiwa kujiua

cha kushangaza sasa matukio ya kujiua yanaongezeka sana mwezi March mwisho wa fiscal year kwa japan

mwaka 2011 watu wengi waliojiua hapo ni walitumia njia ya kujinyonga na wengine drug overdose

siku za hivi karibuni serikali ya Japan imeamua kuficha namba ya watu wanaojiua lakini inasemekana mpaka mwaka huu kwa maana ya mwezi huu tayari kuna waliokwisha jiua msituni 

Ukiwa unaingia Msituni utakuta kuna vibao ambavyo vinaelezea kuhusu msitu na onyo utakaopewa wewe mtalii

msitu wa Aokigahara imewekwa kwenye media ambapo mwandishi maarufu wa vitabu wa japan Seichō Matsumoto mwaka 1960 aliandika kitabu kiitwacho Kuroi Jukai (Black Sea of Trees). Bahari nyeusi ya miti

Holywood na wao hawako nyuma kwani mwaka huu kuna movie inatoka inaitwa the forest iliyoongozwa na mwongozaji maarufu wa filamu jason zada na imetayarishwa na David Goyer ambaye ni mtayarishaji maarufu wa filamu ikumbukwe ndiye aliyatayarisha movie za Blade, Batman Begins na Man Of Steel (superman based movie) the forest imechezwa na Natalie Bormer na Taylor Kinney movie imetoka january 8 mwaka huu 

VIDEO: Gwajima Achimbwa Mkwara na Mchunganji Komando Mashimo..Aambiwa Aache Uzushi na Porojo

Mwakyembe Amjibu Juma Nkamia Juu ya Yeye Kukaa Meza Moja na Roma Mkatoliki Siku Alipokutana na Waandishi wa Habari..!!!

$
0
0

Mwakyembe: Idara ya Habari Maelezo iko ndani ya Wizara yangu, ofisi yangu iko pale, mimi nimefuata mtu au amekuja ofisini kwangu.

Mwakyembe: Roma alivyopotea ndugu zake walikua wananipigia mimi simu na sio Nkamia huyu kijana aliyetekwa ameniomba mimi nimsaidie'

Mwakyembe: Mheshimiwa Nkamia unashangaa mimi kukaa na hawa vijana, unataka ukae naye wewe'

Waziri Mwigulu Nchemba Awachana Wabunge Ridhiwani Kikwete, Hussein Bashe, Zitto Kabwe na Aeshi..!!!

$
0
0

Mwigulu: 'Lazima tutoe fursa kwanza vyombo vilivyo chini yangu vifanye kazi kabla ya mimi kuzungumza' 

Mwigulu:'Wanasema mbona sisemi juu ya kinachoendelea, hii ni Wizara ambayo siyo kila kitu ni habari, Wizara ina vyombo
Viewing all 104808 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>