MWILI wa kichanga umeokotwa eneo la Njiro jijini Arusha juzi baada ya kudaiwa kutupwa na mama mmoja ambaye hakufahamika jina lake mara moja.
Baada ya kichanga hicho kuokotwa, wananchi walitoa taarifa polisi waliofika na kufanikiwa kumkamata mama mwenye kichanga hicho.