Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104793 articles
Browse latest View live

DALILI 7 Za Kuonyesha Anakucheat Na Mwingine..!!

$
0
0

Katika mahusiano huwa kuna changamoto tofauti tofauti. Kwa kawaida ni muhali kupata mahusiano ambayo hayana patashuka moja au nyingine. Inajulikana ya kuwa mahusiano huwa kuna migogoro, kutoelewana, kunyamaziana na mbaya zaidi...vita.

Anyway mambo kama haya huwezi kuyazuia kwa sababu wenyewe ndio wanayaita mapenzi. Utaskia mtu akilalamika kuwa amemiss kugombana ama kuteteshana na mpenzi wake, jambo ambalo huwa ni la kawaida.

Ok. tukija katika mada yetu ni kuwa nataka nikuulize maswali yafuatayo. Je hivi karibuni umeona kama mpenzi wako amekuwa mtu tofauti na ilivyo kawaida? Je mpenzi wako imekuwa muda mrefu tangu mfanye mambo yenu ya kawaida ambayo mlikuwa mkifanya? Je unamshuku kama amepata mwingine?

Kama majibu yako ni NDIO basi hili chapisho nimeliandika spesheli kwako na nataka umakinike kwa kusoma dalili zetu tulizoziandika na kama yote yanawiana na dhana yako basi ni wakati wa kumfungukia mpenzi wako na umwambie kweupe kuwa umechoshwa na tabia yake ya 'kutoka nje', na umuulize kama amechoshwa nawe ili ukate minyororo ya kuwa naye ili uwe huru.

Zama nami!

Dalili #7: Muda mwingi anajaribu kujirembua kuoneka vizuri

Kuvalia vizuri kila wakati si jambo baya la kufanya katika mahusiano, mwanzo wapenzi hupenda sana kuhakikisha ya kuwa wanampendeza mwenza wao.

Lakini, ukiona ya kuwa anamakinika zaidi na upande wa kujifanya aonekane mrembo, basi itakuwa anajaribu kumridhisha mtu mwingine kando na wewe. Kama umemgundua kuwa anajaribu kuvalia vizuri wakati anatembelea hizi sehemu basi weka ? katika mawazo yako: Kazini, supermarket, mkahawa, na hata gym!

Makinika: Zile sehemu zake za kawaida anazozienda kama amezijeuza kuwa fashion show itakuwa ni ishara ya kuwa anakucheat.

Dalili #6: Anakuwa msiri na simu yake, pakatalishi yake nk

Kila mtu ana haki ya kuwa na faragha yake. Mwanzo, watu wengi hawapendi faragha yao ishambuliwe na hata wapendwa wao. But ishu itakuja wakati ambapo anakuwa msiri kuhusu vitu vyake zaidi kuliko awali.

Hii inaweza kumaanisha kuwa kunakuwa na migogoro isioisha wakati ambapo umechukua kuangalia simu yake hadi ule wakati anaudhika wakati umeingia kwa chumba chake akiwa anatumia kompyuta yake. Ukiona mtu akianza kuwa msiri zaidi ni kuwa atakuwa anawasiliana na mchumba mwingine ambaye ako naye.

Dalili #5: Anapunguza hamu ya kufanya tendo la ndoa hadi kukataa asilani

Hata watu waseme nini, kufanya mapenzi ni sehemu muhimu inayohitajika katika mahusiano. Kama hamfanyi mapenzi, utajihisi ya kuwa unabezwa na kukatalika na mpenzi wako.

Wakati umri unaposongea, utagundua ya kuwa kiasi cha mapenzi mnachofanya huwa kinapungua. Hio ni kawaida, lakini kuna hatua nyingine neno 'ni kawaida' linaondolewa.

Kukataliwa katakata kufanya mapenzi ama kutoa visababu inaweza kumaanisha kwa njia rahisi kuwa hajiskii kufanya mapenzi na wewe. Wakati mtu anakucheat, huwa anapoteza ule muungano wa kihisia na wewe na atakuwa hana hamu ya kufanya mapenzi na wewe

Dalili 4: Kuna yule mtu kilinge (mysterious)

Wale watu kilinge ndio unaopaswa kuwaogopa zaidi. Wanaume na wanawake kwa kawaida watakuwa na marafiki wa jinsia ile nyingine, lakini kama utamwona mpenzi wako haachi kuongea kuhusu huyo mtu basi kuna tatizo.

Hata kama nia yake ni nzuri, anaweza kuwa na kitu ambacho ni zaidi ya kuwa marafiki. Kama hatakuruhusu ukutane na huyu mtu kilinge ambaye amekuwa akipoteza muda wake mwingi naye, basi kunaweza kuwa na kitu ambacho ni zaidi ya kuchat pekee.

Dalili #3: Anazozana na wewe zaidi ya kawaida

Kukefyakefya na kukufananisha na wengine ni jambo lisilokubalika katika usuhiano. Wakati ambapo hii itatoka kuanzia mzaha hadi kuwa serious, ni ishara ya kuwa anakucheat.

Mara nyingi, mpenzi akikosana na mwenziwe hujaribu kujitenga na majibizano. Lakini ukiona ya kuwa kila wakati anagombana na wewe kwa sababu ya mahusiano yenu basi ni ishara ya kuwa kuna mwingine ambaye anamwonyesha mapenzi ya dhati...na si wewe

Dalili #2: Anakutenga wewe na marafiki zako wa karibu

Wapenzi wawili ambao wamekuwa pamoja kwa muda mrefu huwa wanagawa marafiki pamoja. Hawa ni wale ambao nyinyi wawili mnawaingiza katika maisha yenu kadri miaka inavyosonga. Wakati umeona kuwa mpenzi wako anapunguza muda wa kuwa na wewe na anachofanya ni kuwatenga watu hawa, kawaida huwa kuna mtu anahusika.

Anaweza kuwa hana moyo wa kukabiliana na marafiki wa karibu na kuwadanganya kuhusu furaha anayopata katika mahusiano yenu. Hii inaweza kutokea baada ya muda mrefu ama akajitenga ghafla.

Dalili #1: Analijeuza neno ''tu'' hadi ''ni'' polepole

Neno ''tu'' katika mahusiano ni takatifu. Huu ni ule wakati ambao mwanaume na mwanamke wamewekeza shina la kuwa pamoja. Wakati mwingi, sana sana wanawake ndio huwa wa kwanza wa kubadilisha neno ''ni'' hadi ''tu'' halafu mwanaume akalizoea.

Hivyo katika mahusiano ukiona mpenzi wako ameanza kurudia kutumia neno ''ni'' itakuwa anajaribu kukutenga katika maisha yake, anajaribu kukufuta katika picha yake.


Mwisho ni kuwa kudanganya katika mahusiano ni swala zito ambalo linaibua hisia nzito, lakini dalili za kucheat zinaweza kutatiza zaidi.

Kukataa kufanya mapenzi ama kujaribu kujirembua inaweza kusababishwa na misongo ama kutojiskia shangwe yeye mwenyewe. Kabla ya kumlaumu kuwa anafanya mabaya, hakikisha ya kuwa kuna ishu inayoendelea, ama inaweza kuwa wewe ndiwe chanzo cha kufanya mahusiano yenu yavunjike

JINSI ya Kutumia Fedha Kidogo Kufanikisha Makubwa Katika Hali ‘Ngumu’..!!!

$
0
0

Katika maisha ya kawaida ya Watanzania tulio wengi, kwa namna moja ama nyingine umewahi kusikia au wewe binafsi kulalama kuwa pesa yako haikai au haiendi kama unavyotegemea. Hiki ni kilio cha kawaida ambacho hakitokani na kutapanya fedha bali kutojua mbinu sahihi ya kawaida tu ya kuzitumia vyema pesa ‘kidogo’ kupata matokeo makubwa.

Moja kati ya tabia ya fedha hasa hizi tunazopata watu wa kima cha chini ni kwamba huwa ni kama zinayaita matatizo au matumizi, pindi tunapokuwa nazo. Yaani mambo yanaweza kwenda tofauti na ulivyokuwa umepanga, matumizi yanaongezeka kidogo-kidogo ila unashtuka umebaki na kisalio ‘kiduchu’ au hata umefilisika kabisa. Ndio hapo kilio cha ‘mishahara haikutani’ kinazidi.

Leo tutakupa mbinu ya namna ya kubadili kidogo mtindo wako wa maisha bila kujibana bali kubana mianya ya kutumia fedha zako bila kufuata mipango uliyojiwekea.

Epuka vishawishi vya ATM, Simu Pesa:

Jitahidi mara kadhaa kukwepa kutembea na ATM au kuweka fedha nyingi kwenye simu yako ya mkononi. Chukua kiasi fulani cha fedha taslimu uliyopanga kutumia siku hiyo au wiki hiyo, ongeza na kiasi kidogo tu cha ‘dharura’. Hii ni kwa ajili ya mahitaji ya kawaida. Itakusaidia kuepuka kutumia fedha za akiba mara kwa mara pale uonapo kitu bila mpangilio kwa sababu tu unajua utaingia ATM na kuchomoa au utaivuta kutoka Simu pesa.

Itakusaidia kukwepa pia kuwapa ofa rafiki na jamaa kwa ‘mizuka’, hasa baada ya kupata kilevi. Hatusemi usiweke fedha kwenye simu, bali usiweke kiasi kikubwa kama akiba tu na kutembea nazo. Hakika utazitumia bila kupanga kama huna msimamo wa ‘bahiri’. Kumbuka kutumia ATM/ simu pesa mara kadhaa unaongeza makato ya fedha kwa huduma.

Epuka tabia za ‘nunua sasa lipa baadae’

Kampeni za ‘nunua sasa, lipa baadae’ zina msaada mkubwa kwa watu wenye mahitaji fulani kwa wakati huo lakini wanategemea kupata fedha baadae kidogo. Lakini ni hatari zaidi kwa usawa huu kwani ni rahisi kunogewa kuchukua vitu ambavyo sio vya lazima sana ukiiwaza fedha ya baadae bila kuweka akilini kuwa hiyo baadae pia itakuwa na mahitaji yake.

Jitahidi kutumia fedha kutoka kwenye mfuko uliopo sasa kama suala hilo sio la lazima sana kwa wakati huo, kama ni kiatu kizuri, kumbuka kinaweza kupatikana kizuri zaidi wakati ujao na ukakilipia kulingana na pesa itakayokuwepo kwa mazingira hayo.

Usifuje pesa yako kwenye majina ya bidhaa

Hakikisha unanua bidhaa unayoihitaji kwa gharama ambazo unaweza kuzimudu bila kufuata mkumbo wa jina la duka fulani. Usitafute jina tu kuwa umeweza kununua sehemu fulani kama fulani. Fikiria kwanza kama bidhaa hiyo haiwezi kupatikana sehemu nyingine unayoweza kufika na kupunguza gharama. Zingatia pia uhalisia wa ubora wa bidhaa husika ili isije kugeuka hasara kubwa na kukugharimu zaidi.

Andaa, pitia na ifanyie tathmini bajeti yako

“Mali bila daftari, huisha bila habari”. Hakikisha sio tu kwamba unaandaa bajeti ya matumizi yako ya mwezi, lakini pia ifanyie mapitio wakati wa matumizi na ifanyie pia tathmini kama umeitumia ipasavyo. Hii itakusaidia kuondoa matumizi yasiyo ya lazima na kujiwekea kiwango cha wastani wa matumizi yako ili kupata nafasi ya kuweka akiba kwa ajili ya maendeleo na mambo mengine makubwa.

Usiogope kuahirisha

Unapaswa kufahamu kuwa kuna wakati inakulazimu kuahirisha mpango wa kufanya matumizi fulani sio kwa sababu hauna fedha inayotosha, bali matumizi ya pesa hiyo yatakupa ukata wa haraka na kilio kabla ya kupata nyingine.

Kama ni hivyo, usiogope kuahirisha mpango wako mzuri. Ni vyema ukaahirisha na kujiandaa vizuri zaidi ili uweze kumudu kufanya matumizi hayo husika bila kilio cha baadae. Kuahirisha kwa sababu za msingi ni bora kuliko kulazimisha kwa shida ya kipindi.

Kumbuka, hakuna fedha nyingi bila fedha ndogo, unapotumia fedha kwa matumizi unayoyaita madogo tu fahamu kuwa unabandua sehemu ya gogo lako. Hivyo, halitakuwa kama ulivyotaka kwa muda husika.

Ukitoa shilingi moja kwenye milioni moja haitaitwa tena milioni moja. Kuwa na nidhamu ya fedha, ni siri ya mafanikio hasa kwenye kipindi kigumu cha maisha.

Hii ni sehemu tu ya unayopaswa kuyafanya kuepuka matumizi yasiyo ya lazima.

UMEWAHI Kujiuliza Nini Lengo La Mfuko Mdogo Mbele Ya Suruali Yako Ya Jeans?

$
0
0

Je unaujua mfuko mdogo katika suruali yako ya Jeans? Ndiyo, ule ambao umeshonwa juu kidogo ya mfuko mkubwa wa kulia.

Umewahi hata mara moja kusimama na kujitafakari kwa nini huo mfuko mdogo mbele ya suruali yako ya jeans upo hapo ulipo na nini hasa lengo la mfuko huo zaidi ya pengine kudumbukiza sarafu au jojo ambayo unataka kuja kuitafuna baadae au kuwaza kama ni fasheni tu katika nguo?

Kama hujawahi kujiuliza hilo swali na bado hujui chanzo na lengo la mfuko huo mdogo mbele ya suruali yako ya Jeans usijali kwani  tovuti hii itakueleza chanzo na lengo la mfuko huo.

Mfuko huu ulikuwa unatekeleza jukumu muhimu sana miaka ya nyuma na ndio sababu kubwa iliyopelekea watengenezaji wa suruali za Jeans kuweka mfuko huo juu kidogo ya mfuko wa mbele wa suruali.

“Ni mfuko maalum wa kuhifadhi saa. Ndiyo, inasemekana miaka ya nyuma ya 1,800, watu wengi walikuwa wanapenda kuvaa saa zao katika cheni na kuzifungia katika viuno vyao. Ili kuweza kuweka salama saa zao zisivunjike na kuharibika, Levi, watengenezaji wa kwanza kutengeneza suruali za Jeans wakaamua kuweka mfuko huo mdogo mahali ambapo watu hao wangeweza kuhifadhi saa zao salama na kwa wepesi zaidi.

Hivyo ulianza kama mfuko wa kuhifadhi salama saa za mifukoni, japo baadae ukaanza kupata matumizi mengine kama kuhifadhia sarafu, tiketi za safari, kondomu, na viberiti hasa kwa watumia sigara.

Tangu hapo suruali za Jeans za aina zote zimekuwa zikitengezwa na mfuko huo mdogo bila kujali fasheni iliyopo kwa wakati huo.

UTAFITI Mpya: Pombe ni Hatari kwa Moyo Wako, Fahamu Kiasi Usichopaswa Kuvuka..!!!!

$
0
0

Ingawa tafiti kadhaa zilizopita ziliwahi kueleza kuwa ni vyema kunywa kiasi fulani cha pombe kwa afya yako, utafiti mpya umebaini kuwa pamoja na hayo, kuna hatari kubwa ya kuvuruga mwendo wa mapigo ya moyo kwa kunywa pombe.

Kwa mujibu wa utafiti huo uliofanywa na timu ya wataalam wa sayansi wakiongozwa na Profesa Peter Kistler wa Hospitali ya Alfred iliyoko Melbourne nchini Australia, pombe ina madhara mengi kwenye mwili wa binadamu ambayo yanaweza kuchangia katika kuvuruga mwendo wa mapigo ya moyo.

Imeeleza kuwa hali hiyo inaweza kuwa chanzo cha magonjwa ya moyo pamoja na stroke (kupooza).

Imeeleza kuwa kunywa pombe kunaweza kusababisha udhaifu katika moyo na inaweza kuharibu mfumo wa mawasiliano unaoweza kusaidia seli za misuli ya moyo pamoja na mfumo wa fahamu ambao unasimamia kazi nyingi za mwili.

Watafiti hao wamewashauri watu ambao hunywa pombe lakini wamekuwa wakisikia mwendo wa mapigo ya moyo hauko vizuri wasitishe ama kupunguza kwa kasi kubwa matumizi ya vilevi.

Wakizungumzia kiwango cha pombe ambacho kinamfaa mtu ambaye ameanza kusikia mapigo ya moyo hayako sawa, apunguze hadi chupa moja ya pombe yenye kilevi cha kawaida na ahakikishe anapata siku mbili kwa kila wiki kutotumia kabisa kilevi.

Kazi hiyo ya watafiti hao iliyochapishwa kwenye jarida la American College of College of ardiology, ilifanya marejeo ya tafiti zaidi ya 100 na iliwahusisha takribani watu 900,000.

JIWE Lenye Ukubwa wa Kipande cha Ardhi cha Kilomita Mita Lapita Karibu na Dunia..!!!

$
0
0

Asteroidi kubwa ambayo inakadiriwa kuwa na ukubwa karibu sawa na wa Jiwe la Gibraltar imepita salama karibu na Dunia.

Asteroidi hiyo ambayo inakadiriwa kuwa na kipenyo cha karibu kilomita 1, ilipita karibu na dunia umbali wa mara tano na umbali kati ya Dunia na Mwezi.

Jiwe hilo ambalo limepewa jina 2014 JO25, ndilo kubwa zaidi kupita karibu na dunia tangu 2004. Wataalamu wa anga za juu walisema fursa nzuri zaidi ya kutazama asteroidi hiyo angani itatokea Jumatano usiku.

Picha za mitambo ya rada zilizopigwa kwa kutumia antena ya Shirika la Anga za Juu la Marekani (Nasa) yenye urefu wa mita 70 (sawa na futi 230) katika kituo chake California zilionesha kwamba jiwe hilo lenye umbo la njugu linazunguka mara moja kila baada ya saa tano.

Asteroidi hiyo iliipita Dunia katika umbali wa kilomita milioni 1.8 (maili 1.1 milioni) saa 13:24 BST, jana Jumatano, Aprili 19.

Inakadiriwa kwamba jiwe jingine kupita karibu na dunia itakuwa mwaka 2027 pale asteroidi ya kipenyo cha karibu mita 800 (nusu maili) iliyopewa jina 1999 AN10 itapita karibu na dunia umbali sawa na wa mwezi kutoka kwa Dunia, takriban 380,000 km (maili 236,000 ).

MCHEKESHAJI Eric Omondi Amuigiza Rais Donald Trump..!!!!

$
0
0

MCHEKESHAJI kutoka Kenya, Eric Omondi, katika projeti yake ya kuchekesha maarufu kama ‘How To Be’, amemuigiza Rais wa Marekani, Donald Trump, wakati alipokuwa akigombea urais wa Marekani.

Video hiyo imemwonyesha Omondi akifanya vituko vya Trump wakati akiomba kura kwa Wamarekani akionekana kuwa mtu jeuri na mwenye kujiamini kupita kiasi wakati wa kinyang`anyiro hicho.

MAITI ya Mtoto Yakutwa Akielewa Mtoni...Chanzo ...!!!

$
0
0

MTOTO wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Ubena, Tarafa ya Chalinze mkoa wa Pwani aliyefahamika kwa majina ya Karim Salum, anasadikika kufariki dunia baada ya kuzama kwenye maji ya mto Ngerengere wakati akiogelea na wenzake huku jitihada za kutafuta mwili wake zikigonga mwamba kutokana na wananchi kuutafuta mwili huo kwa zaidi ya siku mbili mfululizo bila mafanikio.

Chanzo kimeshuhudia wananchi wakiendelea na jitihada za utafutaji wa mwili wa mtoto Karim Salum anayesadikiwa kufa maji huku vijana walioshuhudia mtoto huyo akizama ndani ya maji wakieleza tukio hilo lilitokea majira ya saa kumi Alasiri wakati wakijaribu kuogelea ndani ya mto huo.

Naye Babu wa mtoto huyo Bwana Issa Bung’ombe ameeleza kusikitishwa na tukio hilo na kwamba mtoto huyo aliaga nyumbani akielekea mtoni kuchota maji ndipo kadhia hiyo ilipomkuta.

CHAMELEONE - Ndoa Yangu Haivunjiki Ng’o..!!!!!

$
0
0

Chameleone amekanusha tetesi kwamba mkewe Daniella Atim amekwenda mahakamani kudai talaka.

Taarifa zilisambaa mitandaoni kwamba Daniella alidai kwa kutokuwa na furaha na ndoa yake kutokana na manyanyaso na vipigo anayoyapata kutoka kwa muimbaji huyo mkongwe wa Uganda.

Chameleone ameamua kuvunja ukimya kupitia mtandao wa Facebook kwa kurusha video ya dakika 53 akiongelea mengi kuhusu familia yake, ambayo inaonekana kuwa na furaha tofauti na yanayozungumzwa.

“Kuna habari nyingi zimesambaa zinazohusu mimi na familia yangu. Siwezi kusema kubwa lolote lakini nachotaka kusema ni kuwa sina talaka wa hakuna anayedai talaka,” amesema msanii huyo kwenye video hiyo.

“The beautiful Daniella there. Kumbuka mimi ni mkatoliki, mkatoliki akifunga ndoa hawezi kuachana,” ameongeza.

MAMA Aliyeibiwa Mtoto Hospitali, Afunguka..!!

$
0
0

Asma Juma, mzazi aliyejifungua watoto mapacha na kudai kuibiwa mtoto mmoja katika hospitali ya Temeke, amefunguka kuelezea kilichotokea.

Mzazi huyo anawatuhumu wauguzi wa hospitali hiyo kumuiba mtoto wake huyo akidai, awali wakati alipokuwa na ujauzito picha za Ultrasound alizowahi kupima zilionyesha kuwa ana ujauzito wa mapacha na hata alipokuwa hospitalini hapo alimsikia nesi aliyekuwa akimuhudumia akithibitisha kua ana watoto wawili.

Akiongea na kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM, Asma amesema, “Wakati nipo chumba cha upasuaji, baada ya kuambiwa nafanyiwa operesheni, yule nesi aliyekuwa ananihudumia akiwa na mtu mwingine nilimsikia akisema ‘viko viwili’ akimaanisha wako watoto wawili, yule nesi aliniambia nisijitingishe, baadaye walinichoma sindano nikapoteza fahamu.”

“Nilivyozinduka nikajikuta nipo chumba cha pili nikiwa nasikia maumivu makali sana, niliwaomba dawa wakaniambia nitazikuta wodini hapo hakuna dawa za maumivu. Nilifanyiwa operesheni saa nane hadi saa kumi na mbili ndipo nikapelekwa wodini, kwa muda wote huo sikupewa watoto wangu. Nimeletewa mtoto mmoja saa kumi na moja alfajiri nakumbuka wakati nipo wodini nilimsikia yule nesi aliyekuwa akinihudumia akisema ‘Ultrasound’ zinadanganya. Ilisema ana watoto wawili kumbe ni mmoja. Kwakweli hadi sasa sielewi,” ameongeza.

Tumia Bidhaa za Asili Kupendezesha Mwili Wako Toka Kwa Markson Beauty

$
0
0

OFFER, OFFER, OFFER
Pata bidhaa halisi za MARKSON BEAUTY kwa bei ya punguzo msimu huu wa sikukuu. Bidhaa zetu zina matokeo ya haraka na garantii na zimethibitishwa kiafya.
🍓🍅🍉🍎🍍🍉🍓🍒🍉🍎
HANDSOME UP ni kifaa chenye uwezo wa 99% kuongeza uume kwa uhakika na bila madhara na kuimarisha misuli ya uume iliyo legea. Inapatikana kwa @190,000/=tu.
PIA TUNA👇👇👇👇

1.Gely ya kupaka @120,000/=
2.Vidonge maalum kwa ajili ya kuongeza nguvu za kiume hata kwa wenye kisukari na hamu ya tendo la ndoa kwa wanaume @120,000/=.
3.Spray ya kuchelewesha kufika kileleni kwa mwanaume (pre-mature ejaculation problem solution) @110,000/=
4.Dawa ya kutengeneza shepu (hips, makalio na mapaja) @190,000/=
5 .Kupunguza unene na manyama uzembe @ 140,000/=
6.Kupunguza maziwa na kuyasimamisha hata kwa walionyonyesha @120,000/=
NB.Hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa MARKSON $ CO na garantii ili kukuhakikishia kufanikiwa kwako.
Popote ulipo duniani
Wasiliana nasi kwa (+255)
0767447444 au
0714335378.
Follow us Instagram
@Markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr

Bifu la Mange na Jack Wolper Lafika Pabaya...Wolper Amjibu Mange Hivi

$
0
0

Bifu la Mange na Wolper lililoanza Jana ghafla linaendelea, Wolper Amjibu Mange Hivi :

"Mange Kimambi,Usinitafute sana kwasababu mm naishi nitakavyo sio utakavyo wala watakavyo,pili Ustar wangu nahisi hauna

mvutano wowote na ww wala haudhuru familia yako!Unajua ww unaweza ukawa sawa kwa kile unachokifanya lakini pia unaweza ukawa sawa kutokana na mawazo yako yanavyokutuma,Mimi binafsi nina maamuzi yangu na sipelekeshwi na mtu kwasababu mm ni mtu mzima na nina fikiria kila kitu kabla ya mtu yoyote!Ninapoamua kupost au kusema chochote hayo ni maamuzi yangu chuki zako ww zisipelekee kufanya kila mtu achukie usiowapenda no no no sio mm JACKLINE WOLPER MASSAWE,Nafikiri tunapishana vitu vingi sn km hivyo mm sina akili ww unazo,Sasa ww dada nikuulize kitu ulitaka mm nifanyaje nije ulaya kukusapoti tumchukie Bashite au???maana sikuoni kwenye point yani mm kila kitu kwako naona chuki 😂😂my dear people are different siwezi kumuona mtu mbaya eti kisa ww Mange umemuona mbaya haaaaaa we ni nani?????Ulikuwa na mchango wowote kwenye zile sh@h@w@ zilizompa mama mimba yangu????Kama ww vibabu vyako vya kizungu huko vinakupa M2 basi usifosi tufanane!Kingine mbona unapanic sn kwenye maisha ya watu binafsi kuliko hao watu wenyewe?Sawa najua kuchamba ni ajira yako ya pili huku insta tukiachana na ile ya kutafuta vizungu huko!Lakini sasa naona unatafuta kiki kila mtu umuweke kwa Acc yako,hiyo inaonesha wazi BASHITE ameshakushinda sasa umeona unifate mm 😂😂😂my friend sijaanza kuwekwa kwenye Acc za watafuta followers kwako 😉😉Nimeanza siku nyingi kweeeeli kwahiyo ww nakuona km Repoter tu wa huku Insta so fanya kazi yako mama,Alafu Naywamitego ndo haina gani ya gari jipya hiyo,😳😳Mm nadeal na ww leo sipo kwa ajili ya mwingine... 😆😆😆Mbona unaforce kutaka kujua mambo yangu na huku hujui,Eti nimefumaniwa nifumaniwe na nani mm mjini hapa habari isitapakae wkt unasema nimefumaniwa huna hata EVIDENCE ya chupi...Embu kanywe hata TREVO zile dawa uongeze supu supu za miguu bibi weeeeh usiniletee u SKELETON 😂😂😂Hivi unajua ww una stress za watu sn kuliko zako binafsi,😜😜😜Bashite ananitia vidole wakati huo ww unakua mshika K!s!M! Au vuz!😂😂😂Unajua ww ustake kuniambukiza stress zako na chuki zako STAKI usiniforce tufanane na usinipakazie mambo ambayo yanahusisha chuki zako.."

Uhai wa Ben Saanane Utata Waibuka..Habari Vichwa vya Magazeti ya Leo 21/4/2017..!!!

Bongo Movies Walioandamana na Makonda Wazidi Kukosolewa...Cheki Bella Fasta Alivyowapa Makavu Live

$
0
0

Msanii wa muziki na filamu, Bella Fasta amefunguka kwa kud
ai kuwa hajapendezwa na kitendo cha baadhi ya wasanii wa filamu nchini kuandamana kupinga filamu za nje, kwa madai hatua hiyo ilitakiwa kujadiliwa na wasanii wote wa filamu na siyo vikundi vya watu fulani ndani ya tasnia hiyo.

Wasanii hao ambao waliandamana wakiongozwa na Jacob Stephan ‘JB’, waliiomba ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kupiga marufuku wafanyabiashara wa filamu za nje kwa madai hawalipi kodi wakati wasanii wa ndani wanalipa 30% ya mapato ya filamu zao.

Akiongea na Bongo5 Alhamisi hii, Bella amedai tukio hilo lilitakiwa kuwa na kauli moja ya wasanii wote wa filamu.

“Bongo Movie mmeniudhi, sana siyo wote, ni wachache,” alisema Bella Fasta kwa ukali na kuongeza “Yaani hamuoni aibu mnasema kabisa movie za nje zisiingie Tanzania, nchi gani mambo haya yapo?. Tufanye kazi nzuri ziuze siyo tunaingiza mambo ya siasa kwenye mambo yetu ya kawaida,”

Bella amesema, kama ilikuwa ni ajenda ya wasanii wote kuhusu kuibiwa kazi zao mbona wasanii wa muziki hawakuhusishwa.

“Kama hilo suala lingekuwa ni letu sote yanii wasanii wote tungeungana Bongo Movie wote au na wasanii wa muziki kwanini hawapo? au kuna kitu,” alisema Bella.

Steve Nyerere ni kati ya wasanii wa filamu ambao wamepinga harakati hizo.

BENKI ya Dunia: Uchumi wa Tanzania Utakuwa..!!!

$
0
0

BENKI ya Dunia imeitaja Tanzania kuwa miongoni mwa nchi saba za Afrika Kusini mwa Sahara zinazoonyesha ukuaji wa juu wa uchumi kwa mwaka 2015-2017.

Benki hiyo imesema nchi hizo zinazoendelea zimeonyesha ustahimilivu wa kiuchumi, zikisaidiwa na mahitaji ya ndani ambapo viwango vya ukuaji kwa uchumi wake kwa mwaka ni juu ya asilimia 5.4.

Kwa mujibu wa taarifa ya Benki ya Dunia kwenye ripoti yake iliyotolewa jana kupitia Jarida la Africa Pulse, nchi nyingine za ukanda huo zilizo na ukuaji uchumi unaofanana na Tanzania ni Ivory Coast, Ethiopia, Kenya, Mali, Rwanda na Senegal.

“Wakati nchi zikielekea kwenye marekebisho ya sera za fedha, tunahitaji kulinda mazingira sahihi ya uwekezaji ili nchi za Afrika Kusini mwa Sahara ziweze kupata ukuaji imara,” alisema Albert Zeufack, Mchumi Mkuu wa WB Kanda ya Afrika.

Jarida hilo limeenda mbali na kubainisha kuwa uchumi wa nchi hizo unarudi katika kukua kuanzia mwaka 2017, baada anguko baya zaidi kwa zaidi ya miongo miwili liliotokea mwaka 2016.

Ripoti ya jarida hilo ambalo huchapisha uchambuzi wa hali ya uchumi mara mbili kwa mwaka kupitia Benki ya Dunia (WB) ilisema nchi hizo zina takribani asilimia 27 ya idadi yote ya watu wa kanda na zina asilimia 13 ya Pato Ghafi la Taifa la kanda.

Halikadhalika ripoti hiyo imebainisha kuwa mwelekeo wa uchumi wa dunia unaboreka na utaweza kusaidia kurudisha ukuaji katika kanda.

Jarida hilo linaeleza kwamba ukuaji jumla wa bara unatarajiwa kupanda hadi asilimia 3.2 mwaka 2018 na asilimia 3.5 mwaka 2019, ukiakisi uchumi unaorejea kwenye hali ya kawaida katika chumi kubwa zaidi.

Pia ripoti hiyo inabainisha kuwa ukuaji uchumi utaendelea kuwa mdogo katika nchi zinazouza mafuta nje, wakati nchi zinazouza madini za chuma zinatarajiwa kushuhudia ukuaji wa wastani.

“Ukuaji wa Pato Ghafi la Taifa katika nchi ambazo chumi zake hazitegemei sana madini utaendelea kuwa imara, ukisaidiwa na uwekezaji kwenye miundombinu, sekta za huduma stahimilivu, na kufufuka kwa uzalishaji katika kilimo. Hali hii ni dhahiri kwa nchi za Ethiopia, Senegal, na Tanzania,” ilisema taarifa.

Ripoti hiyo iliweka bayana kuwa kubana zaidi kwa masharti ya fedha duniani kuliko ilivyotarajiwa, maboresho hafifu katika bei za bidhaa na tishio linaloongezeka la sera za kulinda viwanda vya ndani linalotokana na hisia za umma ni hatari zinazoweza kuukumba mwelekeo wa kanda hiyo kiuchumi.

Ilisema kwa upande wa ndani, hatari zinazoweza kuukumba hivyo kurudia ukuaji wa chini wa uchumi ni kasi ndogo ya mageuzi,  kuongezeka kwa vitisho vya usalama na wasiwasi wa kisiasa kabla ya uchaguzi katika baadhi ya nchi.

“Tunahitaji kutekeleza mageuzi ambayo yanaongeza tija ya wafanyakazi wa Kiafrika na kujenga mazingira tulivu ya uchumi mkuu. Kazi bora zaidi na zilizo na tija ni muhimu katika kupambana na umasikini katika bara,” alisema Zeufack.

Alisema mazingira ya ukuaji dhaifu wa uchumi yanakuja wakati bara linahitaji sana kufanya mageuzi ambayo ni muhimu kuinua uwekezaji na kupambana na umasikini.

Mchumi mkuu huyo alisema nchi zinatakiwa kutekeleza maendeleo yanayohitaji fedha nyingi na wakati huo huo kuepuka kuongeza deni la taifa hadi viwango visivyo endelevu.

Alisema katika mazingira hayo, kukuza uwekezaji wa sekta za umma na binafsi, hususani katika miundombinu, ni kipaumbele. “Kanda ilishuhudia mdororo katika ukuaji wa uwekezaji kutoka takribani asilimia 8 mwaka 2014 hadi asilimia 0.6 mwaka 2015,” alisema.

“Wakati viwango vya umasikini vikiwa vingali juu, kufufua kasi ya ukuaji ni muhimu,” anasema Punam Chuhan-Pole, Mchumi Kiongozi wa Benki ya Dunia na mwandishi wa ripoti hii.

Alisema ukuaji unahitaji kujumuisha watu wengi zaidi na utahusisha kukabilina na mdororo katika uwekezaji na gharama za juu za kufanya biashara ambavyo vinazuia uwezo wa kushindana.

MASOGANGE Matatani, Mahakama Yaagiza Akamatwe..!!!

$
0
0


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imetoa hati ya kukamatwa Msanii Agnes Gerald Waya maarufu kama Masogange (28), baada ya kushindwa kufika mahakamani mara kwa mara ya pili kesi yake ilipopangwa kutajwa.

Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Wilbroad Mashauri ametoa amri hiyo baada ya upande wa Jamhuri kudai kuwa kesi hiyo ilipangwa kutajwa lakini mshtakiwa, wadhamini na wakili wa utetezi wote hawakuwepo mahakamani.

Wakili wa Serikali Adolf Nkini alidai kuwa kesi hiyo ilipangwa kutajwa lakini kwa sababu mshtakiwa na wadhamini wake hawakuwepo mahakamani kwa mara ya pili, aliomba hati ya kukamatwa mshtakiwa.

Hakimu alisema kwa sababu mara mbili mfululizo mshtakiwa ameshindwa kufika mahakamani kusikiliza kesi yake bila taarifa mahakama yake inatoa hati ya kukamatwa kwake.

Masogange anakabiliwa na mashtaka mawili ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam.

Katika kesi hiyo namba 77 ya mwaka 2017, Masogange anadaiwa kuwa kati ya Februari 7 na 14,2017 katika maeneo yasiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin (Diacety Imophine).

MREMA: JPM Niruhusu Kutoa Wafungwa Wafichue Wauaji..!!

$
0
0

MWENYEKITI wa Bodi ya Parole, Agustino Mrema, amemwomba Rais John Magufuli amruhusu kutoa wafungwa wenye sifa ya kupata msamaha kutoka bodi hiyo ili wamsadie kufichua majambazi wanaopora na kuua Polisi.

Pia alisema ana imani majambazi wengi wanaoendesha matukio ya uhalifu wametokea magerezani au watakuwa na uhusiano na wafungwa.

Mrema alitoa ombi hilo baada ya kumalizika kwa msiba wa ndugu yake kijijini kwake Kiraracha Marangu mkoani Kilimanjaro.

Alisema kuwa ipo kampeni mbaya ya kumchafua Rais Magufuli katika utawala wake unaofanywa na wahalifu.

"Kwa uzoefu nilionao kuna kampeni chafu ya kumchafua Rais Magufuli ili nchi isitawalike kwamba hata majambazi wanaweza kuua askari hivyo kuna kila haja ya kuwashirikisha wafungwa katika tukio hili ili watisaidie kufichua,"alisema.

Aliongeza kuwa watu wabaya wasioridhika na uongozi wa Rais Magufuli wanafanya kila mbinu kwa ajili ya kumchafua ikiwemo kufadhili vikundi vya uhalifu vinavyohatarisha amani ya nchi.

Mrema alisema ili kukomesha matukio hayo ni vema Rais akaruhusu bodi yake iwakamate na kuwapunguza wafungwa magerezani hasa wale wenye makosa ya kushindwa kulipa faini ili waweze kufichua wanaohusika na uhalifu huo.

Pia alimtaka Rais kuthibiti watu wanaoleta chokochoko za maneno dhidi yake wachukuliwe hatua kwani wameonesha dhahiri hawapendeziwi na utawala wake kwani ndiyo pia wamekuwa wakifadhili matukio hayo.

Mrema alimpongeza Rais Magufuli kwa kumchagua kuwa mwenyekiti wa bodi hiyo kwani amejipanga kumsaidia kwa nguvu zote bila kujali maslahi binafsi na hadi sasa amekuwa hazifanya kazi hizo bila malipo yoyote na hana mpango wa kumdai isipokuwa atakapoona umuhimu wa kumlipa upo.

AMWAGIWA Tindikali Kisa Mapenzi...!!!

$
0
0

MATUKIO yanayohusiana na mapenzi yameendelea kuwa tishio nchini baada ya mwanamke mmoja, Helen John (25) kumwagiwa tindikali na mpenzi wake na kumfanya jicho lake lisione.

Hellen ambaye ni mkazi wa kijiji cha Kwamhosi kata ya Nkumba wilayani Muheza mkoani Tanga, alipata mkasa huo Aprili 17, mwaka huu.

Akizungumza na Nipashe , alisema chanzo cha tukio hilo ni baada ya kukosana na mpenzi wake huyo na kufanya kuishi tofauti bila mawasiliano hadi siku ya tukio ingawa walikuwa wamezaa mtoto mmoja.

Hellen alisema siku ya tukio kijana huyo aliyemtaja kwa jina la Ally Khamis alikwenda nyumbani kwao kwa lengo la kumbembeleza kurudiana lakini alikataa kwa madai kuwa hataki kuishi na mwanaume huyo kutokana na vitendo vya ukatili ambavyo amekuwa akimfanyia.

Alisema baada ya kukataliwa kijana huo usiku alikwenda kumuwmwagia tindikali machoni na kisha kukimbia lakini ulifanyika msako kwa wanakijiji na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa na kupelekwa katika kituo cha polisi Muheza.

Credit - Nipashe

BUNGENI Leo..Mwakyembe Aibuka na Hoja Mpya kuhusu Lowassa Kuhusika na Richmond...!!!

$
0
0

Sakata la Richmond  limechukua sura mpya Bungeni mara baada ya Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari na Mbunge wa Ubungo, Said Kubenea (Chadema) kumtuhumu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe kuwa hakutenda haki wakati alipokuwa akishughulikia suala hilo.

Wabunge hao kwa pamoja wamemtuhumu Waziri huyo kwa kusema kuwa wakati akiongoza Kamati Teule ya Bunge kuchunguza Kamapuni tata ya ufuaji umeme kuwa haikumtendea haki aliyekuwa Waziri Mkuu wa kipindi hicho, Edward Lowassa kwakuwa hakumpatia muda wa kumhoji kitu ambacho kilipelekea kujiuzuru.

Aidha, akijibu hoja hizo Waziri Mwakyembe amesema kuwa kama kuna mtu yeyote ambaye ni jasiri wa kurudisha suala hilo bungeni afanye hivyo ili aweze kulishughulikia kikamilifu na kuamaliza utata.

“Naomba nimalizie kwamba, mimi naahidi kwamba siku ambayo kuna mmoja atakuwa jasiri wa kuleta suala la Richmond hapa, nitamuomba Rais anipumzishe Uwaziri ili niweze kuishughulikia kesi hiyo kikamilifu,”amesema Mwakyembe.

Hata hivyo, ameongeza kuwa Wapinzani watakuwa na kazi kubwa sana kuweza kumsafisha mtu ambaye alikuwa ni mtuhumiwa kwa kuwa wengi hawajui undani wa suala hilo.

LORD Eyes Aamua Kuwachana Weusi Live Bila Chenga...

$
0
0

Msanii wa muziki wa hip hop ambaye aliyekua katika Kundi la Weusi, Lord Eyes, amefunguka mengi kuhusu kundi hilo baada ya kuonekana kufanya kazi peke yake. 

Kundi hilo ambalo lilikuwa likiundwa na wasanii 5, Joh Makini, Nikki wa Pili, G Nako, Bonta pamoja na Lord Eyes, limebaki na wasanii watatu tu ambao ni Joh Makini, Nikki wa Pili na G Nako pekee. 

Akiongea katika kipindi cha XXL cha Clouds FM wiki hii, Lord Eyes amesikika akidai kundi hilo limejaa utengano, ubinafsi na wivu. 

“Hatujawahi kuwa kwenye crew,” alisema Lord “Tuliungana kutanua wigo lakini sio kwa mkataba wala chochote. Weusi ni kampuni. Watu wanasema kila siku, ni kundi lakini ni kampuni, na ndio maana kumekuwa na utengano, ubinafsi na wivu,” 

Pia rapa huyo alisema kila msanii wa kundi hilo anamiliki hisa za asilimia 20 ya kampuni hiyo. 

“Kuna maceo watano ndani ya Weusi na kila mtu alikuwa ana share yake, yaani asilimia 20 kila mmoja. Hii asilimia 20 kila mtu ameifanyia kazi, kwa sababu wigo ambao tulitaka kutanua ni kwenda mbele zaidi, tuwe na nguvu kwani umoja ni nguvu, lakini haikuwa hivyo. Imekuwa kama Weusi ya River Camp,” alisema Lord. 


Lord Eyez pia aliachia wimbo wake mpya ‘Hela Yangu’, aliyoifanya chini ya msaada wa Barakah The Prince.

RAIS Magufuli Afanya Uteuzi Mpya...

$
0
0

UKULU, DAR: Taarifa kutoka kwa Katibu Mkuu Balozi Kijazi zinasema Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Kamishna Msaidizi wa Uchimbaji Mdogo, Mhandisi Benjamin Mchwampaka kuwa Kamishna Mkuu wa Madini.

Kabla ya hapo alikuwa Kamishna Msaidizi wa sehemu ya uchimbaji mdogo wa madini. Aidha uteuzi wake umeanza tarehe 19 April, 2017.

Wakati huo huo Rais amemteua Adelarnus Kilangi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli(Petrolium Upstream Regulatory Authority - PURA). .

Aidha Bi. Kilangi alikuwa Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino Tanzania(SAUT) Kampasi ya Arusha. Pia uteuzi wake umeanza tarehe 19 April, 2017.
Viewing all 104793 articles
Browse latest View live




Latest Images