Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 109660 articles
Browse latest View live

Raia wa Ukraine aliyekwama Visiwani Zanzibar asimulia yaliyomkuta

$
0
0


"MAISHA ya hapa Zanzibar ni mazuri sana kuliko ambayo ningeendelea kuishi nyumbani kwetu Kiev (Ukraine)," Vladyslava Yanchenko (23), raia wa Ukraine anasimulia utofauti wa maisha ya Zanzibar na nchi aliyotoka.
Vladyslava ambaye sasa anaishi Kijiji cha Kizimkazi Dimbani, Mkoa wa Kusini Unguja baada ya kukwama kurejea kwao kutokana na vita, anaendeleza simulizi ya ushuhuda wake, akitamka:

"Kwa kuishi hapa Zanzibar nimejua kufua, kulima na kujipikia. Kule kwetu Kiev zinasikika sauti za mabomu na risasi, hakuna amani, muda wote ni wasiwasi."

Binti huyo ni miongoni mwa watalii 1,200 ambao wakati vita inatokea, walikuwa visiwani Zanzibar kwa shughuli za utalii. Baadhi waliondoka kwenda maeneo mbalimbali duniani na wengine walibaki na kusaidiwa na serikali kupata visa na sehemu za kuishi.

Vladyslava alipata unafuu kuwa siku za nyuma katika safari zake za utalii, alipapenda Zanzibar na kununua ardhi kwa ajili ya uwekezaji, hivyo kulipotokea vita, alijenga nyumba ya kawaida kwenye eneo lake na ndiko anakoishi kwa sasa.


Anasema katika maisha yake hakuwahi kufikiri kuna siku angeishi kijijini kwenye maisha ya kawaida kabisa ya Kiafrika na akamudu kujipikia, kufua na kulima mazao yanayomsaidia, lakini imetokea na sasa amekuwa swahiba wa wenyeji wa Zanzibar.

Vladyslava, katika mazungumzo mahususi na Nipashe visiwani Zanzibar, anasema kwa sasa ameshakuwa mwenyeji na anaendesha biashara zake mtandaoni na kujipatia kipato cha kuendesha maisha yake.

Anasema anafurahi maisha yake mapya kwenye eneo lisilo na msongamano na shughuli nyingi kama ilivyo Kiev.


"Nimepita kipindi kigumu sana cha maisha, msongo wa mawazo uliniandama, niliikumbuka sana familia yangu, kuna wakati hadi nilikuwa ninaumwa kila nikiwakumbuka wazazi wangu, bibi yangu mwenye umri wa miaka 72 na ndugu zangu wengine, nimelia kwa muda mrefu sana, sijaweza kuwasiliana nao kwa muda mrefi hadi hivi karibuni nilipoanza kuongea nao kwa WhatsApp.

"Vita ni mbaya sana, watu wanafikiri Ukraine ni mji mdogo, lakini ni nchi yenye watu zaidi ya milioni 43.8, lakini tumevamiwa na kuharibiwa maisha yetu na nchi yenye watu zaidi ya milioni 143.4, athari ni kubwa sana hasa tukizingatia watu wengi hawana hati za kusafiria," anasema.

Vladyslava anasema alitua visiwani Zanzibar kwa ajili ya mapumziko lakini alishindwa kurejea Ukraine kutokana na vita hiyo, akalazimika kujifunza maisha ya wenyeji, akipokewa na raia wa Ujerumani ambao aliishi nao kwa muda baadaye akaamua kwenda kuishi kwake kwenye nyumba ya matofali ya udongo aliyojenga.

"Ninayafurahia maisha ya hapa kwangu, kwa sasa Ukraine hali ya hewa ni nyuzi joto sita hadi 12, kuna baridi kali sana pia chakula ni cha shida kutokana na vita. Hapa (Zanzibar) nina uhakika wa maisha, watu wanaishi maisha ya kawaida sana lakini ya amani, ninapata chakula, nimelima mapapai nimevuna.


"Hali ya Ukraine ni ngumu sana, watu hawana chakula, mali zimeharibiwa, wengi wako nyumbani hawana uhakika wa maisha. Kuishi hapa Zanzibar kuna ahueni kubwa ingawa muda wote mawazo ni kwa familia yangu.

"Ninapenda hali ya hewa ya hapa, nilikuwa sijui kupika lakini sasa ninapika, tena kwa gesi ya kawaida, sikuwahi kufua kwa mikono, nilifua kwa mashine, sikutarajia nitaishi kwenye nyumba isiyo na umeme wala maji na miundombinu ya kisasa.

"Nilikuwa sijui kutafuta maji lakini sasa ninatafuta maji, ninaishi maisha ya Kiafrika. Kuna wakati ninapitia maisha magumu sana, sina kipato chochote, ninasaidiwa na majirani, ninachofurahia ni amani niliyonayo, sisikii sauti za mabomu," anasema.

Vladyslava anainyoshea kidole Russia kwa anachokiita kuharibu kwa makusudi maisha ya zaidi ya watu milioni 43, akiitaja familia yake kwamba mdogo wake mwenye umri wa miaka 15 sasa anaishi Uswisi kama mkimbizi.


KUNUNUA NYUMBA

Binti huyo anasimulia maisha yake kwamba mwaka 2020 aliingia nchini kwa ajili ya likizo na kusherehekea siku yake ya kuzaliwa na alipapenda Zanzibar na kumwambia baba yake ambaye alimruhusu anunue ardhi.

Alirejea Zanzibar kwa ajili ya likizo nyingine Februari mwaka huu na wakati anajiandaa kuondoka, wakapata taarifa, Russia imeivamia kivita nchi yao.

"Niliwasiliana na baba aliniambia yeye atabaki Ukraine kupigania nchi yetu. Aliniambia nibaki Zanzibar, nisirudi Ukraine kutokana na hali iliyoko, haikuwa rahisi kwangu, tangu Februari hadi Juni nilikuwa ninalia tu kila siku, nimepoteza kila kitu kuanzia nyumba niliyokuwa nimepanga na ofisi ya kampuni yangu, sina ndugu hapa nilipo ila nina Watanzania ambao wamekuwa watu wema kwangu muda wote," anasema.

Vladyslava anasema majirani wanampenda, hasa watoto ambao wakitoka shuleni wanakwenda nyumbani kwake kuongea naye.

"Ninapenda sana watoto hadi ninafikiria baadaye nifungue kituo cha kulea watoto, nina marafiki wengi na ninajulikana," anasema.


Vladyslava anabainisha kuwa alipokuwa Ukraine, alikuwa anaishi maisha yake mwenyewe mbali na wazazi wake na alifungua kampuni inayotoa ushauri wa kibiashara na ujasiriamali na kumpatia fedha nyingi.

"Nilifungua kampuni nikiwa na miaka 19, ilikuwa inafanya vizuri sana, nilipata fedha nyingi lakini kutokana na vita biashara yangu iliharibika yote, nilikuwa na ndoto kubwa sana," anasema.

APATA MCHUMBA

Vladyslava anasema amepata mchumba ambaye ni Mzanzibar na amemwomba wafunge ndoa, lakini anafikiria kama yuko tayari kuishi maisha ya familia na kuwa na watoto.

"Ameniomba anioe ila bado ninafikiria kwa maisha niliyonayo ninaweza kulea mtoto? Watoto wana mahitaji mengi sana, ni lazima nijiandae kuwasaidia ipasavyo, ni lazima nifikirie kwa kina kabla ya kuwa na familia, ni uamuzi mgumu ambao lazima niufanye kwa uangalifu.

"Tumeshaongea, tumebaki kuwa marafiki wakati ninaendelea kutafakari uamuzi wangu, ameniambia anasubiri niamue," anasema Vladyslava na kusita kutaja jina la kijana huyo.  

MAJIRANI WANENA

Ibrahim Rashid, jirani wa Vladyslava, anasema kuwa kijijini kwao ni umbali wa zaidi ya saa moja kutoka mjini Unguja na walimpokea raia huyo na kuishi naye kwa kumsaidia mahitaji ya msingi kutokana na nyumba yake kutokuwa vizuri.

"Awali ilikuwa vigumu sana kuishi naye, alikuwa na msongo wa mawazo, ilikuwa kazi kuzoea watu wengine na hasa maisha yetu haya, nilimsaidia kutafuta mafundi waelewa kujenga kibanda chake kwa kuwa kuna wakati ana fedha na wakati mwingine hana.

"Siku nyingine alikuwa anakuja kuishi kwangu, anataka kuchaji simu zake, lugha haikuwa shida sana kwa sababu nami shughuli zangu ni za utalii, hivyo ninaijua kiasi.

"Nilimpa mtungi wa gesi na mahitaji mengine, siku ninacho namsaidia, siku sina ninamwambia leo sina," anasema Rashid na kubainisha kuwa jirani yake huyo alipanga kujenga jengo la hadhi kubwa lakini akaamua kujenga kibanda kutokana na kukosa fedha.

Mmoja ya wanakijiji wa Kizimkazi, Hassan Ali anasema wanaishi vizuri na Vladyslava na kumwelezea kama binti anayependa kujichanganya na wanakijiji.

Mkurugenzi Uratibu wa Shughuli za Utalii kutoka Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Omar Suleiman Mohammed anasema kulikuwa na raia wa Ukraine 1,200 waliokuja kwa shughuli za utalii ambao wakati vita vinatokea nchini mwao walikuwa visiwani Zanzibar.

Mohammed afafanua kuwa wakati vita vinaendelea, wengi wao waliondoka na kuelekea mataifa mbalimbali ya Ulaya kwa gharama zao, sita walisaidiwa usafiri na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na 12 wamebaki Zanzibar.

"Kati ya hao 12, wapo waliokodi nyumba na wengine wamepewa hifadhi na serikali inawasaidia gharama za viza ili kuendelea kubaki nchini," anasema.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa (UN), vita vya Ukraine na Russia vilivyoanza Februari mwaka huu, vimesababisha zaidi ya raia milioni 6.3 kuikimbia Ukraine

Hatari Mikopo ‘Kausha Damu’

$
0
0



Ongezeko la taasisi zinazotoa mikopo ‘chap chap’ yenye riba kubwa na kugeuka machungu kwa wakopaji, imeelezwa kuwa chanzo cha msongo wa mawazo kwa mdaiwa, kufariki kwa shinikizo la damu au kukimbia kusikojulikana.

Dar es Salaam. Ongezeko la taasisi zinazotoa mikopo ‘chap chap’ yenye riba kubwa na kugeuka machungu kwa wakopaji, imeelezwa kuwa chanzo cha msongo wa mawazo kwa mdaiwa, kufariki kwa shinikizo la damu au kukimbia kusikojulikana.


Mikopo hiyo iliyopachikwa jina la ‘kausha damu’ kutokana na maumivu wanayopata wakopaji wakati wa kurejesha fedha, baadhi ya taasisi zimekuwa zikitoa masharti magumu, ikiwamo kutaifisha mali zikiwemo nyumba, magari na samani za ndani endapo mhusika atashindwa kulipa kwa wakati.



Uchunguzi uliofanywa na Mwanachi umebaini kuwa wanaoshindwa kurejesha mikopo kwa wakati, wamejikuta mali walizoweka kama dhamana zikitaifishwa na kuuzwa katika mazingira yasiyotoa fursa kuweza kupinga uuzwaji wa mali zao hizo.


ALSO READ

Mtoto anapenda soka? Njia sahihi za kumlinda

Makala 6 hours ago

Kampeni zapamba moto uchaguzi UWT

SIASA 6 hours ago



Taasisi ya mikopo yaeleza


Mtendaji wa Kampuni ya Jojo Microfinance iliyopo Pugu Bombani, Alice Zebedayo alisema unapotaka kuchukua mkopo huo lazima ununue fomu kwa Sh5,000 kwanza ili usajiliwe kisha hatua zifuate.


Akizungumza na Mwananchi, Alice alisema fomu hiyo ikisharudishwa anayekopa anatakiwa atoe Sh5,000 nyingine ili viongozi wa kampuni hiyo wanapokwenda kumtembelea nyumbani kwake waangalie samani za ndani vitakavyowekwa dhamana ya mkopo husika.


“Kama ukichukua Sh100,000 utapewa Sh90,000 baada ya kukatwa Sh5,000 ya fomu na Sh5,000 ya kukutembelea nyumbani kwako ili kuangalia vitu vitakavyowekwa dhamana; halafu riba ya mkopo ni Sh30,000, hivyo unatakiwa ulipe Sh130,000 kwa mwezi mmoja,” alisema Alice.


Akifafanua namna ya kulipa, alisema mtu anapochukua Sh100,000 kila siku anatakiwa kulipa Sh4,300, “na ndani ya mwezi mmoja awe amemaliza na akikosa siku moja kulipa faini ya Sh2000 itamhusu kwa kukiuka.


“Kwa anayechukua Sh50,000 atalipa Sh65,000 na riba na kila siku anatakiwa atoe rejesho la Sh2,200 na akikosa siku moja anatakiwa alipe faini ya Sh2,000 na inategemea, siku zikiwa nyingi na hela hiyo inazidi kuwa kubwa.”


Alisema ukiwa mlipaji mzuri wa marejesho hayo hata kama utahitaji kukopa Sh1 milioni unapewa, lakini riba yake ni asilimia 30. “Tutakubaliana kila siku utoe marejesho shilingi ngapi ndani ya mwezi mmoja, ni makubaliano.”

Kanuni ya mkopo ikoje?

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili jijini Dar es Salaam, umebaini kuwepo kwa kasoro nyingi katika baadhi ya wakopeshaji, ujanjaujanja wa kucheza na maneno ya mkataba huku wengi wao wakiweka riba kubwa zinazotakiwa kulipwa ndani ya kipindi kifupi.


Pia, umebaini wapo watu binafsi wanatoza riba hadi asilimia 30 kwenye mikopo hiyo kwa mwezi, vinginevyo mkopaji hupigwa faini kabla ya adhabu nyingine.


Kwa mujibu wa kanuni za mkopo midogo ya mwaka 2019 kifungu cha 37, kinamtaka mkopeshaji kutunga sera ya mikopo ikieleza mchakato wa ukopeshaji na nyaraka, masharti ya kukopa, aina ya mikopo na dhamana inayokubalika. Mengine ni pamoja na ukomo wa mkopo kwa kila mkopaji, vipindi vya mkopo na masharti kama riba, ada na changizo na malipo ya mara kwa mara.


Pia, sera hiyo inatakiwa kuonyesha mchakato wa kuidhinisha mkopo, uwezo wa mkopaji, ufuatiliaji na uthaminishaji na kipindi cha neema kama itawezekana.


Wanachosema wakopaji


Waathirika wakubwa wa mkopo huo ni wanawake ambao wamekuwa wakiishia kufilisiwa mali zikiwemo samani za ndani kama vitanda, majokofu, luninga pamoja na vyombo vya kupikia.


Mfanyabiashara katika Soko la Kitunda, Salama Hussein alisema yeye ni mmoja wa walioathirika na mkopo wa ‘kausha damu’ baada ya kukopa Sh200,000 ambayo riba yake ni Sh60,000 ndani ya mwezi mmoja.


Salama alisema kabla ya kupewa mkopo huo aliotakiwa kurejesha jumla ya Sh260,000, alinunua fomu ya kujiunga Sh10,000 na alitakiwa atoe Sh5,000 wakati alipotembelewa nyumbani kwake na maofisa wanaotoa mkopo ili waangalie vitu vya ndani vitakavyowekwa kama dhamana.


Alisema kutokana na shida aliyokuwa nayo alilazimika kuchukua Sh185,000 baada ya Sh15,000 kukatwa kwenye fomu na kutembelewa nyumbani.


Salama alisema kila siku alikuwa anarejesha Sh8,000, wakati mwingine alikuwa anakosa hela na kutakiwa kulipa faini ya Sh2,000 kwa siku ambayo hapeleki rejesho.


“Kutokana na ugumu wa maisha, biashara yangu ilikufa kwa sababu mkopo niliochukua umerudi kwa walionikopesha, kila siku nilikuwa natoa Sh8,000 bado sijapigwa faini ya Sh2,000 nikikosa kurejesha,” alisema alisema Salama.


“Kuna siku moja nilikuwa nalaza hadi siku tatu nalipa Sh6,000, kutokana na msingi wangu kuwa mdogo ulikufa, hela ya matumizi nayo nilikuwa nachukua kwenye biashara yangu.”


Mfanyabiashara wa Soko la Kigogo, Aisha Salehe alisema alikopa Sh50,000 kwenye taasisi moja ya kukopesha fedha kwa lengo la kuongezea mtaji katika biashara yake, lakini matokeo yake alichukuliwa godoro na sasa analala chini.


Aisha alisema aliambiwa atoe Sh5,000 kwa ajili ya fomu, Sh5,000 za kutembelewa na maofisa wanaotoa mkopo na amana ya mkopo alitoa Sh10,000.


Alisema riba aliyotakiwa kutoa ni Sh15,000, jumla ya fedha anazotakiwa kurejeshwa kwa mwezi Sh65,000 na kila siku alikuwa anatakiwa kutoa Sh2,200 kwa ajili ya rejesho.


“Ukichukua Sh200,000 lazima ulipe pamoja na riba, kila siku ‘kausha damu’ unatakiwa upeleke Sh4,300 na ukituma lazima utume na ya kutolea, usipotoa kwa siku moja faini yake ni Sh2,000 na hela yenyewe wanakupa Sh175,000 baada ya kukata fedha ya fomu, amana na wanapokutembelea nyumbani kwako.”


Aisha alisema kuna wengine wanachukua hadi Sh1 milioni, riba ya mkopo huo ni asilimia 30 nayo unalipa ndani ya mwezi mmoja, kila siku unatakiwa utoe Sh40,000 kama rejesho na usipotoa kwa siku faini yake ni Sh20,000.


Serikali ya mtaa yanena


Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Pugu Bombani ambako baadhi ya wananchi wamelalamikia mikopo hiyo, Amanzi Bundala alisema ‘kausha damu’ katika mtaa wake vikundi vinavyokopesha vipo vingi na vimekuwa kero kwa wananchi wake.


“Mtu akichukua Sh50,000 kuna mambo mawili, la kwanza analipa kila siku Sh2,500 na ya pili wanatoka kwenye uhalisia wa biashara, kisha zinakuwa ngumu; hebu fikiria leo hii mtu akichukua Sh50,000 kwa ajili ya kujikwamua kibiashara haiendi kama alivyotarajia, matokeo yake vyote vinachukuliwa na huyo mkopeshaji,” alisema Bundala.


Hata hivyo, alisema amebaini wanaotoa mikopo hiyo baadhi yao hawana vibali, jambo ambalo ni tatizo kwa kuwa nchi inakosa mapato na Serikali ya mtaa huo hawapati chochote.


Machungu mengine ya mkopo huo yanasimuliwa na mkazi wa Tabata, Ibrahim Abdalla kwa kusema, “mimi nilikopa Sh500,000 kwa mtu binafsi na kila Sh100,000 riba ni Sh30,000 kwa mwezi, aise! Nilikuwa na shida, lakini maumivu yake ni makali sana.


“Kutokana na riba kuwa kubwa, nilijikuta deni linafika zaidi ya Sh1 milioni, kuna nyakati nilishindwa kulipa mkopo na kubaki kulipa riba tu, kwa hiyo hii ni changamoto sana ya mikopo umiza,” alisema Abdalla.


Mkopaji, mkopeshaji nani tatizo?


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kutetea Haki za Wanawake (HDO), Prisca Ngaeshemi alisema wanaochukua mkopo wa ‘kausha damu’ ni wajasiriamali wa chini, wakiwamo mamalishe, wauza vitumbua na mbogamboga.


Prisca alisema wanawake hao wanapochukua mkopo urejeshaji wake ni shida, huku akitolea mfano anayechukua Sh200,000 kila siku anatakiwa atoe Sh8,000, “biashara gani inayomfanya apate faida ya kupata hela hiyo.”


Alisema matokeo yake mtaji unakufa kwa sababu hela hiyo hiyo inampasa atoe ya matumizi ya nyumbani na nyingine kwa jili ya marejesho ya kila siku.


Hata hivyo, Wakili John Seka alipoulizwa kuhusu utendaji wa kampuni hizo, alisema kuna faida ya kila mkopo, huku akieleza wanaokopa huko na kutatua shida zao, ndiyo wanajua umuhimu wake na huenda tatizo likawa ni wateja.


Alisema kabla ya kuangalia uvunjaji wa sheria ni vyema kuangalia hatari kiasi gani wanabeba watu hawa wanaokopesha mikopo hiyo.


“Licha ya mikopo yao kutoka ndani ya muda mfupi, lakini (mkopaji) hana uhakika kama wanatumia muda wa kutosha kufanya ufuatiliaji wa mtu wanayemkopesha kama inavyofanywa na benki,”alisema wakili huyo.


“Benki ukiomba mkopo watakufanyia ufuatiliaji wa vitu vingi ili kujiridhisha kuwa wanayekwenda kumpa mkopo wao atarudisha, lakini hawa wanaweza kukupatia mkopo kwa kutumia kadi ya gari, hawakagui gari ni nzima kiasi gani kama inaweza warudishia pesa zao ila wanakuamini.”


Madalali wafunguka


Potess Moshi kutoka Mem Auctionineer and General Broker Limited alisema kuna tatizo la watu wanaochukua mikopo kutojua wanaenda kufanya nini na kama walikuwa na wazo, tayari hubadilika baada ya kupata fedha.


“Mtu anachukua mkopo anafanya rejesho moja halafu haonekani, sasa hatujui kama ni kwa sababu ya riba kubwa au biashara kuanguka,” alisema Moshi.


Alisema wengine hadi wanapewa mkopo wanakuwa na hela pungufu tofauti na iliyopo kwenye fomu kwa sababu wanatoa rushwa ili waonekane wana vigezo.


Dalali huyo alisema hali hiyo imewafanya kwa mwaka kuwa na uwezo wa kuletewa hadi dhamana 50 za wateja ili ziwekwe sokoni huku akieleza wakati mwingine zinashindwa kuuzika kutokana na uthamini wake kuwa tofauti.


“Kuna dhamana nyingine zinakuja zikiwa zimethaminiwa kwa gharama kubwa, lakini mteja akija kuangalia thamani yake haiendani hivyo haziuziki,” alisema Moshi.


Pia, alisema kwa mwaka unaweza kupata hata dhamana za watu 50, huku akieleza kuwa wingi wa madalali umechangia kazi kugawanywa.


Scholastica Kevela, ambaye ni Mkurugenzi wa Yono Auction Mart alisema kwa mwaka wanaletewa zaidi ya mali 100 za wateja ambao wameshindwa kulipa madeni yao kutoka taasisi za kifedha na Vyama vya Kuweka Akiba na Kukopa (Saccos).


“Kati ya hizo ndani yake ndiyo kuna nyumba, viwanja, kitu chochote alichoweka dhamana mteja,” alisema Scholastica.


Mkurugenzi wa Cops Auction Marts, Mohammed Mmanga alisema kwa miezi miwili wanaweza kupata hata nyumba 30 ambazo ni dhamana kutoka kwa taasisi za kifedha, ikiwamo benki mbalimbali.


Alisema kati ya nyumba hizo wanaweza wakauza au wasiuze hata moja kutokana na wateja kudanganya thamani ya fedha.


“Shida ni kuwa wakopaji wengi huwa hawasomi mikataba kwa sababu wana uhitaji wa hela, wakichukua mikopo wanafanyia kazi tofauti na walichoomba,” alisema Mmanga.


“Riba kubwa zipo kwa baadhi ya taasisi ila sio zote, wakopaji wanapaswa kujua wanakopa ili wafanye nini na wafanye kile walichokusudia, siyo kuchukua mkopo unaenda kumnunulia mke wako Iphone ya Sh3 milioni.”


Alipotafutwa Katibu wa Waziri wa Fedha na Mipango, Twaha Mwakioja alisema kwa mujibu wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2018 na Kanuni Zake za Mwaka 2019, biashara ya huduma ndogo za Fedha inasimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na wameweka ukomo wa riba, kiwango ambacho hakizidi asilimia 3.5 kwa mwezi.


“Kwa mujibu wa kanuni ya huduma ndogo za Fedha (majukumu ya waziri) ya mwaka 2019, wizara imeteua waratibu 212 kila mkoa na halmashauri, hivyo tunaomba nyaraka za mkopaji ikiwa ni mkataba wa mkopo ili tuweze kufuatilia na kuchukua hatua,” alisema Mwakioja.


Kauli ya BoT


Kwa mujibu wa taarifa ya BoT, wananchi wametakiwa kuepuka kukopa au kufanya biashara na taasisi, kampuni, mtu na watu binafsi ambao hawana leseni.


Hiyo ni baada ya kubaini kuna taasisi, kampuni na watu binafsi wanaojihusisha na biashara ya kutoa mikopo bila leseni, jambo ambalo ni kinyume na Kifungu cha 16(1) cha Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018.


“Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuutaarifu umma kuwa taasisi, kampuni na mtu binafsi wasio na leseni husika hawaruhusiwi kufanya biashara ya kukopesha,” inaeleza taarifa ya BoT.


“Kwa mujibu wa Kifungu cha 16(2)(a) cha Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018, hatua zitakazochukuliwa kwa ukiukaji wa sheria hiyo ni pamoja na faini isiyopungua Sh20 milioni au kifungo kwa muda usiopungua miaka miwili.


“Orodha ya taasisi, kampuni na watu binafsi wenye leseni za biashara ya kukopesha zilizotolewa na Benki Kuu ya Tanzania inapatikana kwenye tovuti ya Benki Kuu ambayo ni www.bot.go.tz.”


Mwananchi

Offer ya Viwanja, Bunju B na Mapinga, Bei Rahisi

$
0
0


Ofa ofa ofa...
Tunauza Viwanja bunju mwisho upande wa Mapinga km 4 kutoka main road.kwa sh 12000 tu kwa2 sqm moja sawa na sh 4,800,000 kwa kiwanja cha 20/20
Wahi haraka sana upate kiwanja na ujenge.
Piga simu namba 0758603077 kwa Maelekezo zaidi

Note: Kuja kuona Viwanja ni Bure kabisa

PROFESSOR JAY arejea baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu akipambania afya yake, aweka picha hii

$
0
0


PROFESSOR JAY arejea baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu akipambania afya yake, aweka picha hii

VIDEO1


Utafiti :Wanaume Wanapenda Wanawake Wenye Makalio Makubwa"

$
0
0

 


Je wajua kwanini wanaume wanawapenda wanawake waliojaliwa na makalio makubwa ?

Katika majarida mengi umewaona wanaume wakikodolea macho picha za wanawake wenye makalio makubwa iwe ni kim Kardashian, Jenipher Lopez Nicki Minaj na Vera Sidika kutoka Kenya .

Sasa basi Utafiti umedhibitisha kuwa ni kweli wanaume wanapenda wanawake waliojaaliwa sehemu ya nyuma.

Kulingana na utafiti wa chuo kikuu Bilkent , chuo kikuu cha Texas, na chuo kikuu cha American University kilichoko mjini Beirut

Wanaume wanakisia kuwa mwanamke mwenye makalio makubwa anaweza kufanya kazi kwa bidii zaidi ya mwanamke ambaye hana makalio makubwa.

Hata hivyo kinachowavutia wanaume si makalio haswa bali ni kupinda kwa uti wa mgongo unaosababisha tako kuonekana zaidi.

Utafiti huo unasema kuwa upinde wa 45.5 ndio unaovutia wanaume zaidi.

Wanaume walioneshwa picha za makalio ya wanawake wengi na asilimia kubwa iliwapendelea wanawake wenye makalio yaliyopinda kwa kiwango cha 45.5

Aidha zaidi ya asilimia 30% walisema wangalimchukua mwanamke mwenye makalio makubwa zaidi ya yule waliye naye sasa.

Kwa mujibu wa utafiti huo katika miaka ya awali mwanamke aliyeonekana kuwa na makalio makubwa alipendelewa kutokana na uwezo wake wa kubeba mizigo mgongoni.

Isitoshe mwanamke kama huyo aliwavutia wanaume wengi na hivyo kuwa na uwezo wa kuzaa watoto wengi.

Aidha mwanamke mwenye makalio makubwa angeweza kustahili uzito wa mtoto aliyebebwa tumboni na hata kustahilimi makali ya uzazi kuliko

Ukweli Kuhusu Kupata Watoto Mapacha na Jinsi Wanapatikana

$
0
0
Inasemekana kwamba haijalishi kama mume/mwenza wako ni pacha ama ametoka kwenye familia yenye historia ya mapacha. Mwenye uwezo wa kusababisha watoto mapacha ni mwanamke pekee. Ikiwa na maana mwanamke ambaye ni pacha ama ndugu zake wa kike kama vile dada, mama wana historia ya kuwa na mapacha ama wao ni pacha basi mwanamke huyo ana nafasi kubwa ya kupata watoto mapacha.

Kwa mfano: Mwanamke ambaye mke wa mjomba wake ana mapacha haimpi yeye nafasi ya kupata mapacha kwa sababu hana uhusiano na mke wa mjomba wake kibailojia. Ila mwanamke ambaye dada yake ana mapacha inampa uwezekano wa kupata watoto mapacha kwasababu wana uhusiano wa moja kwa moja.

Hembu tujifunze hatua moja baada ya nyingine. Kwanza tufahamu mimba inatungwa vipi? Na kisha tuone jinsi gani mimba ya watoto mapacha inavyotungwa.

Mimba inatungwaje?

Kipindi cha ovulation ndipo ambapo mwanamke anaweza kushika mimba. Ovulation ni kipindi ambacho yai kubwa ama yai lililo tayari hutoka kuelekea kwenye tumbo la uzazi kupitia mirija ya ovari. Yai hilo kwa bahati nzuri likikutana na mbegu ya kiume hurutubishwa katika kipindi cha masaa 24 (baada ya muda huo yai hupoteza uwezo wake). Iwapo yai litarutubishwa ndani ya muda huo na kisha kujikita katika mfuko wa uzazi basi mimba itakuwa imetungwa. Iwapo yai halikurutubishwa hutolewa nje kama damu ya hedhi.

Mapacha hutokeaje?

Hapa tukumbuke kuwa kuna mapacha wa aina mbili: Mapacha wanaofanana (Identical twins) na Mapacha wasiofanana (Fraternal twins). Mapacha wasiofanana hutokea pale mwanamke anapotoa mayai mawili kuelekea kwenye tumbo la uzazi. Hii ina maana ni mwanamke ama mwili wa mwanamke unaosababisha mayai mawili kuachiliwa kwa pamoja. Baada ya hapo mayai haya hukutana na mbegu za kiume ambapo hurutubishwa ndani ya muda maalumu na kisha hujikita kwenye mfuko wa uzazi. Hivyo basi hata kama mwanaume angetoa mbegu milioni moja lakini yai la mwanamke likitoka moja basi mtoto atakayepatikana atakuwa ni mmoja tu.

Huo ni upande wa mapacha wasiofanana (Fraternal twins). Kwa upande wa mapacha wanaofanana (Identical twins) hadithi ni tofauti kidogo. Baada ya yai kurutubishwa na mbegu ya kiume na kujikita kwenye mfuko wa uzazi kwa sababu zisizofahamika kisayansi huamua kujigawa na kutengeneza watoto mapacha. Mapacha hawa kwa kawaida hufanana sana na huwa ni wa jinsia moja tofauti na fraternal twins ambao huweza kuwa wa jinsia mbili tofauti ama jinsia moja.

Kutokana na maelezo hayo hapo juu inaonyesha kwamba watoto mapacha wanaofanana ama wasiofanana husababisha na mwanamke ambaye kwa sababu moja ama nyingine mwili wake huachilia mayai mawili ama hugawanya yai lake lililorutubishwa na kusababisha watoto mapacha. Japokuwa kumekuwa na mabishano makali ambapo watu wengine wamekuwa na maoni hususani kwa upande wa mapacha wanaofanana kwa kusema kwamba mbegu ya kiume huwa na nguvu zaidi na hivyo kugawanya yai. Sina uhakika na jambo hilo ila kwa tafiti nyingi zilizofanywa na wanasayansi zinasema mwanamke ndiye mwenye uwezo wa kusababisha watoto mapacha yeye ama ndugu zake wa kike (wanaohusiana kibaiolojia).

Sababu nyingine zinazoweza kuchangia watoto mapacha

1. Mwanamke anayetoka kwenye familia ambayo wanawake wana historia ya kupata mapacha.

2. Wanawake wenye asili ya kiafrika na kimarekani.

3. Wanawake wanaobeba mimba wakiwa na umri mkubwa, kuanzia miaka 35.

4. Wanawake wanene na wale warefu.

Hitimisho

Fatma Karume Afunguka "Wanafunzi Wamefeli Law School Alafu Mnapandisha Ada, Huo ni Wizi"

$
0
0



Fatma Karume ametoa maoni kuhusu taarifa ya Shule ya Sheria Tanzania (The Law School of Tanzania) kudaiwa kupandisha ada ya masomo akisema "Kiwango cha kufeli masomo kwa Wanafunzi wa Law School ni 95%, halafu eti wanapandisha ada. Ukiritimba usipodhibitiwa ni wizi tu"

Ameongeza "Baraza la Elimu ya Sheria mko wapi? Hii si kazi ya Serikali, mnatakiwa kuwadhibiti hawa Watu. Wanachukua pesa za Watu na hawatimizi malengo"

Wanawake Wengi Walioolewa ni Wepesi wa Kuchepuka..Yaani Simple Kama Kumsukuma Mlevi

$
0
0
Wanawake wengi walioolewa wamekuwa wepesi (achilia mbali vidada ambavyo havijaolewa, ingawa navyo ni majanga lakini, afadhali mitego yao kidogo ni negotiable).

Wengi wao huwatongozi ila watakutongoza wenyewe! Kundi risky zaidi ni la wamama wa nyumbani au wanawake ambao hawajasoma (I am sorry to say this)!

Unaweza kukuta mme wake ana fedha na kila kitu, lakini kwa sababu jamaa hajaajiriwa serikalini au kwenye taasisi au kampuni (kumbuka tulio wengi tunatamani kujiajiri!), mke wake anamchukulia kama mtu fulani ambaye hana hadhi nzuri ya kuwa mme.

Sumaku kali zaidi ambazo huwavuta wamama wa aina hiyo, ni wale vijana au watu wazima walioajiriwa, wanaotoka asubuhi, wamepiga tai, kiatu kiwi full time, wengine suti, halafu ni watu wa misheni town (wenye magari sijui inakuwaje, mtatuambia), (haata kama kazi zao ni kufagia au kuzunguka na mafile maofisini)!

Wanawake wa aina hiyo huanza kwanza kwa kutafuta ukaribu na mazoea na watu wa aina hiyo kwa udi na uvumba katika harakati za kufanikisha azma zao.

Licha ya uzoefu nilioushuhudia juu ya wamama hapo juu, hivi karibuni nimekumbana na majanga kadhaa yakihusisha wanawake walioolewa kwa ujumla, wengi wao wanaoonekana ni sex hungry moms au gold diggers. Nawapa tu mifano michache kuthibitisha haya ninayoyasema:

1. Mie nakaa mwenyewe mmama from no where akaanza kuniletea chakula (niliogopa sana), akaniambia naona unapata shida unakaa mwenyewe na wewe ni mwanaume huwezi kujipikia.

Siku ya kwanza sikukila (nilikiweka kwenye chombo changu nikampa sahani, baadaye nilikimwaga), maana niliona kama labda kaweka kitu. Siku nyingine akaleta na kuniambia tule wote! Hooooooooo, nikamwambia tutakula wapi?

Akasema kwako, usiogope mme wangu amesafiri! Sasa tukiwa tumekaa, alikuwa amejifunga kanga moja, anatawanya miguu na kuirudisha, nilijikaza sikufanya chochote, vituko anavyonifanyia mpaka sasa ni siri yangu.

2. Mwingine alipata namba yangu kupitia simu ya mmewe ambaye ni rafiki yangu, kila mara hasa usiku ana msgs kama hizi: "shem habari, nahisi wewe ni mcheshi, huna kiburi wala makuu, tena unachat na mimi bila shida, nina hamu siku moja nije Dar nikufahamu, au sio shem?"

Mara nyingi sijibu, akiona hivyo "shem nijibu basi, usiogope maana mme wangu hayupo sasa hivi". Vituko vyake siku hizi havisimuliki!

3. Mwingine, kutwa kulalamika kuhusu maisha yake na ndoa "Yaani shem, we acha tu, maisha magumu, rafiki yako naye kipato hakieleweki na mie sikusoma wala kubahatika kuajiriwa, maisha yanaenda tu kwa nguvu za Mungu, ningekuwa sio mvumilivu sidhani kama hii ndoa ingekwepo, shem unakaa wapi nije kukusalimia au una mke?" Mie najiuliza hivi wakati wa kufunga ndoa hakuapa kuwa na mmewe kwa shida na raha?

4. Mwingine ni mama jirani yangu, tena ni mtu anayejiweza, siku moja akaniita anaomba nimsaidie kurudishia taa imeungua, nilivyopanda juu ya meza alinipa taa - tube light mbovu, kuiweka haiwaki, akaniambia naomba simu yako nimpigie kijana fulani wa mtaani aniletee taa nyingine, nilivyompa kumbe alijipigia, halafiu akaniambia hapatikani, acha.

Tangu awe na namba yangu, utaona mida ya saa 4 usiku anatuma msgs kama vile "Mambo, Jumamosi hii twende tukatembee" au "Nina kitu nataka kukuambia ila tunahitaji faragha", Huwa namjibu, nina mambo mengi, labda siku nyingine.

Ni majanga mengi sana nakutana nayo yanayohusisha akina mama walioolewa. Mliooa kuweni makini na wake zenu, wengi ni washenzi sana na wana sophisticated means za kuwaengage wanaume wengine kwenye mahusaiano na wao! Pia najiuliza tatizo lao la kuzoeana na wanaume wengine na kujifanya wana hamu ya kuchat au kuwa karibu nao na sio waume zao ni nini?

NB: Nawaasa vijana kukaa mbali na mke wa mtu, maana mke wa mtu ni zigo la madawa ya kulevya.

Show ya ZUCHU DMV Marekani ni tofauti na aliyofanya HUSTON TEXAS, wengi wamejitokeza: MR-TZ

$
0
0

 

Show ya ZUCHU DMV Marekani ni tofauti na aliyofanya HUSTON TEXAS, wengi wamejitokeza: MR-TZ

VIDEO:


Kombe la Dunia: Ghana Yakaza Hadi Dakika Ya Mwisho na Kunyoa Wakorea

$
0
0


Timu ya taifa ya Ghana imepambana kwa jino na ukucha hadi kusajili ushindi wao wa kwanza katika mashindano ya mwaka huu ya Kombe la Dunia yanayoendekea nchini Qatar.


Ghana wamevulia madude ya Korea Kusini na kunyakua ushindi. 
Baada ya kupoteza mechi yao ya kwanza kundi H 3-2 dhidi ya Ureno, Ghana wamejikaza kisabuni na kusajili ushindi sawia (3-2) dhidi ya Korea Kusini.

Tanzania Yatoa Uraia zaidi ya Wakimbizi Laki Mbili

$
0
0


Tanzania ni Nchi pekee Afrika ambayo imetoa uraia kwa Wakimbizi 162,000 wa Burundi, 30,000 wa Rwanda na 10,000 wa Somali Bantus.

Mwakilishi wa Shirika la Wakimbizi Duniani upande wa Tanzania, Mahoua Parums ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa Ushirikiano kwenye masuala ya Wakimbizi katika kikao cha ndani alipokutana na Naibu Mwakilishi wa Kudumu Geneva Balozi Hoyce Temu @hoycetemu katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje.

Ikumbukwe kuwa Ofisi za Uwakilishi wa Kudumu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Geneva inasimamia mashirika mengi ya Kimataifa ikiwemo UNHCR, Tanzania hadi leo hi inahifadhi Wakimbizi zaidi ya 260,000 mkoani Kigoma.

Serikali Yatoa Tamko: Wazazi Msiwanunulie Simu Watoto Waliopo Shuleni

$
0
0


Kaimu Mkuu wa Mkoa wa #Geita, Tito Mlelwa amesema watoto wasipewe kila wanalohitaji ikiwemo simu za mkononi ili kuwaepusha na mmomonyoko wa madili unaotokana na mitandao ya kijamii

Amesema wazazi wanatakiwa kubeba mzigo huo kwa kuwa wengi wao wanafanya hivyo ili kumfurahisha mtoto kwa kumpa kila kitu. Huko mitandaoni aina ya ujumbe wanaoutuma na picha wanazozituma zinazidi kuharibu tabia za watoto.

Bwana Harusi Mtarajiwa Ajinyonga Kabla ya Kufunga Ndoa

$
0
0

BWANA HARUSI MTARAJIWA AJINYONGA KABLA YA KUFUNGA NDOA: Daktari mmoja aliyekuwa akihudumu kwenye zahanati katika Kitongoji cha Saghana wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro amefariki dunia kwa kujinyonga kwa kutumia shuka yake ikiwa zimebaki siku 29 kabla ya kufunga ndoa.

Taarifa kutoka kijijini hapo zinasema Joseph Patrick Ngonyani (33) alijinyonga Novemba 26, siku ambayo alipaswa kwenda ukweni kwake Kijiji cha Lotima nchini Kenya kukamilisha taratibu za mahari.

Kocha wa zamani wa Simba SC, Didier Gomez ala Shavu Uarabuni

$
0
0

Kocha wa zamani wa Simba SC, Didier Gomez da Rosa ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa klabu ya Al Ain FC inayoshiriki ligi kuu ya Falme za Kiarabu (UAE)Unapenda Simulizi? Kuna NDOA YANGU na kuna INATOSHA, Zitakukosha sanaa. Bofya Hapa kufurahia sehemu ya 1 bure ndani ya group la telegram.

Mbali na Simba SC Da Rosa amewahi kuvitumikia vilabu vya Rayon Sports, Horoya AC FC na timu ya Taifa Mauritania.

Kocha wa Timu ya Taifa ya Cameroon Rigobert Song Afafanua Kumtimua Andre Onana

$
0
0

 


Kocha wa Timu ya Taifa ya Cameroon Rigobert Song amekanusha taarifa za kumtimua Mlinda Lango Andre Onana, kwa sababu za kukataa kutii amri ya kutimiza jukumu la ushirikiana na kupinga mpango wa Rais wa Shirikisho la Soka nchini humo Samuel Eto’o kufanya mazoezi ya timu hiyo.


Onana aliondolewa kwenye kikosi cha Cameroon saa chache kabla ya mchezo pili wa Kundi G dhidi ya Serbia uliomalizika kwa timu hizo kufungana 3-3.


ong amesema amelazimika kumuondoa Mlinda Lango huyo wa klabu ya Inter Milan ya Italia, kwa sababu za kinidhamu ambazo zilipelekea washindwe kuelewana, hasa alipokataa kucheza mchezo dhidi ya Serbia jana Jumatatu (Novemba 28).


“Ni mchezaji muhimu, lakini tuko kwenye michuano migumu, hivyo ni bora akatupisha ili tumalize hili kwanza,”


“Ninajua ninachopaswa kufanya, na hiyo ni kuhakikisha kuwa timu kwanza halafu mchezaji baadae.” alisema kocha huyo baada ya mchezo dhidi ya Serbia


Alipoulizwa na Shirika la Habari la AFP iwapo angeanza mchezo wa jana dhidi ya Serbia badala ya Onana, Mlinda Lango namba mbili Devis Epassy alijibu “Ningependa hili swali aulizwe Kocha Song, mimi sitakua tayari kujibu”


Ninachojua hakuna tatizo lolote katika kambi yetu hapa QATAR.” alisema Devis Epassy



Wachezaji Young Africans Wapigwa Marufuku

$
0
0

 


Wakati Ligi Kuu Tanzania Bara ikiendelea kushika kasi, Kocha Mkuu wa Klabu ya Young Africans Nasreddine Nabi amewapiga marufuku Wachezaji wake, ili kufanikisha lengo la kuendelea kupambana kwenye michezo inayowahusu.


Young Africans kwa sasa inaongoza msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na alama 32 sawa na Azam FC, huku leo Jumanne (Novemba 29), ikitarajia kucheza dhidi ya Ihefu FC mjini Mbeya katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine.


Nabi amewataka wachezaji wake kueleleza akili zao katika michezo inayowahusu na hataki kusikia mchezaji anafuatilia na kuchekelea matokeo ya wapinzani wowote kwenye Ligi wakiwemo Simba SC.


Kauli hii inawalenga mastaa wote wa Young Africans wakiwemo vinara wao, Fiston Mayele anayeongoza kwa ufungaji wa mabao hadi sasa Ligi Kuu akiwa amefunga manane, Faisal Salum ‘Feitoto’, Aziz Ki, Djigui Diarra na wengine akisisitiza anachotaka ni waangalie michezo yao na kila mchezaji ajipange kutumia mgawanyo wa nafasi za kucheza katika timu hiyo ili kuisaidia timu kushinda.


“Sidhani kama ni sahihi kwa wachezaji au sisi makocha kuanza kuangalia na kufurahia matokeo ya timu pinzani kwetu, hii nimewaambia sitaki kuona mchezaji anazungumzia hilo au kujiona tumeshinda,” alisema na kuongeza;


“Kuna mambo ambayo tunatakiwa kuwaachia mashabiki wetu kufurahia ushindi wetu au matokeo mabaya ya timu zingine. Kila mchezaji wa timu hii anatakiwa kujipanga kwa kuangalia anapambanaje kuingia kwenye timu ya kwanza ili acheze aisaidie timu hii.”


Kocha huyo bora wa msimu uliopita wa Ligi aliyechukua mataji matatu alisema ligi bado ndefu na lolote linaweza kutokea kwa kuwa mchezo wa soka yeyote anaweza kushinda.


“Nani alikuwa anajua Saudi Arabia inaweza kushinda mbele ya Argentina? Huu ndio mchezo wa soka wakati mwingine unashtua, Ligi haijamalizika tena bado ndefu lolote linaweza kutokea.”


“Tunachopaswa kufanya ni kuendelea kuhesabu kwa kushinda michezo yetu mmoja kwenda mwingine kisha tuangalie tumevuna alama ngapi mwishoni mwa msimu, hivyo ndivyo timu inayotaka ubingwa inatakiwa kuishi.”

Aika na Nahreel wa Navykenzo Watangaza Kuachia Ngoma na Fireboy DML

$
0
0


Jumatano hii, tarehe 30, wanamuziki Aika na Nahreel ambao wanaunda kundi la @navykenzoofficial wanaachia kolabo yao wakiwa na mwimbaji nyota toka Nigeria, Fireboy DML.


Wakali hao wanaofanya vizuri na smash hit yao "Manzese", hii inaenda kuwa ngoma yao ya pili kuachia mwaka huu. Kaa tayari kwa ujio huu.


Brazil na Ureno Zatinga Hatua ya 16-Bora Kwenye Kombe la Dunia

$
0
0





Brazil iliungana na Ufaransa katika hatua ya mwondoano kwenye Kombe la Dunia siku ya Jumatatu, Novemba 28, baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Switzerland.

Portugal.

Cristiano Ronaldo (kushoto) na Bruno Fernandes wakishangilia baada ya kushinda mechi ya Kundi H dhidi ya Uruguay. Picha: Odd Andersen. Chanzo: Getty Images
Kiungo wa kati wa Brazil, Casemiro ndiye alifunga bao la kipekee ambalo liliwasadia washindi hao mara tano wa Kombe la Dunia kufuzu katika Kundi G.

Huku Brazil hao wakikosa huduma za nahodha wao nyota Neymar aliyejeruhiwa, walionekana kana kwamba wangekuwa na ulazima wa kusawazisha kwa pointi moja baada ya bao la Vinicius Junior katika kipindi cha pili kukataliwa kwa msingi wa kuotea.


Lakini zikiwa zimesalia dakika saba kwa mechi hiyo kutamatika, Casemiro ambaye huchezea Manchester United, alichonga ndizi hadi kimyani akimchenga Manuel Akanji na kuvunja ngome ya Mswizi huyo mahiri.

Kikosi cha Tite ni timu ya pili kufuzu kwa hatua ya 16 bora baada ya Ufaransa na pia ni timu pekee mbali na watetezi kushinda mechi zote mbili za makundi nchini Qatar.

Brazil walianza kampeni yao nchini Qatar kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Serbia lakini walipata pigo baada ya fowadi wa Paris Saint-Germain Neymar kupata jeraha la kifundo cha mguu.

Ronaldo
Wakati huo huo kiungo wa Manchester United Bruno Fernandes alifunga bao lake la kwanza katika Kombe la Dunia na kusaidia Ureno kufuzu kwa duru ya 16.

Fernandes alifungia Ureno mabao mawili katika mechi dhidi ya Uruguay wakati wa pambano la pili la Kundi H lililosakatwa kwenye Uwanja wa Lusail.

IRENE UWOYA anunua CD ya Rosa Ree kwa MILIONI 1, AMBER LULU ainunua kwa ELFU 50/Baraka the Prince Amwanga Laki 5 kununua CD.

$
0
0

 


IRENE UWOYA anunua CD ya Rosa Ree kwa MILIONI 1,AMBER LULU ainunua kwa ELFU 50/BARAKA amwanga Laki 5 kununua CD.

VIDEO:



Rammy Galis " Filamu inawaka MOTO, Rosa Ree Rapa Bora wa Kike Bongo"

$
0
0


Rammy Galis " Filamu inawaka MOTO, Rosa Ree Rapa Bora wa Kike Bongo"

VIDEO:



Viewing all 109660 articles
Browse latest View live
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>