Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all articles
Browse latest Browse all 109519

Ndoa ya Kanye West na Kim Kardashian sasa Kufungwa Italia na si Ufaransa

$
0
0

Ripoti mpya zinadai kuwa harusi ya rapper Kanye West na mama wa mwanaye Kim Kardashian sasa itafanyika Italia na sio Paris, Ufaransa kama ilivyodhaniwa awali.

Entertainment Tonight imeripoti kuwa wageni waalikwa watakusanyika pamoja Paris, Ufaransa May 23 kwaajili ya chakula cha usiku ‘Pre wedding dinner’, na baada ya hapo couple hiyo itawasafirisha wageni wote kwa ndege binafsi tofauti kuwapeleka Florence, Italy ambako sherehe rasmi ya ndoa yao itafanyika.

Kumekuwa na habari mbalimbali kuhusu ndoa ya Kanye na Kim, huku wengine wakidai kuwa couple hiyo tayari imeshafunga ndoa, habari ambazo Kim Kardashian amezikanusha hivi karibuni kupitia twitter kuwa bado hawajafunga ndoa.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 109519

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>