Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all articles
Browse latest Browse all 109599

IRENE UWOYA Kumpeleka NDIKUMANA Yanga

$
0
0
BINTI aliyejaliwa uzuri wa sura anayeng’ara kwenye filamu za Kibongo, anamshawishi mumewe Hamad Ndikumana aje kucheza Yanga ya chini ya kocha, Marcio Maximo.

Ndikumana ambaye kwa sasa anaichezea Vital’o ya Bujumbura, Burundi ameweka wazi kwamba binti huyo, Irene Uwoya ambaye ni mkewe ni shabiki wa Jangwani na amekua akimshawishi kila mara kwamba atue Jangwani ili awe naye karibu zaidi kwani hana mpango wa kuondoka Dar es Salaam kwenye kazi zake za filamu.

Mchezaji huyo amekiri kushawishiwa mara nyingi lakini alisema hawezi kujipeleka Yanga mpaka timu hiyo itakapomfuata, kama hiyo haitoshi aliongeza kwamba anaogopa kuishi Dar es Salaam kutokana na mambo ya ushirikina yaliyomtokea alipoanza maisha na mkewe ambaye ameshangaa watu wanaozusha kwamba wameachana.

Ananitaka nije kucheza Tanzania alikuwa ananiambia nije Yanga, unajua anaipenda sana Yanga lakini nikamwambia mimi ni mchezaji ninayejiamini siwezi kuja kuomba Yanga wanisajili acha waje wao tuzungumze, yuko tayari kufanya hata ushawishi kwa wadau,” anasisitiza Ndikumana ambaye awali alikuwa akiichezea APOP Kinyras Peyias ya Cyprus.

Ndikumana alisema kilichomtoa Cyprus na kuja Burundi pamoja na uhusiano wake na Uwoya.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 109599

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>